LUSAJO Profile picture
Jun 12, 2023 26 tweets 8 min read Read on X
Biashara ya wife ni kuuza mitumba. Na mimi huwa nashiriki katika hatua mbalimbali za kumsupport

Mpaka ikanifanya niijue vizuri biashara hii. nimejua chimbo zote muhimu za kununua, nimejua chimbo nzuri za kuuzia

Na hii ni stori ya kuwatia moyo wanaotaka kuwekeza ktk biashara hii ImageImageImage
Miezi kadhaa nilishawahi kuleta Uzi flani kuhusu mimi. Na wengi mliusoma na nilielezea ktk hustle zetu me na wife, tushawahi kufanya mishe za kuuza mitumba.

Tulianzaje, tuliendeleaje na ikawaje? Twende pamoja. Leo nitawapa hatua tulizopitia na mwisho mtaona hii biashara
kama itakufaa kuweza kuanza.
Ingawa wengi husema kwamba biashara ya nguo sio nzuri na haifai. Leo natoa Darasa hatua kwa hatua kupitia mifano tuliyoipitia na kujifunza.

Tulipofunga ndoa mimi na mke wangu tulikaa na kujadiliana tuanze na mradi gani.
Wakati huo tulicancel send-off yake na hatukufanya sherehe zaidi ya kutoka kanisani kwenda kupiga picha na kwenda Honeymoon.

Hii tulifanya kutokana na malengo makuu mawili.
1. Kukwepa madeni ya sherehe za harusi.
2. Kupata kianzio cha miradi yetu.

Ambapo tulifanikiwa malengo.
Baada ya Harusi tulikaa na kuona kiasi cha mapato kilichotokana na zawadi ili ni almost Mil.4 kasoro.

Na tulikatisha honeymoon ili tuwahi kurudi Dar mapema na tuanze na mipango yetu.

Those days Mimi nilikuwa nafanya kazi kanisani, na wife alikuwa na ajira ktk
kampuni moja ya mawasiliano. Alipoomba kuhamishwa kutoka Mbeya kwenda Dar, walimkatalia. Akaamua kuacha kazi.

Sasa tulipoanza life, tukaazimia kwamba tufungue biashara ya nguo za mtumba.

Kutokana na uzoefu wa wife, sikuwa na shaka nae. Tulifanya hivyo.
Tukaplan kuanza kuuza kupitia mitandao.

Tukaenda Kariakoo. Lengo ilikuwa kununua balo la blouse aina ya chiffon.

Kutokana na ugeni wa kununulia mizigo Dar, tukaelekezwa twende Kitumbini.

Tukaenda. Tukazunguka sana. Na hatukuwa na guide yoyote. Katika kuzunguka, Image
tulienda mtaa mwingine Mnazimmoja huko. Tukafanikiwa kupata mzigo kwa mpakistani mmoja hivi.

Waakituaminisha kwamba mzigo ni mzuri kabisaa. Kwa jinsi tulivyo ambiwa, nilisuuzika moyo kabisa.

Tukaljpia na kuondoka, kurudi nyumbani. Hapo tuliazimia kununua balo moja kwanza. Image
Tulipofika home bila kulaza damu, tukafungua mzigo wetu. Asalahleeh!! Tulikuta ni kazi mbovu kuliko tulicho tarajia.

Katika blouse almost 260 tulipata 50 pekee. Ikawa ni hasara sana.

Tukawa tumepoteza 350k ya kwanza. Tukawa na rundo la nguo ambalo halina tija ndani. Image
Unaweza kujiuliza kwanini tulichagua chiffon blouses. Kabla hatujaanza tulifanya research ya nguo ambazo zinanunuliwa sana na zinatokea kwa wingi. Ndio maana tulichagua nguo hizo.

Baada ya hapo, tuliingia tena mfukoni kuchukua balo lingine. Ambalo tuliamua kununua duka ingine. Image
Tukaenda pale na kununua chiffon nzuri kweli kweli tulizipenda sana.

Sasa lile balo lilikuwa ni la China. Aiseee... zile blouse zilikuwa Kali sana tena za moto. Na nyingi zilikuja na vile vilable vya kuonesha kwamba ni mpya, haijavaliwa kabisa.

Lakini vilikuwa VIDOGO kwa size Image
Kwahiyo tukauza chache. Na zingine zilibaki na kuingia hasara ya pili.

Tunaendelea kujifunza taratibu taratibu. Tukanunua mzigo wa tatu kutoka Uarabuni.

Aiseee... Zilikuja nguo nzuri sana, hadi saiz za Wanyakyusa zilikuwepo za kumwaga.

Sasa pale ndipo tulipoanza kuona faida.
Tulinunua balo kwa laki 4 na tulipata nguo almost 250 lkn ronya zilikuwa kama 20 tu. So, tukiuza takriban nguo 230×6000tsh ambapo tulipata almost 1.4Mil.

Faida ilikuwa kama Milioni hivi kwa huo mzigo.

Na sisi tulikuwa tunauza kwa jumla ili tuuze kama Ilala. So wateja wengi Image
walikuja home kusasambua na kuondoka na mafurushi hayo.

Ndani ya siku mbili mzigo ulitembea, baada ya siku 2 mbili tukanunua balo 2 kwa 800.

Moja la Canada lingine la Dubai (Arabuni)

Tukawatangazia tena wateja wetu. Uzuri wake, tulitengenezaa database ya wateja wetu.
So mzigo ulikuwa ukishuka tu, nao walikuwa wakisubiria kwa ajili ya kugombea nguo.

Na tulifanikiwa kupata wateja wengi wenye maduka Sinza, Makumbusho, Kinondoni na Mbezi beach.

Sasa tulipofungua yake mabalo mawili, Mungu mkubwa, nguo za Canada zilikuwa nzuri na kubwa
Na kama mjuavyo nguo kubwa ni deal sana. Lile bale lilikuwa na nguo nyingi nzuri na kubwa kubwa.

Na zote zilikuwa ni chiffon. Na karibu kila nguo ilikuwa na kile kikaratasi kinachoonesha ni mpya.

So, wanunuaji walikuwa wanazichukua sana zile nguo.
Kwa mara ingine tuliuza Image
kwa kiwango kikubwa. Nakumbuka baada ya purukushani kuisha, tulijikuta tuna milioni 3 na ushehe.

Tukanogewa 😂😂
This time tukasema tuwaletee magauni ya chiffon. Kwa sababu walikuwa wanahitaji sana.

Tukashusha balo 2 za 650k@1 kwahiyo 1.3mil tuliizamisha kwenye magauni. Image
Tulifungua Moja kwanza kuona trend yake ikoje.

Tulifanikiwa kupata almost gauni 200 hivi na ronya zilikuwa chache sana hata 20 hazikufika. Na magauni tuliza Tsh 8000 kwa jumla. Nikiangalia kwenye daftari hapa naona tulipata 1.5Mil

Na siku hiyo hadi ronya zilichukuliwa 😂😂 ImageImageImage
Tukaambia tena Jumamosi waje ambayo tutatoa magauni. Ila waje mapema sana.

Ile Jumamosi, walifika saa 1 nikatoa mzigo na kuupasua pale. Wkaushanbulia sana. Nguo zake zilitoka ni nzuri sana zote zilikuwa mpya.

Kwa mara ya kwanza tulipata balo lililokuwa na ronya 5 tu😂
Na zile nguo zilivyokuwa nzuri tukibadili maamuzi haraka na wife, na kuwaambia balo hili ni 10k kwa Kila gauni. Na hawakubisha 😂😂

Ile Jumamosi tulipata 2.4 Mil.

Kwahiyo tulijikuta tumepata almost Mil. 4. Na hapo tulikuwa tunauzia kwa njia ya kutangaza kwa simu. ImageImage
Tulipata wateja wengi, na wao walileta wateja wengine. Pale home palikuwa kama Ilala kwa siku za Jumamosi.

Mwenye nyumba alituambia ishakuwa kero kwake. Akatushauri tukapange frame.

Tukawaza namna ya kuingia kwenye frame. Tukaanza kutafuta pa kuwekea. Wakati tunaendelea,
alikuwepo mteja mmoja ambaye tulifahamu hadi duka lake liliko. Pia tulimwamini.

Akaomba achukue mzigo wa laki 7 na turudishie ndani ya wiki moja. Tukaona sio tabu. Tukamuamini, tulimpa.

Jamaa hakuonekana ofisini kwake na hakupokea na baadae hakupatikana Hadi leo.
Tulipitia changamoto kadha wa kadha hapo katikati ikiwa pamoja na kuuguza mpaka tukadrop tena.

Baada ya miezi sita hivi niliokea simu kutoka kwa Rafiki yangu wa Botswana, ambako nikienda familia yao wananipokea na kunitunza hapo Ramotswa, Gaborone.
Alipenda sana nguo ambazo nilikuwa nashare kwenye status. Akaniomba na yeye nimnunulie mabalo 5 ya nguo tofauti kulingana uhitaji wake.

Alinitumia Mil. Tatu na kidogo. Nikamnunulia na Kisha nikabakiwa na faida ya 1. Mil

Sasa kwa sababu sikuwa na simu nzuri Image
kwa ajili ya picha. Simu yangu ilikuwa inatoa ukungu. Nikaamua kununua simu nzuri ya kupigia picha.

Nikazama Kkoo kwa @NjiwaFLow nikajinunulia simu. Though hakunifahamu ila Mimi nilimfahamu 😂😂

Then nikawa na simu ya kupigia picha bidhaa zetu.

Endelea sehemu ya pili 👇🏾

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with LUSAJO

LUSAJO Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @sajo_mwaihabi

Feb 17
Ulishawahi kusikia neno FRANCHISING katika ulimwengu wa kibishara?

Naamini wengi wameshawahi kusikia lakini hawajawahi kufuatilia kwa undani kuhusu FRANCHISE BUSINESS.

Uzi huu usiochosha umeonesha FRICHISE BUSINESS inavyoendeshwa na kuleta mafanikio, bila kusahau changamoto zakeImage
Kufranchise ni nini?

Franchise ni mfumo wa biashara ambapo mwenye BRAND ya biashara (Franchisor) anampa mjasiriamali mwingine (Franchisee) haki ya kutumia jina la biashara, Brand, mifumo ya uendeshaji, na bidhaa au huduma kwa MASHARTI na MAKUBALIANO maalum.
Ni wazi kwamba Tanzania ni baadhi ya watu ambao wana ufahamu na uelewa wa uwekezaji huu.

Kiasi ambacho wengi wangekuwa wanafahamu, wangekubali kufanya INVESTMENT kwa brand ambazo tayari zinajiuza.

Kwahiyo, Frinchisor anakuwa INVESTOR katika Brand ile kwa eneo ulilochagua.
Read 18 tweets
Apr 3, 2024
Siku Moja katika mwezi wa 9 mwaka jana, nilipigiwa simu na kampuni fulani maeneo ya Mikocheni.

Waliniomba nikafanye training ya team yao kwa Sababu MAUZO YAMEDUMAA na yanaelekea kufa kabisa.

Niligundua UGONJWA ambao unatesa kampuni nyingi hapa TZ.

Shuka na 🧵 tujifunze
Nilipofika, kama ilivyo kawaida yangu, siwezi kuanza session mpaka nikae na viongozi waniambie tatizo, ndipo ning'amue tatizo. Na baada ya hapo ndio najua angle ya kuishighulikia kama ni Uongozi au ni Team au wote kwa pamoja.

Na hapa siku yangu ilikuwa ndefu. Stori Iko hivi;
Nilipokelewa na viongozi wakiwepo wamiliki yaani Directors ambao ni Mr & Mrs.

Nikawauliza, "Mmenihitaji, nimekuja. Je, mnataka nifanye session gani kwa team?"

CEO: "Yaani kikubwa sisi tunataka mauzo yapande maana hapa mauzo yameshuka, Nikisafiri ndo basi tena"
Read 23 tweets
Feb 10, 2024
Nasaha za Mzee wangu siku Moja kabla ya Harusi. Soma mpaka mwisho itakusaidia

Mwanangu Lusajo, unapoenda kuishi na mwenza wako, sio kila kitu cha kumfanyia surprise mke wako.

Surprise ni catalyst ya Mapenzi lakini pia shetani anaweza kutumia njia ya surprise kuua ndoa yako.

👇🏾 Image
Sikiliza mwanangu, Surprise sio utamaduni wetu, bali ni utamaduni wa kizungu.

Nilipoenda kusoma St. Catherine Brock University, Ontario Canada mwaka 1976, ndio niliyakuta mambo hayo. Na jamii ya kizungu ndio waliokuwa wakifanya mambo hayo sana.

Nilishangaa sana kuona hayo mambo Image
Maana kipindi hicho hata maswala ya ATM hatukuwahi kufikiria ila nilipoenda nikakutana na mdogo wangu Augustine Mahiga (The Late)

Yeye alikuwa anasoma chuo cha UofT. Na tulikutana Ubalozini nakufahamina.

Kwa kuwa yeye alinitangulia kukaa kule, ndio alinifundisha kutumia ATM 😅 Image
Read 20 tweets
Jul 26, 2023
UJASUSI KATKA BIASHARA

Ili biashara yako IFANIKIWE SOKONI Kuna haja kubwa sana ya kuwa JASUSI. Na hii ndio jambo kubwa ambalo litakusaidia kukaa kwenye soko.

Kwa dakika chache tushuke na uzi mfipi kuona ujasusi huu ukoje, unafanyikaje na una faida gani. 🧵👇🏾 Image
UJASUSI WA KIBIASHARA ni moja ya mbinu inayotumika katika kufanya Tafiti za Masoko (Marketing Research).

Hii itakupa picha ya namna Bora ya kuanzisha bishara au kuingiza bidhaa.

Hakuna Kampuni kubwa isiyofanya hayo mambo kwa mshindani wake.

Hufanya hivyo kwa SIRI kubwa sana Image
Inawezekana hujanielewa!!

UJASUSI ni kutaka kujua SIRI ambazo ziko nyuma ya biashara. Kwa sababu hakuna chenye mafanikio kisicho na Siri yake.

Na SIRI ni MTAJI wa kuendesha biashara yoyote na ikafanikiwa.

Siku zote mfanyabiashara atakupa NJIA na hatakupa SIRI.

Twendelee👇🏾 Image
Read 8 tweets
Jul 8, 2023
Leo asubuhi nilipoamka, na kuingia Twitter, nilikutana na tweet ya @iamKaga ambayo alielezea issue ya vyombo.

Na Mimi nikasema wacha niende nikashuhudie. Na nikivutiwa, nanunua kabisa.

Nilifika pale godown, na kweli nilivutiwa na vyombo vya pale. Kisha nikachukua vyombo vya 9kg
Ambayo vina thamani ya Tsh 40,500/- baada ya kutoka hapo, nikavipeleka home na kupiga picha na kushare kwenye status.

Na sijawahi kuweka status ya kuuza vyombo. Niliamua kuuza kwa set.

Ghafla nikatafutwa na jamaa mmoja, mmiliki wa Pub moja maarufu pale Mbeya.





Anafungua ingine Dodoma.

So alipoona ile status. Akaamua akanichek na kunipa order yake ya vyombo Jumatatu namtumia mzigo wake.

Ahsante sana Kaga kwa kushirikisha fursa, ningepuuzia, huu mtonyo ningeupata wapi leo? 😂😂



Read 4 tweets
Jun 23, 2023
Wiki hii, nimefanikiwa kufika katika ofisi za kampuni tatu kwa ajili ya kufanya consultation za kibiashara.

Kuna mambo ambayo nimebaini na ni changamoto ambazo nimezikuta almost kwenye kampuni zote tatu.

Wacha niwasogezee, kisha nawe ufaidike kwa kujua haya maana yatasaidia
1. Watu wengi hufungua kampuni kwa sababu wana fedha za kufungulia lkn wamekosa kufanya mambo ya msingi kwa ajili ukuaji wa kampuni husika.

Mambo hayo ni:-
◾Hawana DHUMUNI maaalum la kampuni.
◾Hawajafanya RESEARCH juu ya Kampuni.
◾Hawajafanya chaguzi sahihi za JINA
◾Hawajapata elimu nzuri juu ya uendeshwaji wa kampuni mpaka kupelekea kuwa na Kodi na tozo ambazo hawazielewi.
◾Wameandaliwa MEMORANDUM AND ARTICLE OF ASSOCIATION (MEMART) zinazo walimit kufanya shughuli zao. Haziwapi wigo mpana.
Read 13 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(