SANUKAnaCHAPO Profile picture
| Storyteller | Owner @usedpointtz | SON OF BONGO FLEVA | THE WALKING MEDIA | Binamu wa BARAKA MAVIATU |

Nov 5, 2022, 7 tweets

Nimefanikiwa kunyaka copies za mkataba wa wasanii hawa na Konde Gang unaonyesha kuwa wote kwa pamoja walikubaliana kutofata masharti ya mkataba wao hasa kifungu namba 15(a)(b)(c) cha mkataba wao wa tarehe 31/08/2020.

🧵shuka nao👇

Stori kamili iko hivi…
Kumbuka wasanii hawa waliingia mkataba wa miaka 10 na lebo hiyo tajwa hapo juu
na endapo Kama Konde Gang wangevunja mkataba na moja ya wasanii hao basi walipaswa kumlipa kiasi cha milioni 10 kama fidia.

Ikumbukwe Konde Gang ndiyo iliomba kusitisha mkataba

na wasanii hao, waliwaita chini na kukubaliana kuwa mkataba uvunjwe kwani lebo hiyo haikuwa na haja ya kuendelea na wasanii hao, wasanii waliomba kama mkataba ungevunjwa basi vipengele muhimu vizingatiwe ikiwemo fidia ya pesa.

Wasanii wao kupitia mwanasheria wao walitinga

BASATA kama chombo cha kusimamia sanaa wahakikishe haki inafatwa kwenye mkataba huo.

Vikao vikafanyika na baadae wote kwa pamoja(pande 2) zilikubaliana yafuatayo;

• Kampuni kuwarudishia password za account zao ikiwemo Youtube na digital platforms zote

Ambapo kazi ya zao zinauzwa.

•Kampuni kutohusika wala kufaidika na mirabaha au hakimiliki yeyote inayotokana na kazi za wasanii

•Kiasi cha milioni 10 kwa kila mmoja wa wasanii hao kutolipwa na kampuni tajwa na kusamehewa dhidi vifungu vya mkataba vinavyotaka kufanya hivyo

•Wasanii hao kupewa kazi zote ambazo hazijatoka ila zipo kwenye kampuni basi wakabidhiwe

• Wasanii hao kuwa huru kufanya kazi na watu wengine bila kubugudhiwa.

Kutokana na hayo inaonesha namna gani Harmonize hakuwa na bifu wala haja ya kuwakomoa madogo ambao aliweka

Pesa nyingi kwenye kuwa brand na kuwafikisha hapo walipo.

Wakati huo huo pia Harmonize amethibitisha kuachana na first lady wa Konde Gang Bibie Anjella ambapo ametanabaisha hamdai hata senti binti huyo sababu aliamua kumsaidia kwa mapenzi yake.

#TheWalkimgMedia #SanukaNaChapo

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling