HabariTech Profile picture
Sep 1, 2021 6 tweets 2 min read Read on X
Utakubali kuhudumiwa na Muuguzi Roboti Hospitalini?

UVIKO-19 umebadilisha sana mwenendo wa maisha yetu ndani ya miaka 2 iliyopita. Nani aliwaza kwamba leo hii kufanya kazi kutoka nyumbani ingekuwa ni kitu kinachopewa kipaumbele hivi?

🧵
Katika jitihada za kuokoa maisha ya watu wengi zaidi duniani, tumeona uundaji wa roboti ambao wanachukua nafasi za wauguzi katika hospitali.

Kampuni ya Hanson huko Hong Kong imekuja na roboti huyu mwenye muonekano wa kibinadamu.

Amepewa jina la "Grace".
Hanson robotics kwa wale msioifahamu, ni kampuni ile ile ambayo ilimtengeneza Sophia. Roboti mmoja maarufu sana duniani.

Sophia alipewa uraia wa Saudi Arabia. Na sasa Hanson robotics wanatuletea Grace.

Grace atahusika zaidi kutoa huduma kwa wagonjwa wa UVIKO-19 hospitalini.
Grace ameunda kutoa huduma kwa wagonjwa waliopo karantini, hasa wazee. Amepewa uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja.

Miongoni mwa hizo lugha ni English, Mandarin na Cantonese. Pia anaweza endesha mazungumzo ya kumfanya mtu ajiskia vizuri na kuchora picha pia.
Kwa sasa Hanson Robotics wanategemea kuanza kumtengeza Grace kwa wingi zaidi na kuanza kumuuza huko China.

Gharama yake inatemewa kuto tofautiana sana na zile za gari za starehe, ambayo ni kati ya Tsh. 100mil na Tsh. 300mil.
Iwapo siku utafika muhimbili kupata matibabu na ukapewa Roboti huyu akuhudumie. Je, utakubali kupewa huduma yake?

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with HabariTech

HabariTech Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @HabariTech

Aug 30, 2022
⚡Unataka Kupunguza Muda Unaotumia kwenye Mitandao ya Kijamii? Soma Hii

Tunachoongelea ni mitandao ya kijamii. Huduma ambayo inafanya kazi yake vizuri mno.

Kazi yake ni kuhakikisha muda wote tunaangalia screen za simu zetu au PC.
⚡Wazo wa la kusema kwamba tunaweza kabisa kuacha mitandao ya kijamii, ni kama kuamini kwamba mwakani teknolojia ya time travel itakuwepo.

Ni ngumu na haiwezekani kuachana kabisa na mitandao ya kijamii, hivyo kilichobaki ni kujaribu kupunguza muda tunaotumia kwa kufanya haya.
1. Chagua siku moja kila wiki usiingie kabisa kwenye Mitandao ya kijamii

Ukisoma unaweza dhani ni rahisi kufanikisha hili jambo ila ni ngumu kama kushinda njaa zaidi ya siku mbili.
Read 19 tweets
May 31, 2022
🎭Kuona location, SMS & Calls bila yeye kujua

Unaweza kuhack simu/facebook/instagram ya mtu?

Bila shaka hili ni swali ambalo kila IT amewahi kusikia au kuulizwa yeye mwenyewe.

Kwanini watu wanatamani kuwafatilia ndugu/rafiki/wapenzi wao?
🎭Kisayansi hata mimi sijui. Binafsi nadhani ni hali tu ya ubinadamu kutaka kujua nini kinaendelea katika maisha mwingine.

Ni wazi kwamba binadamu tunapenda kuwa wa kwanza kujua kitu na kuwa juu kuzidi mwingine muda wote.
🎭Hii ni kwa sababu ya ubinafsi unaoishi ndani ya kila mmoja wetu.

Je, gharama ya kuwa na hali hii na kuingilia faragha ya mtu ni ipi?

Kulingana na sheria za mitandao za Tanzania “Cyber Act (2015)” ni kinyume cha sheria kutumia kifaa cha mawasiliano cha mtu bila ruhusa yake.
Read 5 tweets
Mar 15, 2022
🎁T O R R E N T S, Zinafanya vipi kazi?

Naweka dau langu kwamba ukisikia torrents, kitu kinakuja kichwani mwako ni software, video au audio za wizi (Pirated Files).

Uko sahihi lakini, torrent protocol haihusiana na hivyo tu.

#HabariTech
🎁Torrents ni nini?

Kwanini pirates wanatumia torrents kusambaza na kupakua files zao?

Huduma nyingine za internet zinazoendana na torrents kwanini hazitumiki katika sharing ya pirated files?

Haya maswali yote yanapatiwa majibu kupitia Bittorrent protocol.
🎁Unapofungua browser ili kuperuzi mtandao, browser inatuma request kwenda kwenye server yenye IP address ya website unayotaka kuifikia.

Request hii inaenda kuiomba server ikupe HTML za hiyo website ili uweze kuiona na kufanya kitu unataka.
Read 28 tweets
Mar 15, 2022
👽Russia hawataweza kuvuka vikwazo vya Teknolojia

24 February 2022, baada ya Russia kuvamia Ukraine, serikali ya Marekani ilitangaza vikwazo vya kwanza Russia.

Katika vikwazo hivyo vilikuwemo vinavyogusia teknolojia.

#HabariTech
👽Moja ya kikwazo kilisema, "Kuzuia zaidi ya nusu ya uagizaji wa Russia kuingiza teknolojia ya juu nchini mwao, Kuzuia Russia kupata pembejeo muhimu za kiteknolojia, Kudhoofisha msingi wao wa viwanda...
👽...na kudhoofisha matarajio ya kimkakati ya Russia ya kuwa na Ushawishi katika jukwaa la ulimwengu." -mwisho wa nukuu.

Inawezekana ilionekana ni kikwazo kikubwa kwa muda huo. Ila ni kidogo sana ukilinganisha na yaliyofata baada ya hapo.
Read 33 tweets
Mar 14, 2022
🍿Nini Kiliwakuta Founders wa Pirates Bay

Pirates bay ni kati ya website bora za kufanya piracy ya Games, Softwares, Movies, Music na aina nyingi ya files zinazokuwepo online.

Ni website ambayo iko kinyume na sheria za hakimiliki na haikutakiwa kuwepo.

#HabariTech
🍿Kampuni nyingi na wanasheria duniani wamejaribu sana kuhakikisha website hii haipatikani mtandaoni bila mafanikio.

Kwa kuwa content zinazokuwepo huko hazikutakiwa kuwepo na mara nyingi zinawakosesha mauzo kwa kuwa ni usambazaji wa content usio sahihi.
🍿Kuna miaka ya nyuma waliwahi fanikiwa kuiondoa online. Bahati mbaya mafanikio yao hayakudumu kwa muda mrefu.

Saa chache baada ya kuondolewa online website ya Pirates bay ilirudi online. Hivyo wakaona wabadili namna ya mashambulizi yao.
Read 41 tweets
Jan 24, 2022
🚀Sifa Kuu ya MATAPELI

Kwa sasa teknolojia imefanya kupata pesa iwe rahisi sana, lakini kupoteza ni rahisi zaidi 😁.

Kutapeliwa ni dakika 0.

Kila unapogusa mtandaoni sasa hivi kuna haya maneno NFT, Cryptocurrency, Bitcoin.

Lengo ni PESA.
🚀Bahati mbaya wengi mnaishia kuumia kwa sababu mnakosa maarifa.

Mnaingia kichwa kichwa katika biashara msizoelewa haswa ziko vipi.

Kwa sababu hiyo unajikuta unajitapeli wewe mwenyewe. Ulikosea mwanzo kutotaka kusoma inakuaje wengine wanapata faida.
🚀Siri kubwa ya matapeli hata sio kubwa kivile. Ila tu kwa kuwa wengi hatuumizi akili huwa tunaipita tu.

Tapeli guru kabisa ana siri moja.

Kipindi ambacho dhahabu inapatikana kwa wingi yeye huwa hajishughulishi na uchimbaji.

Image Credit: @MaujanjaCrypto
Read 9 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(