#TOTTechs Profile picture
Jukwaa la washauri na wataalamu wa Teknolojia || 💻 Computers ||📱 Phones | Softwares | ICT Hardwares | ICT Security || Partnership with Kukeke Gang and L.M.S

Aug 21, 2021, 23 tweets

ARTIFICIAL INTELLIGENCE (AI) [ AKILI BANDIA ]

Akili Bandia (AI) hii ni Teknolojia inayozipatia mashine uwezo wa akili ya kibinadamu ili kuweza kufikiria na kutenda matendo kama kibinadamu.

Je, hizi AI zikoje na zianatumika wapi?

THREAD [ UZI ] 👇

#ElimikaWikiendi

Watu wengi wakiona neno AI ( Artificial Intelligence) hufikiria moja kwa moja ni roboti. Ili iwe AI inahitaji Software(Program endeshi) na Hardware. Software ndio kama ubongo unahitaji kupachikwa data ambazo zitakuwa zinatoka command/maelekezo kwenye hardware.

#ElimikaWikiendi

AI ina jifunza (learning), Fikiri (reasoning) na mtazamo (perception). Ndivyo hivyo sehemu ya akili ya binadamu inafanya kazi. Kwa miaka ya sasa hii Teknolojia inakuwa kwa kasi sana.

Imefikia hatua wataalamu wanataka AI iwe na uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi kama mwanadamu,

AI iweze kutafsiri na kutatua matatizo makubwa bila uhitaji wa binadamu

Teknolojia ya 5G ina changia kwa asilimia kubwa Teknolojia hii kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa.Baadhi ya watu waliopo kwenye nchi zilizoendelea wanaanza kuishi ndani ya hii Teknolojia
#ElimikaWikiendi

Mtu anafanya asilimia kubwa ya shughuli za nyumbani kupitia simu yake au sauti yake pekee.

Makampuni makubwa kama Google, Amazon n.k yamekwisha anza kuitumia hii Teknolojia kwenye majukumu yao ya kila siku. Ni faida kwa dunia pia vivyo hivyo kuna hasara zake.

#ElimikaWikiendi

JINSI AI INAVYOFANYA KAZI

Hapa tunarudi kwenye zile points zetu 3.

🔸Learning processes
Hii ni issue ya algorithm hapa AI inatafuta data na kuweza kuzifanya ziweze kutoa maagizo hatua kwa hatua ili kuweza kukamilisha kazi inayotakiwa ikamilike.

#ElimikaWikiendi

🔸Reasoning processes
Hapa program ya AI inachagua algorithm sahihi ili kufikia lengo linalotakiwa

🔸Self-correction processes
Hii sehemu imeundwa kwenye program ya AI kuweza kuitayarisha vizuri algorithms na kuhakikisha zinatoa matokeo sahihi zaidi iwezekanavyo
#ElimikaWikiendi

AI imegawanyika katika makundi mawili (Weak na Strong AI)

Weak Artificial
Hii inapatiwa uwezo wa kufanya kazi moja kama ilivyo Siri ya Apple, Google assistant, Cortana, Alexa au Ella ya Tecno hapa unamuuliza swali anakujibu kulingana na maulizo yako

#ElimikaWikiendi

Strong Artificial

Hii inapatiwa uwezo mkubwa kama ilivyo akili ya binadamu ambapo inaweza kutatua tatizo gumu bila binadamu kuingilia/kusaidia. Mfano Machine zinazotumika hospitali kwenye vyumba vya operesheni, hizo ni Strong AI

#ElimikaWikiendi

AI INATUMIKA WAPI?

🔸Huduma za afya

Kwa miaka ya hivi karibuni hii Teknolojia imepokelewa vizuri sana kwenye hii sekta ya afya. Zimetengenezwa mashine zenye uwezo mkubwa wa kutambua ugonjwa zaidi ya akili ya binadamu pia zinapunguza gharama za mgonjwa.

#ElimikaWikiendi

Teknolojia inayojulikana sana kwenye hii nyanja inaitwa IBM Watson Healthcare AI. Hii system inachimba taarifa za mgonjwa na vyanzo vingine na kutengeneza hypothesis tuseme ni Nadharia au Maelezo ya hizo taarifa na namna ya kutibu

#ElimikaWikiendi

🔸Elimu

Hii Teknolojia itakuja kuchukua nafasi ya waalimu kutokana na namna inavyookoa muda na kupunguza gharama. Siyo jambo zuri kwenye suala la Ajira na pia ni zuri kwenye uboreshaji na utoaji wa Elimu.

#ElimikaWikiendi

Artificial Intelligence ina uwezo wa kuandaa masomo, kufundisha Darasani, kujibu maswali, kutunga Mitihani, kusahihisha Mitihani, Ku-grade matokeo na kutoa Reports. AI ina uwezo wa kutambua uwezo/uelewa wa kila Mwanafunzi

#ElimikaWikiendi

🔸Kwenye Sheria
Sifa ya hii Teknolojia inaokoa muda na inamboreshea mteja huduma, kuna baadhi ya wanasheria wamekwisha anza kusifia uwezo wa hizi mashine katika kutabiri matokeo.

Tumeona hivi karibuni kuna Roboti wakili ametengenezwa, inauwezo wa kuandaa Ripoti na kusimamia kesi kama ilivyo kwa binadamu, pia AI inasadia idara za usalama kukamata wahalifu, kutambua kama kuna ajali inatokea sehemu flani n.k

#ElimikaWikiendi

🔸Social Media

Social Media hutumia AI Tools kukusanya na Kutambua taarifa za watumiaji, Matangazo kwenye Social Media hutumia AI ili kumfikia mlengwa kulingana na sehemu alipo, kama uko Tanzania utaona matangazo ya Tz tu na baadhi ya vitu unapenda kufanya

#ElimikaWikiendi

AI inakusoma nini unapenda kuangalia kwenye Mtandao, mfano YouTube inakupa Suggestion videos kulingana na Search zako etc

Makampuni yanatumia Chatbots kuwasiliana na wateja wake 24/7, kuna Automated Content creator kutengeneza na ku-manage contents za makampuni

#ElimikaWikiendi

🔸Usafirishaji
Huku hii Teknolojia imepiga hatua kubwa sana sasa kuna magari yanayojiendesha yenyewe, traffic controller 🚥, kutambua muda wa ndege kutua na kuboresha usalama wa usafiri wa maji.

#ElimikaWikiendi

🔸 Huduma za kibenki

Inasahidia kurahisisha customer care kwa wateja mfano Chatbot, kutambua na kutunza taarifa zote za mteja kwa muda mfupi na kutoa muongozo. Kuzuia/kutambua wizi wa fedha, ku-verify malipo ya kibenki N.K, vitu vingi vya kibenki hulindwa na AI Softwares

🔸Viwandani

Huku pia AI inatumika sana, mfano viwanda vya vinywaji hutumia AI kuchanganya na kubalance ingradients etc, Viwandani hutumia AI kutengeneza na ku-process bidhaa kwa wakati, Hii inapunguza ajira maana kazi nyingi hufanywa na AI

#ElimikaWikiendi

🔸Kilimo

Kilimo cha sahihi hutumia teknolojia ya AI kusaidia kugundua magonjwa kwenye mimea, wadudu,na lishe duni ya mimea kwenye shamba. Teknolojia ya AI inaweza kugundua na kulenga magugu na kisha kuamua ni dawa gani inayoweza kutumika kwa usahihi

#ElimikaWikiendi

Kwenye maisha yetu ya kila siku tunatumia Artificial Intelligence, mfano unatumia Google Maps,Siri, Alexa au Cortana au Games kwenye vifaa vyako, Automatic Doors, Smart Home mfano Friji za kisasa unaweza ku-monitor hata kama uko mbali. AI imerahisisha vitu vingi

#ElimikaWikiendi

FAIDA ZA AI
🔸 Inaboresha upatikanaji wa huduma za kijamii.
🔸 Inapunguza gharama.
🔸 Inatoa ajira

HASARA ZA AI
🔸Usiri na Usalama wa taarifa za watu
🔸Gharama za kuweka mifumo
🔸Inapunguza ajira

#ElimikaWikiendi

AHSANTENI

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling