Coxstore  Profile picture
👨🏿‍🎓|Comp Engineer |Lab sc |Tech Reviewer | Found by Jesus Christ,

Jan 26, 2022, 9 tweets

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA MAAMUZI YA KUNUNUA TV(Television )📺 !

Cc @CoxstoreTz 🦅

Kutokana na uzi nilio andika jana kua na maswali mengi sana juu ya vitu kama smart tv,Android tv,UHD,FHD,4k,8k leo nitajubu maswali mengi sana kwenye huu uzi shuka nami 🧵

1.SMART TV AU ANDROID TV
Hapa nitakupa utofauti kati ya smart tv na android tv then wewe ndio utafanya uamuzi uchukue ipi.

Smart Tv -ama kwa jina jingine wanaita internet TV ni Tv yenye uwezo wa kuunganishwa na internet na hufanya kazi kuikaribia sana smartphone

Utofauti wake hii inakuja na already installed applications na huwezi ku download zingine maana haina playstore wala appstore faida ya smart tv ipo fast kuizidi android tv

Android Tv -ni aina ya smart tv ambayo inatumia os(operating system) ya android hii inakuja na playstore

Ambapo utaweza ku download application mpya unazo taka ila tu haipo fast ukilinganisha na normal smart tv.pia bei za android ziko juu ukilinganisha na normal smart tv

2.Resolution (HD,FHD,4kUHD,8kUHD)

Term hizi zote humanisha kiwango cha un’gavu wa tv yako na kadri Resolution

inavyokua kubwa ndio TV inakua na uwezo mzuri zaidi wa kuonyesha picha zenye ubora zaidi na bei pia inakua kubwa zaidi

3.WIRELESS CONNECTIVITY
Hii ni feature nzuri sana kwenye tv jaribu kusoma kwenye box kama kuna features kama wi-fi,Bluetooth,mirroring hizi feature zitakusaidi

a kuunganisha tv yako ku share na simu yako vitu vingi mfano kutumia bando la kwenye simu yako kwenye tv,pia kama una airpods unaweza connect na tv ukaendelea ku enjoy movie zako bila kuwakela wengine

4.CONNECTION NA PORTS
Cheki matundu ya kuunganisha vifaa vyako kwenye TV ili usiwe na haja ya kuchomoa chomoa nyaya unapotaka kuunganisha vifaa vingine

5.TV size(“inch)

Size zilizo zoeleka ni inch 32,40,43,49,50,55 .kufanya maamuzi ya size ipi uchukue ni kupima umbali wa eneo itakapo wekwa tv na eneo ambapo mtazamaji atakaa
Mfano umbali wa futi 4-6 nunua tu inch 32,futi 5-8 unaweza nunua inch 40/43 na kuende

6.Brand
Kila brand zinakua na features tofauti tofauti kujitofautisha na brand nyingine ila tu usikimbilie sana brand zenye majina zilizo zoeleka toka zamani,kuna brand zingine mpya lakini zinafanya vizuri sana sokoni na zina features very unique na bei zako kidogo zipo chini

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling