ODOGWU 𝕏 Profile picture
It's just Twitter | Malume 👊

Aug 10, 2021, 9 tweets

▶️Yoshito Matsushige aliyezaliwa tarehe 2 January 1913, alikuwa manusura wa milipuko ya Hiroshima, na mpiga picha pekee ambaye aliweza kunasa picha za kihistoria zinazoonyesha uharibifu wa bomu la atomiki lililopigwa kwenye mji huo.
👉Mnamo mwaka 1941...... 👇👇
#uzi

.....Yoshito alijiunga na shirika la kuchapisha magazeti la Geibinichinichi, ambalo baadaye liliungana na Kampuni ya Chugoku Shimbun. Alipewa idara ya upigaji picha na baada ya 1944, pia alifanya kazi kama mshiriki wa ripoti ya waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Jeshi ...

..la mkoa wa Chugoku nchini Japan.

👉Mnamo Agosti 6,1945 (kipindi mlipuko unatokea), Yoshito Matsushige alikuwa na umri wa miaka 32, akiishi nyumbani kwake kwenye mji wa Midori-cho, Hiroshima. Nyumba yake ilikuwa maili 1.7 (Sawa na Kilometer 2.7), kutoka sehemu ambayo mlipuko..

...wa bomu la atomiki ulitokea.
👉Kwa hali ambayo watu wengi waliona ni kama ya kimiujiza Bw. Yoshito hakujeruhiwa vibaya na mlipuko huo, badala yake aliingiwa na ujasiri wa kubeba kamera moja na kuanza kupiga picha matukio yaliyojiri kwenye eneo hilo mara baada ya bomu kulipuka.

▶️Akizuiwa na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka kila kona, Bw. Yoshito hakuweza kufika katika ofisi yake ya kuchapisha magazeti kwa hivyo alirudi mpaka kwenye Daraja la Miyuki. Bw. Yoshito alielezea kwamba alipokuwa kwenye eneo hili la daraja la Miyuki alijaribu kuchukua picha za....

...watu waliokuwa wamejeruhiwa na kufa vibaya lakini hakuweza kubonyeza kitufe cha kupigia picha kabisa kwani alijawa hofu na woga mkubwa.

👉Baada ya kuhangaika katika eneo hilo kwa takribani dakika ishirini, mwishowe alichukua picha zake za kwanza. Kwa muda wa masaa kumi.....

....yaliyofuata Yoshito aliweza kubonyeza kitufe cha kupigia picha mara saba tuu.
👉Alisema, "Ulikuwa ni mtazamo mbaya sana kwangu kiasi cha kwamba sikuweza kubonyeza Camera yangu ili kuchukua picha." Kwa kuongezea, Yoshito alisema kuwa aliogopa watu waliokuwa wameungua na.....

....kuumia vibaya watakasirika ikiwa mtu atachukua picha zao kutokana na hali waliyokuwa nayo.

👉Ni picha tano tu kati ya saba zilizopigwa na Bw. Yoshito ndio ziliweza kusafishwa na kuwa ndio rekodi pekee ya uharibifu uliosababishwa na mabomu ya Atomiki huko mjini Hiroshima.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling