JAPHET MATARRA Profile picture
Father | Human Right Activist | Mineral Processing Engineer | Paralegal | Member @ChademaTz | @ManUtd | @YoungafricansSC | Boss Himself | StoryTeller | 430'2023

Jul 29, 2021, 96 tweets

FAHAMU MADINI YA ALMAS 💎 UTAJIRI & VITA YAKE

#Uzi:
📋Asili yake
📋Historia yake
📋Mgunduzi wake
📋Aina & Thamani yake
📋Vita yake duniani na Tanzania
📋🇹🇿 iligunduliwa lini na nani, wapi
📋DE BEERS & Msukuma wa Williamson DIAMONDS, aliyeipenda Mwadui hakuna wa mfano wake!!
🔄👇

Leo nimechagua kuzungumzia Maliasili za Taifa🇹🇿

#Maliasili ni vitu vinavyotokana na maumbile. MFANO:Wanyama, Misitu, Madini n.k kama ulikuwa hufahamu maliasili za nchi huchangia ktk utajiri wa nchi husika.Mojawapo ni South Africa, imenawiri kiuchumi kutokana na utajiri wa madini

Nafahamu ulishawahi kujiuliza, Almasi ni nini? Iko iko je? au Almasi zinatengenezwa na nini?

LEO nakupa Jibu:

#ALMASI: Ni kito Adimu chenye thamani kubwa sana Duniani. Kito hiki ni kigumu sana kushinda Metali au madini yote Duniani. Asili yake hutengenezwa na Carbon (C) 99.95%

#Almasi hutumiwa ktk teknolojia mbalimbali. MFANO: Ktk vyombo vya kukata vitu vigumu au keekee za kutoboa mwamba wkt wa kutafuta mafuta ya Petroli, vyote hutumia vipande vya 💎.
Almasi asili haina rangi ni Colourless Lkn chache sana naomba zenye rangi za njano, buluu au nyekundu.

Madini haya hutumiwa kama mapambo na kutokana ugumu wao pia katika teknolojia ya kukata.

Kikemia Almasi ni umbo moja la kaboni (C) tupu katika hali ya fuwele (crystal) na ni dutu ile ile kama makaa ya mawe. Ila tu kaboni huwa almasi ktk mazingira ya joto kali na shinikizo kubwa.

Almasi ndio kito pekee kimeundwa na elementi moja [C]. Kimuundo Almasi ina 99.95% za Carboni tu. Asilimia nyingine (0.05) zinazobaki zinajumuisha chembe moja au zaidi ambazo ni atomi na sio sehemu muhimu ya kikemikali ya Almasi na nyingine zinaathiri rangi yake au umbo la kioo.

Muonekano wa umbo la Almasi yenye ubora zaidi ni umbo la "Octahedron" ambalo linaonekana km piramidi mbili kutoka upande wa nyuma kwenda mwingine. Fuwele (Crystals) zilizokaribiana ktk umbo huitwa 'Glasi'.

Almasi huwakilishwa na herufi 'C' as chemical symbol yake na Emoji hii 💎

Kufahamu namna madini yanavyojitengeneza inasaidia kutambua aina zake.

Almasi hujitengeneza ktk joto kali na hali ya shinikizo|mgandamizo mkubwa (Ultra-High Pressure Metamorphism) ambao hupatikana huko chini ya miamba ya dunia zaidi ya kilomita 150 mpaka 250 kutoka uso wa Dunia.

Mchanganyiko maalum wa muundo wa kemikali, muundo wa kioo na mchakato mzima wa namna inavyojitengeneza hukifanya kito hiki kuwa na ubora wa tofauti. Lkn isingekuwa mojawapo sababu hizo Almasi ingekuwa sawa na madini mengine na ya kawaida tu.

Muundo wake ni Isometric yaani atomi nyingi za Carbon zimekusanyika ktk sehemu ya muelekeo mmoja.

Madini mengine yanayofanana na muundo wa Almasi ni Graphite ambayo yana Carbon nyingi ila utengenezaji wake na muundo wa Crystals zake uko tofauti. Ndio maana Graphite ni laini kiasi unaweza kutumia kuandikia lkn Almasi ni ngumu kiasi kuiscatch labda utumie kipande kingine cha 💎

Almasi hutengenezwa wkt Carbon imewekwa chini ya shinikizo (pressure) paundi 725,000 kila inchi ya mraba na kwa joto la kati ya nyuzi 900 hadi 1,300

#Unaambiwa jiwe lingine pekee la thamani kwenye sayari ya dunia linaloweza ku-crystallize chini ya hali sawa na hii ni #Peridot tu

Baada ya kujitengeneza kwa miaka takribani Bilioni moja mpaka Bilioni 3.4 hubebwa na uji uji ktk milipuko ya ndani ya Volcano na kisha hukusanyika kwenye maeneo (fissures/faults) ya miamba Tabaka (Igneous rocks) iitwayo #Kimberlite na #Lamproites.

Mpaka Almasi kuonekana ktk uso wa dunia ni aidha kwa nguvu ya kiasili au kwa kuchimbwa na mwanadamu kwa kutumia vifaa mbalimbali ktk uso wa dunia. Ikishachimbwa husafishwa na kisha hukatwa mpaka ambapo mng'ao wake asili huonekana.

Maendeleo ya sayansi na Teknolojia yamesaidia pia kupatikana kwa Almasi (Artificial) zinazotengenezwa na wanadamu kwa kutumia mashine zinazosukuma kaboni kwa shinikizo kubwa na halijoto ya 1,500 °C (chemical vapor deposition-CVD) hadi kuwa almasi yenye tabia zote sawa na 💎asilia

Hivyo wewe unayesoma #Uzi huu hapa ninakufahamisha kwamba sio kila Almasi unayoiona imechimbwa migodini, zingine hutengenezwa na binadamu na zinazofaa pia kwa mapambo.

Kampuni kubwa duniani ya kuchimba almasi ni @DeBeers iliyopo nchini Afrika Kusini.

DE BEERS ni wanamiliki migodi mikubwa Botswana, South Africa, Angola pia walikuwa wamiliki mgodi wa MWADUI hapa 🇹🇿 kwa sasa wamiliki ni @Petra_Diamonds wanaosadikiwa kuwa ni kampuni la DE BEERS.

Mwanzoni mwa miaka ya 1900, kampuni ya madini ya @debeersgroup ilidhibiti karibu asilimia 90 ya uzalishaji wa madini ya Almasi ambayo haijakatwa (rough diamonds) duniani.

Kama unasoma #Uzi hebu toa pongezi ya heshima De Beers sio kwa kuthubutu huko.

DE BEERS ndio kampuni ya kwanza kwa utajiri Afrika wakiwa wana zaidi ya US$ 5.1B kwa mujibu wa record ya mwaka 2020. IKIWA ni kampuni yenye kuzalisha na kuuza zaidi ALMAS kwa 40% duniani ikiwa ni kampuni yenye mafanikio zaidi kwa kushika nafasi ya 13 kwa utajiri Duniani wa madini

Mwanzilishi wa kampuni #DE_BEERS ni CECIL RHODES alikuwa ni kabulu kutoka uingereza mkoloni huko South Africa miaka ya 1886.
Unayesoma #Uzi huu RETWEET uwafikie wengi wajifunze na hii inakuwa FAIDA ya kujiunga na mitandao ya kijamii ikiwemo TL unapata usivyovifaham!!

LET'S GO👇

HISTORIA YA ALMAS

Almasi ina historia ndefu sana kama kito kizuri cha thamani

Historia yake inaanza ktk karne ya 01 BK Mwanahistoria (Italy) #Pliny alisema: "Almas ni kito cha Thamani zaidi, sio tu cha thamani ktk mawe, lakini ni kito cha thamani kuliko vitu vyote ulimwenguni."

PLINY THE ELDER

au GAIUS PLINIUS SECUNDUS alizaliwa mnamo 23AD Kaskazini mwa Italia, huko Novum Comum (baadaye paliitwa kifupi Como) iliyoko 28miles kaskazini mwa Milan leo hii anajulikana kama "Pliny The Elder".
Azaliwa ktk familia tajiri, Babaake alikuwa Mmiliki Farasi wengi.

Huyu ndiye anaaminika km Mgunduzi wa madini ya Almasi.

Baba yake alimpeleka Roma mnamo 35AD ambapo alisoma kisha akajiunga na Jeshi kisha baadaye akasomea mimea (Botany). Utafiti wake wa kisayansi ulikuwa mkubwa na maandishi yake yaliandika masomo mengi katika maisha yake yote.

Wakati wake ktk Jeshi ilikuwa ni lazima asafiri huku anaandika mambo mbalimbali, MFANO: Uchimbaji Madini ya Dhahabu huko Uingereza na ktk mabara ya Afrika na Asia.
#PLINY_THE_ELDER aliandika vitabu vingi sana na ni moja watu mahiri wa Philosophy na semi na alisomea pia sheria.

Kitabu chake "Historia ya Asili" (Historia Naturalis) ni moja ya kazi zake za kushangaza, ambacho kina masomo kama vile Unajimu (Astronomy), Elimu ya viumbe (Zoology), Mimea (Bontany), Dawa za matibabu na Madini (Mineralogy).

IKIWA Unasoma #Uzi huu nikuombe support kwa 🔄 yako

Kitabu hiki ni Encyclopedia yenye maarifa ya zamani ambayo hapo ina juzuu 37 na imetumika kwa karne nyingi na wasomi wengi wasiohesabika.
#PLINY aliandika madini mengi yaliyotumiwa na Warumi kwa mapambo ya binafsi ambapo aliorodhesha:Amber, #Almasi Emeralds, Beryl na Sapphire n.k

Mnamo Agosti 24, 79AD alikuwa akisimamia meli za Kirumi huko Misenum. Kulitokea mlipuko wa volcano mitaa ya Vesuvius.Akiwa anashuhudia anga lote liligubikwa na moshi uliokuwa unatoka mlimani.Alitazama jambo lile huku akiwa na hamu ya kuwaokoa rafiki zake waliokuwa Ghuba ya Naples

Baada ya kukaa kwa muda mrefu akisoma na kuona mlipuko wa volkano alifunikwa na majivu na gesi zenye sumu na alikutwa amekufa mnamo Agosti 26 79 AD baada ya kutawanyika kwa majivu yaliyokuwa yamefunika eneo lote.

RT @balozi_twita @omari_manyama @msangijeff @MabalaMakengeza Up👆

Sehemu ya historia ya maisha ktk masaa ya mwisho ya PLINY iliandikwa na mdogo wake na ilitumwa kwa barua kwenda kwa Mfalme TACITUS miaka 27 baada ya tukio hilo.
#Pliny_The_Elder bado anakumbukwa ktkTopic ya volcanism ambapo neno #Plinian humaanisha mlipuko mkali wa Volkano.

Tangia awali Madini ya Almasi yalikuwepo sehemu nyingi Duniani na nchi ya kwanza kutumia Almasi ni Yemen huko Mashariki ya Kati. Lakini kujulikana kabisa kwa thamani Almasi ulimwenguni, kulianzia nchini India, ambapo almasi zilikusanywa kutoka mito na vijito vya nchi hiyo.

Wanahistoria wengine hukadiria kwamba India ilikuwa ilianza kufanya biashara ya almasi mapema ktk karne ya 4 KK. Zama za kali rasilimali za nchi zilitokana na idadi nyingi ya madini kwenye masoko. Hata hivyo miaka nenda miaka rudi hali za uchumi ktk mataifa zilibadilika.

Almasi iliyotoka India ilikuwa za thamani sana ktk masoko ya magharibi huko Ulaya na kufikia miaka ya 1400, ilikuwa kitu cha thamani kwa matajiri ulaya. Mwanzoni mwa 1700's, upatikanaji Almasi ya India kulianza kupungua na Brazil iliibuka ktk soko na kitovu cha Almasi Duniani

Huko Brazil almasi zilikuwa zikipatikana kwa kuchekecha makarai ya wachimba dhahabu wakati wakipepeta michanga kwenye mito mbalimbali nchini humo. Ilifikia mahala Brazil ikawa nchi yenye Almasi nyingi kuliko yeyote kwa takribani zaidi ya miaka 150.

Baadae soko la almasi lilibadilika baada ya watawala na watumiaji wakubwa wa almasi kupungua mwishoni mwa miaka ya 1700. Mapinduzi ya kisiasa mfano mapinduzi ya Ufaransa yalipelekea mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa utajiri huu.

Miaka ya 1800 ilikuwa ya mageuzi kwenye utajiri huu na kuzidi kuongezeka magharibi mwa Ulaya na Marekani. Walowezi waligundua amana kubwa ya Almasi kwa kwanza nchini Afrika Kusini mwishoni mwa miaka ya 1800 wkt mahitaji ya Almasi yalipoongezeka.

Stori ya soko la kisasa la Almasi huanzia kabisa ktk Bara la Afrika, ambapo ugunduzi wa Almasi ulifanyika mnamo 1866 huko Kimberley, nchini Afrika Kusini.

Mfanyabiashara Mkoloni CECIL RHODES alianzisha kampuni ya @DeBeers Consolidated Mines Limited miaka 22 baadaye, mnamo 1888.

Kufikia 1900 Kampuni ya madini ya DE BEERS kupitia migodi yake ya nchini Afrika Kusini, ilidhibiti soko la Almasi kwa takriban asilimia 90 ya uzalishaji wa almasi yote ulimwenguni. Kupatikana kwa Almasi iliyotoka Afrika Kusini iliathiri sehemu nyingi za masoko ya Almasi.

Kilikuwa ni kito haswa kwani kilichimbwa kutoka migodini moja kwa moja tofauti na zile Almasi za kutengenezwa. Kutokana na gharama kubwa na mapato kidogo watu walifikiria njia bora zaidi na mpya za uchimbaji madini ya haya.

Walitengeneza soko lenye uhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo, ndipo wakachangia uthaminishaji wa Almasi kwa kukata na kuipolish, iliyoongeza ufanisi, kupunguza gharama za uchimbaji na kuongeza thamani mwonekano wa mpya na mzuri wa madini ya Almasi sokoni

Miaka ya 1870, uzalishaji wa Almasi kila mwaka ulikuwa chini ya karati milioni. Kufikia miaka ya 1920, takwimu zilikuwa karibu Carat 3M. Miaka 50 baadaye, uzalishaji wa Almasi kila mwaka uliongezeka karibia 50M, na ktk miaka ya 1990 uliongezeka na kuzidi Carat 100M kwa mwaka.

Mwishoni mwa 1970, wazalishaji wakubwa wa Almasi ulimwenguni walikuwa Afrika Kusini, Zaire (kwa sasa DR-Congo) na nchi za uliokuwa Umoja wa Kisovyeti. Miaka ya 1980 uzalishaji wa Almasi zenye ubora wa hali ya juu ulikuwa nchini Urusi na S.A ilibaki kuwa ya kawaida, Zaire ilishuka

Mnamo 1982, mgodi mpya wa JWANENG nchini Botswana uliongeza uzalishaji wa Almasi ulimwengu. Ulikuwa chanzo kikubwa cha almasi ya hali ya juu mpk Botswana ikashika nafasi ya tatu ulimwenguni kwa uzalishaji mkubwa wa almasi, na ya pili kwa kuwa na Almasi yenye thamani zaidi duniani

DE BEERS iliamua kununua mgodi huo, ikaingia mkataba na serikali kwa ajili ya uzalishaji, ndipo Botswana iliamua kujenga kiwanda chake cha kukata Almasi.

Soko la Almasi liliongezeka baada ya ugunduzi wa mgodi mpya huko Australia mnamo 1985, na baadae mgodi wa Canada mnamo 2000.

DE BEERS ilibidilika kuendana na soko, ikawa haifanani kabisa na De Beers ya 1989, ikapunguza sana usambazaji wa almasi, badala ya kujikita ktk kila soko.

#Tofauti na miaka ya nyuma, kwa sasa madini ya Almasi yapatikana kwenye masoko mengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Ingawa sio kila kitu kilibadilika, lkn bila kujali ni njia gani watu hutumia kupata madini haya sokoni bado Almasi iliyo bora zaidi huchimbwa migodini, na kisha kupitishwa kwenye vituo vya kukatia ndipo huwafikia wateja rejareja.

Kito hiki kimekuwa cha thaman sana kwa karne nyingi, Lkn zaman wachimbaji hawakuwa na maarifa makubwa juu yake.Tangu karne ya 20 elimu juu ya Almasi imekua kwa kasi kutokana na tafiti zilizofanywa na wakemia, wanafizikia, wanajiolojia,wataalamu wa madini na wanahistoria wa bahari

UBORA, THAMANI & AINA ZA ALMASI💎

Kipengele hiki ni kikubwa sana inahitaji Almost siku 3 ili nikielezee vizuri kwa ufasaha. Hivyo nitaomba niandae #Uzi mpya kwa ajili yake lkn nitagusia vichache kukupa muangaza ktk soko la madini haya ambayo pia yameipatia Belgium utajiri mkubwa

Katika ulimwengu wa vito, watu walio wengi wameajiriwa katika uchimbaji wa madini hasa ktk ukataji wa Almasi kuliko kwa jiwe lingine lolote duniani. Upangaji wa ubora wa thamani ya almasi ni muhimu sana, lkn unategemea mfumo thabiti wa upangaji ili kulinda bei nzuri ya Almasi.

Watu wengi hufikiria kuwa uzito wa Almasi ndio sababu pekee ya kuamua juu ya thamani ya Almasi, lakini vigezo zaidi ya hivyo ikiwemo ubora wa rangi ya vito, uzito na ukataji ambao hupimwa zaidi kuliko ukubwa wa jiwe lingine lolote.

Muhimu zaidi, thamani ya uzito sawa wa Carat ya Almasi inaweza kutofautiana sana kulingana na rangi yao, fuwele (clarity) na kukata (cutting). Hizi 4C zinaunda mfumo wa upangaji ambao almasi hupimwa ingawa kuna viwango anuwai vinavyotumika kote ulimwenguni.

Taasisi ya Gemological Institute of America @GIAnews ndio ya kwanza Duniani kuvumbua namna nzuri ya 4C's (Carat, Colour, Cut, Clarity) kupanga ubora wa Almasi ambao ndio mfumo wa Kimataifa wa thaminisha Almasi na wataalam wa viwango na vito vyote vya mapambo hutumia njia hiyo.

Kuna aina 3 za Almasi.
(i) Almasi ya asili
(ii) Almasi asili zenyea rangi,
(iii) Almasi zinazotengenezwa.
Na zina jumla ya madaraja 22 kutoka D-Z huonyesha ubora wa thamani ya aina ya Almasi.

Kwanza kabisa, ni muhimu kukumbuka kuwa Almasi ya asili ni sawa, kiasili. Almasi iliyotenezwa katika maabara itakuwa 'kamilifu', lakini utakapokuwa mlinzi wa almasi halisi, moja ya hazina kubwa utahitaji kuwa na kazi maalumu na kipekee na zaidi na maarifa/elimu ya madini husika.

Kwanza kabisa, ni muhimu kukumbuka kuwa Almasi ya asili ni sawa, kiasili. Almasi iliyotenezwa katika maabara itakuwa 'kamilifu', lakini ikitokea ukaambiaa uwe mlinzi wa almasi halisi utahitaji kuwa na mafunzo kwa7bu hiyo NI kazi maalumu na kipekee inahitaji maarifa zaidi ya kuona

Unapaswa kujua kwamba wakati unachagua Almasi isiyo na rangi, unahitaji kuwa unaangalia 4C's:

1. Cut (Kata

2. Carat (Uzito wa Carat)

3. Colour (Rangi)

4. Clarity (Ufafanuzi)

Ktk #uzi ujao nitakuelezea jinsi viwango hv vinavyofanya kazi, pia kwa nini alama za juu sio chaguo bora ktk soko la Almas

#Aidha: Almasi ni kito kilichozaliwa mwezi Aprili km umezaliwa APRIL unabahati sana, pia hutumika km zawadi ktk maadhimisho ya miaka 10, 60 na 75 ya harusi.

VISA VYA HISTORIA YA ALMAS TZ🇹🇿

#Kwanza: Naomba nikufahamishe kuwa biashara ya madini duniani imekamatwa na familia mbili tu za Kiyahudi. Moja ikijielekeza kwenye madini ya Dhahabu na jamii zake ambayo ndio @BarrickGold na nyingine ktk madini ya Almasi ambao ndio @DeBeers

Hawa ndio wamiliki wa madini yote ya dunia, BILA kujali mipaka ya nchi walipo na kule yalipo madini.

Hata hivyo, biashara ya madini toka enzi na enzi imekuwa ni vita, TENA ni vile vita ambayo havijawahi kumuacha mtu salama. Iwe ni mfanyabiashara au mwanasiasa anayetazama maslahi

Vita hii ilimkumba Dr JOHN WILLIAMSON Geologist (Mcanada) mwanzilishi na mmiliki wa mgodi wa Mwadui, vita hivi vilimsumbua HAYATT MWL. NYERERE, mwana wa Afrika na Rais wa Tanzania. Mapambano haya hayakuziacha salama nchi zenye ukwasi wa madini kama DR-Congo, Angola na Siera Leone

Duniani kote familia ya Kiyahudi ya OPPENHEIMER (waliohamia South Africa) wenye kampuni ya @debeersgroup ndiyo imejimilikisha madini yote ya almasi yaliyopo ktk dunia hii baada ya kumpoka kwa nguvu umiliki wa kampuni CECIL RHODES.

Kuanzia madini ya India na Brazil, Afrika Kusini na Angola, Siera Leone na Botswana, Mwadui Shinyanga hadi Siberia ni Mali ya DE BEERS.

Mwaka 1940 Dr JOHN WILLIAMSON alifungua mgodi wa Almas Mwadui (Shinyanga). Mwadui ilikuwa na mkanda wa #Kimberlite wenye hifadhi nyingi ya Almas.
Dr Williamson raia wa Canada akautengeneza mji wa Mwadui ukawa moja ya miji bora kusini mwa jangwa la Sahara ikaitwa MWADUI TOWNSHIP.

Kufikia mwaka 1947, Dr WILLIAMSON alikuwa amejenga nyumba bora za wafanyakazi. Baadae alijengaa Hospitali ya kisasa, shule za msingi 3, mbili za wafanyakazi wa kiafrika na moja ya wafanyakazi wa kizungu ambayo ndio ilikuwa moja ya "English Medium School" ya kwanza Tanganyika.

Akajenga Chuo cha Ufundi wa aina zote ndani ya MGODI kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi, chuo cha kilimo na shule ya upili (Sekondari). Huko kwao waliita hii shule "School Near The Equator". Ilikuwa shule bora na ya kisasa.

Dr WILLIAMSON akajenga uwanja wa ndege wa kisasa ndani ya mgodi mwaka 1940's, akanunua ndege mbili za mwanzo aina ya DAKOTA DC-3 na CESSNA-180 wkt huo hata serikali ya muingereza ikiwa haina wazo la ndege, Tanganyika ikiwa haina uhakika wa kupokea ndege kubwa aina ya Dakota DC3.

Dr Williamson alikuwa tyr na uwanja huo, ambapo wageni toka London UK, ndege zilitua Malta, Khartoum na baadae Nairobi Airport (Wakati huo Embakasi Airport) na baadae kuchukuliwa na ndege moja kwa moja mpk Mwadui, ambapo Serikali ya kikoloni ilikuwa na afisa mmoja wa uhamiaji.

Akajenga kanisa na msikiti bora na wa kisasa kwa ajili ya wafanyakazi wake. Wkt huo usafiri pekee wa watumishi wakikoloni ilikuwa ni meli maarufu ya "THE BRAEMER CASTLE" iliyokuwa inatoka Ulaya mpaka Mombasa.

Williamson akajenga "Power House" yenye uwezo wa kuzalisha 900kw kwa mitambo ya diesel na 750kw kwa Gas Turbine na hivyo kuwa na umeme wa uhakika kuliko hata jiji la DSM achilia mbali mkoa wa Shinyanga. Wkt huo umeme wa Dar ulitegemea mtambo ulio pale Wizara Nishati km makumbusho

Ndani ya mgodi alijenga "Sailing Club", yaani Club inayoelea ktk bwawa alilochimba eneo la Songwa. Hii ndio ilikuwa Club pekee inayoelea Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara.
May 2, 1952, Gazeti Kongwe la "The Cairns Post" (Est.1882) liliandika juu ya bwawa la Songwa, Mwadui🇹🇿

Gazeti hilo la Australia lilielezea Bwawa la Songwa moja kati ya Artificial dam kubwa zaidi duniani, lenye uwezo wa kuchukua 2000M Gallons of water.Mradi ambao hata mkoloni iliushangaa.Mwadui kulikuwa na mfumo wa maji safi na taka yaliyotibiwa na wataalamu waliosomeshwa na mgodi.

Huduma ya elimu ya watu wazima na elimu ya uchumi wa nyumbani (home economics) kwa wamama waliokuwa nyumbani. Kufikia mwaka 1970, karibu 97% ya wakazi wa mgodi huo ambao walifikia 60,000 walikuwa wanajua kusoma na kuandika, na wamama wakiwa na ujuzi wa ushonaji, upishi nk.

Dr Williamson aliajiri mpishi maarufu toka Ufaransa, ambaye alikuwa akipika na kuandaa chakula ktk #mesi kubwa ndani ya mgodi wa Mwadui.
Mfaransa huyo alifundisha wapishi wengi wa Kiafrika na alikuwa km #Chuo cha wapishi wengi wa maafisa wa serikali ya kikoloni,

Na hata wapishi wa mwanzo wa Ikulu ya DSM baada ya Uhuru, walipita ktk mafunzo Mwadui.
Kufikia 1950 Tanganyika ilikuwa na vyumba 2 tu vyenye hadhi ya kulala Familia ya kifalme ya Uingereza, chumba 1 ktk Ikulu ya sasa ya DSM na kingine kwenye "Rest house" ndani ya MGODI wa MWADUI

Mgodi wa Mwadui chini ya Dr Williamson,uliweza kujenga kiwanja cha golf chenye mashimo tisa, ambacho kilikuwa ni moja ya viwanja vikubwa na vya kisasa Afrika nzima. Mwaka 1952 alishawishi mpaka mashindano makubwa ya kombe la Malikia la Golf nchini Canada yafanyike Mwadui

Kila kitu kilikubalika isipokuwa hali ya uwanja wa Embakasi (Nairobi now) haukuwa sawa sababu ya vuguvugu la vita vya Maumau lililotishia usalama wa kiwanja. Swimming Pool za viwango vya Olympic tatu ndani ya mgodi, viwanja vya tennis, pamoja na viwanja 3 bora vya mpira wa miguu

vilivyokuwa na viwango vya kimataifa vilijengwa ndani ya mgodi wa Williamson.

Timu ya mpira ya Mwadui Mining ilishiriki mashindano ya kitaifa kwa ubora mkubwa. Waamuzi wakongwe wa viwango vya kimataifa kama Mshangama na Mashishanga (RC wa zamani) ni matunda ya Dr Williamson.

Ustawi wa maisha ya mgodi na kushamiri kwa faida ya Dr Williamson kuliwauzi wamiliki wakubwa wa biashara ya madini ya almasi ambao ni DE BEERS Group of Co. Almasi ya Mwadui iliingia kwa kasi sana katika soko la dunia jijini London.

De Beers wakashindwa kumdhibiti Dr Williamson na almasi yake, akafanya almasi ya Afrika Kusini kushuka thamani katika soko la dunia, njia pekee iliyobaki kwa De Beers ilikuwa kumtaka Dr Willy aungane nao katika biashara. Dr Williamson alikataa kuupeleka mgodi kwa namna yake,

hakutaka kuwanyonya Waafrika na wafanyakazi wake, ndoto zake ilikuwa ni kuijenga "Quebec ndogo ndani ya Tanganyika", alitaka kuonyesha tofauti ya thamani ya madini na maisha ya wazawa kwa kuutumia mgodi wa Mwadui kwasababu zamani aliishi Afrika Kusini akaona dhuluma

Dr Williamson hakutaka hali hiyo itokee. Mkoloni na DE BEERS walichukia uamuzi wa Dr Williamson kuufanya mgodi wa Mwadui km Ulaya ya Afrika. Walianza kumshinikiza na kumwekea vikwazo kwa kukataa kuipokea almasi yake ktk viwanda vya wachonga almasi kule London (diamond Cutting).

Mwaka 1950, Serikali ya kikoloni kwa Shinikizo la familia ya OPPENHEIMER wakataka kutaifisha mgodi wa Mwadui ili uwe mali ya serikali ya mkoloni na si mtu binafsi. Hali hii ilichanganya sana Dr Williamson akawa mlevi wa kupindukia wa whisky ya Scotland, akawa 'chain Smoker'.

Mwaka 1952, mwezi Machi, kampuni ya DE BEERS ilimtuma mtoto wa kwanza wa mmiliki wa kampuni, HERRY OPPENHEIMER kuongea na Dr WILLIAMSON namna ya kuuza sehemu ya hisa kwa DE BEERS ili aweze kuwa salama, Dr Williamson alisita akawaza wafanyakazi wake watakavyonyanyasika.

Mwaka 1956 PRINCESS MARGARETH akiambatana na Gavana wa Tanganyika na ujumbe wake walitembelea mgodi wa Mwadui wakiwa ndege ya Dakota DC4 mali ya Dr Williamson. Ulikuwa ni ushawishi kumfanya aachie sehemu ya hisa za mgodi kwa shingo upande akatoa 50% akawauzia De Beers kwa £ 4M.

Miaka michache baadae akagundulika ana saratani ya koo, ugonjwa uliochukua maisha yake miaka michache baadae (baadae ilisimekana ulipandikizwa ili kumuua). Alivyoona hivyo Dr WILLIAMSON aliomba akifariki azikwe ndani ya eneo la Mwadui kwani Mwadui ndio ilikuwa nyumbani kwake.

Mwaka 1958, HERRY OPPENHEIMER ndio akawa M/kiti wa Mgodi wa Mwadui, sehemu ya hisa za Dr WILLIAMSON aliachiwa dada yake, na kwa sababu hakuwa na uzoefu wa mambo na madini, DE BEERS wakamshauri aziuze. De Beers na serikali ya kikoloni wakawa na 50/50 ya umiliki wa mgodi wa Mwadui.

Ndoto za DE BEERS kumiliki Madini yote ya Almasi chini ya ardhi ya Dunia na familia ya OPPENHEIMER ikawa imetimia. MWL. JULIUS NYERERE alipochukua nchi 1961, baadae aliamua kutaifisha mali zote akaunda STAMICO isimamie sekta ya madini. DE BEERS iliwauma sana kufurushwa na Nyerere

Hawa Waisrael wakaunda Team ya namna ya kumkomesha MWL. NYERERE, kwanza waliweka fitna ktk soko la almasi pale London, wakazishawishi Diamond Cutters and Polishing Companies" kule London ziisusie almasi ya Mwadui, Mwalimu akawa mbishi na kuimarisha"TunCut Diamond Co." pale Iringa

De Beers wakazidi kuweka fitna kwenye viwanda vinavyotengeneza vipuri vya mitambo iliyopo Mwadui. Kuanzia mitambo ya kuchimba, kusafisha na kuchambua almasi. Mwishowe vifaa vikachakaa bila kuwa na ukarabati. Uzalishaji ukapungua na almasi ya Mwadui ikapotea katika soko la dunia.

Wataalamu toka nje waliokuwa katika mgodi wa Mwadui wakaondoka. Ikawa ni hasara juu ya hasara. Mwaka 1993, DE BEERS kupitia HERRY OPPENHEIMER yuleyule wa enzi za Dr Williamson walirudi Tanzania kupitia mtoto wao NICOLAUS OPPENHEIMER, wakaishawishi serikali ya Tanzania,

Hatimaye DE BEERS Group of co. wakauziwa 75% ya hisa za MGODI wa MWADUI, ile ndoto yao ya kumiliki madini yote ya almasi ya dunia ikaendelea kutimia. Hawa ndio DE BEERS familia ya Kiyahudi ya OPPENHEIMER. Wanaosadiki kuwa almasi yote inayopatikana ktk uso wa dunia hii ni mali yao

Waliomsurubu Dr JOHN THORBUN WILLIAMSON, mzungu-msukuma aliyetaka mali ya ardhi ya Mwadui ilete thamani kwa Waafrika na Tanganyika. Hawa ndio De Beers waliomtikisa Mwalimu, hawa ndio familia ya almasi duniani, wanaochochea yale ya Angola ya Savimbi, Siere Leone ya Foudah Sankho.

Tanzania tumewahi kujipatia BILIONEA wa madini ya Almasi baada ya mchimbaji mdogo wa madini JOSEPH TEMBA kutoka Maganzo mkoani Shinyanga kuuza almasi yake kwa US$ 1.4M sawa na Tsh. Bilioni 3. Almasi ile ilikuwa na Carat 512 na serikali ilipatia Tshs. 238M kutokana na mauzo yake.

Madini haya yana thamani sana na faida kubwa achilia kwa mtu mmoja mmoja hata kwa serikali pia. MFANO: Takwimu zinaonyesha kwa mwaka 2019/20 madini ya vito ya almasi yenye uzito wa carats 416,749.51 iliuzwa nje kwa US$ 89.3M ambapo mrabaha ulikuwa US$ 5.4M + Ukaguzi US$ 893,346

Almasi ghali zaidi duniani ni ile yenye rangi ya waridi (pink) ambayo ni adimu kupatikana iliuzwa kwa US$ 50.3M kwa karati, ambapo jiwe lote lilikuwa na uzito wa zaidi ya Carat 19. Almasi hiyo ilinunuliwa na chapa ya @HarryWinston kutoka Marekani ktk mnada uliofanyika Geneva.

Almasi kubwa zaidi zipo mbili na zote zilichimbwa nchini Sierra Leone. Moja yenye Carat 476 ikiwa ya 29 kuwahi kupatikana duniani na nyinhine iliuzwa mwaka jana iliyokuwa na Carat 700 ndiyo ni kubwa zaidi kuliko zote.

END_______&&

🔄 and FOLLOW ME @Eng_Matarra

Thanks Much 🙏🙏

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling