My Authors
Read all threads
Watu wengi wamejikuta wanaanza biashara au ujasiriamali kama chaguzi la mwisho baada ya kukosa kazi, mtaji au kuajiriwa.
Hivyo wengi wanajikuta wapo katika kujiajiri wakikosa maarifa sahihi katika kufanya na kuendeleza Biashara. UZI Huu utakusaidia kufikiria katika KUPANGA BEI. Image
KUPANGA BEI

1.Moja ya changamoto kubwa kwa wajasiriamali na wafanya biashara wengi ni katika kumiliki soko ni upangaji wa bei za bidhaa au huduma. #MpangoWaBei @Mkuruzenzi Image
2.Kupanga Bei ni sayansi na hesabu lakini pia ni Sanaa ya biashara. Bila kujua sayansi ya upangaji bei, Sanaa katika kuweka mfumo wa uhimilivu na hesabu katika gharama za uzalishaji basi lazima ushindwe kubakia Sokoni. Image
3.Katika Elimu ya mfumo wa Soko kuna mambo mengi yanafundishwa ila kuna mihimili minne ya Masoko. Kwa lugha ya Mkoloni imezoeleka kama 4P’s of Marketing. Image
4.P ya kwanza inasiamama kama Product (Bidhaa), P ya pili inasimama kama Promotion (Utangazaji na uhamasishaji), P ya tatu usimama kama Place (Eneo la Soko) na P ya nne usimama kama Price (Bei).
5.Hapa ndio Uzi huu unasimama kukusaidia usianguke katika Hesabu na Sanaa katika upangaji bei kwa kutumia Sayansi ya Biashara. Image
6.Upangaji wa bei ni mchakato muhimu sana na ni mchakato wa kipekee. Unapoanza kufanya biashara Bei ndio msukumo wa biashara maana hata ukafanya uhamasishaji, usafirishaji wa huduma au bidhaa lakini kama soko unalolihudumia halina uwezo wa kununua basi Bei inakuwa ni kikwazo. Image
7.Upangaji wa bei ndio njia ya mafanikio au kushindwa kwa biashara. Baada ya kufanya utafiti na kufahamu wateja wako watarajiwa ni akina nani, sasa ni wakati wa kujua kiasi cha Fedha utakazowatoza kwaajili ya Bidhaa au Huduma utakayowauzia. Image
VIGEZO KATIKA UPANGAJI WA BEI

Bei ya bidhaa au huduma hupangwa kutegemea na moja kati ya vigezo hivi au vyote kama vinavyoelezwa hapa;
•Gharama ya Bidhaa au huduma inayotolewa.
•Thamani ya Bidhaa au huduma kwa mteja; hii inajumuisha kama utampelekea
•Bei za washindani wengine katika soko. Mara nyingi hauwezi kuwa mwenyewe katika soko hivyo kuna washindani wako nao wanauza bidhaa au huduma inayofanana. Image
•Idadi ya wateja wanaohitaji huduma na hali ya soko kwa ujumla. Hali ya soko ni sheria ya kiuchumi, kwa mfano uwepo wa bidhaa nyingi kwa wakati mmoja, na kupungua kwa uhitaji, upelekea bei kushuka maana thamani na uhaba upotea.
Wengi mnakumbuka kuhusu Nyanya, kuna wakati inakuwa sokoni kwa bei ya bure na kuna wakati inakuwa sokoni kwa bei ya Apple. Image
Karibu kuendelea kufuatilia kurasa zetu katika mitandao ya kijamii; Facebook, WhatsApp, Instagram ana Twitter kujifunza Zaidi mbinu za kumiliki soko. Image
Ahsante sana. Usisahau kujiunga na channel yetu ya Youtube kwa kufuata kiunganishi katika bio. bit.ly/SUBSCRIBE-Data… Image
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Data Masoko

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!