My Authors
Read all threads
MOBUTU SESE SEKO KUKU NGBENDU WA ZA BANGA.

Aliishi kuanzia 14.10.1930 mpaka 07.09 1997. Alikua mwanasiasa, aliwahi kua Afisa wa juu wa jeshi pia aliwahi kuwa Raisi wa Taifa la Zaire enzi hizo ambalo kwa sasa linaitwa Congo mwaka 1965- 1997.
Mobutu alipata elimu yake katika shule ya kimishenari na alianza rasmi kazi kama mwanajeshi katika jeshi lenye mchanganyiko wa wabelgiji na wa Congo (The Force Publique) na alipata vyeo kadhaa ikiwemo Sergent major cheo kilichokua kikubwa kwa jamii ya kiafrika.
Alichangia na kuandika makala kadhaa katika gazeti la Léopoldville na baadaye alikua ripota katika gazeti la daily L’Avenir na baadaye alikua Mhariri wa Actualités Africaines.
Siku moja Katika mahojiano alikutana na Patrice Lumumba aliyekua katika chama cha Congolese National Movement (MNC) na aliadhimia kujiunga naye kuanzisha vugu vugu muhimu la mapinduzi.
Mwaka 1960 Mobutu alimuwakilisha Lumumba katika kikao kimojawapo katika kuelekea siku za uhuru ambapo Mobutu na wenzake
walishinikiza kuachiwa kwa Lumumba ambaye alituhumiwa kueneza itikadi mpya za siasa katika taifa hilo . Mobutu alitetea hoja za Lumumba. Hatimaye Congo lilikua Taifa huru tangu 30.06.1960
Serikali ya mseto chini ya raisi Joseph Kasavubu na waziri mkuu akiwa Lumumba walimteua Mobutu kuwa katibu mkuu wa ulinzi wa Taifa hilo.
Alianza kucheza rafu, huku akiwa anaendelea kuwahamasisha wanajeshi, alitengeneza makundi kadhaa ndani ya jeshi yanayomsapoti. Si hivyo tu alimshauri raisi Kasavubu wamuondoe madarakani Lumumba ambapo walifanikiwa.
Mwaka 1961 februari Mobutu alipewa cheo cha ukamanda wa majeshi na raisi Kasavubu. Hata hivyo wengi huamini Mobutu alihusika kwenye kifo cha Lumumba.
Baada ya mvutano wamuda mrefu wa Raisi Kasavubu na Waziri mkuu mpya Moise Tshombe,
Mobutu alipanga mapinduzi ya kumuondoa Kasavubu madarakani ambapo alifanikiwa mwaka 1965. Alibadilisha jina la nchi kutoka Congo hadi kuitwa Zaire na hatimaye alibadili jina lake pia kutoka Joseph-Désiré Mobutu na kuitwa Mobutu Sese Seko mwaka 1972.
Alisema hafungamani na upande wowote Si Ubepari, Si ujamaa wala si kati kati. Raisi huyu alikula bata sana kipindi cha utawala wake fedha nyingi zilipotea kwa rushwa na Raia wake waliishi maisha ya kubangaiza sana.
Uchumi uliyumba sana na thamani ya Fedha kushuka sana. Nchi ilikua na Madeni mazito. Misaada iliendelea kumiminika kutoka kwa washirika wake Ubeligiji, Marekani na Ufaransa maana walimuona kama nguzo kubwa iliyodhibiti ujamaa.
Alijenga urafiki na Israeli, Jeshi la Kigiriki pamoja na Serikali ya Afrika kusini. Mwaka 1972 pia alianza kushirikiana na Mao Zedong kutokana na misimamo yake ya Kutokubaliana na Wasovieti. Mao alihitaji kujenga Ukanda wa Afro-Asian Ambao alihitaji kuuongoza.
Fedha alizopata Mobutu zilimsaidia kufanikisha dili zake na Mataifa ya Magharibi. Hivyo hakwenda kwenye Taasisi ya Fedha Duniani (IMF) Kuomba msaada.
Hata hivyo Mobutu alimiliki zaidi ya $4 Bilioni nchini Uswisi ambayo ilikua sawa na kiasi cha deni la nchi hiyo.
Alimiliki gari kali, Mercedes-Benz aliyotumia kutembelea maeneo mbalimbali japo watu wake walikua wakiomboleza tu. Wafanyakazi wa umma walimaliza miezi bila kulipwa mishahara. Mirija ya Fedha za umma zilikua ilibanwa na ilikua inafika kwa familia ya Mobutu, kwa viongozi wa Jeshi.
Mobutu alikua na mjengo mkali na aliuita “The Versailles of the Jungle”. Bwana huyu akienda shopping huko ufaransa alitumia ndege ya France Air. Kwenye makazi yake haya alijenga uwanja mkubwa uliojulikana kama Gbadolite Airport .
Ambao ulikua na run way ya ndege yenye urefu wa kutosha kushuka ndege na kupaa pia na uwanja huo uliwezesha kutua Madege makubwa ya miaka hiyo yaliyojulikana kama Concorde.
Mobutu anasadikika kuuza raslimali za nchi yake zenye zaidi ya thamani ya $5 bilioni huku wananchi wakikwama kujikwamua kwenye lindi la umasikini.
Katika karne ya 20 Mobutu alikua gumzo kwenye masikio ya watu wengi Barani Afrika. Kituo cha Televisheni nchini Congo jioni moja kilimtengeneza kama mtu anaeshuka kutoka mawinguni kama mungu.
Alikua na majina mengi kama Masihi, Baba wa Taifa, mwana mapinduzi, mwokozi wa watu, muasisi, n.k. Enzi zake kutumia mali ya uma kwa matumizi binafsi au kufurahisha kadamnasi ilikua sio jambo gumu.
Mdororo wa kiuchumi wa 1991 ulimfanya kukubaliana na wapinzani kuongoza nchi kwa pamoja. Lakini bado alitumia sana jeshi kufanya mabadiliko na kuteua viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri.
Mpaka 1997, Ambapo kundi la waasi likiongozwa na Laurent-Désiré Kabila walimpindua Dikteta huyu. Kwa msaada wa Raisi Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Paul Kagame.
Alikimbilia uhamishoni kwa muda . Alikufa miezi mitatu baadae akiwa huko Morocco kwa Kansa. Rushwa na fedha alizotumia bila kuandikiwa matumizi yake zinakadiriwa kuwa $4 bilioni mpaka $15 bilioni. Jumba kubwa la thamani kubwa hivi sasa ni mapango tu na makazi ya Nyoka na popo.
Alishawahi kusema “Ukitaka kuiba iba kidogo kidogo katika njia nzuri. Ila ukiiba sana na kuwa tajiri ndani ya usiku mmoja , Utakamatwa”
Si mfano mzuri wa kuigwa kama kiongozi. Alitumia mabavu(mkono wa chuma) na kukandamiza haki za Raia pamoja na uhuru wao huku akijinufaisha peke yake na kusababisha raia walie kwa ukata. 🙏
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with WIlly

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!