My Authors
Read all threads
"KARMA..🎭"

🌡Kama huna kifua basi usisome uzi huu haukufai maana mi natoa visa vya ukweli kama ifuatavyo...👇

Nipo na mwana ananionesha picha af ananiuliza "unaikumbuka hii"..naichek af nacheka ni picha ya kitambo kidgo,tukiwepo sisi na wasichana watatu..mmoja wao akiwa VERO
Vero mi nilimjua kipindi anatoka na mchizi wangu huyo..baada ya kukutana nae viwanja..tulikula sana bata za hapa na pale na huyu manzi,kipindi hicho anakaa mitaa ya sabasaba na wenzake.. walikua wamoto..kila weekend lazima niulizwe "shem leo wap!!nna rafki yangu nataka nikususie"
Kiukweli mchizi wangu alikua sio mtuliaji so wana tulikua tunajua saa yoyote kinaweza nuka..ila cha kushangaza haikua hvyo kwa muda mrefu..nadhani style za maisha ziliendana kiasi kwamba ilikua haiboi..
Basi hapo kati Vee kama nilivyokua namwita akapata mimba ya mchizi
Katika makubaliano yao wakaona watoe maana wote hawakua tayar especially mambo ya chuo na ujana..
Siku zikaenda vee akanasa nyingne..ila sasa hii ikaja kujulikana sio ya mchizi..ugomvi mkubwa tu ukatokea..vee akaona isiwe shida coz anampenda mchizi nayo akaitoa..
Ila baada ya hilo sekeseke mambo yalibadilika..mapenzi yakawa yanashikiliwa na uzi, mwana akarud njia yake ya zamani bila kujali tena kua alikua na mpenzi wake..yani ilikua usiku wanaachana baada ya siku mbili unasikia wamerudiana..hvyo yani
Vee akaona njia moja ya kumtuliza jamaa ni kumzalia..na kweli haikuchukua muda kitu kikanasa..mwana kweli akarudi mstarini..ila ilikaa miezi 4 tu ikaharibika..
Mchizi alikua na big expectations na alikua tayar yani so aliyumba kidgo ilivyotokea...
Kwahyo vee akakosa kitu cha kumshikilia mwana..
Ila jamaa alimweka nyingine ila hii haikukaa hata miezi miwili..na haikuchukua muda sana wakaachana moja kwa moja.

Hapo kati niliwasiliana nae mara chache sana..ila nilijua alikuja pata mtu mwingne..
Kuna muda hatukutafutana sana...ila siku alinipigia simu akanisema sana kwanini nimemtenga akaniomba niende kumchek kuna kitu anataka kunambia..sikuchukulia serious so nilipotezea kimtindo..ila siku natoka mizunguko yangu coz nipo karibu na kwake nikaona sio ishu acha leo niende
Kufika anapokaa mlango nakuta umefungwa...kuna mpangaji wa kiume akanieleza kuwa hapo wamehama ila uzuri alikua anafaham wamehamia wap so akanielekeza maana haikua mbali na hakukua na haja ya kumpigia..in short nilitaka nimsurprise shem wangu wa zaman
Kwakua ni nyumba mpya sijaizoea kwa uani nikakuta mdada nikamsalimia nikamwelezea nnayemtafuta..akaguna..akanyooshea kidole mlango mmoja wa mbao ambayo haikupakwa rangi..nikagonga...yule mdada akaniambia we ingia tu yupo..

Nikafungua mlango..
Kwanza nikakuta ndani hakueleweki..nilivua viatu nje kwahyo suruba ya michanga ndani nilipata kuishuhudia..nguo kadhaa na khanga zikiwa chini zimetelekezwa..vero akiwa amejifunika gubigubi..nilimwita mara mbili ila hakuitika..nikasogea kitandani nikamtikisa kidgo..nikavuta shuka
Akageuka kuniangalia...Dooh..
Alikua amebadilika..kwanza mashavu tu yalikua hamna nyama nilizozoea kumtaniaga..utando mdomoni..nywele kama zimenyolewa kwa mkasi..macho yamemtoka..alivyoniona akataka kujifunika kwa aibu..nikamzuia..hata mambo sikumpa ilibidi nianze kuuliza tatzo
Akaniambia anaumwa...
Moja kwa moja nikajua basi ashaukwaa ugonjwa wetu..nikaogopa kuuliza..ila kwa jinsi nilivyomwangalia nahisi alijua kwamba nilishajipa majibu..alismile kwa shida af akaniambia "sio ukimwi shem"
Akanieleza kua ana uvimbe kwenye uzazi na gonjwa moja la zinaa
Nyumbani hawajui ila chuo alishaacha..ada anayotumiwaga ndo alikua anatumiaga kujikimu na ilishaisha..
Akaniambia "kevi mi nakufa..naomba unipeleke tu nyumbani,atleast ukiwepo ntakua na ujasiri wa kuwaeleza yaliyonisibu"
Ngoma nikaona nzito..nikatoka nje nkampigia mchizi aje
Alifika..bora mimi ila yeye ndo alichanganyikiwa kabsa..
Tukampigia usafi pale wa kishkaji..yule sista wa nje tukampa elf 20 tukaomba amsaidie aoge..amfulie vinguo kadhaa na usiku ampikie..kesho yake amwandae maana tutakuja kumpeleka kwao..
Kesho mapema na mchizi tukampeleka moro
Ile tunamshusha kwao baba ake kumwona alilia..alilelewa na baba ake baada ya mama ake kufariki..tukamweleza matatizo na hali ya mwanae tulivyoikuta akatushukuru akasema mengine atayafanyia kazi ilimradi tulimleta mwanae nyumbani..tukawa tunamjulia hali kila tulipoweza
So mwaka na miezi ishapita..guess what!! Alhamisi hii tukaalikwa kwenye Send-off yake..na mida mida hapa kuna mwana atamfanya wake wa maisha...leo nikawaza..
"KWENYE KILA TATIZO KUNA TUNDU LA KUTOKEA....LITAFUTE"

Acha nipige pasi hapa,kama kawa usiyempenda kaja😅

#fanani✍️ hapa
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Urs truly✍️

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!