James Munisi Profile picture
Creator & Innovator | Electronics & Telecom Engineer | Business Administrator | 1+1=11 | All about Techs | Founder @Njiwa_Store | We are @TOTTechs |#SimuZaNjiwa

Feb 24, 2022, 18 tweets

#UZI
๐Ÿ’จ Juzi Marekani na UE zilizungumza kauli za kibabe dhidi ya Urusi sasa Urusi kaamua kulishambulia jeshi la Ukraine kila pande.

Tusubiri kama Marekani atajaribu kuingiza mguu kuizuia Urusi, kuna nchi kama China zinaitamani sana Super Power japo kwasasa wanajifanya ๐Ÿ‘‡

Wapo kidiplomasia zaidi ila ikianza hii ligi ya wakubwa Xi Jinping lazima aungane na mwanae wa faida Putin kupambana na Marekani.

Hii vita haina tena faida kwa Marekani tuone NATO watachukua maamuzi gani dhidi ya Urusi na mbaya zaidi Urusi kaingia Ukraine akiwa

na Wana Ukraine kibao wanaompa sapoti, anaweza akapambana kuwaua Viongozi wa Ukraine wanaomsumbua na akapachika Viongozi wake na hii kitu Marekani alikwisha isema mwanzo.

Toka mwanzo nilisema Marekani ina uwezo mkubwa sana kijeshi lakini Urusi ni nchi ambayo haitabiriki

Urusi ni nchi ambayo huwa inafanya mambo mengi sirini tofauti na Marekani.

Urusi ina Raisi ambaye in nature ni jasusi (KGB) akili mingi ukiangalia namna anavyoongea kwenye speech zake toka mwanzo wa huu mzozo unaweza kuona ni mtu ambaye

akurupuki kuongea, anaongea kama malaika mwenye kauli tata.

Mtu aliyewaambia UE (Umoja wa Ulaya) msiiunganishe Ukraine na jeshi la NATO, UE wakamwambia hoja yako haina mashiko.

Akapeleka Wanajeshi zaidi ya 100,000 mpakani mwa Ukraine kufanya mazoezi ya kawaida tuh

Tena muda huo wanaita Wanahabari na kuwaambia sisi hatuna mpango wa kuivamia Ukraine ni utaratibu wetu wa kufanya mazoezi "ety Ukraine tumekanyaga ardhi yenu kwani! Ukraine: hamjakanyaga ๐Ÿ˜๐Ÿ˜"

Marekani wanawajua vizuri Urusi wakawa wanasisitiza Urusi wanaivamia Ukraine.

Huku wakawa wanawapatia Ukraine msahada ya silaha nzito nzito na mitambo mikubwa ya kisasa ya computer, NATO nao hawakua nyuma wakawa wanasogeza vikosi karibu na Ukraine.

Wanajeshi wakamaliza mazoezi wakasepa na kuna wengine wakaenda Syria kufanya mazoezi.

NATO nao wakaendelea kusogeza vikosi karibu na wao kufanya mazoezi.

Putin huwa anasema Ukraine ni ndugu zake na watarudi kwenye himaya ya Urusi.

KARATA YA VIKWAZO
Hii inaonekana ni karata ya hovyo iliyochangwa mbele ya Urusi, kuna nchi unaweza kuziwekea vikwazo na zikarudi nyuma kutaka majadiliano.

Marekani ilisimama mstari wa mbele kumuwekea Urusi vikwazo huku nchi nyingi za Ulaya zikiwa zinalia wakiongozwa na Ujerumani

Kuna mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 ambalo linatoa gesi kutoka Urusi kupeleka Ujerumani, hili Bomba limetengenezwa bado halijaanza kufanya kazi.

Sasa Ujerumani ikamtishia Urusi kuwa tutaliwekeza vikwazo ilo bomba lisitumike hapa ni sawa na Rafael awatishie Tanesco anajikatia umeme

Kumbuka bado ile Nord Stream 1 bado inaendelea kusafirisha hiyo gesi kwenda Ujerumani. Kinachotokea sasa Ulaya ni vitu kupanda bei.

Urusi wamewekewa vikwazo vingi vya kiuchumi kitu ambacho kinaziathiri nchi za Ulaya yaani hivi vikwazo vikitoboa miezi 3 bila kulegezwa watanyooka.

Urusi wala hajali yupo kwenye aridhi ya Ukraine na NATO haina uwezo wa kumpiga Urusi zaidi ya kumtegemea Marekani.

Je Marekani atasubutu kuingiza mguu kwenye maji yaliyorojeka? Na kwa faida ya nani? Marekani tumezoea kumuona akizivamia nchi ambazo anajua akifika anazitembezea dozi huku kwa Mrusi haelewi atatembeza au atatembezewa dozi.

Biden ataendelea kuzingumza kauli za kibabe dhidi ya

Urusi? Ikiwa hivyo lazima kidimuliwe.

Putin anasema wanaojiingiza kwenye mzozo wa Ukraine watashuhudia madhara ambayo hawajawahi kuyaona hapo awali.

Hiyo ni kauli inayotoka kwa Mwamba mmoja aliyeko kwenye nchi moja dhidi ya nchi zaidi ya 30 zinazompinga

Putin alitangaza maeneo ya Donetsk na Luhansk kuwa ni maeneo huru akamkemea vikali kwamba anavunja sheria za kimataifa.

Leo Ukraine yote unapigwa moshi tatu tatu mpaka Kyiv mji mkuu wa Ukraine wajuba wamefika. Urusi inaharibu assets za majeshi ya Ukraine.

Urusi wameivamia Ukraine na wanataka Wanajeshi wa Ukraine waweke silaha chini.

Raisi wa Ukraine anasema watapambana kulilinda taifa lao na raia yeyote anayetaka silaha atampa. Muda huo huo Raisi wa Mtata wa Belarus anasema Ukihitajika msahada wa kijeshi Ukraine atamsaidia Urusi.

NATO na Marekani zitathubutu kusaidia?

Raisi wa Ufaransa Emmanuel ameitisha kikao cha dharura cha NATO tusubirie majibu

Umoja wa Mataifa unamsihi Urusi arudishe majeshi nyuma.

Antonio Guterres anawaomba Urusi wafanye amani ndani ya Ukraine ๐Ÿ™Œ
twitter.com/antonioguterreโ€ฆ

Tusubirie hatua zitakazochukuliwa na NATO na Marekani turn on ๐Ÿ””

Je hii ndiyo sehemu ndiyo sehemu ofisi za @SimuZaNjiwa zilipo? ndio ni hapa Infinix Tower, Roundabout ya zamani Uhuru/Msimbazi, Kariakoo.
๐Ÿ“ž 0745100757

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling