LUSAJO Profile picture
Grow your Company/Business Sales with Me | Increase your Market Outreach with Me | I'm the Founder & MD at @ebdigitaltec | JESUS IS MY LORD

Jun 12, 2023, 26 tweets

Biashara ya wife ni kuuza mitumba. Na mimi huwa nashiriki katika hatua mbalimbali za kumsupport

Mpaka ikanifanya niijue vizuri biashara hii. nimejua chimbo zote muhimu za kununua, nimejua chimbo nzuri za kuuzia

Na hii ni stori ya kuwatia moyo wanaotaka kuwekeza ktk biashara hii

Miezi kadhaa nilishawahi kuleta Uzi flani kuhusu mimi. Na wengi mliusoma na nilielezea ktk hustle zetu me na wife, tushawahi kufanya mishe za kuuza mitumba.

Tulianzaje, tuliendeleaje na ikawaje? Twende pamoja. Leo nitawapa hatua tulizopitia na mwisho mtaona hii biashara

kama itakufaa kuweza kuanza.
Ingawa wengi husema kwamba biashara ya nguo sio nzuri na haifai. Leo natoa Darasa hatua kwa hatua kupitia mifano tuliyoipitia na kujifunza.

Tulipofunga ndoa mimi na mke wangu tulikaa na kujadiliana tuanze na mradi gani.

Wakati huo tulicancel send-off yake na hatukufanya sherehe zaidi ya kutoka kanisani kwenda kupiga picha na kwenda Honeymoon.

Hii tulifanya kutokana na malengo makuu mawili.
1. Kukwepa madeni ya sherehe za harusi.
2. Kupata kianzio cha miradi yetu.

Ambapo tulifanikiwa malengo.

Baada ya Harusi tulikaa na kuona kiasi cha mapato kilichotokana na zawadi ili ni almost Mil.4 kasoro.

Na tulikatisha honeymoon ili tuwahi kurudi Dar mapema na tuanze na mipango yetu.

Those days Mimi nilikuwa nafanya kazi kanisani, na wife alikuwa na ajira ktk

kampuni moja ya mawasiliano. Alipoomba kuhamishwa kutoka Mbeya kwenda Dar, walimkatalia. Akaamua kuacha kazi.

Sasa tulipoanza life, tukaazimia kwamba tufungue biashara ya nguo za mtumba.

Kutokana na uzoefu wa wife, sikuwa na shaka nae. Tulifanya hivyo.

Tukaplan kuanza kuuza kupitia mitandao.

Tukaenda Kariakoo. Lengo ilikuwa kununua balo la blouse aina ya chiffon.

Kutokana na ugeni wa kununulia mizigo Dar, tukaelekezwa twende Kitumbini.

Tukaenda. Tukazunguka sana. Na hatukuwa na guide yoyote. Katika kuzunguka,

tulienda mtaa mwingine Mnazimmoja huko. Tukafanikiwa kupata mzigo kwa mpakistani mmoja hivi.

Waakituaminisha kwamba mzigo ni mzuri kabisaa. Kwa jinsi tulivyo ambiwa, nilisuuzika moyo kabisa.

Tukaljpia na kuondoka, kurudi nyumbani. Hapo tuliazimia kununua balo moja kwanza.

Tulipofika home bila kulaza damu, tukafungua mzigo wetu. Asalahleeh!! Tulikuta ni kazi mbovu kuliko tulicho tarajia.

Katika blouse almost 260 tulipata 50 pekee. Ikawa ni hasara sana.

Tukawa tumepoteza 350k ya kwanza. Tukawa na rundo la nguo ambalo halina tija ndani.

Unaweza kujiuliza kwanini tulichagua chiffon blouses. Kabla hatujaanza tulifanya research ya nguo ambazo zinanunuliwa sana na zinatokea kwa wingi. Ndio maana tulichagua nguo hizo.

Baada ya hapo, tuliingia tena mfukoni kuchukua balo lingine. Ambalo tuliamua kununua duka ingine.

Tukaenda pale na kununua chiffon nzuri kweli kweli tulizipenda sana.

Sasa lile balo lilikuwa ni la China. Aiseee... zile blouse zilikuwa Kali sana tena za moto. Na nyingi zilikuja na vile vilable vya kuonesha kwamba ni mpya, haijavaliwa kabisa.

Lakini vilikuwa VIDOGO kwa size

Kwahiyo tukauza chache. Na zingine zilibaki na kuingia hasara ya pili.

Tunaendelea kujifunza taratibu taratibu. Tukanunua mzigo wa tatu kutoka Uarabuni.

Aiseee... Zilikuja nguo nzuri sana, hadi saiz za Wanyakyusa zilikuwepo za kumwaga.

Sasa pale ndipo tulipoanza kuona faida.

Tulinunua balo kwa laki 4 na tulipata nguo almost 250 lkn ronya zilikuwa kama 20 tu. So, tukiuza takriban nguo 230×6000tsh ambapo tulipata almost 1.4Mil.

Faida ilikuwa kama Milioni hivi kwa huo mzigo.

Na sisi tulikuwa tunauza kwa jumla ili tuuze kama Ilala. So wateja wengi

walikuja home kusasambua na kuondoka na mafurushi hayo.

Ndani ya siku mbili mzigo ulitembea, baada ya siku 2 mbili tukanunua balo 2 kwa 800.

Moja la Canada lingine la Dubai (Arabuni)

Tukawatangazia tena wateja wetu. Uzuri wake, tulitengenezaa database ya wateja wetu.

So mzigo ulikuwa ukishuka tu, nao walikuwa wakisubiria kwa ajili ya kugombea nguo.

Na tulifanikiwa kupata wateja wengi wenye maduka Sinza, Makumbusho, Kinondoni na Mbezi beach.

Sasa tulipofungua yake mabalo mawili, Mungu mkubwa, nguo za Canada zilikuwa nzuri na kubwa

Na kama mjuavyo nguo kubwa ni deal sana. Lile bale lilikuwa na nguo nyingi nzuri na kubwa kubwa.

Na zote zilikuwa ni chiffon. Na karibu kila nguo ilikuwa na kile kikaratasi kinachoonesha ni mpya.

So, wanunuaji walikuwa wanazichukua sana zile nguo.
Kwa mara ingine tuliuza

kwa kiwango kikubwa. Nakumbuka baada ya purukushani kuisha, tulijikuta tuna milioni 3 na ushehe.

Tukanogewa 😂😂
This time tukasema tuwaletee magauni ya chiffon. Kwa sababu walikuwa wanahitaji sana.

Tukashusha balo 2 za 650k@1 kwahiyo 1.3mil tuliizamisha kwenye magauni.

Tulifungua Moja kwanza kuona trend yake ikoje.

Tulifanikiwa kupata almost gauni 200 hivi na ronya zilikuwa chache sana hata 20 hazikufika. Na magauni tuliza Tsh 8000 kwa jumla. Nikiangalia kwenye daftari hapa naona tulipata 1.5Mil

Na siku hiyo hadi ronya zilichukuliwa 😂😂

Tukaambia tena Jumamosi waje ambayo tutatoa magauni. Ila waje mapema sana.

Ile Jumamosi, walifika saa 1 nikatoa mzigo na kuupasua pale. Wkaushanbulia sana. Nguo zake zilitoka ni nzuri sana zote zilikuwa mpya.

Kwa mara ya kwanza tulipata balo lililokuwa na ronya 5 tu😂

Na zile nguo zilivyokuwa nzuri tukibadili maamuzi haraka na wife, na kuwaambia balo hili ni 10k kwa Kila gauni. Na hawakubisha 😂😂

Ile Jumamosi tulipata 2.4 Mil.

Kwahiyo tulijikuta tumepata almost Mil. 4. Na hapo tulikuwa tunauzia kwa njia ya kutangaza kwa simu.

Tulipata wateja wengi, na wao walileta wateja wengine. Pale home palikuwa kama Ilala kwa siku za Jumamosi.

Mwenye nyumba alituambia ishakuwa kero kwake. Akatushauri tukapange frame.

Tukawaza namna ya kuingia kwenye frame. Tukaanza kutafuta pa kuwekea. Wakati tunaendelea,

alikuwepo mteja mmoja ambaye tulifahamu hadi duka lake liliko. Pia tulimwamini.

Akaomba achukue mzigo wa laki 7 na turudishie ndani ya wiki moja. Tukaona sio tabu. Tukamuamini, tulimpa.

Jamaa hakuonekana ofisini kwake na hakupokea na baadae hakupatikana Hadi leo.

Tulipitia changamoto kadha wa kadha hapo katikati ikiwa pamoja na kuuguza mpaka tukadrop tena.

Baada ya miezi sita hivi niliokea simu kutoka kwa Rafiki yangu wa Botswana, ambako nikienda familia yao wananipokea na kunitunza hapo Ramotswa, Gaborone.

Alipenda sana nguo ambazo nilikuwa nashare kwenye status. Akaniomba na yeye nimnunulie mabalo 5 ya nguo tofauti kulingana uhitaji wake.

Alinitumia Mil. Tatu na kidogo. Nikamnunulia na Kisha nikabakiwa na faida ya 1. Mil

Sasa kwa sababu sikuwa na simu nzuri

kwa ajili ya picha. Simu yangu ilikuwa inatoa ukungu. Nikaamua kununua simu nzuri ya kupigia picha.

Nikazama Kkoo kwa @NjiwaFLow nikajinunulia simu. Though hakunifahamu ila Mimi nilimfahamu 😂😂

Then nikawa na simu ya kupigia picha bidhaa zetu.

Endelea sehemu ya pili 👇🏾

Share this Scrolly Tale with your friends.

A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.

Keep scrolling