My Authors
Read all threads
Ifahamu safari ya mbu kuanzia anapokung’ata mpaka anasababisha ugonjwa wa malaria: Kitu cha kwanza unachotakiwa kufahamu ni kuwa, Japo kuna mbu jike na dume, Mbu jike pekee ndiye anayeng’ata. Mbu dume hang’ati.
#ElimikaWikiendi Image
Hii ni sababu mbu jike uhitaji damu ili kutengeneza mayai huku dume hana uhitaji wa damu maana hatengenezi mayai hivyo hupata chakula kutoka kwenye majimaji ya maua (flower nector) na mimea.
Damu anayoivuta mbu haina faida yoyote ya lishe kwake. Damu hutumika kutengeneza mayai pekee ambayo baadae huyaweka kwenye maji ili dume arutubishe ili kuzalisha mbu wengine. Ili kuishi mbu jike hupata chakula chake pia kwenye maua.
Inakuaje mbu mpaka anamng'ata binadamu. Mbu huvutiwa na hewa aina ya carbon-dioxide ambayo binadamu huitoa. Hewa hii mwanadamu huwa tunaitoa kupitia kupumua na kupitia ngozi.
Nikurudishe nyuma kidogo, Vimelea (plasmodium) vinapokuwa kwa mbu huzaliana ndani ya tezi za mate (salivary gland). Mate haya upande wa mbu huyatema sehemu anapotaka kuvuta damu ili kumsaidia damu anayoivuta kutoka kwako isigande, Ikumbukwe damu ikiwa nje ya mfumo inaganda.
Sasa akitua kwenye ngozi yako hutema mate haya ili kwanza, usisikie maumivu lakini pili damu atakayoivuta iwe haijaganda. Baada ya hapo huchomeka mdomo wake (proboscis) ili kuvuta damu. Anapochoma mdomo wake kuvuta damu hapa ndipo huruhusu vimelea vya malaria kuingia mwilini.
Kifupi mbu hajui kama anaambukiza Malaria, yeye anakuwa katika safari zake kutafuta damu ili kuongeza familia yake. Baada ya vimelea kuingia kwenye mfumo wa damu husafiri mpaka kwenye seli za ini. Safari hii huchukua muda mfupi sana kiasi hata mtu aliyeng'atwa hawezi kushtuka.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Festo D Ngadaya

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!