Madinidotcom Profile picture
Dec 22, 2022 25 tweets 10 min read Read on X
MAFUTA YANATOKA-GA WAPI?🤔
#PICHALINAANZA...
Mpaka sasa jibu la kisayansi juu ya chanzo cha uwepo wa mafuta, hata mimi sipendagi sana kumuaminisha mtu😅,Tho nitakuelewesha wanasega nini ,ukiona haikuingii basi tuishie kukubali tu MUNGU FUNDI.Lakini wanasema...
ni matokeo ya mgandamizo(presha) wa mimea,viumbe waliowahi kuishi duniani na mazagazaga kibao yaliyovunda-ga ardhini ambapo vilitengeneza hewa ya HYDROCARBON.
Hii HAIDRO-KABONI wala isikuogopeshe,hili jina ni kitu kinachotokeaga pale...
Kemikali za asili wanaita Organic chemical yaani unajua kuna zile kemikali za maabara za mikonoYaWatu na hizi za Asili zinaweza kujiumba zenyewe tu labda umetupa takataka na vyakula sehemu moja,then zinajimix zikivunda huenda kuna chemical zinajitengeneza.
So ile chemical ikikutana na gesi ya Carbon(C) kama tunayopumua,ndo inaitwa HaidRO-KABONI (Hydrocarbon).Hii ndo ambayo mafuta yote hukutwa nayo kwa kiasi kikubwa na ikiondolewa ndo tunapata mafuta safi ya kutumia,ukisikia MAFUTA GHAFI au CRUED OIL ujue...
kabla hayajawa tayari na nitakuelezea process yote.
Mfumo huu pia ndio asili cha MAKAA YA MAWE kwa mujibu wa Sayansi na kwenye episode yetu kuhusu NISHATI ya NYUKLIA tulikuambia pia makaa ni kati ya VYANZO VYA nishati TULIVYONAVYO DUNIANI since
long time NA KABLA YA MAFUTA kugundulika,hata vita ya kwanza ya dunia watu walikuwa wanapigana kwa meli za makaa ya mawe, baadaye wese likaingia na meli zikaanza kubadilishiwa injini kuwa na speed zaidi na pia wepesi wa uendeshaji.
So makaa ya mawe yalitokana na wale viumbe hai na micro organism waliokufa wakiwa nchi kavu na mafuta ni wale viumbe walioitwa MwendaZake wakiwa Baharini Utauliza Viumbe wa kale gani tena?Nini kiliwaua?Well,imagine huu ni mwaka 2022/3 mpakani, it means ukirudi nyuma kutoka hapa
hadi kufika mwaka wa kwanza, bado ni michache sana ukilinganisha na umri wa sayari hii dunia. So hiyo inatupa uelewa tu kwamba before maisha haya,kulikua na maisha mengine ambayo ni ngumu hata kuimagine.
Na labda itakupa swali...
sasa iweje Saudi arabia au uarabuni ndo lilipo wese la kutosha wakati sehemu kubwa ya nchi husika ni jagwa tupu kuliko bahari?well ni kwasababu miaka milioni 100 iliyopita,inaelezwa sehemu kubwa ya jangwa ikiwemo jagwa la sahara likuwa maji matupu,
Yes na bahari hiyo...
iliitwa Tethys Ocean na ukienda ku google utaona .Enzi za skuli tulishafundishwa kwamba HAPOzaManiZAKALE dunia iliku bara 1 lililoitwa PANGEA na kama unatumia vizuri internet yako,youtube kuna story za video za mifano ya bara hili la zamani

au muonekano wa dunia ya zamani sana according to historia.
Kile kilisababisha dunia ikagawanyika na maji kuingia katikati ndo athari hizo ambazo zilifanya kutengenezeka kwa HYDRO-kabon kutoka mazalia ya viumbe hao wa zamani waliokuwa wanaishi duniani
Kuzungumzia nini kilitokea wakati huo,ni topic nyingine pana na tofauti kabisa na hii ya mafuta ,hivi vipindi au Era mbalimbali dunia iliyopitia na viumbe waliokuwepo Zinaitwa geological periods.
Kwahiyo mafuta yanachimbwa au kupatikana baharini na kuna yanayochimbwa nchi kavu
na utofauti huu wa sehemu ya upatikanaji unatofautisha pia quality ya mafuta yenyewe na pia gharama za kuyapata.
Ni kwasababu uso wa dunia tuliyopo umegawanywa kwenye visahani(plates) kadhaa na kila plate ndani yake kuna ujiuji wa moto ambao ndio supagluu(Gundi) yake
so kadri dunia inavyozunguka kuna wakati plate moja husogea na wanasema ardhi ya dunia ina move kwa cm 1 – 13 kila mwaka.Mfano PLATE ya INDIA ilivyosogea na kukutana na plate ya EURASIA ndo kulizaliwa safu ya milima maarufu ya HIMALAYA iliyotenga INDIA na CHINA na nchi nyinginezo
So wakati huu ambao ardhi ya dunia ilikuwa inamoove na kukutana,katikati ya INDIA na EURASIA ndo kulikuwa na bahari hii iliyotoweka Tethys(Te-thi-s) Ocean na baada ya ardhi kusogeleana ndipo eneo lililokuwa chini maji miaka yote lilijitokeza juu ya dunia na eneo hilo siku hizi
linafahamika kama NCHI ZA MASHARIKI YA KATI au kwa kihaya wanaita MIDDLE EAST (mido isti) ambalo lina nchi kama SYRIA,IRAQ,IRAN,SAUDI ARABIA,KUWAIT,BAHREIN(ba-rein),OMAN ,YEMEN,JORDAN,ISRAEL bila kusahau QATAR tulipoenda kuchezea kombe la dunia .
Hii ni 3.4% ya ardhi yote ya dunia lakini karibu nusu ya yaani 48% ya supu yote aina ya wese ilikwenda kujikusanya hapa na nishati asilia nyingine ambapo mashariki ya kati ina 38% ya nishatia asilia yote duniani mbali na mafuta
So wakati dunia inajishape kwa namna nyingine miaka milioni kadhaa nyuma ,kuna maeneo mengi yaliyokuwa chini ya maji ambayo yalijitokeza ardhini lakini hayakuwa kwa ukubwa kama eneo la mashariki ya kati ndio maana asilimia kubwa nyingine ya mafuta inapatikana baharini ya sasa
Mafuta yametumika kwa miaka kibao mfano wahenga wa MESAPOTANIA walioishi miaka ya 3100 kabla ya Kristo ,walitumia mafuta kutengenezea vidani vya kuvaa shingoni kama wamasai.
Then ukafuata utawala wa BABYLON a.k.a kina fundi juma wa mnara wa babeli 1700B.C,walitumia mafuta kupaka
kwenye maboti yao ili maji yasipite.Baadaye wakaja wa MISRI kwa kina Mohamed Salah mwaka 2600 B.C wakatumia kupaka miili waliofariki au sanamu zao na baadaye wazee wa maunyade UGIRIKI walitumia mafuta kuwasha taa .Kifupi ni bidhaa imekuwepo duniani kitambo lakini
ukubwa wa matumizi ya mafuta kama tunavyouona leo ulianzia karne ya 19 na tunavyosema karne ya 19 namaanisha mwaka 1801 to 1900 kamili.
Story ilianza na mwamba 1 mscotland wa kuitwa JAMES YOUNG ,labda unamjua YOUNG KILLER au YOUNG D lakini YOUNG JAMES labda hujawahi kumsikia🤣😅
na sio kosa lako lakini huyu ndiye anatajwa kuwa BABA WA MAFUTA a.k.a FATHER OF PETROCHEMICAL INDUSTRY (tamka petro-kemiko indastri) .Siku moja Ilikuwa 1848 mwamba alipogundua uji-uji flani unaotoka kwenye mgodi wa makaa ya mawe ,alipougusa akasema “jamani hili si wese hili?”
btw hakuwa anajua wese nini,
So jamaa ndo alichukua ujiuji huo na akafanikiwa kuuchemsha na kutumia sehemu ya mafuta mepesi kwa kuwashia taa na yale mazito kutumika kwenye mashine kama oil grisi n.k .Miaka 3 baadaye ndo mwamba mwingine wa kuitwa EDWARD kijana wa mzee WILLIUM
akafanikiwa kutengeneza kiwanda cha kwanza cha kutenganisha mafuta mepesi na yale mazito kutoka kwenye UJIUJI ULE.Kama umewahi kukamua mafuta ya alizeti yakatoka meusi.Basi ni kitu kama hiki.Wanaita UJIUJI huo CRUED OIL kwa kiswaz mafuta ghafi ...
Hii ni 'ka-sehemu'😉 tu ka story yote hii ambayo imeenda deep kwa ENGOZ zote za bidhaa hii.Full inapatikana YOUTUBE anzia kwa click
Whats app tucheki 0712 760276

Tulikuahidi #TaarifaNaMaarifa

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Madinidotcom

Madinidotcom Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @madinidotcom

Aug 25, 2022
SAKATA LA MAUAJI YA RAIS WA CONGO.
🧵🔥

#PichaLinaanza Hili ni picha kuhusu tukio la kuuawa kwa rais wa Congo Laurent-Désiré Kabila,ni kama movie la kutisha lakini BASED ON TRU EVENT. Mwamba ambaye ni Stelingi wetu anaitwa RASHIDI MIZELE,baadaye mastelingi watabadilika. Image
hii ndio story,ambayo tulikugusia episode zilizopita za rais aliyeingia mkataba maarufu wa kuigawa Congo MKABA WA LEMERA.HADI leo Congo juzi kati imekubaliwa kuwa sehemu ya africa mashariki,ni nchi yenye historia nyeusi.Licha ya kwamba imebarikiwa madini... Image
ANZIA HAPA......agiza popcorn kabisa

Acha turewind mkanda ,Lets go back hadi siku ya TUKIO lenyewe la mwamba aliyempiga risasi kadhaa Rais wa nchini na akatoka zake mbio akitarajia kutoroka.Huyu ndo mwenye siri hii nzito ya KWANINI alimuua rais wa Congo Laurent-Désiré Kabila Image
Read 20 tweets
Aug 23, 2022
SAKATA LA BILIONEA JEFF BEZOS NA KING SALMAN WA SAUDIA.

Did you know unaweza kuhack an Iphones? Unafahamu ndicho chanzo cha tajiri namb 1 duniani Jeff Bezos kuachwa na mkewe?unafahamu aliyefanya hilo tukio ni King Salman kiongozi wa Saudi Arabia? #PICHALINAANZA Image
Kuna imani kwamba iphones zina strong security ni ngumu kuichezea,yes inawezekena bhanaa lakini kudakwa ni njenje.Sasa hacking inahitaji vitu flani ambavyo sometimes ni teknolojia ghali au lazima uwe na connections kali .
Juzi kati ikatangazwa BREKING NYIUZ Image
WhatsApp imeishtaki kampuni flani inayodevelp computer programs kutoka Israel. Sababu inashtumiwa kumpa Paul Kagame wa Rwanda program ya computer iliyowezesha kudukua "WhatsApp conversation” za wapinzani wa serikali ya Rwanda wanaoishi uhamishoni wanaojiita 'wanaharakati' Image
Read 37 tweets
Jul 13, 2022
MAUAJI YA Mohsen Fakhrizadeh KAMA MOVIE.

Uzi 🧵

Kuiadhibu Iran kama taifa kwa adhabu za vikwazo vya kiuchumi hakujaweza
kuzuia hatari inayosemwa na mataifa makubwa, na 'NEXT' mbinu ni kudeal namtu mmoja kwasababu kuivamia kijeshi pia ni jambo linalowezekana lakini... Image
unahitaji kujipanga sawa sawa kama asemavyo Rose mhando.Kuna mauaji ya wanasayansi wa nyuklia yameshafanyika lakini huyu aliyeuawa Mohsen Fakhrizadeh,tunasema wahuni wamegonga ikulu. Iran sio mgeni wa hiki kinachowakuta kwasababu kilianzia IRAQ Image
aliyekuwa rais wa marekani George W bush sababu KUU aliyotoa ya kuanzisha vita na Iraq 2003, alisema Iraq ilikua inarutubisha na kununua kiwango kikubwa cha Uranium inayochimbwa Africa.Haya madini tuseme ni kama ndizi ambazo unaweza kuMIX ndizi moja na maziwa ukasaga kwenye Image
Read 25 tweets
Jul 11, 2022
Nni kinaendelea SRILANKA? Sehemu 2

Uzi🧵🙌

#PichaLINAENDELEA anzia post ya jana.

Ankali GOTABAYA alipoingia madarakani 2019 aliahidi kodi za kibwege atazifutilia mbali,wananchi wakaona “eheee,huyu ndo mwaisa mtu mbadi wetu”km ujuavyo ujuavyo kila mtazamo hujengwa na historia Image
so shida ya wana SRI LANKA ilikuwa kuona nchi inarudi kusimama kwa miguu yake,mambo ya wewe ni nduguyakeNani wala hawajali sana. Alipoingia ankali GOTABAYA alionekana ni mtu wa kusimamia maneno yake, akapitisha panga la kupunguza kodi kwa wananchi ,kampeni ambayo ilipunguza 25% Image
yaani robo ya pato la taifa ili wananchi wafurahi.Wakati anafanya hili ni wakati ambao alikuwa akijiandaa na uchaguzi mkuu.Watalamu wa kiuchumi hawakushauri hili lakini yeye alisema anataka biashara ndogondogo za wananchi wanyonge wa hali ya chini zichipue,so wasilipe kodi . Image
Read 25 tweets
Jul 10, 2022
Nini kinaendelea SRILANKA..?

Uzi🧵

#Trustory labda umeshaona story nyingi kuhusu SRI LANKA na labda hujui tumefikaje hapa na ndiyo sababu unasoma hapa,au unajiuliza hivi nchi inawezaje ku collapse kiasi cha kukosa hela?kwanza nchi inakosaje hela?inamaana noti zimepotea? Image
Mwingine hata huelewi SRI LANKA yenyewe ndo wapi. So twende nikupe historia simpo yenye MASUALA Mazima ya uchumi ndani yake. Sri lanka ni kisiwa kipo kusini mwa INDIA zamani sana inasemekana kulikuwa na barabara kabisa kutoka INDIA hadi SRI LANKA ya sasa Image
lakini #Trustory maji yalifukia hilo eneo na sasa wana mpaka wa kwenye maji,ni sawa na kusema SRI LANKA zamani ilikuwa #peninsula na sasa ni kisiwa, ukiangalia watu wake wanafanana na jamii ya wahindi.Ushaskiaga wahuni wanaitwa Tamil Tigers? ImageImage
Read 25 tweets
Jun 23, 2022
UMESIKIA MENGI KUHUSU MGOGORO WA #RWANDA NA #DRC LAKINI PENGINE UNASHINDWA KUELEWA WTF IZ GOING ON?🧐🤭
Kuna njia mbili za kuelewa,ya kwanza ni usome Uzi ufuatao.
Pili usikose show'Jmosi hii eastafricaradio.com
History iliyorahisishwa na #SabulaMaarifa wa #MadiniDigital.
Iko hivi!! Kitambo hicho Rwanda iliwahi ku-operate chini ya mwamvuli wa KIFALME uliokuwa ukiongozwa na mwamba wa kuitwa KIGELI IV RWABUGIRI.
Rwabugiri alikuwa ni jamaa fulani hivi kutokea Kabila la walio wachache (TUTSI) kule Rwanda.
na aliingia kwenye vitabu vya kihistoria kama kiongozi pekee wa taifa hilo aliyeamua kufanya mashirikiano na Serikali za KIKOLONI. By the way kama tunavyojua kuwa RWANDA kuna Makabila makuu mawili, na la 3 ni nyongeza, kuna walio wengi ambao tunawatambua kama Wa-HUTU
Read 23 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(