Fortunatus Buyobe Profile picture
Jan 24, 2022 14 tweets 4 min read Read on X
THIS CASE IS VERY COMPLICATED

Kwenye kesi za mauaji, ili kufikia hukumu ya haki, mahakama hutaka kujiridhisha kama elements mbili zimethibitishwa bila kuacha shaka.

1. Actus reus/ Tendo ovu (lazima liwe limetendeka)

2. Mens rea /dhamira ovu. Image
Dhamira ovu inaangaliwa kwenye angle mbalimbali...

Kwenye kesi hii naangazia matendo ya mshtakiwa kabla na baada ya kitendo kiovu.

Utetezi wake ungekuwa na nguvu sana, lakini matendo yake yalitia shaka.

Hapa namuongelea DAUDI KAPEJA.

Fatilia mkasa huu,

👇 Image
19/04/2014 UYUI, TABORA

Majira ya saa 4 usiku, BARESA RASHID aliambatana na DAUDI KAPEJA nyumbani kwake ambapo alichukua jacket na kumuaga mkewe kuwa wanakwenda kumuona jamaa aitwaye JUMA BUSEGA ili kufanya biashara ya tumbaku.

Wanatumia pikipiki mali ya BARESA RASHID Image
BARESA RASHID tena hakurudi nyumbani kwake usiku ule,

Baadae, mkewe ZAMDA ISSA akapewa taarifa za mwili wa mmewe kuokotwa pamoja na mwili wa mke wa JUMA BUSEGA yule yule ambaye marehemu mumewe na DAUD KAPEJA walisema wanaenda kufanya nae biashara ya tumbaku. Image
Maiti za watu hawa wawili zilikutwa kwenye vichaka katikati ya vijiji vya UFULUMA na MABAMA

Pikipiki ya BARESA RASHID ilikuwa pembeni yao huku miili yao ikiwa na majeraha sehemu mbalimbali.

Taarifa ile ikawafikia polisi

Usiku ule ule ikaanza nusa nusa
Ikiwa sasa siku imeshapinduka, tarehe 20/04/2014 ikafika pale timu ya makachero watatu waliotumwa na OC-CID msaidizi wa Uyui

Hawakuwa peke yao bali waliambatana na daktari kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu.

Jumla ya watu hawa wanne, kila mtu alikuwa na majukumu yake
1.Askari G.348 Detective Corporal OMARY MATESA ndiye alikuwa mpelelezi wa shauri hili.

2. G. 4876 Detective Corporal MATIKU alienda kuchora ramani ya eneo la tukio. Image
3. G.2269 D/Corporal RAJAB alikuwa na jukumu la kuimarisha ulinzi.

4. Dr. SINDABAKILA SEREJIO ailenda kufanya uchunguzi wa kitaalamu wa chanzo cha kifo akitokea hospitali ya wilaya ya Uyui. Image
Kwa mujibu wa daktari, ripoti yake ilisema maiti ya mwanaume ilikuwa na “fracture” kichwani ambapo mfupa wa “parietal” ulikuwa umevunjika kutokana na kupigwa na kitu kizito na kuvuja kwa damu.

Ripoti hii ilipelekwa kwa District Medical Officer Image
Lakini ripoti ilikuwa kimya juu ya maiti ya mwanamke.

Kwa nini?

Tutaona mbele ya safari....

.................................................

Katika nusanusa makachero wakabaini yafuatayo juu ya maisha ya nyuma ya marehemu BARESA baada ya kumuhoji mkewe,
BARESA alikuwa na mke mwingine mkubwa ambaye walikuwa na ugomvi naye.

Chanzo cha ugomvi ni kwamba marehemu alishamfumania mkewe akifanya “horizontal Engineering”na mtu aitwaye NDEBILE

Mwanamke huyu alishaondoka muda mrefu na hajulikani aliko.

Don’t you smell something? Image
Mtu pekee ambaye makachero walielekeza kwake vidole vya tuhuma ni alikuwa ni DAUD KAPEJA

Kwa sababu ndiye alikuwa the only last person known to be seen with the deceased.

Yes! Alikuwa ndiye mtu pekee aliyeonekana kwa mara ya mwisho na marehemu.

Msako dhidi yake ukaanza. Image
Hakuonekana eneo la tukio wala msibani

Baadae zikaja taarifa mpya kutoka kwa kichomi zikisaga kunguni.

Kichomi huyu ni JUMA BUSEGA yule yule ambaye marehemu na DAUDI walisema wanaenda kwake on the fateful night.

Infomer huyu unamwamini ndugu msomaji? Image
Sogelea telegram link 👇

t.me/fbuyobe

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Fortunatus Buyobe

Fortunatus Buyobe Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @fbuyobe

Aug 2
Una uhakika kuwa wewe binafsi ulionana na IGP Sirro?

Unaweza kunieleza kwa ushaidi ni mara ngapi na wapi ulionana naye?

Unajua kuwa tuhuma unazotoa ni nzito ukihusisha watu wakubwa sana nchini?

Ilikuwa zamu yangu kuanza kumhoji mwanamama Jeannie Pollaert raia wa Netherlands Image
Nililazimika kumuuliza mama huyu maswali haya usiku wa manane baada ya kumaliza kusoma makabrasha mengi aliyonitumia kwa njia ya barua pepe.

Nilichokikuta ndani ya makabrasha yale kilifanya usingizi uliokwishaanza kunitongoza utoweke

Infact niliogopa sana

Nilihitaji ushaidi Image
Itakuwaje endapo Simon Sirro atakana kuwahi kukutana na wewe na kufanya na wewe kikao chochote?

Lilikuwa swali langu la kwanza.

Jeannie: Itakuwa vigumu sana kwa Sirro kukataa kuwa hajakutana nami

Akanipa ushaidi wa mawasiliano yao na jinsi Sirro alivyomjibu Image
Image
Read 25 tweets
Jun 27
Mwaka 2012, Blandine Nyoni akiwa katibu mkuu wizara ya afya, alinukuliwa akitoa kauli tata ya kuwabeza madaktari kuwa "wanajiona bora wakati ni wachafu na hawajui kiingeleza" Image
Katibu huyu akaendelea kusema kuwa hata yeye alisoma mchepuo wa PCB na kufaulu vizuri tu lakini kwa kutambua ubovu wa Medicine mzazi wake akamsomesha Accounts so hajui madaktari wanalalamikia nini.

Kauli hii ikang'oa kilaka kwenye jeans ya bishoo! Image
Ni kwamba mwaka huo, madaktari walikuwa katikati ya mgomo wa kihistoria

Kauli hii ikawatibua madaktari wakalianzisha upyaaaaa

Uzi👇

Dr. Ulimboka and total tools down

Nisome Image
Read 76 tweets
May 9
Wiki hii tumeshuudia waliokuwa wanachama wa Chadema wakitangaza kuachana na chama hicho huku wakiahidi kuelezea hatima zao za kisiasa siku za mbeleni

Kati ya waliohama ni waliowahi kuwa viongozi waandamizi wa chama hicho

Hii inamaanisha nini? Image
Kabla sijajibu swali hilo ni vyema tukipitia kwa ufupi mtiririko wa matukio (A quick refresher)

1. Dec 12,2024, Tundu Lissu anatangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA taifa

Nia hii ya Lissu ilikuja baada ya kuwa uchokozi wa wazi dhidi yake ndani ya chama Image
Kabla ya uamuzi huu, Lissu aliyekuwa ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA, alishamwandikia barua katibu mkuu wake kumjuza nia yake ya kuendelea kugombea kubaki kwenye nafasi hiyo.

Ulikuwa ni utaratibu wa CHADEMA kwa viongozi wa juu kutoshindania nafasi moja endapo mmoja ataonesha nia Image
Read 34 tweets
Mar 12
Monday, 24th,
June 1996 10:30 AM
Central Police post, Dsm

Majira ya saa nne asubuhi, anaingia kituoni hapa mfanyabiashara mwenye asili ya Asia ndugu Walji D Ladwa

Hapa kafika ili kutoa taarifa juu ya kuibiwa kwa gari lake lenye namba za usajili TZG 50

THREAD👇👇 Image
Bwana Ladwa alidai gari lililoibiwa ni Nissan Patrol lenye namba nyeupe.

Polisi katika upelelezi wao wakatajiwa kuwa gari ile imeonekana akiwa nayo jambazi mmoja sugu sana ambaye alikuwa kwenye radar za polisi kwa muda mrefu. Image
Jambazi huyu si mwingine bali ni Ernest Joseph Sambua Mushi maarufu kwa jina la White

Taarifa zikadokeza jambazi lile lipo mkoni Kilimanjaro kwa wakati ule

Yule mfanyabiashara akajulishwa juu ya hili na akatoa gari lake na dereva ili kwenda Kilimanjaro

Gari namba TZB 7209 Image
Read 13 tweets
Mar 11
Jan 22, 2024 kwenye kikao cha baina ya CDF na makamanda kwa upande mmoja, na Amiri Jeshi mkuu kwa upande mwingine,Mkuu wa majeshi alitoa kauli iliyoibua udadisi

"Kuna wakimbizi wameteuliwa serikalini kwenye nafasi za maamuzi"

Kauli hii ilikuwa ni nzito kutoka kwa mtu mzito. Image
Nasema mtu mzito kwa kuwa, mtu aliyetoa kauli hii ni mwenye nafasi ya kupata taarifa zote za intelejensia za nchi hii

Kwanza kama mwenyekiti wa kamati ya majeshi ya ulinzi

Pili akiwa kama kiongozi kwenye taasisi yenye chombo kinachofanya "military intelligence" siku zote. Image
Kwa hiyo CDF Mkunda alikuwa anajua anachokizungumza ni sahii kutoka vyanzo sahii

Undisputed and not farfetched facts

Kauli hii kwa mtu asiyeutumia ubongo wake vizuri, ataisoma tu kwenye magazeti na kuachana nayo bila kuusumbua ubongo kuona yale yasiyoonekana. Image
Read 28 tweets
Feb 25
Kumekuwepo na taarifa za kukamatwa kwa wahusika wa kampuni ya LEO BENEATH LONDON (LBL) inayoendesha biashara ya upatu, kukusanya amana, na kutoa riba kwa wanachama wake.

Victims wengi wa kampuni hii wakiwa ni watumishi wa kada ya ualimu Image
Image
Image
Pia Benki kuu imetoa taarifa ya kutoitambua wala kuipatia leseni kampuni hiyo.

Hapa ndipo napata maswali kuhusu umakini wa taasisi zetu zinazohusika na ukusanyaji wa taarifa za kiitelejensia

Taasisi hizi huwa hazipati fununu ya uwepo wa kampuni hizi kabla watu hawajatepeliwa? Image
Sasa hivi kuna kampuni nyingine inayojiita FIC

Kampuni hii inajinadi kuwa imesajiliwa BRELA na kupata cheti No. 177461385

Imepata TIN ya TRA No. 177-461-385 na kupewa cheti cha Tax Clearance Image
Image
Image
Read 8 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(