My Authors
Read all threads
PAULINE OPANGO LUMUMBA; mke wa Patrice Emery Lumumba, alizaliwa 1937 na kufariki 2014 akiwa nyumbani kwake jijini Kinshasa, taarifa ya msiba wake ulitangazwa na Lambert Mende msemaji mkuu wa serikali ya Kongo, Pauline anajulikana pia kama "Pauline Opangu Mama wa Taifa" THREAD 👇
Pauline alikuwa ni mwanaharakati wa Kongo na mke wa Patrice Lumumba, Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huru. Alizaliwa kijiji cha Wembonyama, Tarafa ya Sankuru, Jimboni Kasai katika iliyokuwa Belgian Kongo. Aliolewa na Patrice Lumumba mnamo Machi 15, 1951
Kwa mujibu wa Karen Bouwer katika kitabu chake cha Gender and Decolonization in the Congo, watu wengi Afrika wanamuona Lumumba kama kiongozi wa pili bora karne ya 20 nyuma ya Nelson Mandela kwa alama ya uhuru wa kweli wa Afrika. Leo tumtazame mkewe. Pauline Opangu Lumumba
Pauline anasema mumewe alikuwa hapatikani mara nyingi nyumbani. Ni mara chache kumpata nyumbani.Akiwepo ni kusoma vitabu au kuandika. Pauline alikuwa hajui kusoma/kuandika. Anasema mumewe alikuwa akilala muda mfupi, kunywa sana Kahawa, kuoga maji ya baridi.
Pia, asipoenda kazini kwake, atashinda muda mwingi maktaba, huko atakutana na makundi mbalimbali kujadili mchakato wa uhuru wa Congo, atatumia muda mwingi kuandika makala za ukombozi wa watu wa Congo kwa ajili ya kuchapishwa kwenye magazeti mbalimbali nje na ndani ya Congo.
katika maisha yao Pauline alimzalia Lumumba watoto wanne, ambao ni Patrice, Juliana, Roland na Marie-Christine.

Lumumba na Pauline waiishi katika mazingira magumu katika uhusiano wao na hii ni kutokana na maisha ya kisiasa ya Patrice Lumumba kwani Pauline alitengwa na Lumumba
kwa kifungo cha Patrice kwa mara kadhaa, hata hivyo Pauline alivumilia na kuendelea kuwa pamoja na Lumumba katika harakati za ukombozi katika kipindi chote cha kudai uhuru wa Kongo.

Pauline alikua mke wa Lumumba akiwa na umri wa miaka 23 tu alishuhudia mumewe akikamatwa,
Alishuhudia kuteswa na hadi kuuwawa kwake chini ya vibaraka wakiwa wanaongozwa na mabepari.

Pauline alimsaidia mumewe kwenye harakati za siasa, ni miongoni mwa wanachama wa mwanzo kujiunga na chama kilichoanzishwa na mumewe kilichoitwa "Mouvement National Congolais" (MNC)
Hadi mumewe anakamatwa walikua pamoja kwenye gari aina ya Reunalt 219 ambapo Lumumba alikua anajaribu kutoroka kuelekea Stanleyville (sasa Kisangani), kufatia uasi uliokuwa ukiongozwa na Mobutu Seseseko, kwa bahati mbaya hakufanikiwa kufika Kisangani (Stanleyville wakati huo)
Kwani maadui zake (maadui wa Patrice Émery Lumumba) walimnyakua kama mwewe anavyonyakua kifaranga cha kuku na kwenda kupora uhai na kwenda kumtesa hadi kufikia kifo chake kwa kupigwa risasi na kuyeyusha mwili wake kwa kutumia acid (tindikali) huko jimboni Shaba (Katanga ya sasa).
Hakukuwepo na mazishi rasmi ya Patrice Emery Lumumba maana maadui zake waliamua kuupoteza kabisa mwili wake na lengo ilikua ni kutaka asahaulike kabisa kwa watu katika historia ya Kongo na Afrika nzima. Pauline hakupewa hata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwa mumewe.
Mwanzoni baada ya Kifo cha Lumumba Pauline aliungana na wakina Mulele, Antonne Kizenga na Lindula huko kisangani katika kuongoza jeshi liloitwa "Simba" kupinga kupinduliwa Lumumba, na kuilisha serikali halali madarakani. Familia yake ilikuwa inapitia kipindi kigumu wakati huu.
Pauline alikua na miaka 23 tu na ilibidi akabiliane nayo yote yanayoendelea katika umri wake kutokana na njia ya mumewe aliyoamua kuishi kwa kuwapigania watu wa taifa lake, Pauline ndio kiigizo cha Jonsina Muthemba Machel, mke wa kwanza wa rais wa kwanza wa Msumbiji Samora Machel
Patrice Emery Lumumba aliishi maisha yake yote katika ndoto ya kuwakomboa ndugu zake wakongo kutoka kwa wabelgiji ndio maana alipo kuwa gerezani Katanga alimuandikia barua mke wake kumpa moyo na mategemeo ya kumtaka aendeleze harakati za ukombozi na uhuru wa ardhi yao ya Kongo.
Lumumba aliamini lazima atauawa na kumwandikia Pauline barua akimtia moyo aendelee na kazi yake ya ukombozi hata baada ya kifo, barua hiyo ya Lumumba kwa Pauline ni moja ya barua maarufu duniani ni moja ya nyara zinazoifadhiwa Kongo na kubaki kama kumbukumbu kubwa kwa nchi hiyo.
Mnamo Februari 14, 1961, Pauline alitembea katika vitongoji vya jiji la Kinshasa (Leopoldville) akiwa kifua wazi (yaani matiti hadharani), akifuatana na wanafunzi 100 na wafuasi wengine wa marehemu Lumumba, kwenda makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Maandamano hayo yalikusanya wanawake na wanaume ambao walitembea nyuma ya Pauline huku vichwa vyao vikiwa vimeinama chini, kitendo ambacho kilionesha kupinga mauaji ya Patrice Lumumba. Maandamano hayo yalielekea makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Leopoldville
Katika makao makuu ya UN, Pauline, pamoja na Albert Lumumba, Joseph Lutula na mtoto mdogo (aliyeitwa Marie-Christine) wa Pauline, ambaye alikuwa amembeba mgongoni, alikutana na Rajeshwar Dayal, mwakilishi wa UN nchini Kongo.
Kufuatia mkutano huo, UN ilikubali kusaidia kuupata mwili wa Lumumba ili ufanyiwe mazishi ya Kikristo katika mji mkuu wa Leopoldville (sasa Kinshasa).

Hata hivyo Maombi hayo hayakufanikiwa na mwili wa Lumumba haukupatikana kabisa, jambo hilo lilimuumiza sana Pauline.
Pauline na waliomuunga mkono kwa kutembea kwa miguu katika mitaa ya mji wa Leopoldville (sasa Kinshasa). Huko mitaani, alikua kifua wazi (matiti nje) aliifanya kuonyesha hasira zake na kupinga mauaji yaliyomkuta mumewe Lumumba kwamba ni ya uonevu hakustahili kufanyiwa hivyo.
Lakini ishara hiyo ya mwanamke kutembea huku matiti yakiwa nje kwa mila za kiafrika ni ishara ya kutoa Laana na hisia kali kwa watendaji walio husika, kwa Pauline tukio lile alifanya kutoa laana kwa kuwalaani wote wakongo walio husika katika Mauaji ya mume wake Patrice Lumumba
Miaka 48 baadae raia wa Congo wanasema alichokifanya Pauline Opangu Lumumba kutembea matiti nje katika mitaa ya Kinshasa mwaka 1961 yalilipa kwa Mobutu Seseseko kwani alikufa kifo cha hovyo na aibu kwa kansa ambayo ilitafuna na kuozesha hadi korodani zake na kuzikwa na watu 4 tu
Wengi ya watu walio husika katika mauaji ya Patrice Emery Lumumba kinachoitwa "laana kutoka kwa Pauline" iliwafuata kwani vifo vyao vilikuwa kama mbwa wa jalalani wasiokuwa na makazi maalum, kwani wengi wao walikufa kwenye vita ya kuuangusha utawala wa Mobutu Seseseko mwaka 1997.
Pauline Opango alitembea umbali wa 10km kuelekea kwenye kituo cha umoja wa mataifa, lilishatokea pia nchini Nigeria mwaka 1929, wanawake wa Aba walipokua wanawapinga wakoloni wa kiingereza pia Kenya wakati wa utawala wa Daniel Arap Moi, Wangari Mathai alifanya hivyo kumpinga Moi
Pauline baada ya kuomboleza msiba wa mumewe kwa mtindo ule aliamsha hisia kwa wauaji wa mumewe na kuanza kumuandama hadi alipo amua kukimbilia uhamishoni nchi mbalimbali ikiwemo Misri ambako huko alipokelewa na Nasser Gamal (rafiki wa Mumewe) na kupewa hifadhi ya kisiasa.
Pauline alirudi Kongo mwaka 1990 baada ya serikali kumtabua Lumumba kama shujaa wa taifa hilo. Aliishi maisha ya dhiki kwa miaka 54 hadi mwisho wa uhai wake, kila siku alishuhudia propaganda na uongo wa aina mbalimbali ukizushwa, kusambazwa na kuzungumzwa kila kona juu ya mumewe.
Hakuwa na namna nyingine. Alibaki na familia na alipaswa kuitazama. Na mtoto wake mmoja mdogo alifariki miezi kadhaa baada ya kifo cha mumewe. Pauline aligoma kuolewa na hadi anafikia kufariki akiwa na miaka 78 bila ya kuwa na mwanaume mwingine.
Na hii aliifanya kwa ajili ya kulinda heshima ya mumewe, kuonyesha mapenzi aliyokua nayo juu ya mumewe na pia alisema hakuona mwanaume mwenye kufanana na mumewe Patrice Lumumba. Desemba 23, 2014, akiwa na umri wa miaka 78, Pauline alifariki akiwa amelala nyumbani kwake Kinshasa,
Pauline alifariki siku kadhaa baada ya kurudi kutoka Paris, France alipokwenda kupata matibabu.

Pauline anakumbukwa kama mwanamke shujaa, mwenye msimamo katika historia ya ukombozi wa taifa la Kongo, aliyesimama upande wa mumewe ambae ni mwasisi na mpigania uhuru wa Kongo.
Pauline ni kioo cha ukombozi wa taifa lake na Afrika nzima maana hadi mauti yake yanamfika 2014 alikuwa bado anapigania kutambuliwa kwa mumewe kama shujaa na mzalendo aliyepata mauti kwa kuwapigania wakongo na waafrika. Ndoto yake ilitimia. Hakuwahi kuacha kumpigania mumewe
Ndoto yake ilitimia kwa Lumumba kupewa heshima kama baba wa taifa na muasisi wa Kongo, hata hivyo serikali ya Laurent Kabila na Joseph Kabila zilimtunuku Patrice Lumumba heshima ya kuwa shujaa mkuu wa Kongo, sanamu la Lumumba limejengwa katika ya jiji la Kinshasa eneo la Limete.
Pauline Opangu Lumumba mama wa taifa Kongo ni alama ya ukombozi katika ardhi ya Kongo ambayo sasa inaitwa DRC na kwa heshima yake, mitaa, shule, vyuo na maeneo kadhaa nchini Kongo yamepewa jina lake kwa kuenzi heshima yake. Ni kati ya alama kubwa Afrika zilizosahaulika

Mwisho!
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Martin M. M

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!