#TOTTechs Profile picture
Jukwaa la washauri na wataalamu wa Teknolojia || 💻 Computers ||📱 Phones | Softwares | ICT Hardwares | ICT Security || Partnership with Kukeke Gang and L.M.S

Jun 22, 2021, 19 tweets

DARASA LA CRYPTO:
SEASON 1: UZI/THREAD

MEME COINS/SHITCONS

Meme Coins au Shitcoins unaweza kuziita coins za majitaka au futuhi coins

Ni coins ambazo zimekua zikipendwa sana na watu wa Crypto kwa kuwa zinaweza kukupa faida hata mara 1000 ya mtaji wako kwa muda mfupi. 👇

Meme coins zimeundwa bila kuwa na matumizi yoyote muhimu kasoro kiki inayotokana na Jina la hiyo coin.

Katika msimu huu wa Crypto, shitcoins zimekua zikipatikana sana katika Blockchain inayoitwa Binance Smart Chain (BSC) kupitia website inayoitwa Pancakeswap

na kununua inabidi uwe na salio la coin ya BSC inayoitwa BNB na iwe ndani App ya TrustWallet...utatumia adress ya hiyo coin yako ili kuinunua

Kwa kawaida tumezoea Coin inakua na project fulani ili watu wawekeze.
Sasa hizi MemeCoins hazina project yoyote zaidi ya kupigiwa Kiki

Namna ya kununua Coins itaelezwa zaidi kwenye threads zijazo.

Meme Coins zipo nyingi, baadhi yake ni

Doge Coin
Mona Coin
Shiba Inu
Banano
Cum Rocket
Doge Swap
Safe Moon

Meme Coin kubwa kuliko zote ni Dogecoin na inaongozwa na kiki za tajiri Elon Musk

Dogecoin iliundwa kama utani kwa lengo la kuwatania watu kuwa sikuhizi watu wanaunda coin za kijinga kwahyo yeye ameunda yake inaitwa Dogecoin ikiwa na Picha ya mbwa wa kijapani anaeitwa Shiba Inu

Hii Dogecoin inapanda thamani tu pale inapokuwa inatangazwa na watu kwa lengo la kuwa watakuja kutajirika siku moja

Katika msimu huu wa Soko la Crypto (2021) tumeona hizi futuhi coins zikiingia sokoni kila leo zikiongozwa na Safemoon coin ambayo

walioiunda walikiri kuwa waliiunda bila kujua itatumika kufanyia nini na hawakujua itavuma kama ilivyovuma.

Hizi Meme Coins au Futuhi Coins, zinaweza kukupa faida kubwa ndani ya mda mfupi endapo ukiweza kuzifahamu siri zake na ukazinunua katika msimu wake na muhimu zaidi

ukijua ni muda gani wa kuziuza, Msimu wa Shitcoins huanza baada ya Bitcoin na coins nyingine nzuri kuingiza pesa na waliotajirika kuanza kutambia wenzio hapo ndio wale ambao hatujui kitu kuhusu crypto tunaingia tunakuta hakuna coin za kununua ili tutoboe

...sasa ndio shitcoin zinaundwa kutudanganya kuwa tutatoboa.

Futuhi Coins siku inavyoingia sokoni hua zinanunuliwa haraka na wamiliki na watu wanaitwa 'Whales' au 'Nyangumi' kwa kutumia software maalum zinaitwa 'trading bots' ambazo zinafanya manunuzi haraka kuliko binadamu

zinakuwahi kununua kabla yako

Whales au Manyangumi ni watu wenye pesa nyingi kiasi cha kufanya bei ya Coin ipande haraka kwa muda mfupi..hawa watu hua wanapanga dili na wamiliki wa coins Wakishanunua awali ndio sisi tunakuja kuskia coin fulani ina trend

imeongezeka thamani mara 5 au 10 hapo ndio muda watu wengi tunainunua Tukishainunua inapanda thamani tena kwa kua tupo wengi, ila sasa huu ndio muda wale Manyangumi na wamiliki hua wanauza hizo Coins zao.

Ukichelewa hapo utaambulia hasara kubwa kwa kuwa wakiuza wale wakubwa utapata hasara , njia pekee ya kuzuia hii hasara ni kuipigia promo hiyo coin wenzio wanunue ili bei isishuke...

Kwa kua hiyo coin haina matumizi yoyote ni ngumu mno kuhamasisha watu wainunue..

hivhyo mbinu chafu hutumika mfano kukuambia kuwa utatajirika kwa muda mfupi pale utakaponunua na usiuze(hodl) hadi bei itakapopanda kufika mwezini au "To the moon" .
Mbinu nyingine chafu ni wamiliki walivogundua kuwa wakiweka thamani ya coin iwe na bei ndogo watu ndio watanunua

....zaidi wakiwa na imani kuwa itafika dola $1 au $10 Hivyo Shitcoins hizi hua na bei kama $0.00000001 na kwa kuwa watu hawajui basi hununua wakitegemea kuwa wamewahi ipo siku itafika dola moja watatajirika

Ukweli ni kuwa ukinunua Meme Coin mfano ShibaInu, ili ifike thamani ya $10 inahitaji fedha zote duniani tena uzidishe mara sita , zitumike kuinunue hiyo coin ndo itafika $10
Wengi hawajui haya mambo wanashindwa kujua ni muda gani sahihi wa kuuza hivyo hupata hasara mno

Hizi meme coins hua zina majina yanayovutia wageni wa hili soko na pia zinakuwa na majina yanayofanana au yanayoendana na Coin maarufu.

Pia kuna muda unaweza kuuziwa shitcoin ambayo utashindwa kuiuza pale faida zinapopatikana

kwakuwa wamiliki wanakua wamesepa na pesa zote zilizopo kwenye 'Float' (Liquidity) ya kubadlishia fedha zako
Shitcoins zina faida kubwa mno ila jua muda wa kuingia na wa kutoka, Pia watu wakubwa na ma rolimodo wako wanaweza kulipwa au kukudanganya makusudi ununue hiyo Shitcoin

ili yeye atajirike kwa kua anayo tayari Mara nyingine hata hao watu maarufu hili soko hawalijui watakuhamasisha ununue tu na kwa kua unawaamini unainunua...utaumia ndugu yangu. Usiamini sana watu kwenye cryptocurrency bila kufanya tafiti zako binafsi

TO THE MOOOOOOOOOOOOOOOOOOON!!!!

Imeandaliwa na @NNgailo [ Nicky ] pamoja na @TOTTechs

Cc: @BankOfTanzania
@wizaraMTH
@TanzaniaSA
@ZMuhaji

SOMO 2. TUTAELEZA KUHUSU BITCOIN.

SOMO 3. NAMNA YA KUNUNUA NA KUUZA COINS

STAY TUNED, WEKA NOTIFICATION ON

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling