Wakati huu tunapo kwenda likizo za sikukuu za Christmas na mwaka mpya, huwa ni muda mzuri kukaa na familia zetu, ndugu, jamaa na marafiki kutafakari mwaka ulivyokuwa na kujiandaa na mwaka unaofuata.
Pia ni kipindi ambacho watu wengi hupendelea kuwepo mitandaoni. Wakati unatumia mitandao ni vyema ukapata ujuzi mpya wa namna unaweza faidika na mitandao.
Tutakuelezea baadhi ya ujuzi wa mtandaoni unaoweza kuwa na faida kwako kwa namna moja ama nyingine.
ni utangazaji wa bidhaa/huduma ya chapa/Brand Fulani kwa kuunganisha biashara hiyo na wateja kupitia internet na miundo mingine ya mawasiliano ya mtandao. Hii inahusisha utumiaji wa email, mitandao ya kijamii na mesejii.
Kwenye digital marketing unaweza kuwa unatangaza biashara yako au biashara ya mwingine na faida yako iko katika kipato utakachopokea kupitia matangazo hayo
• Content Marketing
• SEO
• Affiliate Marketing
• Pay-per-click Marketing
• Social Media Marketing
Na kumshawishi mtumiaji kuendelea kutumia mfumo huo.
UI/UX haikuhitaji kuwa na elimu tofauti na uelewa wa watu wanatumia vipi simu/PC zao na kutengeneza muonekano mzuri wa system unaoshawishi mtu kutumia.
Kipindi cha sikukuu kubwa kama hizi za Christmas na Mwaka mpya, huwa kuna uhalifu kwa kiwango kikubwa hasa wizi manyumbani na biashara. Hii ni kwasababu watu wengi husafiri na kuacha biashara zao bila usalama wa kutosha.
Boresha usalama wa nyumbani au biashara yako kwa kufunga CCTV cameras, Alarm systems, Funga taa janja zinazajiwasha giza linapoingia, kuwa makini na vitu unapost mtandaoni na usiache ishara yoyote kwamba umesafiri
Dunia ya leo ni tofauti na dunia ya miaka ya 1980's, tupo kwenye digital/Information age ambapo mambo mengi yanafanyika kupitia mtandao. Kuanzia kuwasiliana, ununuzi na malipo ya bidhaa, usafirishaji, Masomo mtandaoni etc
Tukiangalia kwa Amazon pekee, zaidi ya Packages million 1.6 hununuliwa kwa siku, zaidi ya Order 66,000 kwa saa, na kuna wauzaji wa kujitegemea zaidi ya 9.1 Million Duniani, kwahiyo unaweza kuona Pesa inayozunguka Mtandaoni
Tupo kwenye Dunia ya Digitali na malipo kwenye baadhi ya huduma yanafanyika kwa Fedha ya mtandaoni, ni muhimu sana kwa sasa kujifunza au kuwa na uelewa wa Cryptos, NFT na Blockchain maana tunakoelekea itakulazimu kuzitumia kulingana na ushawishi mkubwa wa soko la mtandaoni
INTERNET OF THINGS (IoT)
Teknolojia inakua na matumizi ya internet yanaongezeka, vifaa vinavyotengenezwa sasa ni "Smart Devices" Je uliwahi kufikiri kama unaweza kuunganisha Jokofu/Friji na simu yako ya mkononi, unaweza kuzima au kuwasha TV hata kama uko mbali?
Umewahi kufikiria kama unaweza kupata taarifa zote za gari yako kupitia simu yako? Yote hayo yanafanyika sababu ya Internet of Things ( IoT ), Internet of Things maana yake "Everything is Connected" Jifunze namna IoT inavyofanya kazi uendane na dunua ya leo
Hapo awali watu wengi waliamini ili kujifunza Graphic designing lazima uwe umesomea IT, lakini nikwambie kitu mtu yeyote anaweza kujifunza designing, Dunia inahamia mtandaoni hasa upande wa Biashara ni muhimu kuwa na uelewa/skills za Graphics
Hivi karibuni tumeona matukio ya simu kulipuka zikiwemo simu za Oneplus Nord 2, Galaxy Note 7 na
baadhi ya simu ya nyingi zikiwemo simu kutoka kampuni ya iPhone, Oppo, Xiaomi, Vivo, n.k
Powered by #ElimikaWikiendi × @fiidzsocial
UZI MFUPI 👇
Kati ya matukio makubwa ya simu kulipuka ilikuwa ni simu za
Galaxy note 7 hii ilipelekea Samsung kuomba simu hizo zirudishwe kiwandani kwa uchunguzi zaidi.
Matukio ya simu kulipuka yanajirudia kila siku japo kuna makosa ya kiufundi makosa na mtumiaji.
#ElimikaWikiendi
SABABU KWANINI SIMU ZINALIPUKA.
1. Kasoro za utengenezaji.
Moja ya sababu au kasoro inayofanya simu zilipuke ni kutoka kwa watengezaji (kiwandani), Betri ya Lithium-ion ambayo hutumika kwenye smartphone inahitaji kujaribiwa vizuri kabla kusafirishwa.
• Kama wewe ni Fan/shabiki wa kitu au kampuni flani, unatakiwa ujue kuheshimu mawazo ya watu wengine, unatakiwa ujue kutofautisha kizuri na kibaya, unatakiwa ujue kutofautisha Facts/ukweli na Opinions/maoni. 👇
• Acha kuhoji na kubeza maamuzi ya watu, ingawa unaweza kutoa maoni yako kuhusu maamuzi yao.
• Unapoibeza kampuni nyingine kwa kufanya kitu, lakini unatetea kampuni unayoipenda kwa kufanya kitu kile kile, hiyo inamaanisha WEWE ndiye tatizo.
• Wakati mtu X anakejeli kikundi cha watu flani, usitarajie hicho kikundi cha watu kusema kitu cha busara kujibu taarifa ya mtu X.
• Unapomwambia mtu jambo la hovyo/ajabu usitegemee kukuheshimu au kupata majibu ya heshima kutoka kwake
Watu wengi wakiona neno AI ( Artificial Intelligence) hufikiria moja kwa moja ni roboti. Ili iwe AI inahitaji Software(Program endeshi) na Hardware. Software ndio kama ubongo unahitaji kupachikwa data ambazo zitakuwa zinatoka command/maelekezo kwenye hardware.
AI ina jifunza (learning), Fikiri (reasoning) na mtazamo (perception). Ndivyo hivyo sehemu ya akili ya binadamu inafanya kazi. Kwa miaka ya sasa hii Teknolojia inakuwa kwa kasi sana.
Imefikia hatua wataalamu wanataka AI iwe na uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi kama mwanadamu,
Bitcoin ni toleo la pesa taslimu ya ki-mtandao ( peer-to-peer version of electronic cash ) ambayo unaweza kutuma moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine pasipo kupitia taasisi za fedha kama benki, Mobile money etc, unahitaji kuwa na internet tu
Kitu muhimu kwenye Bitcoin huwezi kugushi/forge, miamala fake haiwezi kufanyika, siyo lazima uwe na kitambulisho cha Taifa ( National ID) wala Bank account, Bitcoin iko decentralized ( imegawanyika ), mwamala ukifanyika hauwezi kubadilishwa na ina ulinzi sana
Je! Unampango wa kununua MacBook mpya? Kabla ya kufanya ununuzi unahitaji kuielewa MacBook.
Aina nyingi za MacBook zinapatikana sokoni. Tutakusaidia kununua MacBook bora kulingana na mahitaji yako
Uzi mfupi 👇
Kabla ya kufanya ununuzi wowote angalia toleo la MacBook ambalo utaenda kununua. Kila Mwaka Apple hutoa toleo jipya la MacBook, unaweza kutembelea Apple’s official website, news, na social media kujua mda ambao Apple watatoa toleo Jipya
AINA ZA MacBook:
Kuna aina mbili za MacBook, MacBook Pro na MacBook Air: MacBook Air ni Nyembamba, nyepesi na ni rahisi kusafiri nayo wakati MacBook Pro ni nene kidogo.
Zote ni nzuri lakini zina utofauti sana kwenye Miundo ya ndani ( Internal Architecture & Specs)
Tesla Motors ni moja ya kampuni zenye ubunifu zaidi katika magari. Elon Musk, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo kwa sasa ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni. Hivi karibuni, C.E.O wa Tesla na SpaceX alisema kwamba alijaribu kuuza kampuni yake ya gari kwa Apple 👇
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Apple, Tim Cook aliripotiwa kukataa kupanga mkutano kujadili ofa hiyo. Hiyo ilibainika baada ya Musk Ku-tweet kwenye Page yake juzi alipoulizwa na Mwandishi wa BBC Kuhusu Habari iliyovuma kuwa alitaka kuwa CEO wa Apple mwaka 2016
Kulingana na ripoti hiyo, Elon anadai kwamba hakuwahi kuzungumza na wala kumwandikia Tim Cook. Lakini bilionea huyo alisema aliwahi kuomba mkutano kati yake na Tim Cook juu ya Apple kuichukua Tesla, na hakupata majibu yoyote wala mkutano haukufanyika.