Miaka miwili tangu kuanza kwa sheria na kanuni za UWEZESHAJI WAZAWA (LOCAL CONTENT) kwenye madini hapa Tanzania je tunasonga mbele na kupata matokeo yaliyokusudiwa?
Je ushiriki wa Wazawa kwenye uchumi wa madini (manunuzi, ajira na uongezaji thamani) ukoje hata sasa?
Makampuni yanayomilikiwa na wazawa yanawezeshwaje ili kushiriki na kushindana kupata zabuni kwenye sekta ya Madini?
Makampuni yanayomilikiwa na Wazawa yanapata taarifa za kutosha juu ya fursa na zabuni mbalimbali zinazotelewa na makampuni ya madini na migodi hapa Tanzania? #localcontent
Wadau wa UWEZESHAJI WAZAWA wanatimiza wajibu wao?
Je kuna haja ya kuwa na mjadala wa pamoja wa wadau juu ya suala la UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya Madini na sekta zingine zinazoingiliana?
UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya madini una husiana na UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta zingine za kiuchumi hapa Tanzania?
Nani anawajibika kuandaa nguvu kazi (labourers) wa kufanya kazi migodini na sekta nzima ya madini katika kuona wazawa wanakuwa tayari na ajira za sekta ya madini?
Panapo uzima tutajadili fursa, changamoto, na nini kifanyike ili mpango wa UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya madini uweze kuwa na matokeo chanya. Hii ni kutokana na ujuzi, uzoefu na majadiliano ya hapa na pale na wadau. Kwa sasa Alamsiki!
@MadiniTanzania @neecempowerment Ni vipi suala la UWEZESHAJI WAZAWA kwenye sekta ya madini linafungamanishwa na harakati za UWEZESHAJI WAZAWA kuelekea uchumi wa viwanda? Kuna mikakati ya pamoja?
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Ili uweze kuchangamkia fursa zinazotokana na sheria na kanuni za local content kwenye madini ni lazima kwanza ujue kuna nini jikoni. Kwa ufupi madini ni sekta inayokadiriwa kuzungusha Tsh trilioni 4 kwa mwaka kwenye manunuzi. Sasa tambua ni nini kipo ndani.
Fursa zipo za aina mbili
Moja utoe huduma kwenye migodi na sekta ya madini kwa ujumla, yaani huduma kama chakula (catering), ujenzi, Maintenance, huduma za meno na kinywa, bima, data, mawasiliano, usafirishaji, utafiti na kadhalika.
Naambatanisha tangazo hapa kama mfano
Fursa namba 2 kwenye manunuzi ni kuuza bidhaa. Hapa tunazungumzia bidhaa ambazo migodi na wadau wake wanahitaji. Hizi ziko nyingi sana, mfano grinding media, vilainishi, ground support, kemikali, baruti, vyakula kama nyama, matunda, ni vingi sana sana.
Mining Local Content - Insurance and reinsurance opportunities
A contractor, subcontractor, licensee or other allied entity engaged in a mining activity in the country shall comply with the provisions of the Insurance Act
The insurable risks relating to Mining activity in the country shall be insured through and indigenous brokerage firm or where applicable on indigenous reinsurance broker
Local Insurance companies, this is a real deal, know what is in.
Post Tender Negotiations: Majadiliano baada ya kuwasilisha Zabuni.
Haya ni majadiliano yanayolenga kuboresha uelewa wa pande mbili za zabuni yaani MNUNUZI NA MUUZAJI (buyer/procuring entity and Seller/Supplier)
Majadiliano haya hufanyika baada ya wasilisho rasmi la zabuni na kabla ya kutolewa hati ya mahindi 'award notice'. Ni lazima yafanyike kwa uwazi na kwa kushirikisha wadau wote muhimu, taarifa zitunzwe kama ukaguzi utahitajika.
Majadiliano haya hulenga maeneo muhimu kama
-gharama ya zabuni, mradi
-taratibu za malipo
-garantii na waranti
-gharama za 'Maintenance na Msaada' mwingine
-nk
Moja kati ya njia bora ya #uwezeshajiwazawa yaani #localcontent ni ushirikishwaji na uwezeshwaji wa wafanyabiashara wa ndani. Nitaandika namna tuliwahi fanya katika safari ya uwezeshaji wazawa katika sekta ya madini hasa utoaji huduma kwenye migodi mikubwa hapa Tanzania
Mwaka 2014 kulikuwa na mradi mkubwa wa uzuiaji kutu 'corrosion control' kwenye matenki ya process plant ya mgodi. Manunuzi yalikuwa yafanyike kwa manunuzi ya moja kwa moja 'sole source' kwenda kwa mkandarasi wa nje ya nchi. Gharama za mradi zilikuwa zaidi ya dola milioni moja.
Wakati tunaanza hatua za majadiliano akabadilishwa Meneja Mkuu wa mgodi na huyu mpya alipoingia moja ya kitu aliona kinaweza badilishwa ni pamoja na utekelezaji wa mradi huu. Alikuwa na mawazo tofauti. Kwa wasifu yeye ni mbobezi wa sekta nje na ndani ya Tanzania
Miaka miwili iliyopita nilikutana na kampuni ya Kitanzania wakiwa wanasaka fursa za kufanya kazi na makampuni ya madini, migodi mikubwa na ya kati
Nikaomba taarifa zao, tukazipitia taarifa zao na kisha wakasajiliwa kama suppliers nilipokuwepo. Wakaanza kidogo kidogo
Nikafanya mazungumzo na Mkurugenzi wao juu ya matakwa ya #localcontent na kwa namna gani wanaweza kunufaika zaidi na sheria hizo.
Lazima watafute wabia wa nje ambao kwa sheria mpya za uwezeshaji wazawa wanaelekezwa kufanya kazi na kampuni za wazawa kwa ubia.
Nikawaunga na kampuni za Australia na Uchina. Jamaa akasafiri kwenda Uchina akafanya mazungumzo na akafunga dili. Kisha jamaa wa Australia wakaja Tanzania wakakutana wakafunga dili.
Akawa 'Sole Authorised Distributor' kwa Ukanda wa East Africa wa makampuni matatu hivi.
Mwaka 2018 nikiwa kwenye majukumu yangu nilifuatwa na supplier mmoja wa bidhaa za migodini. Akaniambia natafuta fursa ya ku-supply hapo 'kwenu'. Nikamuambia nitumie profaili yenu halafu tutawasiliana.
Baada ya wiki kadhaa ya ukimya nikakutana naye tena, nikamuuliza kimya?
Mara hii akanitumia profaili yao. Ilikuwa vyema na alikuwa ameniambia wana uwezo wa kukidhi vigezo vyote.
Ili kampuni iwe mtoa huduma lazima isajiliwe kwenye mifumo ya manunuzi hivyo inapaswa supplier alete nyaraka zake za kampuni
Tukamuomba akaleta karibu zote.
Katika nyaraka zile hakukuwepo na hati safi ya mlipa kodi 'tax clearance certificate'. Nikamuomba, akaituma.
Nikamuuliza swali lingine je una mashine ya EFD? Na naweza pata nakala ya risiti ya EFD ya kampuni yako ikionesha unatoa risiti zinazokubalika? Maana bila EFD hakuna kitu