My Authors
Read all threads
UZI.
THOMAS SANKARA CHE GEUVARA WA AFRIKA ALIENYANG’ANYWA KIGODA KWA RISASI YA KISASI.
Thomas Isidore Noel Sankara kiongozi kijana aliyependwa na raia wake na kusalitiwa na rafiki yake wa muda mrefu, alijulikana pia kama Che Geuvara wa Afrika kutokana na harakati zake za kuwapambania wanyonge wa taifa lake tukufu la Burkinafaso ambapo awali lililiitwa Upper Volta.
Alizaliwa mwaka 1949 katika familia ya watoto kumi huku yeye akiwa ni mtoto wa tatu wazazi wake walitamani sana Sankara awe Padre wa kanisa katoliki na kufuata falsafa za Mtakatifu Thomas wa Akwino lakini Thomas Sankara alipenda sana walichopenda rafiki zake.
Marafiki zake wengi wa rika yake walikuwa ni wanamgambo ambao walitumwa sehemu mbalimbali na serikali iliyokuwa chini ya Rais Saye Zerbo basi na yeye alifanya uamuzi mgumu wa kuongoza miguu yake katika kambi ya jeshi na baadae kuwa mwanajeshi,
wazazi hawakuwa na namna walimuacha mtoto wao mwenye misimamo migumu kufuata ndoto yake.
Sankara alianza masomo yake katika chuo cha kijeshi mwaka 1966 akiwa kijana mdogo wa miaka 19 mwaka mmoja baadae alitumwa kumalizia masomo yake huko Antsirabe nchini Madagaska , Taifa ambalo lilikuwa chini ya Rais Philbert Tsiranana.
Akiwa jeshini alikuwa akipokea mafunzo kemkem na mwaka 1971-1972 alishuhudia wananchi wa taifa hilo wakifanya shinikizo la kuondoa serikali ya Rais Philbert na kweli nguvu ya umma ya raia wa Madagasca walimuondoa kiongozi wao.
Alitazama sana kwa umakini namna raia wa madagasca walivyoondoa serikali ya kidhalimu, alijiona kama mtu aliyebeba maono ya kuwasaidia raia wenzake wa Upper Volta kuondoa mizozo ya mipaka na taifa jirani la Mali na kwakweli alijibebea umaarufu mkubwa mwaka 1974..
baada ya kushinda vita nzito na kurejesha mpaka wa taifa lake.
Mji mzima wa Ougadougou walimfahamu huyo mwanajeshi shupavu, Mzalendo wa kweli na mtetezi wa wanyonge Thomas Sankara, naye akaanza kuvutiwa na siasa akawa anawasoma wakina Karl Marx na Falsafa za Vladimir Lenin baba
wa muungano wa mataifa ya kisosholisti (Soviet state).
Kijana huyu mdogo wa miaka 32 akaanza kupata vyeo tena za nafasi za juu zaidi cheo chake cha kwanza kilikuwa ni Katibu mkuu kiongozi na siku aliyokuwa anaenda kuongoza kikao cha mawaziri jamaa huyu aliingia ikulu na ....
Baiskeli, viongozi wenzake walimuona bwana mdogo mshamba sana na anatuaibisha sisi ‘Big man’ lakini yeye wala hakujali.
Aprili ya tarehe 21, 1982 aliamua kujiuzuru nafasi yake kama katibu baada ya kuona namna serikali inavyoendesha nchi kwa kunufaisha matumbo ya viongozi
na wala sio taifa, sera za kilimo na utekelezaji wake zikiwa zimedorora, ajira ikiwa sio kipaumbele kikuu.
Lakini Novemba 7, Mwaka 1982 yakafanyika mapinduzi yaliomuweka madarakani Jean Baptiste Ouedraogo na Januari 17,1983 Sankara akala shavu kama Waziri Mkuu wa taifa hilo,
sema sasa alizidisha mapenzi na raia wake kitu ambacho boss wake akaamua kumuachisha kazi baada ya kudumu kazini kwa miezi mitano tu Rahaula!
Siku hiyo hiyo hiyo Sankara aliamuliwa kuwekwa kifungo cha ndani ya nyumba yake mwenyewe ilikuwa ni hatari sana hakuna kutoka nje.
Mwaka huo huo swahiba wake kipenzi waliofundika wote katika jeshi la Upper Volta Blaise Compore aliandaa mapinduzi ambayo yalifanikiwa kwa aslimia mia na kumfanya kijana wa miaka 33 Sankara kuwa Rais wa taifa hilo hapo mtihani wa kutimiza yale ambayo alikuwa hayaoni yalianza rasm
Alilibadilisha jina la taifa lake kutoka Upper Volta na kuwa Burkinafaso akiimaanisha Nchi ya watu Alihamasisha sana kilimo mpaka taifa lake likawa linaongoza kuwa na chakula kingi Afrika Magharibu, aliwatia nguvuni vibaka wa kisiasa,
mathalani alitengeneza ajira mpya kwa vijana wasomi na wasio wasomi hakubagua kabisa, alianza mapema Mipango endelevu kama ya UN sasa ya usawa wa kijinsia na katika serikali yake wanawake ‘kibwena’ walipata nafasi kubwa za uongozi.
Ushupavu wake uliwakasirisha wengi na kupelekea wengine kuuza vipande vya sarafu kwa mayuda ili wammalize, aliyemuweka kitini ndiye aliyemtoa kwenye kigoda kwa zawadi ya kifo Oktoba 15, mwaka 1987 kundi la wanajeshi kumi na mbili likiongozwa na swahiba kipenzi Blaise Compore..
ndio walihusika.
Wananchi wa Burkinafaso walisaga meno kwa miaka 27 chini ya Rais Compore mpaka pale walipomuondoa kwa maandamano mwaka 2014.
Ndoto ya Thomas Isidore Noel Sankara iliwaachia ‘mang’amnga’m’ watesi wake , raia wote walibaki kusononeka na kuenzi maisha ya kiongozi aliowapenda wao na maendeleo bila kubagua.
Mwisho
@threadreaderapp unroll this please
Wapwa Uzi huu nimewaandalia @abdulazackabdul @mpambazi_ @DosaRahma
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with MSAFIRI

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!