JAPHET MATARRA Profile picture
Father | Human Right Activist | Mineral Processing Engineer | Paralegal | Member @ChademaTz | @ManUtd | @YoungafricansSC | Boss Himself | StoryTeller | 430'2023

Aug 11, 2021, 158 tweets

๐…๐€๐‡๐€๐Œ๐” ๐€๐’๐ˆ๐‹๐ˆ ๐˜๐€ ๐Œ๐€๐‰๐ˆ๐๐€ ๐˜๐€ ๐Œ๐ˆ๐Š๐Ž๐€๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

#๐•ฟ๐–๐–—๐–Š๐–†๐–‰:
Tanzania ni nchi iliyoko Africa
Jina "๐“๐š๐ง๐ณ๐š๐ง๐ข๐š" lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na ๐Œ๐จ๐ก๐š๐ฆ๐ž๐ ๐ˆ๐ช๐›๐š๐ฅ ๐ƒ๐š๐ซ ndiye aliyelibun.Hivi unafaham asili ya jina la mkoa wako?

Ktk kipind cha ๐”๐ค๐จ๐ฅ๐จ๐ง๐ข Tanzania ilikuwa na utawala wa majimbo 8, Lkn baada ya #๐”๐ก๐ฎ๐ซ๐ฎ mikoa ilianzishwa kwa miaka tofauti na mpk Leo hii ninavyoandika #Uzi huu ๐Œ๐ข๐ค๐จ๐š 31 imeanzishwa kutoka pande zote Visiwani na Tz Bara.Najua ulishawahi kujiuliza asili ya Mkoa wako

Kila Jina unalosikia lazima kuna chimbuko ambalo ndio Asili ya jina hilo. Aidha, yawezekana limetoholewa ktk lugha za kigeni na kuchukuliwa kutokana na matumizi yake, muonekano, lugha za asili ktk Eneo fulani, tukio ama hata tabia za watu wa eneo fulani na makosa ya kimatamshi

#Wakati mwingine historia ya neno ni kama safari ktk historia ya kibinadamu. Leo nakuletea Elimu ya asili ya maneno mbalimbali [Etimolojia]. Ukitaka kujua umuhimu wa "๐„๐ญ๐ข๐ฆ๐จ๐ฅ๐จ๐ฃ๐ข๐š" Basi jiulize ni nini tofauti kati ya ๐‡๐š๐ฒ๐š๐ญ๐ข na ๐Œ๐š๐ซ๐ž๐ก๐ž๐ฆ๐ฎ.

RT ๐Ÿ”„Tuendelee๐Ÿ‘‡

๐€๐‘๐”๐’๐‡๐€

Arusha ni Jiji la kaskazini mwa Tanzania na Makao Makuu ya Mkoa wa Arusha. Mji huu upo kando ya Mlima Meru kwenye ncha ya mashariki mwa Bonde la Ufa na ina mandhari mazuri miongoni mwa miji iliyopo barani Afrika ukiwa na mbuga za wanyama.

Hifadhi za Wanyama Arusha, Serengeti, Ziwa Manyara, Tarangire, pamoja na Bonde la kihistoria ๐—ข๐—น๐—ฑ๐˜‚๐˜ƒ๐—ฎ๐—ถ ๐—š๐—ผ๐—ฟ๐—ด๐—ฒ, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro vipo karibu na mji huu.

Mji huu umezungukwa na milima kaskazini na mashariki, na mazingira yake ni mchanganyiko wa misitu ya savanna na misitu mabaki. Hali ya hewa ni nzuri sana na hadi sasa ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na ndipo ilipo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu barani Africa

Jina la ๐—”๐—ฟ๐˜‚๐˜€๐—ต๐—ฎ

Neno Arusha limetokana na neno la Kimaasai "๐€๐ซ๐ฎ๐ฌ" lenye maana ya eneo lenye majani mazuri ya malisho ambapo inadaiwa kuwa baada ya Wamasai kufika eneo hilo walikutana na watu wengine waliokuwa wafugaji pia.Wakiwa hapo walifanya ufugaji wa ng'ombe ndipo๐Ÿ‘‡

siku moja akazaliwa ndama waliyemuita '๐‘๐จ๐ง๐จ๐ฅ๐š๐ซ๐ฎ๐ฌ๐ฎ' yaani mwenye rangi mbili tofauti ya kijivu wenye madoadoa. Kutokana na uzuri wa eneo hili kimalisho kabila la wamasai na wameru waliweka makazi kwa sababu ya uhakika wa chakula cha mifugo yao. Ng'ombe wale ..

walinona sana ndipo eneo lile wakaliita "๐ข๐ฅ๐ฅ๐š๐ซ๐ฎ๐ฌ๐š" na alipozaliwa yule ndama walipaita "Arus", hivyo tokea kipindi hicho wageni walipofika maeneo ya ukanda huo walishindwa kutamka vizuri wakaita Arusha.Baada ya mji huu kuwa eneo maarufu la malisho idadi ya watu iliongez..

...eka na shughuli mbalimbali haswa za kibiashara zikaanza ambapo ziliweza kuvutia Wakoloni. Wakoloni wa kwanza kuja Arusha ni wajerumani na waliwatanguliza wamishionari kwa Lengo kutwaa eneo hili na kuwa makoloni yao. Waarusha hawakukubali kutawaliwa kirahisi na waliresist na

kupigana na wamishenari hao na kuwaua. Hata hivyo baadae kidogo Wajerumani walikuja tena na kupigana vita na Mangi wa Arusha Lavaito/Meingeanga Ndemi mwaka 1890-1900.

๐Œ๐€๐‘๐€

Mkoa wa Mara una eneo la Kilomita za mraba 30,150. Kati ya hizo 49.2% ni Hifadhi za Wanyamapori, ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mapori ya Akiba ya Ikorongo na Grumeti na Hifadhi za Jamii Grumeti na Ikorongo. Asimilia 50.7 ya eneo ni nchi kavu kwa ajili

...ya kilimo, mifugo na makazi.Mkoa unapakana na Nchi ya Kenya na Uganda kwa upande wa Kaskazini, mikoa ya Kagera na Mwanza upande wa Magharibi, Mkoa wa Simiyu kwa upande wa Kusini na Mkoa wa Arusha kwa upande wa Mashariki.
Historia ya Mkoa huu inaanzia mwaka 1961 ukiwa pamoja..

mikoa ya Mwanza na Shinyanga ya sasa wkt huo ikijumuishwa kwenye "๐„๐š๐ฌ๐ญ ๐‹๐š๐ค๐ž ๐๐ซ๐จ๐ฏ๐ข๐ง๐œ๐ž", Makao Makuu yakiwa Mwanza. Miongoni mwa Wilaya zilizounda ๐„๐š๐ฌ๐ญ ๐‹๐š๐ค๐ž ๐๐ซ๐จ๐ฏ๐ข๐ง๐œ๐ž ni pamoja na wilaya za South na North Mara, ambazo ndiyo chimbuko la Mkoa wa Mara

Mkoa Mara ulianzishwa mwaka 1963 na sasa ni miongoni mwa Mikoa 31 ya sasa.
Tangu wakati huo Makao Makuu yakawa Musoma mpaka sasa. Mkuu wa Mkoa wa kwanza akiwa Mhe. ๐—๐—ผ๐—ต๐—ป ๐—ฆ. ๐— ๐—ฎ๐—น๐—ฒ๐—ฐ๐—ฒ๐—น๐—ฎ kati ya mwaka 1963 hadi 1965. Tangu mwaka 1963, mkoa umeongozwa na Wakuu wa Mikoa 17.

Mkoa wa Mara ni Chimbuko la Viongozi mashuhuri akiwemo Rais wa kwanza na muasisi wa Taifa hili Hayati ๐Œ๐–๐‹. ๐‰๐”๐‹๐ˆ๐”๐’ ๐Š๐€๐Œ๐๐€๐‘๐€๐†๐„ ๐๐˜๐„๐‘๐„๐‘๐„.
Makabila ya Mara ni mengi kuliko mikoa yote ya Tanzania, kama vile Wajaluo, Wajita, Waruri, Wazanaki, ๐–๐š๐ค๐ฎ๐ซ๐ข๐š,...๐Ÿ‘‡

.....Wakabwa, Wakiroba, Wasimbiti, Wangoreme, Wakwaya, Waikoma, Wanata, Waisenye, Waikizu, Wasizaki, Wasukuma, Wataturu na makabila mengine Wanandi, Wakisii, Wamaragori. Kuna jumla ya makabila 30 yanayodai kujitegemea. Jamii zinazosahaulika huunganishwa ktk kundi la Suba ...

(Wategi, ambao pia huitwa Abhathegi maarufu kama Abhagirango, Waugu (Ugu), Warieri, Wakine, Wasweta na Waganjo, Wagire, Wakiseru, Wakamageta na Waturi). Baadhi ya jamii hizi zilimezwa na mila, lugha na desturi za Wajaluo zikaitwa Suba-Luo katika kipindi cha utawala wa DC Engram.

Baadhi ya jamii zilisambaa mpk upande wa Kenya zipo ktk wilaya za Kuria na South Nyanza huitwa Suna, Wagwasi, Ungoe, Kajulu na Kadem. Hatahivyo habari hizi bado zinafanyiwa utafiti kuangalia muingiliano wa lugha na tofauti za kilahaja kati ya jamii 1 na nyingine hasa zilizopo ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Kimsingi Mkoa wa Mara una jamii hizo zipatazo 30 lkn lugha kuu ni saba tu na nyingine ni Lahaja kutokana na makundi ya lugha hizi: ๐‹๐ฎ๐จ, ๐Š๐ฎ๐ซ๐ข๐š, ๐’๐ฎ๐ค๐ฎ๐ฆ๐š, ๐’๐ฎ๐›๐š, ๐’๐ก๐š๐ฌ๐ก๐ข, ๐™๐š๐ง๐š๐ค๐ข, ๐ง๐š ๐“๐š๐ญ๐ฎ๐ซ๐ฎ. Yapo makundi ya Wanata, Waisenye na Wataturu.

Wazanaki (kundi lake ni Wakabwa, Wakirobha, Wasimbiti, Wairienyi, Waikizu na Wangoreme), Luo (Wakowak, Wakamoti).

Wakuria (Wakira, Wanyabhasi, Wanyamongo, Wanchari, Wasweta, Wakenye, Warenchoka, Watimbaru, Wairege, hizi ukizitaja zinafika hadi 14), Sukuma (Wanyantuzu) na...๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Shashi (Wajita, Wakwaya, Waruri, Wakerewe, Wakara). Jamii zote hizi hujikuta zikimezwa katika makundi saba ya lugha kuu lakini kila jamii inajitofautiana kwa lahaja yake na matamshi.

Jina la Mara.

Asili ya jina la mkoa Mara ni "๐Œ๐ญ๐จ ๐Œ๐š๐ซ๐š" ambao unaanzia nchi jirani ya Kenya na kupita ktk Hifadhi na mbuga za Serengeti, kisha Tarime na maji yake humwaga ๐™๐ข๐ฐ๐š ๐•๐ข๐œ๐ญ๐จ๐ซ๐ข๐š.Neno hili limetokana na neno la Jamii za kisemitiki za Washeba wa Mzee Kushi

kutoka Babeli ambao ni "Wakurya" na Wanailotiki "Wajaluo".

๐Œ๐š๐ซ๐š kwa kikurya lina maana nyingi, "Mara" = "๐Š๐ฎ๐ฆ๐š๐ฅ๐ข๐ณ๐š", "๐Š๐ข๐œ๐ก๐ฎ๐ซ๐ข," au ๐ค๐ฎ๐Ÿ๐š๐ง๐ฒ๐š ๐ฃ๐š๐ฆ๐›๐จ ๐ฅ๐ข๐ฅ๐ž๐ฅ๐ข๐ฅ๐ž ๐›๐ข๐ฅ๐š ๐ค๐ฎ๐ฌ๐ข๐ญ๐š ๐š๐ฎ ๐ค๐ฎ๐œ๐ก๐ž๐ฅ๐ž๐ฐ๐š.
Wakurya) walipotoka huko Kaskazini mwa

Africa kupitia Nubia (Sudani) Napata (Ethiopia) mpk Kenya kisha Tanzania walifikia mkoa wa Mara Eneo la Tambarare za Serengeti waliamua kupumzika na kuanzisha makazi.
Lkn historia ya nyuma inasema kwamba huko walikokuwa wametokea walikuwa na desturi ya kupunguza machungu kwa..๐Ÿ‘‡

kuchinja wanyama kisha kula "๐Š๐ข๐œ๐ก๐ฎ๐ซ๐ข" (mavi/majimaji yaliyopo kwenye utumbo mdogo wa mnyama yenye asili uchungu mithili ya nyongo ya ini) kwa ajili ya kupunguza machungu na hasira. Hivyobasi, walikuwa wanawinda wanyama ktk mbuga za Serengeti na kula hicho "๐Š๐ข๐œ๐ก๐ฎ๐ซ๐ข".

kwa lugha fasaha ya kikurya na watu waliofika maeneo waliwashangaa na kuwauliza walichokuwa ni kitu gani ndipo wakawajibu "ghano na "Mara" lenye maana haya ni mara.
Neno "Mara" au Kichuri Likachukuliwa hapo na kila aliyekuwa akienda huko alisema anatoka kwa Wa-mara.

๐Œ๐–๐€๐๐™๐€

Historia ya mkoa wa Mwanza inanzia wakati mkoa huu ukiwa chini ya tawala za kitemi za Wasukuma, Wazinza, Walongo, Wakara na Wakerewe kabla ya ukoloni. Wajerumani walipotawala Tanganyika eneo la Mwanza likawa mojawapo ya wilaya katika himaya ya utawala wa Kijerumani.

Utawala wa kikoloni wa Mwingereza ulipokabidhiwa uangalizi wa Koloni la Afrika Mashariki baada ya vita kuu ya Dunia, ulianzisha utawala wa majimbo yaani Provinces. Tanganyika ilikuwa na majimbo ya kiutawala manane (8) na mojawapo likiwa ni Lake Province.

Jimbo la Lake Province liliundwa kwa kujumuisha maeneo ya wilaya za Mwanza, Biharamulo, Bukoba, Maswa, shinyanga, Musoma na Kwimba. Baadaye Lake Province liligawanywa na kuunda majimbo mawili la Lake Province (Sukuma Land) na Western Province.

Utawala wa Mwingereza ulimalizika na Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961. Baada ya uhuru Mwanza iliendelea kuwa sehemu ya Lake Province chini ya mtawala wake kwanza wa jimbo (Provincial Commissioner) aliyeitwa Gen. JOHN B. WALDEN, ambaye alikabidhi madaraka kwa RICHARD WAMBURA.

Mkoa wa Mwanza ulianzishwa rasmi mwaka 1963 ukiwa na wilaya Nne:Ukerewe, Geita, Mwanza na Kwimba. Mwaka 1972 baada ya sera ya madaraka mikoani wilaya nyingine zilianzishwa, wilaya Magu mwaka 1974 na Sengerema imwaka 1975 ambapo awali ilikuwa ni Tarafa mojawapo ya wilaya ya Geita.

Misungwi ilianzishwa mwaka 1995 ambapo awali ilikuwa ni eneo la tarafa za wilaya ya Kwimba, Ilemela na Nyamagana zilianzishwa mwaka 2002 ambazo zilikuwa zinaunda wilaya ya Mwanza.

๐‰๐ข๐ง๐š ๐ฅ๐š ๐Œ๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐š.

๐Ÿ“‹Mwanza inatokana na jina la Ng'wanzalima, Mfugaji alieishi ๐๐ž๐ซ๐š (Machemba). Usichokijua ukienda usukumani kama wewe ni YOHANA wao wanaweza kukuita YOHA, MOHAMED utaitwa MOHA au MED. Hadithi ya asili ya jina la Mwanza inaanza kuwa kulikuwa na ๐Ÿ‘‡

Wafugaji na wakulima waliokuwa wakitokea maeneo tofauti kwenda ulipo leo mji wa Mwanza kwa shughuli mbalimbali.Walikuwa wakivukia mwalo wa "๐Š๐š๐ฆ๐š๐ง๐ ๐š" kisha wakitaka kuoga wanaenda mwalo wa "๐๐ž๐ซ๐š" alipokuwa akiishi Bw ๐๐ '๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐š๐ฅ๐ข๐ฆ๐š, wakishamaliza kuoga.....๐Ÿ‘‡

..walikuwa wanapumzika maeneo hayo.Hivyobasi kutokana na tabia ya wasukuma ya kufupisha majina walikuwa wakimwita "๐๐ '๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐š".Wakoloni walipofika eneo la Mwanza waliamua kuweka makao maeneo karibu na kwa Ng'wanza [lima] ikaanzia hapo kuitwa Ngw'anza kutokana na wajerumani..

kushindwa kuitamka na ๐๐ '๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐š wakawa wanatamka 'Mwanza' ambayo ipo hadi leo, pia kwa kuongezea tu wasukuma hawaiti Mwanza bali huita "๐๐ '๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐š" Labda wakiwa wanazungumza kiswahili ndo hutumia Jina la Mwanza.
Kesho tutaendelea na GEITA
#RT ๐Ÿ”„ Follow me @Eng_Matarra

๐†๐„๐ˆ๐“๐€

Mkoa Geita ni moja ya mikoa 31 nchini Tanzania.Awali Geita ilikuwa wilaya, ilipata hadhi ya wilaya mwaka 1962. Mnamo 1975 wilaya ya Geita iligawanywa na kupata wilaya ya Sengerema.
Mwaka 2004 ikawa Mamlaka ya Mji, 2012 ikapewa hadhi ya Halmashauri na hadhi ya Mkoa..๐Ÿ‘‡

Kabla ya kuingia kwa wakoloni (Wajerumani na Waingereza) Geita ilikuwa na tawala za asili 7.Wakoloni wa kwanza kuingia walikuwa "๐–๐š๐ฃ๐ž๐ซ๐ฎ๐ฆ๐š๐ง๐ข" ambao walikuwa na utawala wa moja kwa moja (Direct rule), historia inasema Wajerumani walishindwa kabisa kuitawala Geita kwa7bu๐Ÿ‘‡

...Wawakilishi waliokuwa wakipelekwa huko kutoka makao makuu ya wakoloni Bagamoyo waliuawa na wenyeji hao. Utawala wa pili ulikuwa wa waingereza baada ya WWII, ambao walitumia utawala wa Indirect rule yaani kwa kuwatumia machifu/watemi wa maeneo husika ili kutekeleza malengo yao.

Eneo la mji wa Geita aliwekwa Liwali aliyeitwa ๐๐ž๐ญ๐ซ๐จ ๐๐ฒ๐š๐ง๐ ๐จ, ambaye alifanya kazi chini za utawala na kulikuwepo na Baraza la Jadi. Baraza lilikuwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Wilaya (DC) wa kikoloni, liliundwa na watemi 7 na Liwali mmoja kutoka serikali ya Wakoloni.

Mwenyekiti wa baraza hilo alitokana na watemi hao.
Aidha, Katibu wa Baraza hilo alitokana na Watemi au karani kutoka ofisi ya DC. Makao makuu ya baraza hilo yalikuwa mjini Geita eneo la jirani ilipo Benki ya CRDB (w) Geita, kila mtemi alijengewa nyumba ya kupumnzikia na kulala.

๐—๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐—š๐—ฒ๐—ถ๐˜๐—ฎ

Asili ya neno "Geita" imetokana na maneno matatu ya kabila la Wayango (๐–๐š๐ซ๐จ๐ง๐ ๐จ), maneno hayo ni "๐‘จ๐’Œ๐’‚๐’ƒ๐’‚๐’๐’ˆ๐’‚ ๐’Œ๐’†๐’Š๐’•๐’‚ ๐’‚๐’ƒ๐’‰๐’‚๐’๐’•๐’–" likiwa na maana 'kupotea kwa mazingira ya mlima huo wa ๐ด๐‘˜๐‘Ž๐‘๐‘Ž๐‘›๐‘”๐‘Ž ๐‘˜๐‘’๐‘–๐‘ก๐‘Ž ๐‘Ž๐‘๐’‰๐‘Ž๐‘›๐‘ก๐‘ข uliokuwa....

...ukitumiwa na #Warongo kama eneo la kufanyia matambiko yao ya kojadi. Jina hili la ๐†๐ž๐ข๐ญ๐š lilikuwa maarufu kutokana na wazungu kushindwa kutamka maneno "๐€๐ค๐š๐›๐š๐ง๐ ๐š ๐ค๐ž๐ข๐ญ๐š ๐š๐›๐ก๐š๐ง๐ญ๐ฎ" na hivyo kukatisha kuwa "๐†๐ž๐ข๐ญ๐š" , ikaendelea kuitwa hivyo hadi leo hii.

Makabila asili yaliyokuwepo Geita kipindi hicho cha Wakoloni au tuseme waanzilishi ni ๐–๐š๐ณ๐ข๐ง๐ณ๐š, ๐–๐š๐ฌ๐ฎ๐ค๐ฎ๐ฆ๐š, ๐–๐š๐ฌ๐ฎ๐ฆ๐›๐ฐ๐š na ๐–๐š๐ฌ๐ฎ๐›๐ข, hao ndio waliigiza matamushi ya wazungu "๐†๐ž๐ข๐ญ๐š" na hivyo neno la "๐ด๐‘˜๐‘Ž๐‘๐‘Ž๐‘›๐‘”๐‘Ž ๐‘˜๐‘’๐‘–๐‘ก๐‘Ž ๐‘Ž๐‘๐’‰๐‘Ž๐‘›๐‘ก๐‘ข" likapotea.

๐Œ๐€๐๐˜๐€๐‘๐€

Mkoa Manyara upo Kaskazini mwa Tanzania. Unapakana na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi, Dodoma upande wa kusini, mkoa Tanga upande wa mashariki na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro Upande wa kaskazini. Makao makuu yake ni ๐๐š๐›๐š๐ญ๐ข ๐Œ๐ฃ๐ข๐ง๐ข.

Mkoa wa Manyara ulianzishwa mwaka 2002 baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha ambao kabla na baada ya Uhuru ulijulikana kama Jimbo la Kaskazini (๐๐จ๐ซ๐ญ๐ก๐ž๐ซ๐ง ๐๐ซ๐จ๐ฏ๐ข๐ง๐œ๐ž). Arusha ilianzishwa mwaka 1963 ikiwa na wilaya za Mbulu na Maasailand maeneo yake sasa yapo Manyara.

Baadae wilaya hizo ziligawanywa, ambapo Mbulu ilianzisha Hanang mwaka 1969 na Hanang ikaanzisha Babati (1985), wakati wilaya ya Maasailand iligawanywa kuwa wilaya ya Kiteto (1974) na Kiteto pia iligawanywa na kuanzisha wilaya ya Simanjiro mwaka 1993. Aidha, baada ya kugawanywa...

...kwa mkoa wa Arusha, wilaya nne za ๐Œ๐›๐ฎ๐ฅ๐ฎ, ๐‡๐š๐ง๐š๐ง๐ โ€™, ๐๐š๐›๐š๐ญ๐ข, ๐Š๐ข๐ญ๐ž๐ญ๐จ ๐ง๐š ๐’๐ข๐ฆ๐š๐ง๐ฃ๐ข๐ซ๐จ ziliuunda Mkoa wa MANYARA.

๐‰๐ข๐ง๐š la ๐Œ๐š๐ง๐ฒ๐š๐ซ๐š

Asili ya jina la mkoa Manyara imetokana na Jina la "Ziwa Manyara", Lkn neno lenyewe 'Manyara' Limetokana neno la lugha ya Wamasai linaloitwa "๐„๐ฆ๐š๐ง๐ฒ๐š๐ซ๐š" ambalo ni maana ya mmea wa kiasili uitwao '๐Œ๐ง๐ฒ๐š๐š' kwa kiswahili Hope wengi tunaufahamu.

Mmea huu unafahamika km '๐„๐ฎ๐ซ๐ฉ๐ก๐จ๐ซ๐›๐ข๐š ๐ญ๐ข๐ซ๐ฎ๐œ๐š๐ฅ๐ข๐ข' (kisayansi) au '๐‘ด๐’Š๐’๐’Œ ๐’ƒ๐’–๐’”๐’‰|๐‘ญ๐’Š๐’๐’ˆ๐’†๐’“ ๐‘ฌ๐’–๐’“๐’‘๐’‰๐’๐’“๐’ƒ๐’Š๐’‚' (Kiingereza) bila shaka mtaalam @IssaKalenge anaweza kutuelezea zaidi. Mmea huu huwa unatoa utomvu mweupe ambao ukipenya ktk macho huleta upofu.

Mimea mwingine jamii hiyo ya Eurphorbia ni '๐Œ๐ญ๐จ๐ฆ๐ฏ๐ฎ' au '๐„๐ฎ๐ซ๐ฉ๐ก๐จ๐ซ๐›๐ข๐š ๐‚๐š๐ง๐๐ž๐ฅ๐š๐›๐ซ๐š๐ฆ' (Kiingereza). Hivyo Wamaasai hutumia mmea huo ktk kutengeneza uzio wa maboma (nyumba) wanayoyatumia kama makazi. Na huko ndipo mimea hiyo hupatikana kwa wingi ikapelekea...

..neno la "Emanyara" kubadilika na kuwa "Manyara" kutokana na wakoloni kushindwa kutamka kwa ufasaha kama wenyeji walikokuwa wanatamka.
Hifadhi ya Ziwa Manyara inapatikana mji maarufu wa kitalii wa ๐Œ๐ญ๐จ ๐ฐ๐š ๐Œ๐›๐ฎ uliopo ndani ya Bonde la Ufa ambalo ni eneo la mkoa Arusha.

๐’๐‡๐ˆ๐๐˜๐€๐๐†๐€

Mkoa Shinyanga ulikuwa ni sehemu ya Lake Province mpk mwaka 1963 ulipoanzishwa rasmi ukiwa na wilaya 3: Maswa, Shinyanga na Kahama iliyomegwa kutoka Tabora. Mwaka 1972/82, Serikali ilikuwa mfumo wa madaraka mikoani ambapo vyama vya ushirika na Utemi zilifutwa.

Mkoa uliongozwa na Mkuu wa Mkoa akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa (RDD) yeye alisimamia wakuu wa idara mbalimbali. Muundo huu wa utawala ulitumika hadi mwaka 1997 ambapo ulibadilishwa kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa (Regional Administration Act No.19 of 1997).

Sheria iliyofuta cheo cha Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa na kuanzisha cheo cha Katibu Tawala Mkoa (mtendaji mkuu shughuli za Serikali Mkoani).Shinyanga ilikua na maeneo mapya ya utawala yalianzishwa na kufikia wilaya 7; Kahama, Bukombe, Maswa, Kishapu, Bariadi,Meatu na Shinyanga

Kuanzia mwaka 2012 kutokana na mkoa kukidhi vigezo muhimu vya kitaifa vya uanzishaji maeneo mapya ya utawala, serikali ilifanya uamuzi wa kuanzisha maeneo mapya ya Utawala ambapo mikoa mipya ya Simiyu na Geita ilianzishwa ikiwa imemega baadhi ya wilaya za mkoa wa Shinyanga.

Bariadi, Maswa na Meatu zilimegwa kuanzisha mkoa wa Simiyu na Bukombe ilipelekwa mkoa mpya wa Geita. Baadae Shinyanga iliongeza maeneo ya ki-utawala kwa kuanzisha halmashauri mpya za Kahama Mji (2012), Msalala na Ushetu (2013) ambazo zilitokana na kugawanywa kwa wilaya ya Kahama.

๐‰๐ข๐ง๐š ๐ฅ๐š "๐’๐ก๐ข๐ง๐ฒ๐š๐ง๐ ๐š"

Asili ya neno "Shinyanga" imetokana na "๐ข๐ฒ๐š๐ง๐ ๐š" au "๐ก๐ข๐ฒ๐š๐ง๐ ๐š". Jina la Mganga mmoja maarufu wa kienyeji aliyeitwa 'INYANGA' aliyekuwa anaishi hapo Shinyanga ktk eneo linaitwa Chalo.Kwahiyo, watu walipokuwa wakienda kwa Inyanga..๐Ÿ‘‡

ambapo kwa kisukuma eneo linaitwa 'Chalo' wakawa wanasema "๐‘ก๐‘œ๐‘™๐‘’๐‘—๐‘Ž ๐‘˜๐‘œ ๐ถ๐’‰๐‘Ž๐‘™๐‘œ ๐‘ ๐’‰'๐‘–๐‘›๐‘ฆ๐‘Ž๐‘›๐‘”๐‘Ž" yaani tunaenda Chalo kwa Inyanga.
Mtu huyu alikuwa maarufu sana kwa kutibu na kusaidia watu ktk matatizo mbalimbali. Alipofariki wasukuma waliendelea kufanya maombi ktk

mti mkubwa uliokuwa alipokuwa anaishi. Hivyo ktk mikutano ya wananzengo ndipo walikutania, mpiga mbinja alipoalika watu kukutania kwa Hinyanga, alisema "๐ข๐ฅ๐ข๐›๐š๐ง๐ณ๐š ๐ฅ๐ข๐ฌ๐ฐ๐ž ๐ฅ๐ข๐ ๐ฎ๐›๐ข๐ณ๐š ๐‡๐ข๐ง๐ฒ๐š๐ง๐ ๐š" (kisukuma) yaani mkutano wetu utafanyikia chini ya mti Inyanga.

Wakoloni walipofika Shinyanga walikutana na viongozi (Watemi) wa eneo hilo wakimuenzi Mganga huyo aliyejulikana kwa jina la "INYANGA" na mti huo ulikuwa unatumika km sehemu ya mikutano yote ambayo watemi walifanya. Hivyo kutoka "๐ข๐ง๐ฒ๐š๐ง๐ ๐š au ๐ก๐ข๐ง๐ฒ๐š๐ง๐ ๐š ikawa Shinyanga.

๐Š๐€๐†๐„๐‘๐€

Kabla ya Uhuru na hadi kufikia mwaka 1961, eneo la sasa la mkoa wa Kagera, lilikuwa ni moja ya maeneo yaliyounda Jimbo la ๐‹๐š๐ค๐ž ๐๐ซ๐จ๐ฏ๐ข๐ง๐œ๐ž. Jimbo hili lilijumuisha wilaya za Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora.Baada ya uhuru mwaka 1962 mkoa ulibadilishwa...

jina na kuitwa 'West Lake Region' (Mkoa Ziwa Magharibi) uliojumuisha wilaya nne ambazo ni Wilaya ya Ngara, Biharamuro, Karagwe na wilaya Bukoba. Jina hili la Ziwa Magharibi lilidumu ktk kipindi cha ukoloni na baada ya uhuru mwaka 1961 mpk mwaka 1975 ulibadilishwa na kuitwa....

Mkoa wa Kagera kutokana na MTO KAGERA.
Mkoa huu ni moja ya mikoa iliyopitia matukio na majanga makubwa ikiwemo tukio la nzige kula mazao yote, Vita vya Kagera (1978/79), janga la UKIMWI (1983/87), kuzama kwa meli ya Mv Bukoba (1996), tetemeko la ardhi (2016) but still uko Imara.

Ndio maana ktk vita kati ya Tanzania na Uganda vilifahamika ๐•๐ข๐ญ๐š ๐ฏ๐ฒ๐š ๐Š๐š๐ ๐ž๐ซ๐š.

Jina 'KAGERA'

Asili ya jina hili ni neno "๐€๐ค๐š๐ ๐ž๐ซ๐š" Kinyarwanda lenye maana ya "Mto" unaotiririsha maji. Mto huu huanzia Kaskazini, hupita Rwanda na kumwaga maji yake Ziwa Victoria.

TABORA

Tabora ni moja ya mkoa unaopatikana upande wa magharibi mwa nchi yetu na miongoni mwa mikoa mikubwa Tanzania.
Ukiwa Tabora jitahidi ufike ktk wilaya zenye historia na vivutio vya utalii km wilaya ya Sikonge, Uyui, Urambo, Nzega, Kaliua, Igunga na Manispaa Ya Tabora Mjini.

Makabila yanayopatikana Tabora ni 'Wanyamwezi' kwa wingi na ndio wenyeji, mengine ni Wasukuma, Waha na makabila mengine wakiwa kama wageni. Ukitoka Dar kuna umbali wa kilomita zaidi ya 800 kufika Tabora. Na unaweza kufika mkoani Tabora kwa usafiri wa mabasi, ndege na treni.

Wakazi wengi hulima sana zao la Tumbaku na mazao mengine ya chakula na biashara, pamoja na ufugaji wa Nyuki kwa ajili ya asali.
Tabora ni miongoni mwa mikoa mikongwe sana. Hapa ndipo nyumbani kwa aliyekuwa Mtemi Mirambo na viongozi wengi waasisi wa nchi hii wamesoma mkoani hapa.

๐‰๐ข๐ง๐š ๐‹๐š "๐“๐š๐›๐จ๐ซ๐š"

Baada ya kufahamu machache kuhusiana na mkoa wa Tabora, ni wakati sasa wa kufahamu historia ya asili ya jina la mkoa huu.
Tabora km ilivyokuwa baadhi miji mingi barani Afrika asili ya jina lake imetokana na uwepo wa lugha za kabila la Wanyamwezi.

Asili ya jina la "๐“๐š๐›๐จ๐ซ๐š" inahusiana historia kwamba kpnd Waarabu wanafika Tabora miaka ya 1830 walikuta mji huo umeendelea hasa ktk maeneo ya '"๐Š๐ฐ๐ข๐ก๐š๐ฅ๐š na ๐ˆ๐ญ๐ž๐ญ๐ž๐ฆ๐ฒ๐š", na ulikuwa na idadi kubwa tu ya watu. Ijapo Waarabu hawakuwa na mpango wa kukaa hapo ila...

kwa kuwa walilazimishwa kutoa kodi, wakaanzisha vita na Wanyamwezi. Baada waliyachukua maeneo hayo walijenga tembe ambalo lipo mpk Leo. Wakaanza kufanya biashara mbalimbali ndipo akaletwa mwarabu mmoja aliyeitwa Bw. KAZEH aliyemwakilisha Sultan wa Zanzibar kiutawala hapo Tabora.

Akatokea kuheshimiwa sana na wakazi wa Tabora. Hata yale maeneo aliyokuwa anakaa yalijulikana kama kwa Kisehi (walivyotamka Wanyamwezi).
Na mpaka wamishionari na wapelelezi wanafika ktk mji wa Tabora (Dr. Livingstone na Henry Stanley) waliufahamu mji huu kwa Jina la "Kwa Kisehi"

KISEHI lilikuwa jina la huyo mwarabu Kaze na lilifahamika zaidi hivyo awali mji wa Tabora ulifahamika kama '๐Š๐š๐ณ๐ž๐ก' ukiwa mkoani humo jaribu kuuliza. Najua unajiuliza mbona sasa haliendani na Jina la "TABORA"?? ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚. Hapo juu nilikuwa naweka kumbukumbu sawa lkn asili yake ๐Ÿ‘‡

Utamaduni wa wenyeji wa Tabora ilikuwa kilimo cha viazi vitamu. Na hapa ndipo asili inaanzia.
Kwamba baada ya viazi hivyo kuvunwa vilikuwa vinachemshwa na vingine kukatwa vipande vidogo (michembe) na kuanikwa juani, kwa kinyamwezi hiyo michembe iliitwa "๐Œ๐š๐ญ๐จ๐›๐จ๐ฅ๐ฐ๐š".....

Hivyo kutokana na muingiliano kati ya wazawa (Wanyamwezi), Waarabu pamoja na Waswahili kutoka Pwani ndio kulileta ugeuzi wa matamshi hayo kutoka โ€œ๐ฆ๐š๐ญ๐จ๐›๐จ๐ซ๐ฐ๐š" ๐š๐ฎ "๐ฆ๐š๐ญ๐จ๐ก๐จ๐ฅ๐ฐ๐š" na kuwa "๐“๐š๐›๐จ๐ซ๐š". Hivyo neno Tabora limetokana na kushindwa kutamka matamshi hayo.

Lakini zamani ulikuwa ukitaka kwenda Tabora unasema "Naenda kwenye mji wa Matoborwa", siku baada ya siku matoborwa ikafa ikaibuka Tabora.
Nadhani watu wa Tabora mjini wanafaham sehemu inaitwa '๐Š๐š๐ณ๐ž๐ก ๐ก๐ข๐ฅ๐ฅ' ni sehemu ambayo Liwali KAZEH alikuwa akiishi na familia yake.

Leo hii Tabora ni moja ya mkoa wenye kubeba historia kubwa sana, ukizungumzia historia ya TANU huwezi kuacha kutaja mji wa Tabora. Na pia ni moja ya mikoa wenye vivutio vingi sana Mfn; ktk ๐Œ๐š๐ค๐ฎ๐ฆ๐›๐ฎ๐ฌ๐ก๐จ ๐ฒ๐š ๐Š๐ฐ๐ข๐ก๐š๐ฅ๐š, Misitu ya Asili, mabonde na milima yenye kuvutia.

Makumbusho ya mito mbalimbali na bila kusahau ukiwa wilaya ya Sikonge kuna kaburi la mchungaji wa kwanza wa kinyamwezi wa Kanisa la Moraviani.
Pia Kanisa la Moravian la pili kujengwa Tanzania lililojengwa mnamo miaka ya 1897 na linatumiaka mpaka leo. Hii ndio Tabora kwa ufupi.

KIGOMA

Kigoma iko kati ya mikoa 13 inayolinda mipaka ya JMT upande wa nchi kavu. Kigoma imepakana na Burundi na Kagera upande wa Kaskazini, Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa la Tanganyika ilipo njia ya kwenda DR-Congo.

Miji ya Ujiji na Kigoma ni mikongwe, ilipata kukua zamani hata kabla ya ujio wa wageni (wakoloni) kwenye maeneo hayo. Hivyo kabla ya mji huo kuitwa Kigoma mwisho wa reli eneo hilo lilikuwa linaitwa "๐‹๐”๐’๐€๐Œ๐๐Ž ๐†๐ฐ๐š ๐๐ฒ๐š๐ง๐ ๐ž" na "Ujiji" palikuwa panaitwa #๐”๐›๐ฎ๐ฃ๐ข๐ฃ๐ข.

Historia inaeleza kwamba miji hii ilipata majina kutokana na watu maarufu waliopata kuishi na kujiwekea historia ktk miji hiyo. Ndugu hao walikuwa wawili na walifahamika kwa majina ya ๐Š๐š๐ฃ๐ข๐ฃ๐ข na ๐Š๐š๐ ๐จ๐ฆ๐š (BUGOYE).
Ukiwa mkoani humo utapata Stori mbalimbali zinazowahusu.

Bw. ๐Š๐š๐ฃ๐ข๐ฃ๐ข alikuwa mtu mkarimu, mpole na mwenye upendo kwa watu. Lkn kwa upande wa ๐Š๐š๐ ๐จ๐ฆ๐š alionekana tofauti kidogo kwa jamii. Kutokana tabia za ndugu hao wawili, wengi walimpenda sana KAJIJI na maeneo aliyokuwa akiishi yalipendwa na watu wengi walikuwa wakimtembelea.

Watu waliongezeka kuhamia maeneo ya mbalimbali ktk eneo hilo, waliokuwa wanakwenda kwa Kajiji walikuwa wanasema tunaenda "Ubujiji" kulingana na lugha yao. Bw Kajiji baadae alifariki lkn maeneo aliyokuwa akiishi yalikuwa yameendelea kiasi cha kuwa km Center fulani ya kutembelea.

Eneo alilokuwa akiishi KAJIJI liliendelea kukua mpk ukawa kamji kadogo na watu wengi walikuwa wakienda kwa shughuli mbalimbali. Hata waarabu walifika maeneo hayo (1800's) walikuta mji huo ukikaliwa na idadi kubwa sana ya watu na walikuta Jina la #Ubujiji ndio linatumika hapo.

Kadri ya miaka ilivyoenda wageni kutokea sehemu mbalimbali walizidi kuingia na kuweka makazi UBUJIJI, lkn kutokana na matamshi yake kuwa ktk lafudhi ya kikabila wageni hasa Waarab walishinda kutamka ubujiji wakawa wanatamka "UJIJI" na baadae karibia wakazi wote wakapaita hivyo.

Kwa upande wa Bw ๐๐ฎ๐ ๐จ๐ฒ๐ž, ambaye ndiye alikuwa mdogo kwa KAJIJI, alihamia maeneo ya juu kidogo. Sehemu aliyoishi BUGOYE palijulikana kama '๐ˆ๐›๐ฎ๐ ๐จ๐ฒ๐ž' ambapo kwa sasa panaitwa Mwanga. Aliishi hapo kipindi kirefu lkn naye pia baadae alikuja kufariki dunia akaacha ukoo.

Ktk miaka ya 700 eneo la IBUGOYE lilipokea wageni waliongia Kigoma kutokea nchi jirani Zaire ambayo kwa sasa inajulikana DR-Congo wakiongozwa na shujaa wao aliyekuwa anaitwa "๐๐๐ข๐ฒ๐ฎ๐ง๐ณ๐ž ๐Œ๐ฌ๐ก๐ข๐ฅ๐ฐ๐š๐ฆ๐ฉ๐š๐ฆ๐›๐š" pamoja na Sultani wao aliyeitwa SULTAN SIMBA.

Kwa vile lugha zao zilikuwa zinaelekeana walijieleza vizuri, kuwa wanatafuta sehemu ya kuishi baada ya walipokuwa wakiishi kuvamiwa na jamii nyingine kutokea Kusini. Basi wenyeji wakawapa eneo la kuishi huko BANGWE ambako ndiko walijenga makazi yao, wakafanya shughuli za kilimo.

Mshilwampamba akashirikiana na vijana wa kabila lake (Wagoma) akajenga ngome ya Ikulu kumlinda Sultani wao maeneo ya ๐‘๐ฎ๐ฌ๐š๐ฆ๐›๐จ.
#Wagoma wakaujenga mji wao ukazidi ule "Ubujiji" na walifurahia kukaa eneo hilo kwa7bu aliwahi kukaa (Kagoma) mtu mwenye jina sawa na kabila lao.

Kufifia kwa umaarufu wa eneo kongwe la UJIJI kulichangiwa na sababu nyingi, ikiwemo kuanzishwa kwa mji mpya ambapo wagoma walikuwa wakiishi.

Jina La KIGOMA

Asili ya jina ๐Š๐ข๐ ๐จ๐ฆ๐š ilitokana na wageni hasa Warundi pindi walipokuwa wakitembelea mji huo walikuwa wakisema....

"Tugende kubagoma". Kubagoma ikawa KIGOMA.
Hata wageni wengine waliongia mji huo walitamka hivyo hivyo.Jina liliendelea kubadilika mdogo mdogo kutokana na matamshi mpk mjerumani alipofika mji huo alikuta mkoa wa Kigoma ukiitwa hivyo, na hiyo ndio asili ya Kigoma mwisho wa reli.

9. SINGIDA

๐—ฆ๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ถ๐—ฑ๐—ฎ ni moja ya mikoa inayopatikana katika maeneo ya kanda ya kati hapa nchini.Wenyeji asilia wa mkoa huu ni ๐–๐š๐ง๐ฒ๐š๐ญ๐ฎ๐ซ๐ฎ na ๐–๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ซ๐š๐ฆ๐›๐š.Mji wa singida ni moja ya maeneo yenye historia kubwa sana ya Tanzania.Wakazi wa mwanzo kabisa waliopata..

kuishi maeneo ya mkoa huu wa Singida walikuwa ni Jamii ya Mbirikimo (๐๐ฒ๐ ๐ฆ๐ข๐ž๐ฌ), inasemekana waliishi ktk miaka ya 1000 BK, Lkn miaka ya baadae maeneo hayo yalivamiwa na kukaliwa na jamii za '๐๐ข๐ฅ๐จ-๐‡๐š๐ฆ๐ข๐ญ๐ž๐ฌ' ambao ndio hawa ๐‘Š๐‘Ž๐‘›๐‘ฆ๐‘–๐‘Ÿ๐‘Ž๐‘š๐‘๐‘Ž na ๐‘Š๐‘Ž๐‘›๐‘ฆ๐‘Ž๐‘ก๐‘ข๐‘Ÿ๐‘ข

Kabila la Wanyaturu asili yao kabisa ni Ethiopia ambako kunasadikiwa kuwa na watu wanaotumia lugha ambayo kwa asilimia kubwa inafanana na Kinyaturu. Inadhaniwa pia kuwa Wanyaturu na Wakushi wa Ethiopia asili yao ni moja.Walipoingia Tanganyika walichangamana na Wanyatunzu pamoja..

...na Wasukuma, ndiyo maana mila na tamaduni zao zinashabihiana kwa kiasi kikubwa. Sometimes ni vigumu kumpambanua Wanyaturu na Wanyatunzu.Wanyaturu wengi sura na nywele zao, hasa kina mama, zinafana sana na watu wa jamii ya Waoromo akina @AbiyAhmedAli Waziri mkuu wa
Ethiopia.

Jina La Singida.

Asili ya jina la Singida limekuwa na utata kwa kiasi fulani kutokana na masimulizi mengi yaliyotolewa. Kuna wengine walisema jina la SINGIDA limetokana urembo unaovaliwa na mabinti wa kabila la wanyaturu uitwao "๐ฆ๐š๐ฌ๐ข๐ง๐ ๐ข๐๐š" neno linalomaanisha 'Heleni'..

urembo unaotengenezwa kutokana na miti ya porini, Lkn km tunajuavyo kuwa Waafrika hatukuwa na utamaduni wa kuhifadhi historia zetu kwa njia ya maandishi.Ukichukua hiyo na ukizingatia jamii nyingi za Kiafrika mabinti walikuwa wakivaa heleni kietemolojia hiyo tahajia inakosa nguvu.

Hivyo basi kwa kumrejelea Abdalah Bashir tunapata asili ya jina Singida kuwa ni uwepo wa '๐Œ๐ข๐ญ๐ฎ๐ฆ๐›๐ฐ๐ข' na kwa 'Kinyaturu' mitumbwi huitwa ๐’๐ข๐ง๐ ๐ข๐๐š.Anaelezea kuwa Mitumbwi hiyo ilikuwa kwenye ziwa ambalo leo linajulikana kama ZIWA SINGIDANI. Wakati Wanyaturu wanafika...

maeneo hayo wakitokea maeneo ya kaskazini walisema wamefika โ€œ๐’”๐’Š๐’๐’ˆ๐’Š๐’…๐’‚๐’๐’Šโ€ wakimaanisha kwenye mitumbwi. Na ndio maana mpaka leo mkoa huu unaitwa Singida. Nimewahi kulala ktk hoteli ya #Regency nikafaidi view nzuri na upepo kutoka ziwa hili na hiyo not historia ya singida.

๐Œ๐๐„๐˜๐€

Mkoa wa Mbeya ni kitovu cha Nyanda za Juu za Kusini na wazalishaji wa mazao mengi na kijiografia mji huu umeenea ktk bonde kati ya safu za milima ya Mbeya na Uporoto.Mlima mkubwa unaoonekana kutoka mjini ni Mlima wa Mbeya (๐Œ๐›๐ž๐ฒ๐š ๐๐ž๐š๐ค) wenye urefu wa Mita 2818

Mkoa huu unapakana na nchi za Zambia na Malawi upande wa kusini,Rukwa upande wa Magharibi, mikoa ya Tabora na Singida kwa upande wa Kaskazini,ambapo kwa upande wa mashariki unapakana na Iringa.Kupitia Mbeya mpk Tunduma ndipo milango ya kuingilia na kutokea Zambia na Malawi ilipo.

Katika enzi za ukoloni wa Waingereza, mkoa wa Mbeya ulikuwa ukijulikana kwa jina la "๐’๐จ๐ฎ๐ญ๐ก๐ž๐ซ๐ง ๐‡๐ข๐ ๐ก๐ฅ๐š๐ง๐ ๐๐ซ๐จ๐ฏ๐ข๐ง๐œ๐ž".
Mkoa ulikuwa ukiunganisha baadhi ya maeneo ya mikoa mitatu ya sasa ambayo ni Mbeya, Iringa na Rukwa. Mji wa Mbeya ulianzishwa na Waingereza..

Mnamo 1927 kufuatia kushamiri kwa upatikanaji wa dhahabu ktk milima ya Loleza na mkondo wake kufika Chunya eneo la Lupa Tingatinga. Hata leo eneo la kati la Jiji la Mbeya huitwa ๐‹๐ฎ๐ฉ๐š ๐–๐š๐ฒ kama ilivyozoeleka miaka hiyo ambapo mahema ya wafanyabiashara wa Kihindi yaliwekwa...

yaliwekwa wakiwa njiani kwenda migodi ya Lupa karibu na milima iliyopo Mbeya hadi Chunya. Hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa, hali iliyosababisha mji wa Mbeya kupewa jina la utani kama "The Scotland of Africa" kwa hali ya hewa.

Pamoja na muonekano wa milima (hills) inayozunguka mji wa Mbeya kufanana na hali ya hewa huko nchini Scotland. Mkoa huu ni moja kati ya mikoa mikongwe nchini Tanzania iliyokuwepo mpk wakati wa uhuru mwaka 1961.

Ktk kipindi hicho makabila makuu ktk Mkoa wa Mbeya yalikuwa ni ๐–๐š๐ฌ๐š๐Ÿ๐ฐ๐š, ๐–๐š๐ง๐ฒ๐š๐ค๐ฒ๐ฎ๐ฌ๐š, ๐–๐š๐ง๐๐š๐ฅ๐ข, ๐–๐š๐ฌ๐š๐ง๐ ๐ฎ, ๐–๐š๐ฆ๐š๐ฅ๐ข๐ฅ๐š, ๐–๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ก๐š, ๐ฐ๐š๐ค๐ข๐ฆ๐›๐ฎ ๐ง๐š ๐–๐š๐ง๐ฒ๐š๐ฆ๐ฐ๐š๐ง๐ ๐š, Jamii ambazo ni maarufu kwa shughuli za kilimo na ufugaji mdogo mdogo

Mji wa Mbeya uliendelea kupanuka pande zote isipokuwa eneo la Kaskazini lilitawaliwa na milima. Ujio wa Wanyakyusa kutoka Rungwe ndiyo uliowaondoa kabila la ๐–๐š๐ฌ๐š๐Ÿ๐ฐ๐š ambao wenyeji kiasili wa Mji wa Mbeya kuondoka na kuhamia milimani kupisha wageni.

Leo hii eneo la wilaya ya Mbeya ambako ndipo jiji lilipo imetawaliwa zaidi na kabila la ๐–๐š๐ง๐ฒ๐š๐ค๐ฒ๐ฎ๐ฌ๐š na ๐–๐š๐ฆ๐š๐ฅ๐ข๐ฅ๐š huku ๐–๐š๐ค๐ข๐ง๐ ๐š wakiwa ndiyo wafanyabiashara wakubwa pamoja na Wahindi. Wenyeji wa wilaya za Rungwe na Kyela ni "๐–๐š๐ง๐ฒ๐š๐ค๐ฒ๐ฎ๐ฌ๐š".

Wenyeji wa Ileje ni ๐–๐š๐ง๐๐š๐ฅ๐ข, wenyeji wa wilaya Chunya ni ๐–๐š๐›๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ ingawa watu waishio huko zaidi ni ๐–๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ก๐š. Wenyeji wa wilaya Mbozi ni ๐–๐š๐ง๐ฒ๐ข๐ก๐š na ๐–๐š๐ง๐ฒ๐š๐ฆ๐ฐ๐š๐ง๐ ๐š, lkn mji wa Tunduma zaidi ni ๐–๐š๐ค๐ข๐ง๐ ๐š ambao ndio wamiliki uchumu wa mji huo.

Wenyeji wa wilaya Mbarali ni ๐–๐š๐ฌ๐š๐ง๐ ๐ฎ, ๐–๐š๐ฐ๐š๐ง๐ฃ๐ข, ๐–๐š๐›๐ž๐ง๐š na ๐–๐š๐ค๐ข๐ง๐ ๐š.

Jina #Mbeya

Asili ya jina la mkoa wa Mbeya imetokana na neno '๐ˆ๐›๐ก๐ž๐ฒ๐š' Lenye maana ya ๐‚๐ก๐ฎ๐ฆ๐ฏ๐ข ktk lugha ya kabila la Wa๐ฌ๐š๐Ÿ๐ฐ๐š. Inasemekana miaka ya nyuma wafanyabiashara

..wengi kutokea maeneo mbalimbali walikuwa wakifika mahali hapo kubadilishana mazao yao kwa bidhaa ya chumvi.Walipokuwa wakikaribia mlima mkubwa ulio karibu na Mbeya walisema wamefika ktk mji wa "๐ˆ๐›๐ก๐ž๐ฒ๐š" hivyo ikawa 'Mbeya'. So, jina la mji lilitokana na mlima huu wa Mbeya.

KATAVI

Mkoa wa Katavi ni moja kati ya mikoa mipya inayojumuisha mikoa 31 ya Tanzania na ulianzishwa rasmi mwaka 2012 baada ya kuigawanya halmashauri ya wilaya ya Mpanda na kupata wilaya 3 na halmashauri za wilaya 5. Wilaya hizo ni wilaya Mpanda ambayo ina halmashauri za wilaya 2

..ambazo ni halmashauri ya Manispaa ya mpanda na halmashauri ya wilaya ya Nsimbo. Nyingine ni wilaya ya Mlele ina halmashauri 2 ambazo ni halmashauri (w) Mlele na Mpimbwe pamoja na wilaya ya Tanganyika yenye halmashauri 1 ambayo ni halmashauri ya wilaya Mpanda (halmashauri mama).

Jina "๐Š๐š๐ญ๐š๐ฏ๐ข"

Asili ya jina la mkoa Katavi lilitokana na uwepo wa vitu viwili; Ziwa Katavi na Hifadhi ya Taifa ya Katavi iliyoanzishwa mwaka 1974. Hifadhi hiiinapatikana Kusini Magharibi mwa Tanzania karibu na Ziwa Tanganyika ktk wilaya za Mpanda na Mlele Mkoa wa Katavi.

Jina la 'Katavi'

Asili ya jina hili ๐Š๐š๐ญ๐š๐ฏ๐ข imetokana na neno "๐Š๐š๐ญ๐š๐›๐ข" linalomaanisha '๐“๐š๐ฐ๐ข' kwa lugha ya kabila la Wabende.Kabila la ๐–๐š๐›๐ž๐ง๐๐ž walitokea DR-Congo (1810's) wakiongozwa na mtemi wao aliyeitwa ๐‘๐ฎ๐ญ๐ฎ๐ค๐š, baadae waligawanyika ndipo wengine..

wakasambaa kwenda Mpanda ilipo mihofi migodi ya Mperuki. Inasemekana Wabende walikuwa na ndugu yao Mpimbwe aliyeanzisha kabila la 'Wapimbwe' hivyo walikuwa na eneo moja la kutoa sadaka na kuomba mahitaji kwa njia kutambika kwenye mti wa "Mzimu wa KATABI",

wazungu walipokwenda ktk eneo hilo wakawa wanashindwa kutamka neno "๐Š๐š๐ญ๐š๐›๐ข" badala yake wakawa wanatamka 'KATAVI', kwa vile wakoloni walitawala kwa kipindi kirefu huo ndio ukawa mwanzo wa jina hilo kushika na kuitwa mpk leo.

Mpk Leo watu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya mkoa wamekuwa wakifika ktk Hifadhi ya Katavi na kwenda kwenye mti ulioko kwenye Ziwa Katavi wakiamini kuwa ๐Œ๐ณ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐Š๐š๐ญ๐š๐›๐ข alikuwa akiishi hapo zamani kabla ya kuwepo ๐‡๐ข๐Ÿ๐š๐๐ก๐ข ๐ฒ๐š ๐“๐š๐ข๐Ÿ๐š ๐ฒ๐š ๐Š๐š๐ญ๐š๐ฏ๐ข.

Ina-Endelea_____

MUHIMU nachokuomba unayesoma #Uzi huu, kama Support yako na Appreciation yako

RT ๐Ÿ”„ FOLLOW Me @Eng_Matarra Turn On Notification

#BreakTime kidogo , nikirejea IRINGA, DODOMA, KILIMANJARO, TANGA, UNGUJA mpk PEMBA. Yaani Hakiachwi kitu Wazee iwe Ruvuma, Lindi n.k

MORNING..

If u're reading this #tweet
๐Œ๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž๐ณ๐ข ๐Œ๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ has given us the privilege to see TODAY, despite of all challenges we face, know still he loves us so much.

So, wherever u are say AMEN๐Ÿ™

SHUKRANI WOTE mlioRt๐Ÿ”„ Uzi huu, sasa Tuendelee๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐Œ๐Š๐Ž๐€ ๐–๐š ๐ˆ๐‘๐ˆ๐๐†๐€

๐ˆ๐‘๐ˆ๐๐†๐€ ni mkoa uliopo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania na ulianzishwa mwaka 1892 na mkoloni (Wajerumani) kama kituo cha kijeshi walichokiita "๐๐ž๐ฎ ๐ˆ๐ซ๐ข๐ง๐ ๐š" ukimaanisha '๐ˆ๐ซ๐ข๐ง๐ ๐š ๐ฆ๐ฉ๐ฒ๐š'.
Hii ilikuwa baada ya wajerumani kuanza...๐Ÿ‘‡

kushindwa na Jeshi la Wahehe ktk vita ya kwanza maeneo ya Lugalo vilivyoanza mwaka 1891.Wajerumani walitumia jina hili baada ya kuharibu boma la Mtemi Mkwawa huko Kalenga 31 Oktoba 1894.Kalenga ilikuwaย makao makuuย yaย ๐Œ๐ญ๐ž๐ฆ๐ข ๐Œ๐ค๐ฐ๐š๐ฐ๐š aliyeongozaย waย Wahehe kupigana dhidi...

...yaย ukoloni wa Kijerumaniย ktk miaka yaย 1891/96. Huko Kalenga MKWAWA aliwahi kujengaย boma imara yaย maweย baada ya kujifunza kuhusu uenezi wa Wajerumani kutoka sehemu zaย pwani. Boma hii liliitwa "๐‹๐ข๐ฉ๐ฎ๐ฅ๐ข".ย Ujenziย ulianza mnamoย 1887ย ukachukua miaka minne kukamilika.

Kalenga ilikuwa na sehemu mbili zilizotengwa na mto; upande wa kulia wa mto uliitwa "๐”๐ง๐ ๐ฎ๐ฃ๐š ", upande wa kushoto "๐๐š๐ ๐š๐ฆ๐จ๐ฒ๐จ". Mwaka 1891 kila sehemu ilikuwa na msimamizi wake walioitwa ๐๐ ๐จ๐ณ๐ข๐ง๐ ๐จ๐ณ๐ข na ๐Œ๐ญ๐ž๐ฆ๐ข-๐ฎ๐ฆ๐š, wote waliuawa ktk mapigano yaย Lugalo.

Baada ya kushindwa kwaย jeshiย la Kijerumani laย SCHUTZTRUPPEย ktk mapigano yaย Lugalo, Wajerumani walirudi kwa nguvu zaidi wakiishambulia Lipuli (Kalenga) kwenyeย Oktobaย 1894ย kwaย silahaย kwa silaha nzito pamoja na mizinga ya mabomu ndipo walipofanikiwa kubomoa ngome hiyo.

MKWAWA alizaliwa mwaka 1855 akaitwa ๐๐ƒ๐„๐’๐€๐‹๐€๐’๐ˆ maana yake "Mtundu au Mdadisi" ktk utu uzima aliitwa:
"๐Œtwa ๐Œkwava ๐Œkwavinyika ๐Œahinya ๐˜๐ข๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฐ๐ข๐ ๐š๐ง๐ ๐š ๐Œkali ๐Š๐ฎ๐ฏ๐š๐ ๐จ ๐Šuvadala ๐“age ๐Œatenengo ๐Œ๐š๐ง๐ฐ๐ข๐ฐ๐š๐ ๐ž ๐’๐ž๐ ๐ฎ๐ง๐ข๐ฐ๐š๐ ๐ฎ๐ฅ๐š ๐†๐ฎ๐ฆ๐ ๐š๐ง๐ ๐š"

maana yake:"๐Œ๐ญ๐š๐ฐ๐š๐ฅ๐š, ๐ฆ๐ญ๐ž๐ค๐š๐ฃ๐ข ๐ฐ๐š ๐ง๐ฒ๐ข๐ค๐š, ๐ฆ๐ค๐š๐ฅ๐ข ๐ค๐ฐ๐š ๐ฐ๐š๐ง๐š๐ฎ๐ฆ๐ž ๐ฆ๐ฉ๐จ๐ฅ๐ž ๐ค๐ฐ๐š ๐ฐ๐š๐ง๐š๐ฐ๐š๐ค๐ž ๐š๐ฌ๐ข๐ฒ๐ž๐ญ๐š๐›๐ข๐ซ๐ข๐ค๐š, ๐š๐ฅ๐ข๐ž๐ฌ๐ก๐ข๐ง๐๐ข๐ค๐š๐ง๐ข๐ค๐š,๐ฆ๐›๐š๐›๐ž ๐ฆ๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ง๐ ๐ฎ๐ฏ๐ฎ ๐ฎ๐๐จ๐ง๐ ๐จ ๐ฉ๐ž๐ค๐ž๐ž ๐ง๐๐ข๐จ ๐ฎ๐ญ๐š๐ค๐จ๐ฆ๐ฎ๐ฐ๐ž๐ณ๐š"

Jina la MKWAWA ni kifupisho cha MUKWAVA, ambalo pia ni kifupisho chaย  MUKWAVINYIKA, lililokuwa jina lake laย heshimaย likimaanisha "Kiongozi aliyetwaa nchi nyingi". ๐Œ๐ญ๐ž๐ฆ๐ข ๐Œ๐ค๐ฐ๐š๐ฐ๐š alizaliwa mahali palipokuwa panaitwa ๐‹๐ฎ๐ก๐จ๐ญ๐š karibu naย Iringa Mjini. Alikuwaย mtotoย wa...

CHIFUย MUNYIGUMBA aliyefariki mwaka 1879 kipindi hicho Mkawa akiwa na miaka 22.
MUNYINGUMBA aliunganisha Temi ndogo za Wahehe na makabila ya majirani kuwaย dolaย moja. Aliiga mfumo wa kijeshi wa WASANGU waliokuwa na nguvu kutoka kwa kabila za 'Wangoniย na Impi' asili yaย Shaka Zulu.

Hadiย miaka ya 1870ย eneo la Wahehe lilipanuliwa mbali kuanzia kusini hadi katikati ya Tanzania ya leo. Baada ya kifo cha chifu mzee watoto wake walishindania urithi wake na MKWAWA alishinda akawa kiongozi mpya. Aliendelea kupanua utawala wake. Hadi mwisho waย miaka ya 1880ย ..

alitawala sehemu muhimu za njia ya misafara kati yaย Pwaniย naย Ziwa Tanganyika. Misafara hiyo ambayo ilikuwa ikibebaย bidhaaย za nje km vitambaa, visu na silaha kutoka Pwani, ikirudi na watumwa naย pembe za ndovu, ilipaswa kumlipiaย kodi. Milki yake ilipanuka kwa kununua watumwa ktk...

misafara hiyo ndipo jeshiย lake likaongezeka na kuwa kubwa. Mnamo Julai 1891 VON ZELEWISKI (Kamanda wakijerumani) aliongozaย kikosiย cha maafisa 13, Waafrika (hasa kutoka Sudan) wapatao 300 pamoja na wapagazi 113 wakiwa naย bundukiย za kisasa na mizinga huku akiwadharau Wahehe..

kabla hajafika aliangamiza vijiji kadhaa.Taarifa zikamfikia MKWAWA akatuma wajumbe 03 ili wafanye mazungumzo, akadhania wanavamia akaagiza wauawe. Kisha akaanza kunyemelea kambi aliyokuwa MKWAWA, akawawekewa mtego bila wao kujua walipokaribia tu wakauawa wengi na ZELEWSKI.

Ilibidi kikosi cha nyuma kirudi nyuma, kutafuta namna ya kupambana na WAHEHE. Baadae walipata kilima kidogo walipoweza kutumia bunduki wakajitetea na kuua Wahehe wengi tu lkn bado hali ya Vita iliwaendea vibaya na WAHEHE wakashinda wakachukua bunduki zao takriban 300 na mizinga 2

Vita ikatulia kidogo. Akatokea askari mmoja wa kihehe akajaribu kutumia ile mizinga akajipiga akafa, lkn ali7bisha mlipuko uliowashtua watu wengi. MKAWA alipofika eneo mlipuko ulitokea akastaajabu, akaitupa ile mizinga yote mtoni. Zile bunduki zikahifadhiwa ghalani na ulinzi juu.

Baada ya mapigano Mkwawa alihesabu Wahehe waliofariki, kisha akskataza watu kulia, kwa sababu alitaka kuficha idadi ya askari waliokufa. Vile vifo vilimshtua sana akawaza aina silaha wanazotumia Wajerumani, ikabidi atume tena wajumbe kwa gavana VON SODEN akitaka amani.

Lakini madai ya Wajerumani yalikuwa magumu, mojawapo ilikuwa kuwaruhusu wafanyabiashara kupita njia yake TENA asiwashambulie, Mkwawa akakataa kwa kuhofia inaweza kuwa njia ya wazungu kumshambulia. Wkt huo kiongozi mpya wa kijeshi kwa Wajerumani alikuwa anaitwa TOM VON PRINCE.

Akaanzisha tena vita dhidi ya Wahehe. Mkwawa alijibu kwa kushambulia vikosi vidogo vya jeshi la kikoloni mpk GAVANA SODEN akatuma wajumbe akidai kusitisha mapigano. Mnamo 1893ย akaondoka bara la Afrika na Gavana mpya VON SCHELE akaletwa, akataka kulipiza kisasi cha ZELEWISKI..

Kiufupi Wahehe walikuwa na Jeshi zuri, sema walijisahau kuwa wazungu walikuwa na Silaha nzito ikiwemo hayo mabomu. Hivyo round ya 2 Wahehe walivamiwa na Ngome ikalipuliwa ukiongezea MKWAWA hakuwagawia askari wake bunduki zile inasemekana ni 100 tu ndio alitumia zingine akafungia.

Magobore na mikuki ya Wahehe hazikuweza kufua dafu kushindana na mabomu ya Wajerumani, yeye mwenyewe akakikimbilia milimani akiwa na askari wanaokadiriwa zaidi ya 2000. Lakini kabla hajakimbia inasemekana aliamua kumuua mganga aliyekuwa amemwambia hiyo vita atashindwa.

Mkwawa alijifichaย msituniย pamoja na askari wake akasubiri Wajerumani, huku VON SCHELE akishindwa kuendelea na vita kwa7bu ya gharama kuwa kubwa, na kule Ujerumani wabunge wa upande wakaanza kupinga vita kutokana na gharama kubwa kutumika huku Afrika na raia wakiachwa watupu...

Kidogo amani ikapatikana na Mkwawa akarudi Kalenga, ambapo alijenga boma jingine jipya. Ilipita kipindi Mkwawa akatuma wajumbe kupatana na Wajerumani na Wajerumani walikubali kutambua uchifu wa Mkwawa km Kiongozi wa Wahehe. Inasemekana yalipofikiwa makubaliano Mkwawa alimtuma...

Mjomba wake akatie 'sahihi' makubaliano lkn alikataa kwa kuogopa kuuawa na Wajerumani. Hivyo, wahehe walikubaliana na Wajerumani kupandisha bendera ya kijerumani ktk milki yao na kuruhusu wafanyabiashara wa kitumwa kupita njia ya maeneo ya uhehe.

Pamoja na kurudisha silaha walizokuwa wamechukua mwanzo kwa Wajerumani. Basi, hali ya UTULIVU ikapatikana mpk kuna kpnd kabila la "Wabena" waliposikia Wahehe wamejisalimisha kwa wakoloni wakajua wamelegea, wakawavamia, ikabidi Mkwawa aombe msaada ktk Jeshi la Wajerumani.

Hali ya amani iliisha siku moja ambayo askari mmoja wa kijerumani alikwenda kumtembelea Mkwawa, alipofika geti la kuingia Kalenga maskaari wakamzuia kuingia kwamba mpk awape hongo ya bunduki 5 ndipo aruhusiwe kuingia katika eneo la Mkwawa. Ikawa ni kosa jingine, maafisa wa jeshi

...la Wajerumani waliokuwa wakilindaย mpaka, ambao bado walikuwa wakitafuta nafasi ya kulipiza kisasi cha Lugalo, wakadai kuwa chifu amevunja mkataba. Ikawa sasa ni vita baridi.
Kapteni TOM VON PRINCE akajenga boma jipya karibu na Kalenga ("Iringa Mpya") akaanza kuwasiliana na..

machifu wadogo wa Wahehe.

Mkwawa alijaribu kujenga mapatano na majirani zake Wabena na makabila mengine lkn walikataa wakaungana na Wajerumani. Siku moja MKAWA akapata Taarifa kuwa kuna machifu wawili (Wahehe) aliosikia walionekana kujadiliana na VON PRINCE, akawaua wote.

Baadae alijua kumbe sio wao (machifu aliowaua) peke yao walikuwa hawamtii, mara baada ya kupata habari ya kwamba hata mdogo wake MPANGILE alikuwa ameshajiunga na Wajerumani. Mnamo Septemba1896ย Wahehe wakagawanyika na sehemu kubwa ya viongozi waliokuwa wamechoka kupigana vita..

Wakajiunga na Wajerumani. Ndipo Wajerumani wakaligawa eneo lao.

WASANGU wakarudishwa krk eneo lao la awali wakarudi "Usafwa" ktk mji mkuu waย Utengule Usangu. Mdogo wake Mkwawa (Mpangile) akawa kiongozi mpya wa Uhehe, lkn baada ya siku 50 aliuawa na Wajerumani waliomshtaki, eti

alikuwa anamsaidia kaka yake kisiri kisiri. Chifu MKWAWA alikuwa ameondoka sehemu za Iringa mwezi Agosti 1896 alipoona mgawanyiko.Alifuata mwendo waย mto Ruahaakilindwa na wenyeji waliokuwa tayari kumficha na kumlinda dhidi ya vikosi vya Wajerumani waliokuwa wakimtafuta kila siku.

Mnamo Desemba 1896 akahamia ktk milima ya UDZUNGWA kujificha. Akiwa huko alikuwa akishuka mara kwa mara mabondeni kutafuta vyakula na kushambulia vikosi vidogo vya Wajerumani. Mnamo
Julaiย 1897ย kikosi kikubwa cha WASANGU pamoja na Wahehe chini ya uongozi wa Wajerumani walikuta....

kambiย la Mkwawa mlimani wakalishambulia huku Mkwawa akiwa ameshatoka.
Baadae hapo kambini wajerumani wakaahidi zawadi ya pembe za ndovu yenye thamani yaย rupiaย 5000 kwa kila mtu atakayewasaidia kumkamata Mkwawa, akiwa hai au amekufa.

Mwakaย 1898ย Mkwawa aliendelea kujificha kwenye misitu huku akilindwa na kikosi kitiifu cha vijana wachache. Akaishi huko akitegemea chakula kwa kuwinda wanyama.
Inasemekana mnamo Julai 1898 alikutana na vijana wanne, ambao wawili kati yao walikuwa Mme na mke kabila la WAZUNGWA.

Mnamo Desemba 1896 akahamia ktk milima ya UDZUNGWA kujificha. Akiwa huko alikuwa akishuka mara kwa mara mabondeni kutafuta vyakula na kushambulia vikosi vidogo vya Wajerumani. Mnamo
Julaiย 1897ย kikosi kikubwa cha WASANGU pamoja na Wahehe chini ya uongozi wa Wajerumani walikuta....

kambiย la Mkwawa mlimani wakalishambulia huku Mkwawa akiwa ameshatoka.
Baadae hapo kambini wajerumani wakaahidi zawadi ya pembe za ndovu yenye thamani yaย rupiaย 5000 kwa kila mtu atakayewasaidia kumkamata Mkwawa, akiwa hai au amekufa.

Mwakaย 1898ย Mkwawa aliendelea kujificha kwenye misitu huku akilindwa na kikosi kitiifu cha vijana wachache. Akaishi huko akitegemea chakula kwa kuwinda wanyama. Inasemekana mnamo Julai 1898 alikutana na vijana wanne, ambao wawili kati yao walikuwa Mme na mke kabila la WAZUNGWA.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling