HabariTech Profile picture
Ulimwengu wa Teknolojia kiganjani mwako. #HabariTech

Jan 24, 2022, 9 tweets

๐Ÿš€Sifa Kuu ya MATAPELI

Kwa sasa teknolojia imefanya kupata pesa iwe rahisi sana, lakini kupoteza ni rahisi zaidi ๐Ÿ˜.

Kutapeliwa ni dakika 0.

Kila unapogusa mtandaoni sasa hivi kuna haya maneno NFT, Cryptocurrency, Bitcoin.

Lengo ni PESA.

๐Ÿš€Bahati mbaya wengi mnaishia kuumia kwa sababu mnakosa maarifa.

Mnaingia kichwa kichwa katika biashara msizoelewa haswa ziko vipi.

Kwa sababu hiyo unajikuta unajitapeli wewe mwenyewe. Ulikosea mwanzo kutotaka kusoma inakuaje wengine wanapata faida.

๐Ÿš€Siri kubwa ya matapeli hata sio kubwa kivile. Ila tu kwa kuwa wengi hatuumizi akili huwa tunaipita tu.

Tapeli guru kabisa ana siri moja.

Kipindi ambacho dhahabu inapatikana kwa wingi yeye huwa hajishughulishi na uchimbaji.

Image Credit: @MaujanjaCrypto

๐Ÿš€Ndio kama hiki kipindi cha miezi 5 iliyopita. Kulikuwa na kelele nyingi na crypto projects nyingi zilianzishwa.

Ila kuna mtu alisubiri mpaka aone wengine wanapost faida zao ili nae aanza jishughulisha.

๐Ÿš€BOOM alikula za uso ๐Ÿ˜

Tapeli mzuri hapo ambacho angefanya sio kuchimba dhahabu, yeye angeuza vifaa vinavyotumika kuchimba dhahabu.

Maana yake usiende kichwa kichwa kwenye hiyo biashara, soma kwanza uelewa vizuri.

๐Ÿš€Usiwe mtu wa 100,001 kununua Bitcoin kipindi wenzako wanaongelea sana.

Lazima utapata hasara. Ndicho kitu kimewakuta wengi sasa hivi.

Kipindi cha Gold Rush wewe kaa utulie soma mchezo unavyoenda alafu andaa strategy nzuri ya kuwekeza.

Content nimeiba kwa huyu jamaa ๐Ÿ˜

๐Ÿš€"Buy the Rumors, Sell the News"

"Nunua tetesi, uza habari"

Maana yake ni hii, kipindi kitu kinatangazwa sana ujue kishafika maturity unaweza pata hasara, hivyo siku zote nunua kipindi unasikia tetesi.

๐Ÿš€ ili kuelewa nitumie kauli ambayo @Raphahustler amewahi kuniambia. Aliniambia

"Ukiona Mtanzania anaisifu sana biashara ni nzuri achana nayo faida yake ni ndogo sana. Biashara ambayo Mtanzania anakwambia uachane nayo ndiyo huwa ina faida kubwa".

Tumia akili yako kuamua.

๐Ÿš€ Sasa kama umesoma mpaka hapa si ufanye ku RT tweet ya kwanza wengi wajue hii siri ya MATAPELI.

Alafu tuendelee kusoma magazine yenye madini mengi kupitia link hii habaritech.gumroad.com/l/habaritech3

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling