Fortunatus Buyobe Profile picture
Mar 12, 2023 18 tweets 6 min read Read on X
CODE AND DECODE

The Dark day 11st Sept 2017
 
Ni jumatatu Kisiwani
 
Jamaa fulani anaona pikipiki mbili zinampita kwa mwendo wa kasi sana.
 
Kila pikipiki imebeba abiria wawili(mshikaki)
 
Hii ni baada ya kusikika milio mitano ya risasi
 
Yes A Dark day indeed Image
Baadae zikasambaa habari pale kisiwani kuwa Mlinzi mmoja wa mpaka wa shamba alikuwa “kalambwa vyuma” vitano na majambazi.
 
Naam!
 
It was a news tailored for journalists digest
 
Lakini nyuma ya pazia walinzi wa mipaka walikuwa wamegombana na bwana shamba two years back. Image
Kwanza walimchukia bwana shamba kwa kumleta kijana mdogo tu ndio awe kilanja wao lindoni.
 
Kijana huyo hakuwa na elimu dunia ya kutosha zaidi yao.
 
Yeye elimu dunia yake iliishia tu shule ya upili. Image
Elimu pekee aliyokuwa amebobea ni maswala ya mipaka.
 
Hakutegemewa kuwa Kilanja
 
Wakulima waliendelea kula ubwabwa na maharage na kwenda kulala.
 
Bila kujua mpakani mwa shamba kuna chess inachezwa.
 
Sasa Bwana shamba kuna maelekezo alitoa kwa kilanja akawaambie wenzake. Image
Ule haukuwa utaratibu
 
Namaanisha nini?
 
Yaani pale mpakani huwa kuna wazee ambao kiutaratibu kukiwa na jambo lolote, basi bwana shamba anatakiwa aongee nao pamoja akiwemo kilanja wao.
 
Sasa huu utaratibu wa kumtuma kilanja aongee nao hawakuupenda.
 
Na zaidi ya yote, Image
Maelekezo yaligusa maslahi yao
 
Unajua pale mpakani kulikuwa na Zabuni nyingi sana kuanzia catering services, Mafuta n.k
 
Zabuni hizi zilikuwa kiutaratibu zinachukuliwa na wazee ili nao wafurahie keki ya shamba kidogo. Image
Kwani wazee walikuwa wanaona wizi mkubwa tu pale shambani na kukaa kimya.
 
Zile zabuni angalau zilikuwa zinawafanya wazee wakae kimya na kutoingilia kwani uwezo wa kuingilia wanao na wanaweza kumweka bwana shamba yeyote kutokea kwenye kundi lao la wazee. Image
Sasa maelekezo yakatolewa kwa kilanja kwenda kwa wazee.
 
Kuwa zabuni sasa basi!
 
Yaani mchakato wa zabuni mpakani utakuwa unafanywa na bwana shamba kuanzia siku ya maelekezo hayo.
 
Mkutano ulikuwa wa moto!
 
Wazee wakafura!
 
Wakamuuliza kilanja huyo bwana shamba yuko wapi? Image
Kwa nini kakutuma wewe asije hapa azungumze hayo mbele yetu?
 
Wakamwambia unajua wewe ingawa ni kilanja lakini wewe ni bwana mdogo sana.
 
Wakamwabia kwanza wewe umeishia shule ya upili.. wewe sio size yetu, kamwite bwana shamba aje atueleze hayo. Image
Kilanja akarudisha zile taarifa kwa bwana shamba.

Bwana shamba alikuwa na tabia za ujeuri,
 
Hakuwa anapenda hata siku moja aonacho yeye ni sahii atokee mtu wa kukipinga. Image
Alishapewa ushauri na kilanja wa zamani kuwa kuna nyaya za kuchezea pale shambani lakini sio nyaya za transformer.
 
Hata bwana shamba wa zamani alimshauri hilo
 
Yeye hakutaka kusikia,

Sasa taarifa zile za mkutano wa mpakani zikamjia.
 
Akapuuzia kwenda mkutanoni. Image
Yeye akaanza kuwa anajihusisha na zabuni za watu wa mpakani.
 
Yaani wazee waliendelea kuhudumiwa bila wao kumtafuta muhudumu.
 
Bwana shamba hakujua kama swala lile ni nyeti.
 
Hakujua kama vikao vya usalama ndivyo vilivyoamua kuwa wazee wajipe zabuni wenyewe za kujihudumia. Image
Sababu kubwa ilikuwa kuwa kama mtu kutoka nje angewahudumia, angeweza kuwafanya chochote walinzi wa mpaka.
 
Mtu wa nje angeweza kuwa compromised akawawekea hata sumu kwenye chakula Image
Wazee walipoona tu Bwana shamba amewakwepa na kuanza kuwawekea watu wa nje kuwahudumia wakaamua kuandika barua kwa pamoja kuomba kuacha ulinzi.
 
This action a distress message security wise
 
Ikabidi bodaboda guy amfate bwanashamba. Image
Bodaboda guy without mincing words dared to inform Bwana shamba kuwa “Mzee hapa inamaanisha umeng’oa kiraka kwenye jeans ya bishoo”
 
Akamwambia “Find a way to resolve the matter before this deteriorated relationship with “wazee” sours much more.
 
Kama kawaida jamaa hapangiwi Image
Jamaa akaona hakuna threat yoyote
 
Lakini akawa ni mtu wa wasiwasi mwingi
 
Mara siku nyingine asilale kwenye nyumba ya bwana shamba.
 
Mara ajizungushie ulinzi wa “bahima”
 
Sasa akaamua naye atume ujumbe kwa wazee Image
Ujumbe  kuwatisha wazee
 
Hili lilikuwa ni moja ya kosa lake kubwa Image
Sogelea telegram link 👇

t.me/fbuyobe

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Fortunatus Buyobe

Fortunatus Buyobe Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @fbuyobe

Sep 6, 2025
Huko Harare, Zimbabwe katika barabara ya Borrowdale, kuna eneo la maduka makubwa maarufu kwa jina la Ballantyne Park Shopping Centre

Mwaka 2008, ilikuwa ukienda katika duka No. 19 kwenye maduka haya, ungekutana na mgahawa maarufu wa Millers Cafe

Mgahawa huu umebeba simulizi Image
Siku moja mchana mwaka 2008, nikiwa nimeboreka, niliingia kwenye mgahawa wa Millers

Niliongoza kwenye kiti kimojawapo ndipo nikasikia sauti ya mtu aliyekuwa ameketi nyuma yangu ikiniita

Nilipogeuka nikashtuka kubaini anayeniita ni mchungaji Uebert Angel Mudzanire Image
"Kijana, tangu ulipokuwa unaingia ndani ya mgahawa nimekuwa naona namba 33 kwenye paji la uso wako"

Aliniambia Mchungaji Angel

Sikumuelewa hivyo ikabidi nimuulize mchungaji:-

"Unataka kumaanisha nini?"

Jibu alilonipa lilikuwa mbali na uhalisia Image
Read 24 tweets
Sep 5, 2025
𝐒𝐨𝐦𝐞𝐭𝐢𝐦𝐞𝐬 𝟐𝟎𝟐𝟑

𝐋𝐨𝐠𝐢𝐬𝐭𝐢𝐜𝐬 𝐂𝐚𝐦𝐩
𝟖𝟑𝟏 𝐊𝐉
𝐌𝐆𝐔𝐑𝐀𝐍𝐈

𝟎𝟓𝟒𝟐 𝐇𝐑𝐒

Lutueni Kanali E.A Sambila ambaye ndiye Commanding Officer wa 831 KJ anapokea taarifa nyeti ofisini kwake kutoka kwa askari wake wawili wahusikao na ulinzi amani kikosini (MPs) Image
Askari hawa wawili ambao ni P.12925 Captain Theresia Cylil Massawe na MT. 88710 Sergeant Mohammed Faki Haji walifika ofisini kwa Lt.Gen Msambila wakieleza kuwa wana taarifa ya dharula

Kuwa kuna uwezekano wa muda wowote amani kutoweka mle kikosini

Wakaruhusiwa kuingia Image
Taarifa inayotolewa mbele ya CO, inalazimu muda mfupi unaofuata, askari wale wawili, kwa maelekezo ya CO wavamie ofisini kwa serviceman MT. 85115 Sergeant Sahani

Askari yule anawekwa chini ya ulinzi, na kwenye upekuzi, wanachukua simu mbili anazomiliki

Upekuzi ukahamia nyumbani Image
Read 13 tweets
Aug 30, 2025
Tarehe 28 August 2025, chama tawala, CCM kilizindua kampeni zake za uchaguzi mkuu wa urais na wabunge katika viwanja vya Tanganyika packers

CCM walilazimika kutumia jukwaa hilo la uzinduzi wa kampeni kujibu mashambulizi kutoka kwa mwanachama wake mwandamizi Humphrey Polepole Image
Image
Tangu kujiuzuru kwake July 13, mwaka huu kwa kile alichoeleza kama "kutoridhishwa na mienendo" ya serikali yake, balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Cuba, amekuwa akitoa tuhuma mbalimbali dhidi ya viongozi waandamizi wa chama chake na serikali Image
Image
Polepole ameeleza juu ya uwepo wa kikundi anachokiita "CCM mtandao" ambacho huakikisha wanaohodhi madaraka ya rais

Kuwa mtandao huo nchini tangu mwaka 1995 zilipoanza siasa za vyama vingi na mtandao huu una agenda ya kuhakikisha kila rais anakuwa chini ya himaya yao Image
Read 45 tweets
Aug 2, 2025
Una uhakika kuwa wewe binafsi ulionana na IGP Sirro?

Unaweza kunieleza kwa ushaidi ni mara ngapi na wapi ulionana naye?

Unajua kuwa tuhuma unazotoa ni nzito ukihusisha watu wakubwa sana nchini?

Ilikuwa zamu yangu kuanza kumhoji mwanamama Jeannie Pollaert raia wa Netherlands Image
Nililazimika kumuuliza mama huyu maswali haya usiku wa manane baada ya kumaliza kusoma makabrasha mengi aliyonitumia kwa njia ya barua pepe.

Nilichokikuta ndani ya makabrasha yale kilifanya usingizi uliokwishaanza kunitongoza utoweke

Infact niliogopa sana

Nilihitaji ushaidi Image
Itakuwaje endapo Simon Sirro atakana kuwahi kukutana na wewe na kufanya na wewe kikao chochote?

Lilikuwa swali langu la kwanza.

Jeannie: Itakuwa vigumu sana kwa Sirro kukataa kuwa hajakutana nami

Akanipa ushaidi wa mawasiliano yao na jinsi Sirro alivyomjibu Image
Image
Read 25 tweets
Jun 27, 2025
Mwaka 2012, Blandine Nyoni akiwa katibu mkuu wizara ya afya, alinukuliwa akitoa kauli tata ya kuwabeza madaktari kuwa "wanajiona bora wakati ni wachafu na hawajui kiingeleza" Image
Katibu huyu akaendelea kusema kuwa hata yeye alisoma mchepuo wa PCB na kufaulu vizuri tu lakini kwa kutambua ubovu wa Medicine mzazi wake akamsomesha Accounts so hajui madaktari wanalalamikia nini.

Kauli hii ikang'oa kilaka kwenye jeans ya bishoo! Image
Ni kwamba mwaka huo, madaktari walikuwa katikati ya mgomo wa kihistoria

Kauli hii ikawatibua madaktari wakalianzisha upyaaaaa

Uzi👇

Dr. Ulimboka and total tools down

Nisome Image
Read 76 tweets
May 9, 2025
Wiki hii tumeshuudia waliokuwa wanachama wa Chadema wakitangaza kuachana na chama hicho huku wakiahidi kuelezea hatima zao za kisiasa siku za mbeleni

Kati ya waliohama ni waliowahi kuwa viongozi waandamizi wa chama hicho

Hii inamaanisha nini? Image
Kabla sijajibu swali hilo ni vyema tukipitia kwa ufupi mtiririko wa matukio (A quick refresher)

1. Dec 12,2024, Tundu Lissu anatangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA taifa

Nia hii ya Lissu ilikuja baada ya kuwa uchokozi wa wazi dhidi yake ndani ya chama Image
Kabla ya uamuzi huu, Lissu aliyekuwa ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA, alishamwandikia barua katibu mkuu wake kumjuza nia yake ya kuendelea kugombea kubaki kwenye nafasi hiyo.

Ulikuwa ni utaratibu wa CHADEMA kwa viongozi wa juu kutoshindania nafasi moja endapo mmoja ataonesha nia Image
Read 34 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(