My Authors
Read all threads
UZI: Acha leo niwajuze mambo mengine ninayofahamu, Leo nitawapa tips chache kuhusiana na gari yenye mfumo wa kiautomatiki (automatic transmission). Kitaaluma pia niliwahi kuwa mkufunzi wa udereva. Sasa je hizi: P, R, N, D, 2, L Kwenye gari automatic zina maana gani hasa?
Mfumo wa (uwiano wa kiautomatiki) automatic transmission,auto, self shifting au AT ni mfumo wa ubadilishaji gia unaojiendesha wenyewe haihitaji dereva kubadili gia zaidi tu atailekeza gari kwenda mbele au nyuma. Mfumo huu uligunduliwa miaka ya 1900s na ndugu wa-sturtevan, boston.
Ford ni moja ya makampuni ya mwanzo kabisa maarufu kuanza kutumia mfumo huu. Gari hizi huwa na mfumo wa mpangilio wa gia ukipangiliana kutoka P, R, N, D, 2 na L.

1. P - Parking: Hufunga gearbox hivyo kuzuia gari kutembea. Gia/Mfumo huu hutumika pale ambapo mtu ameegesha gari.
2. N-Neutral/ No gear: Hakuna gear yoyote uliyoweka, gari huwa free. Unaweza kutumia mfumo huu mfano gari imeharibika unataka kuiweka pembani ya barabara.

Wengi hawajui, kama gari yako imezima na unataka kuweka N ili itembee unaweza bonyeza hii batani 👇(shift lock) itakubali.
3. R - Reverse: Hutumika pale mtu akitaka kurudi nyuma.

4. 2-Second: Hutumia gear mbili za mwanzo, kwa wale walioendesha manual ni kama unatumia gear namba moja na namba mbili pekee. Unaitumia wakati upo kwenye mteremko mkali kwani itaifanya gari ya kuwa nzito, inakula mafuta.
5. D - Drive: Huruhusu gear zote za kwenda mbele.

6. L - Low: Ukiweka gia hii unaifanya gari yako kutumia gia ya chini iwekenavyo ambayo ni namba moja. Gia hii hutumika sehemu za milima maana hufanya gari kutumia nguvu huku ikitembea polepole.
7. D-3 - Kama ilivyo 2, hapa utatumia gia tatu za mwanzo, baadhi ya magari hutumia mfumo huu sio magari yote. Unatumia gia hii pale ambapo hutaki gari itembee kwa spidi kubwa mfano unapokua mjini au umebeba kitu kizito.
Nyingine:

OD, O/D - Over Drive: Hapa unahitaji gari iongeze nguvu zaidi, kwa gari nyingi za automatic hazina four-wheel drive hivyo hii ni kama mbadala wa 4WD (four wheel drive).
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Festo D Ngadaya | #BongeLaAfya 🇹🇿

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!