James Munisi Profile picture
Creator & Innovator | Electronics & Telecom Engineer | Business Administrator | 1+1=11 | All about Techs | Founder @Njiwa_Store | We are @TOTTechs |#SimuZaNjiwa

Feb 23, 2022, 19 tweets

#UZI
💨 MAREKANI KUMNYAMAZISHA URUSI?

Biden ametoa speech ambayo inaonyesha Trump alikuwa anamdekeza sana Putin.

Belarus jirani wa Ukraine na Urusi ndiye rafiki mkubwa Putin na Biden kasema Urusi isipotoa majeshi yake huko atalituma jeshi 👇

la Marekani ndani ya Belarus 🇧🇾

Tunaweza kuona ni namna gani Marekani wanaendelea kuzichanga karata zao vizuri dhidi ya kumdhoofisha Urusi.

Belarus chini ya Raisi ambaye watu wa haki wanamuita Dictator Alexander Lukashenko aliyekaa madarakani toka 1994 alisema

"Ikiwa ina maana kuweka askari wa Kirusi hapa, tutawaweka kwa muda mrefu iwezekanavyo. Ninasisitiza kwa mara nyingine tena: hili ni eneo letu na uamuzi huu ni wetu.”

Umoja wa Mataifa unasema Urusi kuingiza jeshi lake Donbas, Ukraine kuwalinda raia wanaowasapoti Urusi ni kosa

Marekani 🇺🇸 wanataka kuliingiza jeshi lake Belarus 🇧🇾 likaliondoe Jeshi la Urusi 🇷🇺
▪️Atakaye umia ni Belarus 🇧🇾
▪️Vita itapiganwa kwenye aridhi ya adui wa Marekani.
▪️Marekani hana cha kupoteza.
▪️Ndio mwanzo wa Marekani kuishambulia Moscow.

Pia tukumbuke Donbas, Ukraine 🇺🇦 ndio inayochochea vita vya huu mgogoro na bado mpaka sasa Majeshi ya serikali yanapigana na Vikundi vinavyopewa sapoti na Urusi.

USHAWISHI WA MAREKANI UNAMFANYA URUSI AONEKANE MTOTO M-BAYA

Tunashuudia
Japan aliyewahi kuwa adui mkubwa wa Marekani anasema anasimama upande aliosimama Marekani.

Ujerumani iliyokuwa inataka huu mgogoro umalizike ki-diplomasia ili kulinda maslahi ya nchi yake juu 👇

Ya bomba la Gesi la Nord Stream 2 inayotoka Urusi. Leo hii analiongezea vikwazo Urusi isiwauzie gesi.

Qatar inawaambia Ujerumani mnataka nini? Mafuta? au nini sisi tuwape.

Marekani na Ulaya umeziwekea vikwazo Taasisi za kifedha za Urusi hakuna miamala ya kuamisha pesa

Kutoka Urusi kwenye nyingine za Ulaya hii ni hatari sana kwenye uchumi wa Urussi.

Marekani imewazuia baadhi ya biashara za matajiri wa kubwa wa Urusi hii ni mbaya mno ugomvi wa kijeshi kuamishiwa kwa watu ambao hawana hatia.

Putin anazidi kufundishwa uoga.

👉 Marekani ina Teknolojia kubwa mno kwenye Majeshi yake ana uwezo wa kuifanya hii dunia kitu chochote anachotaka.

👉 Urusi ni nchi ambayo haitabiriki.

Sio kwamba Marekani inaipenda sana Ukraine, lengo kubwa la Marekani kwa miaka mingi ni kuishambulia Moscow na kuisambaratisha.

Mpaka leo hii Moscow ipo kwasababu ya uwepo wa Putin.

Trump alikuwa anaizungumza Urusi huku akiwa na hofu ya silaha za Nyuklia za Urusi.

Biden anaizungumza Urusi bila kuziwekea maanani silaha za Nyuklia anazozoimiliki Urusi zinazoweza kuifuta dunia yote ndani ya muda mfupi.

NATO wanafikiria kuingia Ukraine Marekani inafikiria kuingia Moscow na Urusi inafikiria kuingia Marekani.

Kwa hivi vikwazo alivyowekewa Urusi ni hatari sana kwa uchumi wao na ni ngumu kuvulimia. Vuta picha biashara zinazofanyika kati ya Urusi na China leo hii zisifanyike!!

Raisi wa Urusi Putin amesema yupo tayari kwenye mazungumzo ya kidiplomasia na nchi za Ulaya juu ya mzozo wa Ukraine lakini kuhusu suala la usalama wa raia wake hilo halihitaji mjadala.

Kwasasa Urusi ni sawa na yupo mwenyewe ile nchi imezungukwa na kambi nyingi za jeshi la USA.

Lakini ana makombora hatari ya Hypersonic ambayo hakuna mtambo yoyote yenye uwezo wa kuyazuia hayo makombora kama tulivyokuwa tunashuudia Iron Dome za Israel zilivyokiwa zinazuia makombora ya Palestina.

Urusi anaweza rusha kombora likazunguka dunia nzima bila kuonekana
Source: Putin

Hiyo Teknolojia Marekani anayo iliyo advanced zaidi ya Urusi, wakifikia level hiyo atakaye anza ndiye atakayeshinda japo hakuta kuwa na mshindi.

Marekani na Urusi wana mbinu zinazofanana katika vita kudeal na Viongozi.

Katika mazungumzo mengi ya Marekani wanamlenga moja kwa moja Putin kama mkosaji wanayemuhitaji na Urusi kule Ukraine kwa mujibu wa Majasusi wa Marekani ni wamepanga majina

Ya Viongozi wa Ukraine wanaotaka kuwaua, kuwateka na pia kwenda kuwatesa. Tuendelee kusubiri Urusi atajibu nini juu ya hivi vikwazo.

Pia huku Tanzania kuna habari zinasambaa kwa kasi sana kuwa 👇

Wauzaji wa @SimuZaNjiwa kuna simu mpya wameingiza sokoni 2022 kuanzia 270K hadi 3.5m

📍Infinix Tower, Kariakoo | Tunasafirisha Mikoani 🚚
📞 0745100757

Nyuzi zitakazofuata sitakuwa specific.

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling