My Authors
Read all threads
Inakuaje mpaka mtu anapata kitambi? Katika kipindi hiki cha kukaa ndani watu wamepunguza mizunguko ambayo inasaidia kama mazoezi madogo madogo. Sasa leo naomba tujifunze ni namna gani mtu anapata kitambi, Kitambi ni nini hasa? Nitatumia njia ya input na output.
Nimechagua mfumo wa input na output maana hiki ndio kinachotokea hata kwenye mwili mpaka mtu anapata kitambi. Input nikiwa na maana "kinachoingia" na output ''kinachotoka". Nikwambie tu hicho kitambi ni store ya mwili ya kutunzia chakula.
Mwili unahitaji nishati (energy) ili kufanya kazi, Nishat kubwa ya mwili ni sukari (glucose) tofauti na sukali tunayokunywa kwenye chai, Chanzo kikuu cha sukari hii ya mwili ni wanga (carbohydrate). Je inakuaje mpaka wanga unakua sukari?
Unapokula chakula hiki kinapofika tumboni mwili hukichanganya na kukilainisha chakula kwa kutumia kemikali na enzymes. Sasa niseme tu mwilini chakula kinapoingia kuna askari kazi yao ni kusubiri chakula kilainishwe kisha wakichukue kukipeleka sehemu husika. (askari ni mfano).
Kama ilivyo huku uraiani, kila askari ana kikosi chake na kazi yake maalumu. Kuna atakaebeba protein, kuna wa wanga, kuna wa vitamin n.k. Kila askari na aina ya chakula chake. Leo acha tuongelee wanga ambayo ndio aina ya chakula inayotufanya tujadili mada hii ya kitambi.
Sasa baada ya wanga (carbohydrate) kulainishwa hubadilika na kuwa glucose ambayo ndio sukari ya mwili. Basi askari ataibeba ile glucose tayari kuipeleka kwa ajili ya matumizi mwilini. Askari huyu ataipeleka kwenye mfumo wa damu ili isafirishwe sehemu zote za mwili.
Sasa akifika katika lango kuu la mfumo wa damu anakutana na askari wengine wanaitwa Insulin. Askari hawa kazi yao kubwa ni kuhakikisha kiasi cha sukari kilichopo kwenye damu hakizidi kiwango kinachohitajika ndio maana kutokuwepo au utendaji mbovu wa isulin husababisha kisukari.
Insulin atakapoipokea sukari hii kabla ya kuruhusu iingizwe kwenye damu au la anaangalia kama kwenye damu kuna kiwango cha sukari kinachofaa. Kama hakitoshi, inaruhusu kuingizwa, Lakini kama kinatosha inazuia sukari zaidi kuingia na kuamuru sukari hiyo ipelekwe kwenye stoo.
Stoo za mwili ni ini na misuli (liver and muscles). Baada ya insulini kusema sukari inatosha, Sasa ili sukari hii ihifadhiwe kwa matumizi ya baadae inabidi iwe katika mfumo utakaodumu kwa muda mpaka mwili utakapoitaji sukari ya ziada. Mfumo huu unaitwa glycogen.
Glycogen inahifadhiwa kwenye ini, mwili ukihitaji sukari na tumboni kukiwa hamna kitu basi hutuma askari kwenye stoo hii na kuchukua gkycogen kisha kuibadilisha kuwa glucose na kisha kuingiza kwenye mfumo wa damu. Glycogen ndio sababu hatuli kila baada ya dakika kadhaa.
Sasa ukila kwa wingi carbohydrate (wanga) kiasi cha kufanya stoo ya mwili (ini) kushinwa kuhifadhi wanga huo na kwasababu mwilini wanga unatambulika kuwa muhimu mwili hauwezi kutupa bali hubadilisha kuwa mafuta (fats or adipose tissue) ambayo itatuzwa kwa muda mrefu.
Hizi fats na adipose tissue hupelekwa na kutunzwa kwenye tumbo, hips, mapaja na makalio. Hivyo basi utumiaji wako wa sukari ya mwili ndio utasababisha mwili aidha uendelee kutunza mafuta au uyabadilishe na kuyatumia. Hapa ndio tunafikia hatua ya input na output.
Input inabidi iwe sawa na output. Unachoingiza mwilini inabidi kiwe sawa na unachotumia, Kama mwili haujishughulishi inabidi uzingatie nini unakula, ukiendelea kula wanga kwa wingi huku huzingatii matumizi yake unalimbikiza mafuta mwilini. Kazi kubwa ya wanga ni kuupa mwili nguvu
Unaposikia njaa haimaanishi mwili unahitaji chakula la hasha bali ni kwa sababu umeuzoesha mwili, ukiuzoesha mwili muda muda flani ukifika unaweka kitu tumboni basi kila muda ukifika mwili unajiandaa kupokea chakula, askari wanakua tayari kusafilisha chakula, kemikali zinamwagwa.
Utashangaa ukiacha kula muda mrefu njaa itauma lakini itafikia wakati itaacha mwili ukiona hamna chakula na kama una uhitaji wa chakula safari kwenye stoo na kuchukua chakula kilichotuzwa. Ndio maana mtu mwembamba na mnene wakikaa muda mrefu bila kula mwembamba atadumu muda mfupi
Ushauri wangu, kula endapo tu unasikia njaa, usile kwa sababu muda wa kula umefika. Ahsante sana kama umesoma mpaka hapa, Mungu akubariki.
Sasa kuongezea hapa. Hizi adipose tissue pia ndio hutumika kulinda organs muhimu mwilini kama vile moyo, husaidia pia kama shock absorber. Uwepo wake katika kiwango kikubwa ni hatari kwa usalama wa organs hizo.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Festo D Ngadaya | #StayHome

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!