My Authors
Read all threads
#Library4Future

Habari wapwa!
Sasa nimekuja kuelezea ahadi yangu niliyoitoa kuhusu👇👇👇
💢Kuflash simu ni nini?
💢Tools zitumikazo kuflash simu
💢Tofauti kati ya hard reset vs kuflash simu
💢Kuroot simu ni nini?

#Uzi 👇👇👇
💢Kuflash simu ni kitendo cha kubadili mfumo endeshi wa mwanzo na kuuweka mwingine. Ule mfumo endeshi wa mwanzo kabisa baada ya kununua simu mpya huitwa "Stock firmware" na mfumo endeshi unaouweka badala ya wa mwanzo huitwa "Custom firmware".
Kuna sababu kadhaa hupelekea simu kuflash mojawapo ni kama hizi:-
*Simu kukataa kuwaka
*Simu kuwaka ila inaishia kwenye logo
*Simu kijiwasha na kujizima yenyewe
*Virusi kuvamia simu na kupelekea simu kusumbua sumbua kila utumiapo
*Simu kuwa na matangazo mengi
...na sababu nyingine nyiingi japo najua kuna watu humu wanafahamu matatizo yanayopelekea wao wakaiflash simu zao.

Unapoflash simu huwa kuna vitu vinaangaliwa zaidi kabla ya kuflash hiyo simu maana ukiweka wrong firmware simu inaweza ikabrick(kuzimika)
...kubrick kwa simu kuna mawili ambayo ni:-
*Softbrick
*Hardbrick

SOFTBRICK
-Hii ni hali ambayo pindi unaflash simu kabla haijamaliza process nzima simu inazimika yenyewe au ukaweka wrong firmware na simu ikazima au tatizo la umeme kuzimika, n.k
Endapo simu itazimika nawe ukaamua kujaribu kuichomeka kwenye charger ikaonyesha kuwa charge inaingia ila simu haiwaki hii huitwa "softbrick". Ambayo husababishwa na software ya simu husika na hapa ukianza process upya inaweza ikapona bila shida.
HARDBRICK
..Hii hali hufanana na softbrick lakin tofuati ni moja tu, hardbrick simu inaweza ikazima pindi unaflash kwa kuweka wrong firmware au tatizo la umeme, n.k sasa kabla hujamaliza simu ikazimika na kukataa kuwaka kabisa hata ukichomeka...
....hata ukichomeka kwenye charger simu haiwaki kabisa wala haionyeshi dalili za kuwaka au kuonyesha kuwa charge inaingia maana yake imebrick na hapo hakuna cha zaidi ni kuipeleka "Museum" ikapumzike tu.
*Hivyo tuwe makini sana pindi tunaflash simu...
💢Tools zitumikazo pindi unataka kuflash simu...
*Computer
*Simu husika
*Firmware(hii niliwahi kuelezea uzi uliopita)
*USB cable
*USB drivers
*Akili zako(Utaalamu wa kuflash simu)
*Software ya kuflash simu husika

Baada ya hizo tools kukamilika....👇👇
...baada ya hizo tools kukamiliza sasa utaanza process nzima ya kuflash simu.
Kwanza kabisa unawasha computer yako, fungua USB drivers(Hapa panahitaji elimu kidogo, maana mwanzoni pindi unajifunza ni ngumu kuinstall drivers kuna mlolongo utaufuata),
...ukimaliza kuinstall drivers ndipo ukarun ile flashing software na kuna sehemu utaambiwa upload ile firmware nawe utafanya hivyo baada ya hapo chukua simu husika zima kisha chomeka USB cable kwenye computer kisha nenda kwenye software iruhusu ianze kazi..
...ukiruhusu tu itakuambia chomeka simu, wewe utachukua simu uliyozima utabonyeza batan ya kupunguzia sauti na kuwashia simu kisha chomeka ile USB cable kwenye simu utaona maandishi detected yenye maana ya imesoma hapo hapo achia zile batani ulizoshikiria..
...ukiachia tu zile batan computer itaanza kuhesabu files zinazotakiwa kuistall.

Warning: Kumbuka kuwa na firmware husika ukikosea utaua simu, usitikise simu au USB cable, kwenye kuchague file wewe toa tick kwenye Preloader....
Haya mengine nitaelezea kwenye #uzi mwingine nitakaondaa wa kuflash simu.

💢Hard reset vs kuflash simu.
Hard reset ni kitendo cha kurejesha mfumo wa simu kama awali, yaan ukifanya tu hivyo unaweza kufuta data zako zote na apps ambazo uliinstall mwenyewe..
Hard reset haiwezi kuharibu simu ambayo haijawahi kuflashiwa au kubadili IMEI. Maana simu ambayo ulibadili au kurepair IMEI ukifanyia hard reset zile IMEI pia hupotea.
Why?
...because, kwenye IMEI repair kuna temporary na permanet repair sasa ukitumia...
....ukifanya temaporary IMEI repair na ukihard reset zile IMEI hupotea yaan nazo zinafutika kana kwamba zilivyofutika data zako. Kuflash simu ni kubadili mfumo mzima wa simu na kuuweka mpya ambao umedownload(Reinstalling custom firmware).
💢Kuroot simu..
...hiki ni kitendo cha kuondoka umiliki wa simu kujipa wewe mwenyewe(administrative privilege).
...ukiroot simu ile warrant nayo inatoka, ukiroot simu unaweza kuifanyia chochote upendacho kama vile kuzitoa apps zote ambazo zimekuja na simu...
...apps zote ambazo ziliwekwa na watengenezaji huitwa Pre-installed apps. Hizi apps ukinunua tu simu unazikuta na huwa hakuna sehemu ya uninstall(kuziondoa kwenye simu). Sasa ukiroot unaweza kuziondoa zote kadri upendavyo
Kuna baadhi ya apps huwa zinakataa kukaa kwenye simu mpaka uroot, apps kama vile Kali NetHunter ambayo hutumiwa na wadukuzi. Hii app ni sawa na Kali Linux kwenye computer ila kwa simu hutumia hiyo au Termux
Warning: Ukiroot simu na ukiletewa system updates usiiruhusu ifanyie updates maana ukiiruhusu tu simu inacrash au inaweza kuishia kwenye boot logo.

Mwishoo
__________________________
@TOTTechs @razaqdm01 @knwlerKIKoti @FettyDamass
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with InfoLab

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!