#TOTTechs 🇹🇿 Profile picture
Washauri na wataalamu wa Teknolojia || 💻 Computers ||📱 Phones || 🎮 Games ||🎯 Softwares || ⚙️ICT Hardwares || 🛡ICT Security || 📧tottechstz@gmail.com

Dec 18, 2021, 18 tweets

Wakati huu tunapo kwenda likizo za sikukuu za Christmas na mwaka mpya, huwa ni muda mzuri kukaa na familia zetu, ndugu, jamaa na marafiki kutafakari mwaka ulivyokuwa na kujiandaa na mwaka unaofuata.

#ElimikaWikiendi

STADI/SKILLS ZA MUHIMU KUJIFUNZA

UZI [THREAD] 👇

Pia ni kipindi ambacho watu wengi hupendelea kuwepo mitandaoni. Wakati unatumia mitandao ni vyema ukapata ujuzi mpya wa namna unaweza faidika na mitandao.

Tutakuelezea baadhi ya ujuzi wa mtandaoni unaoweza kuwa na faida kwako kwa namna moja ama nyingine.

#ElimikaWikiendi

ONLINE SHOPPING

huu ni ununuzi wa bidhaa na huduma mtandaoni bila ya wewe kuwepo katika duka au biashara husika kimwili.

Ni rahisi sana kujifunza namna ya kununua vitu mtandaoni kutoka sehemu yoyote ile Duniani na malipo hufanyika kwa njia ya mtandao.

#ElimikaWikiendi

HOME WIFI NETWORK

Inawezekana nyumbani kwako kuna shida ya mtandao hasa upande wa internet na kila mtu humo ndani analalamika kuhusiana na hili.

Home WiFi network ni mtandao ambao unakupa uwezo wa kupata internet kupitia kifaa kimoja kiitwacho router

#ElimikaWikiendi

Home wifi network unaweza kupata kwa urahisi kutoka kwa mtoa huduma ( Internet Service Provider) yeyote anayetoa huduma maeneo ya nyumbani kwako.

Mfano nunua WiFi Router na Modem kutoka TTCL, jifunze kuunganisha na vifaa vyako kama Simu, Computers, Smart TV

#ElimikaWikiendi

DIGITAL MARKETING

ni utangazaji wa bidhaa/huduma ya chapa/Brand Fulani kwa kuunganisha biashara hiyo na wateja kupitia internet na miundo mingine ya mawasiliano ya mtandao. Hii inahusisha utumiaji wa email, mitandao ya kijamii na mesejii.

#ElimikaWikiendi

Kwenye digital marketing unaweza kuwa unatangaza biashara yako au biashara ya mwingine na faida yako iko katika kipato utakachopokea kupitia matangazo hayo

• Content Marketing
• SEO
• Affiliate Marketing
• Pay-per-click Marketing
• Social Media Marketing

#ElimikaWikiendi

UI/UX DESIGNING

Websites na apps zote unazoziona hazikuundwa tu hivi hivi. Kuna watu wenye ujuzi wa kufanya designing tunaowaita UI/UX designers.

Watu hawa huwa na ujuzi wa kuandaa michoro au designs za namna muonekano uwe ili kurahisisha utumiaji wa mfumo

#ElimikaWikiendi

Na kumshawishi mtumiaji kuendelea kutumia mfumo huo.

UI/UX haikuhitaji kuwa na elimu tofauti na uelewa wa watu wanatumia vipi simu/PC zao na kutengeneza muonekano mzuri wa system unaoshawishi mtu kutumia.

Unaweza kujifunza UI/UX Designing kupitia mtandao

#ElimikaWikiendi

BORESHA USALAMA

Kipindi cha sikukuu kubwa kama hizi za Christmas na Mwaka mpya, huwa kuna uhalifu kwa kiwango kikubwa hasa wizi manyumbani na biashara. Hii ni kwasababu watu wengi husafiri na kuacha biashara zao bila usalama wa kutosha.

#ElimikaWikiendi

Boresha usalama wa nyumbani au biashara yako kwa kufunga CCTV cameras, Alarm systems, Funga taa janja zinazajiwasha giza linapoingia, kuwa makini na vitu unapost mtandaoni na usiache ishara yoyote kwamba umesafiri

#ElimikaWikiendi

BLOCKCHAIN, NFT & CRYPTOCURRENCIES

Dunia ya leo ni tofauti na dunia ya miaka ya 1980's, tupo kwenye digital/Information age ambapo mambo mengi yanafanyika kupitia mtandao. Kuanzia kuwasiliana, ununuzi na malipo ya bidhaa, usafirishaji, Masomo mtandaoni etc

#ElimikaWikiendi

Tukiangalia kwa Amazon pekee, zaidi ya Packages million 1.6 hununuliwa kwa siku, zaidi ya Order 66,000 kwa saa, na kuna wauzaji wa kujitegemea zaidi ya 9.1 Million Duniani, kwahiyo unaweza kuona Pesa inayozunguka Mtandaoni

#ElimikaWikiendi

Tupo kwenye Dunia ya Digitali na malipo kwenye baadhi ya huduma yanafanyika kwa Fedha ya mtandaoni, ni muhimu sana kwa sasa kujifunza au kuwa na uelewa wa Cryptos, NFT na Blockchain maana tunakoelekea itakulazimu kuzitumia kulingana na ushawishi mkubwa wa soko la mtandaoni

INTERNET OF THINGS (IoT)

Teknolojia inakua na matumizi ya internet yanaongezeka, vifaa vinavyotengenezwa sasa ni "Smart Devices" Je uliwahi kufikiri kama unaweza kuunganisha Jokofu/Friji na simu yako ya mkononi, unaweza kuzima au kuwasha TV hata kama uko mbali?

#ElimikaWikiendi

Umewahi kufikiria kama unaweza kupata taarifa zote za gari yako kupitia simu yako? Yote hayo yanafanyika sababu ya Internet of Things ( IoT ), Internet of Things maana yake "Everything is Connected" Jifunze namna IoT inavyofanya kazi uendane na dunua ya leo

#ElimikaWikiendi

GRAPHICS

Hapo awali watu wengi waliamini ili kujifunza Graphic designing lazima uwe umesomea IT, lakini nikwambie kitu mtu yeyote anaweza kujifunza designing, Dunia inahamia mtandaoni hasa upande wa Biashara ni muhimu kuwa na uelewa/skills za Graphics

#ElimikaWikiendi

Kuna Tools ambazo unaweza kuanza nazo na unaweza kutumia hata simu yako ya mkononi endapo kama hauna Computer, baadhi ya hizo tools

• Canva
• Pixlr
• Affinity Designer
• Figma
• Fotor
• Adobe Photoshop

Zipo nyingi ila unaweza kuanza na hizo.

#ElimikaWikiendi

SHARE

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling