My Authors
Read all threads
Anaitwa Anna Ecklund Raia wa US Aliyezaliwa Mwaka 1882. Akiwa na Umri wa Miaka 14 tuu Alianza Kuandamwa na Roho Chafu za Ndugu Zake Waliofariki. Marehemu Baba Yake Alikuwa Anamuingilia Kingono, Hakuna Aliyeweza Kumsaidia. Bado Yuko Hai Hadi Leo. #UZI 👇👇
Simulizi ya kusikitisha ya Anna ni moja ya simulizi za kweli maarufu Amerika, kuna vitabu kadhaa vimechapisha simulizi hii kikiwemo kitabu cha Begone Satan kilichoandikwa na Carl Vogl mwaka 1935 na baadaye kuandikwa tena na mchungaji Celestine Kaspsner wa UK mwaka 1973.👇👇
Anna alikuwa anaishi na roho nyingi katika mwili wake zikiwa zinamsumbua, na moja ya roho hizo zilikuwa ni roho za marehemu baba yake Jacob Ecklund, marehemu shangazi yake na marehemu Bibi wa baba yake Mina, wote walifariki, lakini bado roho zao zimekuwa zikiishi ndani yake.👇👇
Anna alizaliwa mwaka 1882 mjini Wisconsin US lakini akiwa na umri wa miaka 14 tuu alianza kuonyesha dalili mbaya, alianza kuchukia na kupata tabu kila akikiona kitu chochote kinachohusiana na dini. Ilikuwa kila akipita maeneo yenye nyumba yoyote ya ibada anapata shida, 👇👇
anakua kama mtu aliyechanganyikiwa, na kwa umri huo mdogo alikiri kuwa alikuwa akiingiliwa kingono na roho ya baba yake mzazi Jacob. Hali hii iliendelea katika maisha yake yote na alipofikisha umri wa miaka 26 alikuwa ameshamilikiwa kwa asilimia 100% na roho hizo mbaya, 👇👇
ndipo mchungaji Theophilus Riesinger wa Wisconsin aliamua kufanya uchunguzi juu ya Anna, Juni 18, 1912 alikua amemaliza kufanya uchunguzi huo. Hata hivyo kwa bahati mbaya inaelezwa kuwa uchunguzi huo wa baba mchungaji uliokuwa na lengo na kumsaidia Anna kutoka katika mateso 👇👇
hayo haukufanikiwa kabisa kutokana na roho hizo kuwa 'zimeota mizizi' na zimeanza kumuachia laana Anna. Roho zilitoa laana kwa chochote ambacho Anna angepatiwa na watu wadini ili kisifanye kazi, zilitoa laana kwa yeyote aliyejifanya mstaari wa mbele kumsaidia Anna kutoka 👇👇
katika mambo hayo ya ajabu. Katika uhai wake shangazi yake alikuwa mshirika mkubwa wa imani za kishirikina alizorithi kwa Mina, baada ya kufa walihitaji kumtesa Anna ili warejee kuwa na nguvu za kichawi tena hata baada ya kufa kwakua inaaaminika mchawi akirudi kuwa na nguvu 👇👇
zake zinakuwa kubwa mara saba zaidi ya zile za awali. Inaelezwa kuwa kilichowaudhi sana ndugu zake hao kabla ya kufariki ilikuwa ni kitendo cha Anna kupenda sana kwenda kanisani, ilifika kipindi alikuwa analala kanisani, alikuwa ni mtoto mwenye imani kitendo kilichowaudhi 👇👇
sana baba yake na shangazi yake. Miaka 20 baadaye mchungaji Theophilus alianza mchakato wa kumsaidia Anna kuondokana na roho hizo zilizokuwa zikimtesa maisha yake yote, lakini licha ya kusaidina na mchungaji mwingine Joseph Steiger wa Earling, Lowa US lakini waliahindwa, 👇👇
wakaamua kuacha kwa kuogopa. Waliogopa kwasababu waliamini kuwa roho hizo zilikuwa na nguvu mara saba zaidi ya vile ambavyo zilikuwa na nguvu wakati watu hao wapo hai, kwahivyo zingeweza kuwamaliza na wao. Awali mch. Theophilus aliamini kuwa ikiwa atamchukua Anna kutoka 👇👇
mji anaoishi na kwenda kumfanyia maombi katika mji mwingine basi ingesaidia, lakini maombi yalivyoanza tuu akagundua kuwa itakua hatari kwake, akaacha. Anna akachukuliwa na kanisa moja na kuanza kuhudumiwa na watawa ili wajaribu kuziondoa roho hizo, lakini bado walishindwa, 👇👇
chakula chochote ambacho kitaombewa kwanza na akapewa Anna ili ale, basi atabadilika na kuanza kutoa sauti za Paka zinazotisha, atakua na hasira akitaka kumdhuru mtu. Ilikuwa ni kama uchawi, hata chakula kikiombewa bila yeye kuona lakini Anna atajua na kubadilika ghafla, 👇👇
watawa waliogopa sana, na sasa akawa anapewa tuu chakula ambacho hakijaombewa japo kuna muda alikuwa anakikataa kabisa. Wakati huu wote roho ya baba yake Anna, Jacob ilikuwa inaendelea kumuingilia mwanae huyu kingono, inaelezwa kuwa shangazi yake enzi za uhai wake alikuwa mchawi,
aliwauwa watoto wanne ambao walikuwa ni watoto wake mwenyewe kabla nayeye hajafariki. Anna alikaa kanisani hapo kwa muda mrefu, lakini ilikuwa ni ngumu sana kumuondoa roho hizo, kuna muda alikuwa anakaa vizuri tuu kama kawaida, lakini muda mwingi alikuwa anafungwa na minyororo 👇
ama kushikiliwa na zaidi ya watu 6 kwasababu alikuwa na nguvu za ajabu. Kuna muda Anna alikuwa nawekwa ndani lakini anabomoa mlango na kutoka nje, kuna muda alikuwa anatukana watu matusi makali lakini midomo yake haichezi kuonyesha kuwa anaongea, sauti inatoka kooni mwake 👇👇
lakini midomo yake imetulia tuu, ni wazi kuna vitu vilikuwa vinaongea ndani yake. Kuna muda Anna alikuwa anatapika vitu vya ajabu kama vile majani na vipande vya nyama ambavyo haikuwahi kujulikana vilikuwa ni vipande vya nyama gani, wakati mwingine kichwa chake kilikuwa 👇👇
kinavimba na kuwa na ukubwa usio wa kawaida, na tumbo lake lilikuwa linajaa kama mjamzito wa miezi 9, lakini linarudi tena na kuwa kawaida. Kuna muda pia midomo yake ilikuwa inavimba hadi kufikia lips zake kuwa na unene unaokaribia kiganja cha mkono, mwili wake ulikuwa 👇👇
una nguvu hadi kitanda cha chuma alichokuwa anakilalia kikawa kinapinda, alikuwa anaongea lugha nyingi ambazo hakuna aliyewahi kuzifahamu ni lugha gani. Anna alikuwa na uwezo wa kuwapiga watumishi wa dini wanaomsogelea na kuanza kueleza kila kitu kuhusu wao na madhambi yote 👇👇
waliyowahi kuyafanya tangu utotoni anaanza kuyaeleza hadharani huku kila mmoja akibaki mdomo wazi. Amewahi sema kua mchungaji Steiger atafariki baada ya kupata ajali mbaya ya gari, na ni kweli siku chache tuu baadaye ilikuwa hivyo. Kuna muda watawa walikuwa wanahisi harufu ya 👇
uwepo wa binadamu ndani, lakini hawakuwa wakionekana, badala yake kulikuwa kunaonekana nzi na mbu wengi kisha wanatoweka. Mchungaji Theophilus alisema kuwa kuna muda alikuwa akiwaona watu wawili wa ajabu katika kona ya chumba cha Anna, mmoja alimuelezea kuwa ni mrefu sana 👇👇
mwenye manyoya meusi, alikuwa anamtazama sana kwa hasira mchungaji huyo aliyekuwa akijitahidi kumsaidia Anna bila mafanikio. Usichokijua ni kwamba Anna au kwa jina lingine Emma Schmidt hadi leo hii bado yuko hai, alizaliwa March 23, 1882 mjini Wisconsin US na hadi sasa ana 👇👇
umri wa miaka 138, anaendelea kusaidiwa katika taasisi mbalimbali za dini mjini Early, Lowa. Ni vitabu na movie nyingi sana zimetoka hadi sasa kuielezea story hii ya kusikitisha ya Anna, mwaka 2016 ilitoka movie ya The Exorcism of Anna Ecklund.👇👇
Pole na Jongera kwa Kumaliza Uzi huu Mrefu, Nyuzi kama hizi hapa ndo nyumbani, Kama una telegram basi jiunge hapa t.me/fm_facts utamishukuru Baadaye.

@KaribuSanaMjini
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with FM facts

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!