Fortunatus Buyobe Profile picture
Pool of thoughts. A commander of the hand to mouth battalion. Environmental Pioneer. Social Engineer. #CertifiedMchapaUzi . Telegram: https://t.co/aEEOOryJWO

Mar 12, 2023, 18 tweets

CODE AND DECODE

The Dark day 11st Sept 2017
 
Ni jumatatu Kisiwani
 
Jamaa fulani anaona pikipiki mbili zinampita kwa mwendo wa kasi sana.
 
Kila pikipiki imebeba abiria wawili(mshikaki)
 
Hii ni baada ya kusikika milio mitano ya risasi
 
Yes A Dark day indeed

Baadae zikasambaa habari pale kisiwani kuwa Mlinzi mmoja wa mpaka wa shamba alikuwa “kalambwa vyuma” vitano na majambazi.
 
Naam!
 
It was a news tailored for journalists digest
 
Lakini nyuma ya pazia walinzi wa mipaka walikuwa wamegombana na bwana shamba two years back.

Kwanza walimchukia bwana shamba kwa kumleta kijana mdogo tu ndio awe kilanja wao lindoni.
 
Kijana huyo hakuwa na elimu dunia ya kutosha zaidi yao.
 
Yeye elimu dunia yake iliishia tu shule ya upili.

Elimu pekee aliyokuwa amebobea ni maswala ya mipaka.
 
Hakutegemewa kuwa Kilanja
 
Wakulima waliendelea kula ubwabwa na maharage na kwenda kulala.
 
Bila kujua mpakani mwa shamba kuna chess inachezwa.
 
Sasa Bwana shamba kuna maelekezo alitoa kwa kilanja akawaambie wenzake.

Ule haukuwa utaratibu
 
Namaanisha nini?
 
Yaani pale mpakani huwa kuna wazee ambao kiutaratibu kukiwa na jambo lolote, basi bwana shamba anatakiwa aongee nao pamoja akiwemo kilanja wao.
 
Sasa huu utaratibu wa kumtuma kilanja aongee nao hawakuupenda.
 
Na zaidi ya yote,

Maelekezo yaligusa maslahi yao
 
Unajua pale mpakani kulikuwa na Zabuni nyingi sana kuanzia catering services, Mafuta n.k
 
Zabuni hizi zilikuwa kiutaratibu zinachukuliwa na wazee ili nao wafurahie keki ya shamba kidogo.

Kwani wazee walikuwa wanaona wizi mkubwa tu pale shambani na kukaa kimya.
 
Zile zabuni angalau zilikuwa zinawafanya wazee wakae kimya na kutoingilia kwani uwezo wa kuingilia wanao na wanaweza kumweka bwana shamba yeyote kutokea kwenye kundi lao la wazee.

Sasa maelekezo yakatolewa kwa kilanja kwenda kwa wazee.
 
Kuwa zabuni sasa basi!
 
Yaani mchakato wa zabuni mpakani utakuwa unafanywa na bwana shamba kuanzia siku ya maelekezo hayo.
 
Mkutano ulikuwa wa moto!
 
Wazee wakafura!
 
Wakamuuliza kilanja huyo bwana shamba yuko wapi?

Kwa nini kakutuma wewe asije hapa azungumze hayo mbele yetu?
 
Wakamwambia unajua wewe ingawa ni kilanja lakini wewe ni bwana mdogo sana.
 
Wakamwabia kwanza wewe umeishia shule ya upili.. wewe sio size yetu, kamwite bwana shamba aje atueleze hayo.

Kilanja akarudisha zile taarifa kwa bwana shamba.

Bwana shamba alikuwa na tabia za ujeuri,
 
Hakuwa anapenda hata siku moja aonacho yeye ni sahii atokee mtu wa kukipinga.

Alishapewa ushauri na kilanja wa zamani kuwa kuna nyaya za kuchezea pale shambani lakini sio nyaya za transformer.
 
Hata bwana shamba wa zamani alimshauri hilo
 
Yeye hakutaka kusikia,

Sasa taarifa zile za mkutano wa mpakani zikamjia.
 
Akapuuzia kwenda mkutanoni.

Yeye akaanza kuwa anajihusisha na zabuni za watu wa mpakani.
 
Yaani wazee waliendelea kuhudumiwa bila wao kumtafuta muhudumu.
 
Bwana shamba hakujua kama swala lile ni nyeti.
 
Hakujua kama vikao vya usalama ndivyo vilivyoamua kuwa wazee wajipe zabuni wenyewe za kujihudumia.

Sababu kubwa ilikuwa kuwa kama mtu kutoka nje angewahudumia, angeweza kuwafanya chochote walinzi wa mpaka.
 
Mtu wa nje angeweza kuwa compromised akawawekea hata sumu kwenye chakula

Wazee walipoona tu Bwana shamba amewakwepa na kuanza kuwawekea watu wa nje kuwahudumia wakaamua kuandika barua kwa pamoja kuomba kuacha ulinzi.
 
This action a distress message security wise
 
Ikabidi bodaboda guy amfate bwanashamba.

Bodaboda guy without mincing words dared to inform Bwana shamba kuwa “Mzee hapa inamaanisha umeng’oa kiraka kwenye jeans ya bishoo”
 
Akamwambia “Find a way to resolve the matter before this deteriorated relationship with “wazee” sours much more.
 
Kama kawaida jamaa hapangiwi

Jamaa akaona hakuna threat yoyote
 
Lakini akawa ni mtu wa wasiwasi mwingi
 
Mara siku nyingine asilale kwenye nyumba ya bwana shamba.
 
Mara ajizungushie ulinzi wa “bahima”
 
Sasa akaamua naye atume ujumbe kwa wazee

Ujumbe  kuwatisha wazee
 
Hili lilikuwa ni moja ya kosa lake kubwa

Sogelea telegram link 👇

t.me/fbuyobe

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling