THIS CASE IS VERY COMPLICATED
Kwenye kesi za mauaji, ili kufikia hukumu ya haki, mahakama hutaka kujiridhisha kama elements mbili zimethibitishwa bila kuacha shaka.
1. Actus reus/ Tendo ovu (lazima liwe limetendeka)
2. Mens rea /dhamira ovu.
Dhamira ovu inaangaliwa kwenye angle mbalimbali...
Kwenye kesi hii naangazia matendo ya mshtakiwa kabla na baada ya kitendo kiovu.
Utetezi wake ungekuwa na nguvu sana, lakini matendo yake yalitia shaka.
Hapa namuongelea DAUDI KAPEJA.
Fatilia mkasa huu,
👇
19/04/2014 UYUI, TABORA
Majira ya saa 4 usiku, BARESA RASHID aliambatana na DAUDI KAPEJA nyumbani kwake ambapo alichukua jacket na kumuaga mkewe kuwa wanakwenda kumuona jamaa aitwaye JUMA BUSEGA ili kufanya biashara ya tumbaku.
Wanatumia pikipiki mali ya BARESA RASHID
BARESA RASHID tena hakurudi nyumbani kwake usiku ule,
Baadae, mkewe ZAMDA ISSA akapewa taarifa za mwili wa mmewe kuokotwa pamoja na mwili wa mke wa JUMA BUSEGA yule yule ambaye marehemu mumewe na DAUD KAPEJA walisema wanaenda kufanya nae biashara ya tumbaku.
Maiti za watu hawa wawili zilikutwa kwenye vichaka katikati ya vijiji vya UFULUMA na MABAMA
Pikipiki ya BARESA RASHID ilikuwa pembeni yao huku miili yao ikiwa na majeraha sehemu mbalimbali.
Taarifa ile ikawafikia polisi
Usiku ule ule ikaanza nusa nusa
Ikiwa sasa siku imeshapinduka, tarehe 20/04/2014 ikafika pale timu ya makachero watatu waliotumwa na OC-CID msaidizi wa Uyui
Hawakuwa peke yao bali waliambatana na daktari kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu.
Jumla ya watu hawa wanne, kila mtu alikuwa na majukumu yake
1.Askari G.348 Detective Corporal OMARY MATESA ndiye alikuwa mpelelezi wa shauri hili.
2. G. 4876 Detective Corporal MATIKU alienda kuchora ramani ya eneo la tukio.
3. G.2269 D/Corporal RAJAB alikuwa na jukumu la kuimarisha ulinzi.
4. Dr. SINDABAKILA SEREJIO ailenda kufanya uchunguzi wa kitaalamu wa chanzo cha kifo akitokea hospitali ya wilaya ya Uyui.
Kwa mujibu wa daktari, ripoti yake ilisema maiti ya mwanaume ilikuwa na “fracture” kichwani ambapo mfupa wa “parietal” ulikuwa umevunjika kutokana na kupigwa na kitu kizito na kuvuja kwa damu.
Ripoti hii ilipelekwa kwa District Medical Officer
Lakini ripoti ilikuwa kimya juu ya maiti ya mwanamke.
Kwa nini?
Tutaona mbele ya safari....
.................................................
Katika nusanusa makachero wakabaini yafuatayo juu ya maisha ya nyuma ya marehemu BARESA baada ya kumuhoji mkewe,
BARESA alikuwa na mke mwingine mkubwa ambaye walikuwa na ugomvi naye.
Chanzo cha ugomvi ni kwamba marehemu alishamfumania mkewe akifanya “horizontal Engineering”na mtu aitwaye NDEBILE
Mwanamke huyu alishaondoka muda mrefu na hajulikani aliko.
Don’t you smell something?
Mtu pekee ambaye makachero walielekeza kwake vidole vya tuhuma ni alikuwa ni DAUD KAPEJA
Kwa sababu ndiye alikuwa the only last person known to be seen with the deceased.
Yes! Alikuwa ndiye mtu pekee aliyeonekana kwa mara ya mwisho na marehemu.
Msako dhidi yake ukaanza.
Hakuonekana eneo la tukio wala msibani
Baadae zikaja taarifa mpya kutoka kwa kichomi zikisaga kunguni.
Kichomi huyu ni JUMA BUSEGA yule yule ambaye marehemu na DAUDI walisema wanaenda kwake on the fateful night.
Infomer huyu unamwamini ndugu msomaji?
Sogelea telegram link 👇
t.me/fbuyobe
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.