My Authors
Read all threads
🎥 U Z I

Kuna..
Mengi Sana Nyuma Ya Pazia Kutoka Hii Series Ya LA CASA DE PAPEL. Ndio! Tunajua Inatamba Tena Sana Tu, Ila Ushajiuliza Vile Vinyago, Zile Nguo Na Aidia Ya Series Vilitokea Wapi. Au Ilikuwaje Mpaka Leo Ipo Kuna Hii Series

Kama Unataka Kujua (twenzetu)
2) UTANGULIZI

Dah!.. Unajua Nini,
Wakati Nachimba Chimba Huku Mgodini Kwangu. Imebidi Tu Nipunguze Punguze Sana Mana Mzigo Wa Taarifa Ni Mkubwa Na Hauwezi Kutosha Wote Hapa! Kwahiyo Nlichofanya Nmechuja Chuja Na Kubakia Na Madini Ya Msingi Ya Kuwapa Nyie. Watu Wangu
3) UTANGULIZI

Mwanangu @chapo255 Alitamani Kumjua Mwanzilishi Kiini Wa Series Ya LA CASA DE PAPEL, Kwahiyo Nkaona Wacha Nifanye Kama Kawaida Yangu Niende Deep Zaidi. So Huu Uzi Utakuwa Mrefu Zaidi Tangu Kuanza Kwangu Kuwahi Kuandika UZI

Hivyo Nisikuchoshe Usinchoshe
4) UTANGULIZI

Naona Kwanza Kabisa Kutokuchanganyana Na Kupata Maswali Mengi, Nataka Kwanza Tujue Kwanini Majambazi Kwenye LA CASA Ambao Ndo Wahusika Wakuu Wanavaa Vinyago Vya Namna Ile, Kwanin Vile Na Si Vingine

Mana Kuna Kastori Katamu Kidogo Nyuma Yake Nataka Kushea Na Nyinyi
5)BIOGRAFIA

Kwanza Niwaambie Tu, Hivi Vinyago Vimetokana Na Binaadamu Mmoja Ambae Anaheshimika Duniani Kote, Hasa Kwa Upande Wa Watu Wanao Fatilia Sana Sanaa Za Uchoraji. Mana Uchoraji Umegawanyika Sana Asee Sio Tu Kuchora Na Peni Na Karatasi Lako Basi. HAPANA
Kuna Kila Namna Ya
6) BIOGRAFIA

Ya Uchoraji Huusishwa Mpaka Kupatikana Kwa Sanaa Iliyo Kusudiwa. Sasa Mtu Alie Nyuma Ya Vinyago Hivi Vya Watu Wanaovaa Kwenye LA CASA Vimemuakisi Mmoja Kati Ya Mchoraji Huyu Mashuhuri Duniani

Na Unaambiwa Dunia Ya Sanaa Haitomsahau
7) BIOGRAFIA

Ingawa Atakumbukwa Kwa Mengi Huyu Jamaa Maana Mwaka 1982 Mkewe Alifariki Baada Ya Kuonekana Ilitokana Na Kesi Nyingi Kali Zilizohusisha Mafua (flu) Ilikuwa Ni Juni 10 Mwaka Huo! 😦 Sasa Shida Ikaja Baada Ya Kuaminika Kuwa Eti Inawezekana Jamaa Alimla Nyama Mkewe 😕
8) BIOGRAFIA

Askwambie Mtu, Swala Hili Lilisumbua Bana. Sababu Hata Hivyo Pengine Watu Walihisi Ni Kutokana Na Aina Namna Ya Uwasilishaji Wa Kazi Zake Za Kisanaa, Ingawa Jamaa Alipo Fariki Mkewe 1982. Hakuwa Tena Kama Binaadamu Wa Wakawaida Anavyotakiwa Kuwa, Alisikitisha Sana
9) BIOGRAFIA

Mwaka 1982 Juni 10 Baada Ya Kufiwa Na Mkewe GALA DALÍ , Huko Port Lligat Nchini Hispania Akaanza Kuwa Mtu Ambae Kama Kapoteza Uwezo Wa Kujua Chochote, Yaani Yupo Yupo Tu, Haongei, Kapooza Sana, Hata Hamu Ya Kula Hana

Kitaalamu Inaitwa "dull" Hii Hali Ya Kuwa Hivi
10) BIOGRAFIA

Kuna Kipindi Jamaa Akawa Akikaa Anapiga Sana Makelele Bila Sababu Au Analia Machozi Sana, Dah! Mapenzi Nyie Acheni Tu Ndo Hivi Ukiskia Mtu Kawa Chizi Kwa Mapenzi Usishangae Kama Hujawahi Kupenda. Mana Mbaya Zaidi Kuna Kipindi Akawa Ana Ukwangua Uso Wake Mwenyewe🤔
11) BIOGRAFIA

Najua Mlikuwa Mnataka Kumjua Ni Nani Huyu,

Jamaa Anaitwa SALVADOR DOMINGO FELIPE JACINTO DALÍ i DOMÈNECH ,Kudaadeki Jina Lefu Sana Bwana Naona Nitatumia Tu SALVADOR Kumuelezea Hilo Lote Litatuchosha😊, Kwanza Mi Mwenyewe Litanchosha Kuliandika Andika Hapa 😒
12) BIOGRAFIA

Sasa Tukimwangalia SALVADOR Kama Mwasisi Wa Vinyago Vinavyotumika Kwenye Series Ya LA CASA DE PAPEL Yeye Alizaliwa Zamani, Yaani Tunaweza Kusema Huyu Ni Mhenga Haswaa

Sababu Mwaka 1904 Mei 11 Kule Nchini Hispania Ndio Alizaliwa, Na Alifariki Mwaka 1989, Ilikuwa Ni
13) KIFO

Ni Januari 23, Huko Huko Hispania. Sasa Ukitaka Ujue Kuwa SALVADOR Alikuwa Mkali Sana Kwenye Sanaa Ya Uchoraji, Baada Ya Hicho Kifo Chake Unaambiwa Mpaka Leo Kuna Makumbusho Iko Kule Marekani Jijini Florida Eneo La St. Petersburg Inaitwa Makumbusho Ya,
14) MAKUMBUSHO YAKE

Ya THE SALVADOR DALÍ MUSEUM Yaani Ni Maalumu Hiyo Makumbusho Kwaajili Ya Kazi Alizowahi Kuzibuni Yeye Kwa Kuchora. Yaani Ukiingia Humo Unakutana Na Kazi Zake! Nenda Kama Unataka Utakutana Nazo. Labda Tu Nkwambie Umashuhuri Wa SALVADOR Ulitokana Na Aina Ya,
15) UPEKEE

Ya Uchoraji Wake. SALVADOR Alikuwa Anachora Picha Zilizokuwa Zinawapa Watazamaji Mitazamo Mingi Ya Kufikirisha Na Kubakia Na Maswali

Alikuwa Kitaalamu Anaitwa "Draftsmanship" Na Picha Zake Zenye Utata Ziliitwa "bizarre images"
(Picha Za Chini Ni Ndani Ya Makumbusho)
16) UPEKEE

Alikuwa Na Kipaji Haswa Sio Cha Kawaida Yaani (prodigy), Ukiachana Na Kuchora Pia Amewahi Kuchonga Vinyago Vya Aina Tofauti, Navyo Pia Jamaa Amechonga Kwa Upekee Aliozoeleka Nao, Sababu Huyu Jamaa Bwana Haikutokea Tokea Tu Akawa Hivyo Alivyowahi Kuwa Enzi Za Uhai Wake
17) UPEKEE

Unajua Bana Muhispania SALVADOR Kwa Watu Wote Enzi Za Uhai Wake Alitambulika Kama Surrealism, Expressionism. Ikiwa Na Maana Mtu Mwenye Shauku Ya Watu Kujua Kile Anakifanya, Wakati "Expressionism" Ikiwa Na Maana Kuwa Ni Aina Ya Uchoraji Ambayo Msanii Ana,
18) MICHORO

Ana Kusudia Kuelezea Uzoefu Wa Hisia Zake Kuliko Dhana Ionekanayo 😊 Nadhani Unaona Jinsi Jamaa Kazi Zake Zilivyokuwa Na Utata. Na Ni Kazi Zake Karibia Zote Zilikuwa Hivi, Sasa Cha Ajabu Mwenyewe Wakati Wa Uhai Wake Aliwahi Kusema "Watu Wanashangaa Jinsi,
19) MICHORO

Jinsi Athari Zangu Katika Sanaa Ya Uchoraji" (his impact) Na Walikuwepo Wachoraji Tatanishi Wengi Wa Aina Yake Ila Yeye Alikuwa Wa Kipekee Kutoka Pale Nchini Hispania, Nadhani Unaona Hata Kwenye Picha Mwonekano wake Na Mustachi Zake Kama Panya 😄 Jamaa Alikuwa Wa
20) KIFO

Wa Kipekee Sana, Na Akasema Kuwa Yeye Mpaka Kuwa Hivyo Alishawishiwa Sana (inspired) Na Mfululizo Wa Ndoto Alizokuwa Akiota Na Maono Aliokuwa Akipata

Mwaka 1988 Aliwahi Ingia Hospitali Huku Moyo Wake Ukikaribia Kufeli😦, Lakini Baadae Akajiskia Vema Mwaka Uliofatia Aka
21) KIFO

Akafariki Dunia Baada Ya Moyo Kufeli Akiwa Na Umri Wa Miaka 84, Huko Nchini Hispania, Baada Ya Miaka 7 Ya Kusumbuliwa Na Umiliki Wa Penzi La Mkewe GALA DALÍ (possessed)

Hakuna Muhispania Asiemfahamu Huyu Jamaa Nawaambieni. Ameacha Alama Kubwa Kwa Upande Wa Sanaa Zake
22) UOGA

Alafu Nmekumbuka Bana Jamaa Alikuwa Na Tatizo Liitwalo Kitaalamu 'phobias', Unaambiwa SALVADOR Alikuwa Anaogopa Sana Panzi, Wale Watoto Wanaitaga Balale 😄 Na Alikuwa Anaogopa Mtu Akibadilika Usoni Katika Hali Ya Aibu Tangu Utotoni Mwake, Kitaalamu Iliitwa ereuthophobia
23) TASWIRA

Tukirudi Kwenye Hivi Vinyago Sasa!. Hivi Vina Wakilisha Kitu Kinaitwa Kitaalamu "Resistance" Kwa Kiswahili Tunaweza Kusema (tafsiri isio sahihi) Ni Ile Hali Ya Kupinga Kitu Au Kukikataa Kwa Dhumuni La Kutaka Haki Itendeke, Hivyo Wale Vibaka Wa Kwenye LA CASA Walikuwa
24) TASWIRA

Walikuwa Na Lengo La Kutuonesha, Mtu Unaweza Kuvaa Vile Vinyago Kwa Lengo La Kuwa Mpinzani Katika Kupinga Jambo Flani Ambalo Si La Haki. Najua Unajiuliza Hapo Wale Vibaka Walikuwa Wanapinga Nini Sasa😄

Ndio! Walikuwa Wanapinga Na Kutaka Haki Na Wao, Hawakuvaa Bure
Na Vinyago Vile Vya Plastiki Walivovivaa Kwenye LA CASA DE PAPEL Ndio Vime Wakilisha Uso Wa Mchoraji Mashuhuri SALVADOR. Tukiachana Na SALVADOR, Em Tumfahamu Sasa Alieianzisha Hii Series Aliku....

Ebana Hapatoshi😄 Itaendelea !
#NindiJrSERIES #NindiJrLACASADEPAPEL
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Nindi.Jr ㄷㄱㅑㅊ

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!