My Authors
Read all threads
A) Asili ya Kiswahili ni lugha kamili na wala si lugha chotara kwa maana ya mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha ya Kibantu

ukopaji wa maneno katika lugha yoyote ile ni dalili tu ya kukua kwa lugha husika

#NenoTokaMwambao
B) muundo wa maneno na miundo wa sentensi za Kiswahili yadhihirisha kufanana na lugha za Kibantu kuliko Kiarabu
Ni lugha kamili iliokopa kwa Kiarabu kama ambavyo kiingereza kilikopa kwa lugha kongwe kama Kilatini, Kigiriki na Kifaransa na kubaki kuwa lugha kamili
#NenoTokaMwambao
C) Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyoathiriwa na Kiarabu hasa kimsamiati na pia kilitokana na mchanganyiko wa lugha kadhaa za Kibantu zilizokuwa katika upwa wa Afrika Mashari #NenoTokaMwambao
D) vigezo vya kuibaini lugha ni ya kiisimu ni kuzingatia msingi wa Kiswahili ki fonolojia, mofolojia na sintaksia
kukopa kutoka katika lugha nyingine hakuifanyi lugha hiyo ionekane imetokana na hiyo lugha ngeni
#NenoTokaMwambao
E) tofauti na kiarabu, Kiswahili ina taratibu k.m. herufi kama konsonanti na irabu ambapo huweza kuunda silabi kama ba, ma, ka, la; au konsonanti, konsonanti na irabu kama kwa, gha, mwa, n.k.; au konsonanti, konsonanti, konsonati na irabu kama, mbwa, ng’we n.k.
#NenoTokaMwambao
F) Lahaja zote za Kiswahili ni lugha zinazojitegemea.
Lahaja hizi zinafanana na lugha za Kibantu.
Lakini zinatofautiana kidogo na Kiswahili sanifu kwa sababu Kiswahili sanifu kina maneno mengi ya kukopa
*msamiati siyo msingi pekee wa kuzingatia uasilia wa lugha
#NenoTokaMwambao
G) lahaja za Kiswahili ni ki Miini ya eneo la Barawa.
Kitukuu na Kibajuni
Kisiu sehemu za Pate, Kiamu huko Lamu,
Kimvita sehemu za Mombasa,
Kivumba na Kimtang’ata kaskazini mwa Tz.
Kimakunduchi, Kihadimu, Kitumbatu Unguja na Kipemba na Kimrima cha Kilwa
#NenoTokaMwambao
H) Kiswahili hakikuiga. Kuiga nikufatilia tendo au jambo kama lilivyo. Kinyume na Kiswahili kilivyokopa. Kimeazima misamiati iliokuwa na upungufu nayo nakuibadili kibantu. Km kiarabu 'ruh' na 'samaga' kiswahili samaki au roho na samaki
#NenoTokaMwambao
I) Mfano wa lahaja kujitegemea tofauti na Kiswahili sanifu iliokopa toka kiarabu;
sanifu lahaja
Samaki - nswi
Roho - mtima
Gilasi/balasini - bilauri
#NenoTokaMwambao
J) tujadili asili ya Kiswahili sanifu. kimesanifisha au kuchafua na kuboronga Kiswahili cha asili yaani lahaja kongwe kwa kukopa pasipo stahili. Pia, kuwa sio kazi ya waswahili bali waingereza na wajerumani na wasiokuwa waswahili
#NenoTokaMwambao
K) Asili ya Kiswahili ni lugha kamili na wala si lugha chotara kwa maana ya mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha ya Kibantu

ukopaji wa maneno katika lugha yoyote ile ni dalili tu ya kukua kwa lugha husika
#NenoTokaMwambao
L) muundo wa maneno na miundo wa sentensi za Kiswahili yadhihirisha kufanana na lugha za Kibantu kuliko Kiarabu
Ni lugha kamili iliokopa kwa Kiarabu kama ambavyo kiingereza kilikopa kwa lugha kongwe kama Kilatini, Kigiriki na Kifaransa na kubaki kuwa lugha kamili
#NenoTokaMwambao
M) Kiswahili ni lugha ya Kibantu hasa kimsamiati
#NenoTokaMwambao
N) Kiswahili sio chotara kutokana na Kiarabu na kibantu. walikuwepo waswahili mwambao na zilikuwepo Lahaja za kiswahili. Ila kilicho buniwa na kuzaliwa ni Kiswahili sanifu
Wakoloni walikikuza Kiswahili ili wapate wafanyakazi kuwapa usaidizi katika ngazi ya chini
#NenoTokaMwamabo
O) Wakoloni wali kidhamini kikao cha kujadili utumiaji wa Kiswahili kama lugha ya mawasiliano 1925 na 1928 wakachagua kiunguja kama lahaja teule
1930 iliundwa Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki (Inter-Territorial Language (Swahili) Committee
#NenoTokaMwambao
N) Baadhi ya majukumu ya Kamati ya mkoloni ya lugha ni:

Kusanifisha ortografia itakayotumika katika Afrika Mashariki.
Kuweka ulinganifu wa maneno yaliyopo na yale mapya kwa kusimamia uchapishaji wa kamusi
ulinganifu wa sarufi katika uchapishaji wa vitabu
#NenoTokaMwambao
O) Hawakuzingatia Lahaja ambazo zinafanana na lugha za Kibantu. Lakini zinatofautiana na Kiswahili sanifu kwa sababu K. sanifu kina maneno mengi ya kuazima. Lahaja zote hizo ni lugha zinazojitegemea
#NenoTokaMwambao
P) Wanaodai kiswahili sio lugha asilia au sio kibantu eti ni lugha chotara iliokopa kwa Kiarabu na Kibantu wamekosea. Kilichoibuka geni ni K. sanifu iliokopa misamiati
Ndiswi Nyali kuu ndiswi,Ndiswi mwapigana naswi (gongwa la maana mkasi)- ndiswi ni kimijikenda
#NenoTokaMwambao
Q) Mfano; lahaja hai
Rwaphwera wosi wavijue, kuwa sisi ruwa vumba

Kivumba nchakinena, naphwera rusikizane
Sababu sasa naona, umuhimu rujuane
Kivumba nichakinena, muphweralo mulinene

Wavumba wanako kwao rangu huko wauyako
Na ushirazi si wao, kuwera hivi ni miko
#NenoTokaMwambao
R) Mfano wa kiswahili kongwe kilicho nukuliwa karne ya 19 (19th Century) na ushahidi wa alie inukuu. Utungo huu unadhihirisha Kingozi na lahaja kongwe zilikuwepo ila zatofautiana na kizalia chao, Kiswahili sanifu
#NenoTokaMwambao
S) Rada kwa wanao dao kiswahili sio lugha asilia au sio kibantu eti ni lugha chotara inayotokana na Kiarabu na Kibantu
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Swahili~Pundit

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!