Costantine Profile picture
Laboratory scientist | Found by Jesus Christ,

Dec 30, 2021, 11 tweets

👨🏿‍🎓TEKNOLOJIA 5(tano) ZILIZOLETWA NA UJIO WA COVID-19 DUNIANI .

Ujio wa Covid-19 duniani unalazimisha idadi kubwa ya nchi kuanza kutumia teknolojia tano(5) muhimu ambazo zina athiri utendaji kazi wa watu moja kwa moja huku idadi kubwa ya ajira tulizo zizoea zikipotea ifikapo2025

Jitahidi kuzisoma hizi nyuzi maana zimebeba mambo muhimu sana yatakayo kusaidia kufanya maamuzi mazuri juu ya skills gani unatakiwa kuwa nazo na ni fani gani umshauri mdogo wako au mtoto wako ama ndugu yako ambazo zitakua na soko miaka ijayo

Zifuatazo ni Teknolojia 5 muhimu

1. Artificial Intelligence (AI) and Machine Learning

Ikiwa na maana ya uwezo wa computer 💻 ama 🤖 robot kufanya kazi ambazo ilitakiwa zifanywe na binadamu teknolojia hii ina lenga kupunguza msongamano wa watu kwenye taasisi ,hapa computer inakua na uwezo wa kujifunza kila siku

tabia tofauti tofauti ambazo wateja wanaonesha,baadhi ya nchi zimeanza kutumia teknolojia hii na ajira nyingi sana za watu kwenye malls,hotels,industries zimepungua na kutoa ajira nyingi sana kwa fani zifuatazo.

-AI Research Scientist
-AI Engineer
-Machine Learning Engineer

-AI Architect

2.Robotic Process Automation (RPA)
Chuo alichosoma kaka @JemsiMunisi wana upiga mwingi sana wako mbele ya dunia 😇 pale kuna fani inaitwa automation engineering

Teknolojia hii haiendi mbali sana na AI maana hapa kazi nyingi zinakua automated

Ikiwemo kujibiwa emails na 🤖 robot,kufanya business advertisement,kuchakata miamala,na shuguli zenye kujirudia rudia mfano shuguli za viwandani nyingi sana zitakua automated na kundi kubwa la watu kupoteza ajira

Ajira zitakazo zaliwa
-RPA Developer
-RPA Analyst
-RPA Architect

3. Block chain
Ni mfumo wa uhifadhi taarifa za miamala ambao ni ngumu kubadili taarifa zilizo hifadhiwa,ni ngumu kwa hacker ama cheater kuweza kuingilia taarifa za miamala kwenye block chain maana hapa kila muamala utakao fanyinka kila block inatunza kumbukumbu zake

Mfano wa block chain ni Bitcoin na Ethereum ambazo zinaendelea kukua kwa kasi kubwa sana ,hii pia inasaidia ulinzi kua mkubwa kwenye miamala

Hapa kuna ajira kama

-Risk Analyst
-Tech Architect
-Crypto Community Manager
-Front End Engineer
Zinazaliwa

4. Internet of Things (IoT)
Vitu vingi kwa sasa vinatengenezwa vikiwa na wi-fi ikiwa na maana ya vtu vingi sasa vitaweza kuunganishwa na internet mfano vitu vya nyumbani,magari yetu,watu wanaweza kufunga milango ya majumba yao wakiwa mbali,watu wanaweza kuwasha majiko yao

Wakiwa njiani kuelekea nyumbani ili kufaidi ajira kwenye hii teknolojia utatakiwa kujifunza vtu kama

-Information security,
-AI and machine learning
-networking,
-hardware interfacing,
-data analytics,
-automation engineering

5.5G(fifth generation wireless)
Teknolojia hii imeletwa kwa lengo la kuongeza speed kwenye upatikanaji wa taarifa kutoka kwenye internet mtu asitumie muda mrefu akisubiri taarifa,hii itasaidia Vitu vingi vilivyo na internet access kuweza kuwasiliana kwa uharaka zaidi

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling