My Authors
Read all threads
"LAANA...."🧞‍♂️

Wiki moja baada ya kuanza darasa la kwanza kutokana na umbo langu kua dogo kidgo kuliko wengne ilinipa ugumu maana nilishindiliwa uonevu wa kila namna..ila siku,mmoja wa wanafunzi alinikingia kifua..na si mwingine bali ni "MUDI" kama wengi tufupishavyo, jembe langu
Sikuwah kuonewa kuanzia siku hiyo na ndipo nilipojifunza ubabe..sikuwah kumwambiaga ila alikua kama kaka angu japo tulikua umri sawa ila kwa mwili wake na udogo wangu tofauti ilikua kubwa,alikua ndo rafiki wangu wa kwanza kishule shule. Alinifunza kujihami,kujilinda na ni yeye
alinifunza utukutu..asee shule nzma ilikua inamtambua. Kwa kila walimu walichomsema basi na mm nilihusika ila kwakua wengi hawakuamini mi kuhusika ivo mudi alichkua adhabu zote na hakuwah kunitaja. Ila nami nilihakikisha hafeli mitihani kwa njia yoyote na hakuwahi kuniangusha
Ni yeye aliyegunduaga kutoonekana kwangu nilivyotekwaga kwa siku tatu na kutoa taarifa kwenye uzi wangu uliopita. Alisemwa vibaya kila kona ila haikuwah kubadili urafiki wetu mpaka tunamaliza shule ya msingi kwani kwangu hakuwahi kunitendea kibaya. Hvyo ndivyo tulivyokua na mudi
Tulipotezana baada ya kuanz sekondar..kuonana kulipungua maana alikuja kuhama kipind nipo shule na sikufaham alihamia wap.
Siku nipo zangu kariakoo hivi karibuni ikiwa imepita miaka zaidi ya kumi na..nilipigwa push moja kubwa na mbeba mizigo,kwa jazba nilitukana,kugeuka ni Mudi
Tulishangaana..akacheka,,neno la kwanza alilotoa lilikua "nifate" af akaanza kupenya katikati ya watu mwana nipo nyuma,kidgo tu nimpoteze.
Aliposhusha mzigo aligeuka akaniangalia "Dah,mwebe.." niliona machozi yakimlenga na alijaribu kuyawah kufuta kabla hayajaonekana,alichelewa.
Alinishika mkono bila kujali ilivyokua tukaenda kibaraza cha duka moja lenye ngazi..tukakaa..akaomba tule,tukaagiza pale nguna na mbogamboga tukala na stori za hapa na pale..muda wote namshangaa nikijaribu kutengeneza scenario ni vipi amefikia huku..hadi alisema najua unanshangaa
Nikacheka kicheko cha huzuni kidgo..nikiangalia alivyoisha. "Dah umekua kichiz.."alisema
Vyombo vikatolewa na kelele za hapa na pale,nikaona hataa acha niulze
"Kulikoni???"
Akaangalia chini kwa sekunde kadhaa alivyonyanyuka akasema "mwanangu,nailipia laana yangu" sikumwelewa.
Alinieleza kua baada ya tulivyoachana walihama kwenda moro na alisoma kidgo ila aliacha shule hapo kati,maisha ya kule hakuyaelewa,hvyo akaiba pesa za mama ake akarud Dar mzee wake alishafariki kipind hicho,kufika Dar alikuja mpaka home kwetu aliniulizia ila mfanyakaz aliekuwepo
alimwambia nipo shule hvyo akasepa..kitaani kwao hakupata shida maana alijulikana hvyo alikaa na kupata mishe ya boda..alipiga hela nying sana maana ndo biashara ilikua imeanza pamba moto mjini Dar ila haikuchukua muda mrefu ile boda illibiwa na walimwacha na majeraha makubwa
Alikutwa nusu mfu..wenzake walimsaidia mpaka alipojiweza na kupona.. ikatokea mishe ya mererani arusha..alichimba madini akafanikiwa kimtindo kupiga pesa akarud Dar ambapo alizitumbua vya kutosha..huko moro mama ake alikua anaumwa na habari zilimfikia ila hakujali..
Kutumbua kwake hela alikutana na marafiki na mabinti wa kila aina..ni jina la binti mmoja tu "Hamida" ndo aliweza kunitajia nahisi ndo aliyemshikaga kimapenzi kwamba ndo alitumbua nae sana mpaka hela zikaisha na kuanza kuwa madeni.. so hamida akamkimbia..maana vitisho kila kona
Mudi akaona hali si hali..akakimbia Dar akarud Moro..kufika Moro akakuta maza ake alishakufa na kuzikwa..baadhi ya ndugu walimsema na kumwambia mama ake alimlaani kwa kumwacha kipindi chote hicho ilhali akisikia habar zote kuhsu yeye na kushndwa kumsaidia japo kumjulia hali
Mudi alijutia maamuzi yake na bdo kidgo achukue maisha yake kama sio ndugu aliokaa nao kumwahi..maneno ya mama ake kwamba "..hataishi kwa raha labda amfate atakokuwa na kumwomba msamaha" ndo yaliyompa tabu mudi..
Aliamua kurudi Dar maana alikua hana la msingi Moro na pale ilikua
Imepita mwezi akiwa mbeba mizigo pale kkoo..nilimchek mchizi moyoni nikiwa natamani nimseme na pia nikimwonea huruma,nikawaza ni lipi ningefanya tofauti tangu tulivyokua watoto labda haya yote yasingetokea..moyoni nilijuta pia nikihisi na mi nimehusika kwa namna moja
Nikalipia chakula nikampa na elfu 15 ambyo ndo nilikua nimepanga kununua raba,nikamwambia anipe namba yake ya simu ili tuweze kuwasiliana zaidi, alinieleza kuwa hana simu ila nikimwachia yangu atafanya jitihada kunitafuta..basi tukaagana
Nakumbuka alisema "sijawah kuwa na furaha kwa kipindi kirefu ila leo nimekuona mwebe,dah nna mzuka sana..najua hamna anayekuonea maana sio kwa tusi lile.."nikasepa.
Zilipita wiki tatu au nne hakuwah kunitafuta..nikiwa tena kkoo nikaona si mbya kupita sehem yake ya kazi labda
Nitambahatisha..kufika sikumwona na watu wa pale walisema jamaa hajaonekana kama wiki hivi na wameshindwa kumsaka maana hanaga simu ye ndo huwa ana namba za watu..nikaona poa..nikamwachia mchizi mwingine namba ili jamaa akirud ampatie labda aliipoteza nikisisitza anitafte
Hazikuisha wiki mbili..nikapigiwa simu na yule mchizi kuwa Mudi alifariki..alikua ameathirika na wenyewe walipata hzo habari kibahati kutoka kwa mchiz mwingne aliyefahamiana nae..mwana alizikwa Moro..
MAZEE MOYO ULINIUMA KICHIZI..
Ilibidi niende Moro kutoa heshima za mwsho
Nimshukuru kwa yote mema aliyoweza nitendea..na mabaya aliyonikingia. Natumai alipoenda ameomba msamaha na amepumzika kwa amani.

" Huyo ndo MUDI mazee,jembe langu"

#fanani hapa✌
Pitia pinned tweet katika account yangu kwa nyuzi zaidi..like na kuretweet✌
Support yenu kwa kusoma ku like na kuretweet 🙏@McinikaWaLamar @Micky_dee_ommy @mpambazi_ @Mkuruzenzi @mkandamizaji
✍️
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Urs truly✍️

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!