@TilasMusa @EugeneOngeri @franckluyz_2012 @ishaqearly @ayogo_do @LucyM50876035 @mlimakenya @yosefu_jk @DaudiMuya1 @OmwanaOmageto
Ijapokuwa maneno haya yanafanana, hayatumiki kama visawe, yana Tofauti. kufikiri ni kutumia akili ili kutatua jambo pia kutafakari au kuwaza. Kudhani ni kufikiri bila kuwa na uhakiki.
Maneno haya yanatokana na neno gharama (nomino). Kitenzi chake ni ghar-I mia sio ghar-A-mia.
Haya ni maneno yaliyokopwa kutoka neno ‘hotel’ la Kiingereza. Kwa misingi sahihi ya kisarufi hatuna wingi wa hoteli. Kwa hiyo kiambishi ma hakitakiwi. Hivyo sahihi ni hoteli kwa umoja na kwa wingi na wala si ‘mahoteli
Wanaotumia neno hovyo, hasa wapwani, kwa muktadha wa Kiswahili sanifu(sio kilahaja) wanakosea. Neno sahihi ni ovyo.
Maneno hayo sio kiswahili, Sahihi ni kuandika au kutamka huhusiki; hutaki
Haya maneno mawili yanatokana na neno la Kiingereza ‘digit’. Neno hili ni nomino na kwa kawaida tunatohoa nomino badala ya kitenzi, kivumishi au kielezi. Kwa msingi huo neno sahihi ni ‘digiti’ badala ya digitali ambalo linatokana na ‘digital’ ambalo ni kisifa
Neno sahihi hapa ni baadaye
neno aidha lina maana ya tena, basi, zaidi ya hayo, vilevile, n.k.
Wanaokosea kulitumia ni wale wenye misingi ya Kiingereza wanaofuata mtindo wa kutumia ‘either … or ’