Utakubali kuhudumiwa na Muuguzi Roboti Hospitalini?
UVIKO-19 umebadilisha sana mwenendo wa maisha yetu ndani ya miaka 2 iliyopita. Nani aliwaza kwamba leo hii kufanya kazi kutoka nyumbani ingekuwa ni kitu kinachopewa kipaumbele hivi?
🧵
Katika jitihada za kuokoa maisha ya watu wengi zaidi duniani, tumeona uundaji wa roboti ambao wanachukua nafasi za wauguzi katika hospitali.
Kampuni ya Hanson huko Hong Kong imekuja na roboti huyu mwenye muonekano wa kibinadamu.
Amepewa jina la "Grace".
Hanson robotics kwa wale msioifahamu, ni kampuni ile ile ambayo ilimtengeneza Sophia. Roboti mmoja maarufu sana duniani.
Sophia alipewa uraia wa Saudi Arabia. Na sasa Hanson robotics wanatuletea Grace.
Grace atahusika zaidi kutoa huduma kwa wagonjwa wa UVIKO-19 hospitalini.
Grace ameunda kutoa huduma kwa wagonjwa waliopo karantini, hasa wazee. Amepewa uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja.
Miongoni mwa hizo lugha ni English, Mandarin na Cantonese. Pia anaweza endesha mazungumzo ya kumfanya mtu ajiskia vizuri na kuchora picha pia.
Kwa sasa Hanson Robotics wanategemea kuanza kumtengeza Grace kwa wingi zaidi na kuanza kumuuza huko China.
Gharama yake inatemewa kuto tofautiana sana na zile za gari za starehe, ambayo ni kati ya Tsh. 100mil na Tsh. 300mil.
Iwapo siku utafika muhimbili kupata matibabu na ukapewa Roboti huyu akuhudumie. Je, utakubali kupewa huduma yake?
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.