Madinidotcom Profile picture
Show ya radio kwa #TAARIFANaMAARIFA kila wiki.Tunajadili ya dunia kwa lugha rafiki na nyepesi. kila Jumamosi 9alasiri - 10jioni Eastafrica Radio..Subscribe👇

Jul 11, 2022, 25 tweets

Nni kinaendelea SRILANKA? Sehemu 2

Uzi🧵🙌

#PichaLINAENDELEA anzia post ya jana.

Ankali GOTABAYA alipoingia madarakani 2019 aliahidi kodi za kibwege atazifutilia mbali,wananchi wakaona “eheee,huyu ndo mwaisa mtu mbadi wetu”km ujuavyo ujuavyo kila mtazamo hujengwa na historia

so shida ya wana SRI LANKA ilikuwa kuona nchi inarudi kusimama kwa miguu yake,mambo ya wewe ni nduguyakeNani wala hawajali sana. Alipoingia ankali GOTABAYA alionekana ni mtu wa kusimamia maneno yake, akapitisha panga la kupunguza kodi kwa wananchi ,kampeni ambayo ilipunguza 25%

yaani robo ya pato la taifa ili wananchi wafurahi.Wakati anafanya hili ni wakati ambao alikuwa akijiandaa na uchaguzi mkuu.Watalamu wa kiuchumi hawakushauri hili lakini yeye alisema anataka biashara ndogondogo za wananchi wanyonge wa hali ya chini zichipue,so wasilipe kodi .

Hawajakaa vizuri,GHAFLA ankali Gotabaya akaja na ajenda kwamba kuanzia sasa wakulima wote watatumia mbolea asilia ,waachane KABISA na mbolea za chemikali,ni mwendo wa maviYaNg’ombe,maviYaKuku na mimea. ndani ya usiku mmoja alitaka kuigeuza Sri lanka kuwa na kilimo organic 100%

yaani mbolea ya kiwandani ni kama ukutwe na bangi.Hakuna nchi duniani imefanikiwa kutegemea mbolea ya asili kwa chakula 100%,hata nchi kama ujerumani ni 10-15% tu ya chakula inategemea mbolea ya asili yaani ya wanyama na mimea. So ndani miaka michche kilimo cha mpunga kilishuka

50% (NUSU YA UZALISHAJI) na nchi ina watu zaidi ya milioni 21 .Hii ilifanya kulazimika kuagiza mchele nje ya nchi,jambo la ajabu kutokea kwenye nchi ambayo Mpunga ndo shughuli yao.
Ghafla ikaja COVID 19 kisiwa ambacho Utalii ulichangia 22% YA PATO LA TAIFA

liliyeyuka ndani ya muda mfupi. Hata hivyo kabla ya COVID,ndani ya 2019 kulitokea tukio la kigaidi kwenye mji mkuu COLOMBO,wahuni walilipua makanisa na majengo kadhaa kuua watu 269 palepale na 25 kati yao walikuwa raia wa kigeni,tukio hili lilishusha utalii kwa 70% nchini humo.

Covid ikamalizia mchezo. Chanzo kingine cha pesa za kigeni ilikuwa wananchi waishio nje ya nchi waliokuwa wanatuma pesa kwa ndugu zao, wanalipwa pesa za kigeni wanazituma nyumbani,covid ikaua hili. So hapa ndipo watu wakaanza kuhisi maumivu halisi na ukumbuke covid 19 iliingia

2019 ambapo GOTABAYA ndio kwanza amechaguliwa ,ndiyo maana akawa anafanya blandaz zote nilizokwambia, nchi iliishiwa pesa za kigeni kiasi kwamba alipiga marufuku mbolea za viwandani ili kuepuka kuagiza nje ambapo wangetumia pesa za kigeni.
mbali na hilo kuna blanda nyingine

iliyoharibu mambo,nadhani umewahi kusikia kuna nchi ambazo zina michezo au uhuni wa kupandisha thamani ya pesa zao kinyemela,yaani wanavaa kigodoro cha kiuchumi.Kama hujawahi kusikia au umewahi kusikia basi SRI LANKA ni moja ya nchi hizo.Kivip?

Mfano,Kama Tanzania tunaagiza mchele Kenya,na kilo 1 ya mchele KENYA inauzwa $1 (biashara duniani inafanyika kwa dola nilivyokwambia) na labda dola 1 ni sawa na buku 2 za kitanzania, serikali inaweza kutumia bank kuu yake kuaminisha kila mtu kwamba DOLLA 1 ndani ya Tanzania ni

sawa na 1,500, means mchele utauzwa kwa bei ya chini ya uhalisia.Mbinu hii hutumika na nchi zinazoingiza bidhaa nyingi kuliko inazouza nje ili kumaintain pesa yao lakini huwapunguzia wananchi mzigo wa gharama na hivyo serikali iliyo madarakani inajiweka pazuri kisiasa kwasababu

wananchi wanaona vitu vinashuka bei au atleast hakuna mfumuko wa bei,hata kama duniani kwingine mambo yamebadilika.Utajiuliza sasa kwanini nchi nyingine hazitumii mbinu hii kabambe?well,jibu ni simpo, kwasababu ya hiki kilichoitokea SRI LANKA leo.🥳

So sri lanka walifanya uhuni huu na kumaintain pesa yao (Rupee) tangu APRIL 2021 wakifanya mchezo wa wakiaminisha watu kwamba dola 1=buku jero wakati kiuhalisia ni buku 2.Utajiuliza inafanyaje kazi kwenye mazingira halisi?
Iko hivi..mfano unaenda bank unawapa dola 1 ya kimarekani

then wanakupa buku jero(1500), Ukienda kwenye duka binafsi la kubadilisha pesa wanakupa BUKU 2.Bila shaka haichukui muda mrefu sana watu wataanza kuambiana kwamba usibadilishe au usiweke pesa zako za kigeni kwenye bank kwasababu wananunua kwa bei chee.

so wale raia wa kigeni hawatumi tena pesa kwa ndugu zao kupitia bank au njia rasmi ambazo zitaingia serikalini.Kupitia hili bank kuu ambapo mzunguko wa pesa zote huishia inakosa pesa za kigeni kumaintain UCHUMIwaKati FEKI waliojitengenezea.

So ni mambo 3 yaliyojimix yameishusha sri lanka ,Kwanza hazina imeishiwa pesa za kigeni kwa uongozi mbaya ,pili waliotunza pesa zao zina thamani ndogo kuliko ilivyokuwa mwanzo kutokana na mfumuko wa bei duniani,so kama ulikuwa na pesa inayoweza kununua kilo 10 jana,

leo pesa yako inaweza kununua kilo 5 pekee za mchele.Hivyohivyo kwenye bidhaa nyingine kama mafuta.
Hawajakaa vizuri Vita ya UKRAINE ikaanza na kwa nchi inayotegemea kuingiza zaidi kama SRI LANKA ilipigwa na kitu chenye ncha kali kwasababu UKRAINE na URUSI zinasambaza 28%

ya mahindi na ngano yote duniani. Ukraine tu yenyewe inalisha watu milioni 400 duniani kwa export yake ya chakula.Russia inasambaza 15% ya mbolea za mazao duniani na mafuta yanayotumika kutengeneza hizo mbolea pia yanapatikana Russia.

Mbali na hilo BEI ya mafuta ikapanda duniani na katika kupambana na hali ya kupanda kwa vyakula,nchi nyingi duniani zimepiga marufuku kuuza nje baadhi ya bidha za vyakula,so kwa nchi kama SRI LANKA ambayo mbolea hakuna,chakula na vitu vingi wanaagiza nje,

bila shaka sio ajabu kusikia yanayo wapata. So uchumi huwa una collapse kwa namna hii lakini kuna njia ya kutatua hili linapotokea,kwasababu nchi kushindwa kulipa madeni yake na kukosa sifa ya kukopesheka lkn kukosa hazina ya pesa ya pesa ya kigeni sio mchongo mpya dunia

imeshaweka njia ya kupambana nayo,na hapa ndipo mashirika ya kimataifa huingia kama IMF shirika la fedha na kutoa msaada wanaziita BAILOUT.
SRI LANKA ishapokea mpunga wa aina hii mwaka 2006 na nchi kibao hukopeshwa kwa namna hii kuokoa uchumi,unakumbuka UGIRIKI pia,

lkn kuna KIPENGELE ambacho kinafanya SRI LANKA inashindwa kusaidika.Hizo BailOUT sio pesa zinazotolewa hovyo tu kwasabab nchi ina matatizo,ila kuna vigezo maalum ikiwemo uimara wa serikali,sera za nchi kuhusu maendeleo na kifupi IMF hutaka kujiridhisha kwamba situation ya nchi

kwamba situation ya nchi husika ni salama kuwapa pesa hizo au ndo watajikuta kwenye same situation miezi 6 baadaye.Hiki kigezo ndo SRI LANKA inakikosa,kwasababu wananchi wapo barabarani wakiandamana na wana sababu kwa wanachokifanya,lkn wanazidi kuchelewesha msaada wa kimataifa

Mfumuko wa bei duniani,vita na covid 19 vimekutana na uongozi mbaya/dhaifu ndani ya nchi na hii ndio UN waliita A PERFECT STORM. hope umepata idea ya kinachotokea Sri SRI LANKA

Imeandaliwa na @Gplanet5
Usikose kutuskiliza kila jumamosi kuanzia saa 9 alasiri mpk saa 10 jioni

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling