Madinidotcom Profile picture
Show ya radio kwa #TAARIFANaMAARIFA kila wiki.Tunajadili ya dunia kwa lugha rafiki na nyepesi. kila Jumamosi 9alasiri - 10jioni Eastafrica Radio..Subscribe👇

Dec 22, 2022, 25 tweets

MAFUTA YANATOKA-GA WAPI?🤔
#PICHALINAANZA...
Mpaka sasa jibu la kisayansi juu ya chanzo cha uwepo wa mafuta, hata mimi sipendagi sana kumuaminisha mtu😅,Tho nitakuelewesha wanasega nini ,ukiona haikuingii basi tuishie kukubali tu MUNGU FUNDI.Lakini wanasema...

ni matokeo ya mgandamizo(presha) wa mimea,viumbe waliowahi kuishi duniani na mazagazaga kibao yaliyovunda-ga ardhini ambapo vilitengeneza hewa ya HYDROCARBON.
Hii HAIDRO-KABONI wala isikuogopeshe,hili jina ni kitu kinachotokeaga pale...

Kemikali za asili wanaita Organic chemical yaani unajua kuna zile kemikali za maabara za mikonoYaWatu na hizi za Asili zinaweza kujiumba zenyewe tu labda umetupa takataka na vyakula sehemu moja,then zinajimix zikivunda huenda kuna chemical zinajitengeneza.

So ile chemical ikikutana na gesi ya Carbon(C) kama tunayopumua,ndo inaitwa HaidRO-KABONI (Hydrocarbon).Hii ndo ambayo mafuta yote hukutwa nayo kwa kiasi kikubwa na ikiondolewa ndo tunapata mafuta safi ya kutumia,ukisikia MAFUTA GHAFI au CRUED OIL ujue...

kabla hayajawa tayari na nitakuelezea process yote.
Mfumo huu pia ndio asili cha MAKAA YA MAWE kwa mujibu wa Sayansi na kwenye episode yetu kuhusu NISHATI ya NYUKLIA tulikuambia pia makaa ni kati ya VYANZO VYA nishati TULIVYONAVYO DUNIANI since

long time NA KABLA YA MAFUTA kugundulika,hata vita ya kwanza ya dunia watu walikuwa wanapigana kwa meli za makaa ya mawe, baadaye wese likaingia na meli zikaanza kubadilishiwa injini kuwa na speed zaidi na pia wepesi wa uendeshaji.

So makaa ya mawe yalitokana na wale viumbe hai na micro organism waliokufa wakiwa nchi kavu na mafuta ni wale viumbe walioitwa MwendaZake wakiwa Baharini Utauliza Viumbe wa kale gani tena?Nini kiliwaua?Well,imagine huu ni mwaka 2022/3 mpakani, it means ukirudi nyuma kutoka hapa

hadi kufika mwaka wa kwanza, bado ni michache sana ukilinganisha na umri wa sayari hii dunia. So hiyo inatupa uelewa tu kwamba before maisha haya,kulikua na maisha mengine ambayo ni ngumu hata kuimagine.
Na labda itakupa swali...

sasa iweje Saudi arabia au uarabuni ndo lilipo wese la kutosha wakati sehemu kubwa ya nchi husika ni jagwa tupu kuliko bahari?well ni kwasababu miaka milioni 100 iliyopita,inaelezwa sehemu kubwa ya jangwa ikiwemo jagwa la sahara likuwa maji matupu,
Yes na bahari hiyo...

iliitwa Tethys Ocean na ukienda ku google utaona .Enzi za skuli tulishafundishwa kwamba HAPOzaManiZAKALE dunia iliku bara 1 lililoitwa PANGEA na kama unatumia vizuri internet yako,youtube kuna story za video za mifano ya bara hili la zamani


au muonekano wa dunia ya zamani sana according to historia.
Kile kilisababisha dunia ikagawanyika na maji kuingia katikati ndo athari hizo ambazo zilifanya kutengenezeka kwa HYDRO-kabon kutoka mazalia ya viumbe hao wa zamani waliokuwa wanaishi duniani

Kuzungumzia nini kilitokea wakati huo,ni topic nyingine pana na tofauti kabisa na hii ya mafuta ,hivi vipindi au Era mbalimbali dunia iliyopitia na viumbe waliokuwepo Zinaitwa geological periods.
Kwahiyo mafuta yanachimbwa au kupatikana baharini na kuna yanayochimbwa nchi kavu

na utofauti huu wa sehemu ya upatikanaji unatofautisha pia quality ya mafuta yenyewe na pia gharama za kuyapata.
Ni kwasababu uso wa dunia tuliyopo umegawanywa kwenye visahani(plates) kadhaa na kila plate ndani yake kuna ujiuji wa moto ambao ndio supagluu(Gundi) yake

so kadri dunia inavyozunguka kuna wakati plate moja husogea na wanasema ardhi ya dunia ina move kwa cm 1 – 13 kila mwaka.Mfano PLATE ya INDIA ilivyosogea na kukutana na plate ya EURASIA ndo kulizaliwa safu ya milima maarufu ya HIMALAYA iliyotenga INDIA na CHINA na nchi nyinginezo

So wakati huu ambao ardhi ya dunia ilikuwa inamoove na kukutana,katikati ya INDIA na EURASIA ndo kulikuwa na bahari hii iliyotoweka Tethys(Te-thi-s) Ocean na baada ya ardhi kusogeleana ndipo eneo lililokuwa chini maji miaka yote lilijitokeza juu ya dunia na eneo hilo siku hizi

linafahamika kama NCHI ZA MASHARIKI YA KATI au kwa kihaya wanaita MIDDLE EAST (mido isti) ambalo lina nchi kama SYRIA,IRAQ,IRAN,SAUDI ARABIA,KUWAIT,BAHREIN(ba-rein),OMAN ,YEMEN,JORDAN,ISRAEL bila kusahau QATAR tulipoenda kuchezea kombe la dunia .

Hii ni 3.4% ya ardhi yote ya dunia lakini karibu nusu ya yaani 48% ya supu yote aina ya wese ilikwenda kujikusanya hapa na nishati asilia nyingine ambapo mashariki ya kati ina 38% ya nishatia asilia yote duniani mbali na mafuta

So wakati dunia inajishape kwa namna nyingine miaka milioni kadhaa nyuma ,kuna maeneo mengi yaliyokuwa chini ya maji ambayo yalijitokeza ardhini lakini hayakuwa kwa ukubwa kama eneo la mashariki ya kati ndio maana asilimia kubwa nyingine ya mafuta inapatikana baharini ya sasa

Mafuta yametumika kwa miaka kibao mfano wahenga wa MESAPOTANIA walioishi miaka ya 3100 kabla ya Kristo ,walitumia mafuta kutengenezea vidani vya kuvaa shingoni kama wamasai.
Then ukafuata utawala wa BABYLON a.k.a kina fundi juma wa mnara wa babeli 1700B.C,walitumia mafuta kupaka

kwenye maboti yao ili maji yasipite.Baadaye wakaja wa MISRI kwa kina Mohamed Salah mwaka 2600 B.C wakatumia kupaka miili waliofariki au sanamu zao na baadaye wazee wa maunyade UGIRIKI walitumia mafuta kuwasha taa .Kifupi ni bidhaa imekuwepo duniani kitambo lakini

ukubwa wa matumizi ya mafuta kama tunavyouona leo ulianzia karne ya 19 na tunavyosema karne ya 19 namaanisha mwaka 1801 to 1900 kamili.
Story ilianza na mwamba 1 mscotland wa kuitwa JAMES YOUNG ,labda unamjua YOUNG KILLER au YOUNG D lakini YOUNG JAMES labda hujawahi kumsikia🤣😅

na sio kosa lako lakini huyu ndiye anatajwa kuwa BABA WA MAFUTA a.k.a FATHER OF PETROCHEMICAL INDUSTRY (tamka petro-kemiko indastri) .Siku moja Ilikuwa 1848 mwamba alipogundua uji-uji flani unaotoka kwenye mgodi wa makaa ya mawe ,alipougusa akasema “jamani hili si wese hili?”

btw hakuwa anajua wese nini,
So jamaa ndo alichukua ujiuji huo na akafanikiwa kuuchemsha na kutumia sehemu ya mafuta mepesi kwa kuwashia taa na yale mazito kutumika kwenye mashine kama oil grisi n.k .Miaka 3 baadaye ndo mwamba mwingine wa kuitwa EDWARD kijana wa mzee WILLIUM

akafanikiwa kutengeneza kiwanda cha kwanza cha kutenganisha mafuta mepesi na yale mazito kutoka kwenye UJIUJI ULE.Kama umewahi kukamua mafuta ya alizeti yakatoka meusi.Basi ni kitu kama hiki.Wanaita UJIUJI huo CRUED OIL kwa kiswaz mafuta ghafi ...

Hii ni 'ka-sehemu'😉 tu ka story yote hii ambayo imeenda deep kwa ENGOZ zote za bidhaa hii.Full inapatikana YOUTUBE anzia kwa click
Whats app tucheki 0712 760276

Tulikuahidi #TaarifaNaMaarifa

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling