ODOGWU 𝕏 Profile picture
Aug 10, 2021 9 tweets 4 min read Read on X
▶️Yoshito Matsushige aliyezaliwa tarehe 2 January 1913, alikuwa manusura wa milipuko ya Hiroshima, na mpiga picha pekee ambaye aliweza kunasa picha za kihistoria zinazoonyesha uharibifu wa bomu la atomiki lililopigwa kwenye mji huo.
👉Mnamo mwaka 1941...... 👇👇
#uzi Image
.....Yoshito alijiunga na shirika la kuchapisha magazeti la Geibinichinichi, ambalo baadaye liliungana na Kampuni ya Chugoku Shimbun. Alipewa idara ya upigaji picha na baada ya 1944, pia alifanya kazi kama mshiriki wa ripoti ya waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Jeshi ... Image
..la mkoa wa Chugoku nchini Japan.

👉Mnamo Agosti 6,1945 (kipindi mlipuko unatokea), Yoshito Matsushige alikuwa na umri wa miaka 32, akiishi nyumbani kwake kwenye mji wa Midori-cho, Hiroshima. Nyumba yake ilikuwa maili 1.7 (Sawa na Kilometer 2.7), kutoka sehemu ambayo mlipuko..
...wa bomu la atomiki ulitokea.
👉Kwa hali ambayo watu wengi waliona ni kama ya kimiujiza Bw. Yoshito hakujeruhiwa vibaya na mlipuko huo, badala yake aliingiwa na ujasiri wa kubeba kamera moja na kuanza kupiga picha matukio yaliyojiri kwenye eneo hilo mara baada ya bomu kulipuka. Image
▶️Akizuiwa na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka kila kona, Bw. Yoshito hakuweza kufika katika ofisi yake ya kuchapisha magazeti kwa hivyo alirudi mpaka kwenye Daraja la Miyuki. Bw. Yoshito alielezea kwamba alipokuwa kwenye eneo hili la daraja la Miyuki alijaribu kuchukua picha za.... ImageImage
...watu waliokuwa wamejeruhiwa na kufa vibaya lakini hakuweza kubonyeza kitufe cha kupigia picha kabisa kwani alijawa hofu na woga mkubwa.

👉Baada ya kuhangaika katika eneo hilo kwa takribani dakika ishirini, mwishowe alichukua picha zake za kwanza. Kwa muda wa masaa kumi..... ImageImage
....yaliyofuata Yoshito aliweza kubonyeza kitufe cha kupigia picha mara saba tuu.
👉Alisema, "Ulikuwa ni mtazamo mbaya sana kwangu kiasi cha kwamba sikuweza kubonyeza Camera yangu ili kuchukua picha." Kwa kuongezea, Yoshito alisema kuwa aliogopa watu waliokuwa wameungua na..... ImageImageImage
....kuumia vibaya watakasirika ikiwa mtu atachukua picha zao kutokana na hali waliyokuwa nayo.

👉Ni picha tano tu kati ya saba zilizopigwa na Bw. Yoshito ndio ziliweza kusafishwa na kuwa ndio rekodi pekee ya uharibifu uliosababishwa na mabomu ya Atomiki huko mjini Hiroshima.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with ODOGWU 𝕏

ODOGWU 𝕏 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @sangasaimon_

Jul 30, 2021
▶️Josephine Myrtle Corbin alikuwa mtu wa kwanza kuzaliwa na sehemu za siri mbili na miguu minne, huko Tennessee mnamo 1868.

👉Josephine ilikuwa azaliwe akiwa na pacha wake, lakini waliungana kutoka kiunoni kwenda chini. Ugonjwa huu ambao unaitwa Dipygus, unatokana na... Image
....hali isiyo ya kawaida ya mapacha kuungana.  Alikuwa ameongezeka maradufu umbo lake kutoka kiunoni kwenda chini kwa sababu ya hali hiyo isiyo ya kawaida, lakini kuanzia kiunoni kwenda juu alikuwa wa kawaida (kama anavyoonekana pichani) 📸👇 Image
👉Miguu miwili (ambayo ndio ilikuwa ya pacha wake) kati ya minne ilikuwa midogo kuliko miguu yake halisi, lakini ilikuwa imeungana pamoja hivyo haikuwa ikimsumbua sana.

 Josephine aliolewa na Clinton Bicknell akiwa na umri wa miaka 19, na walifanikiwa kupata watoto watano..... Image
Read 5 tweets
Jul 5, 2021
▶️ Kifahamu Kivuko cha kwanza kabisa kuwahi kutumika Ulimwenguni..!!
#vitukuntu
#uzi

👉Je! Unajua kwamba kivuko cha kwanza ulimwenguni kilijengwa na Waturuki wakati wa Dola ya Ottoman..??

👇👇 U S I O N D O K E 👇👇
▶️Katika miaka ya 1800, usafirishaji uliofanyika katika pande zote za Bosphorus ulifanywa kwa kutumia boti. Katika miaka ya 1840, vivuko vidogo pia vilianza kutoa huduma za usafirishaji kwenye eneo hilo la Bosphorus lilopo nchini Uturuki.
📸👇(Bosphorus)
👉Mnamo mwaka1850, kivuko cha "kirket-i Hayriyye" kilianzishwa na huduma ya usafirishaji baharini ilianzishwa kwa watu wa Istanbul kupitia kivuko hiki. Hüseyin Haki Efendi, mmoja wa mameneja wa kivuko hicho, alikuwa mtu mbunifu na alikuwa akifikiria kwa miaka mingi juu ya...
Read 5 tweets
Apr 25, 2021
▶️FAHAMU BAADHI YA REKODI ZA KUSHANGAZA ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA REKODI ZA DUNIA CHA GUINESS.
#uzi
#vitukuntu

01. Msichana mwenye miguu mirefu zaidi duniani.

👉Naam huyu ni "Maci Currin", binti wa miaka 17 tu akitokea kwenye nchini Marekani. Maci ameweka rekodi hii....

📸👇
....mwaka huu huu wa 2021. Maci ana urefu wa futi sita na inchi kumi, lakini miguu yake tuu imechukua karibu asilimia 60 ya urefu wake wote.

(Unaweza ukaangalia picha zake zaidi Instagram kwenye account yake ya @ _maci.currin_)

📸👇
02. Familia yenye nywele nyingi.

👉Familia ya Ramos Gomez iliweka rekodi ya ulimwengu kuwa familia kubwa zaidi yenye nywele nyingi za mwilini mnamo mwaka 2000. Ndugu wanne wa familia ya watu 19 kutoka Mexico walioitwa Victor Larry Gomez, Gabriel Danny Ramos Gomez,......

📸👇
Read 18 tweets
Apr 24, 2021
▶️WAFAHAMU WATU MASHUHURI WALIOUWAWA KWA KUPIGWA RISASI.
#uzi
#vitukuntu

01. ABRAHAM LINCOLN
👉Alikuwa raisi wa 16 wa marekani na ndiye raisi wa kwanza wa marekani kuuawa akiwa madarakani. Aliuwawa mwaka 1865 na John Wilkes Booth aliyeudhiwa na maamuzi ya Lincoln ya kutambua....
....haki za watu weusi. Lincoln alipigwa risasi na John Wilkes Booth alipohudhuria kwenye maonyesho ya muziki. Booth nae aliuawa siku mbili baadae baada ya jaribio la kutoroka kushindikana.

(📸👇 John Wilkes Booth)
02. BENAZIR BHUTTO
👉Alikuwa waziri mkuu wa 11 wa Pakistani na kiongozi wa chama chenye ushawishi mkubwa cha PPP. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa la kiarabu akichagizwa na siasa zake safi za kidemokrasia. Aliuwawa disemba 27 mwaka 2007 akiwa kwenye gari yake aina ya....
Read 24 tweets
Jan 18, 2021
▶️LEO NIMEKULETEA HAPA BAADHI YA PICHA ZA "BEHIND THE SCENES" ZA FILAMU MAARUFU YA "APOCALYPTO" 🎥
#uzi
#vitukuntu
📸👇🏾 Image
▶️Filamu hii maarufu kutoka kiwanda cha kutengeneza filamu cha nchini Marekani (Hollywood) inayokwenda kwa jina la "Apocalypto" imekuwa ni mojawapo ya filamu nyingi zenye mafanikio na pia mvuto mkubwa kwa watamazaji.

👉🏾Filamu hii iliachiwa mnamo mwaka 2006.

Tuendelee..

👇🏾 👇🏾
▶️Filamu hii ilikuwa na lengo la dhati la kuelezea maisha ya kale ya wanadamu waliokuwa wakipatikana kwenye maeneo ya Amerika ya Kusini hususani wakazi waliokuwa wakiishi kwenye msitu mkubwa wa Amazon.
👉🏾Muongozaji mkuu wa filamu hii anajulikana kwa jina la "Mel Gibson"
Read 10 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(