JINSI YA KUANZISHA BIASHARA UKIWA UMEAJIRIWA: Biashara yoyote iwe mpya au ya zamani ina changamoto zake especially kwenye mazingira yetu. 50% Ya biashara zote ndogo zinakufa katika mwaka wake wa kwanza kuanzishwa. UZI #ElimikaWikiendi
Mtandao wa Investopedia ulitoa sababu ya biashara ndogo kufa, 1. Mtaji Mdogo, 2. Uendeshaji Mbovu, 3. Mpangilio Mbovu wa Biashara na Bidhaa yako au huduma yako haihitajiki sokoni (Hakuna wateja wanahitaji bidhaa zako). Pamoja na sababu zingine nyingi.
Sasa kama tulivyoona hapo juu changamoto ni nyingi. Kabla ya kufikiria kuanzisha biashara ukiwa umeajiriwa inabidi ujipange. Kitu kimoja kikubwa ambacho Ajira itakusaidia kipindi unataka kuanzisha biashara ni MTAJI pamoja na muda wa kujipanga kabla ya kuanza biashara full time.
Kuna watu hua wanafikiria kuacha kazi ndio waanzishe biashara. Ndio unatakiwa kufuata ndoto zako lakini sikushauri hicho kitu. Asilimia kubwa ya biashara mpaka zianze kuingiza pesa inachukua hata mwaka mzima. So its either uwe ume save hela za kutosha kukusaidia muda wote huo
Hizi ni hatua chache za kufuata ili uanzishe biashara ukiwa umeajiriwa. Kwanza hakikisha mkataba wako na mwajiri wako unakuruhusu kufanya biashara ukiwa mwajiriwa wake. Kuna baadhi ya makampuni huwezi kuanzisha biashara ukiwa bado mwajiriwa wao. Soma Mkataba wako wa kazi
MUDA: Tambua kwamba biashara mpya inahitaji muda wako wa kutosha. Kuna muda wa kazi yako na muda wa biashara yako. Panga muda wako vizuri. Punguza au ondoa vitu ambavyo vinakumalizia muda wako na sio vya maana mfano Kuangalia Netflix, Social Media, Video Games, etc
WAZO LA BIASHARA: Usichague wazo la biashara na aina ya biashara ambayo hutaweza kuifanya part time. Mfano umefungua mgahawa au bar kama hautokuepo hapo full time kipindi cha mwanzo au huna msaidizi. UTALIA. Kama tulivyoona hapo juu moja ya sababu biashara kufa ni usimamizi mbovu
Kuna mawazo ya biashara (Business Ideas) na mfumo wa biashara (Business Models) nyingi sana ambazo unaweza kuchagua na kufanya on side ukiwa umeajiriwa full time. Kwa mawazo machache unaweza ingia hapa adesanmivictor.com/business-ideas…
Kabla hujachagua wazo la biashara uchague au ufanye jipime skills, abilities, and weaknesses zako. Kisha focus biashara ambayo itakufanya utumie strength zako. Kama huna hio skill ambayo biashara unayotaka kuifanya tumia muda wako kujifunza au mpe hio kazi mtu mwingine akusaidie.
Tuseme ushachagua wazo lako la biashra. Kibinadamu ni rahisi kuona wazo lako ni zuri na litakufanya upige hela. That’s the TRAP. UTAFELI. Kabla ya kutumia muda wako mwingi VALIDATE your idea first. Fanya utafiti, Market research. Soma Uzi Huu hapa
Malengo yako ni kuanzisha biashara ambayo inaongeza thamani kwa watu. Haitakua namaana kama utakua na bidhaa ambayo hakuna mtu anahitaji. Kusanya maoni kutoka kwa watu/wateja wako walengwa tokea unaanza biashara na usiache kuwaskiliza.
Tengeneza detailed, measurable, and realistic goals. Ni ngumu kwenda popote kama hufahamu unakwenda wapi. Panga mipango yako ya siku, wiki, mwezi. Kisha panga mkakati jinsi gani jinsi utayafikia malengo yako.
Biashara ina mahitaji mengi ili ifanikiwe na wewe kwa sababu umeajiriwa huna muda wa kutosha kuyafikia mahitaji yote. Mfano unahitaji Social Media Makerting kwa biashara yako na wewe huna muda. Hio kazi mpe mtu mwingine. Focus kwenye vitu muhimu vinavyokuza biashara yako
Faida inayopatikana kwenye Side Business yako Re Invest kwenye biashara yako na kiasi kingine kinachopatikana SAVE itakusaidia pale ambapo utaamua kuacha kazi na kufanya biashara full time. Hakikisha umeweka mipango na bajeti ya jinsi utatumia hela zako.
ANGALIZO: Usitumie mali za kampuni/mwajiri wako kwa kazi zako binafsI. Usitume email, printer, laptop, etc. Hii ni pamoja na muda wa mwajiri wako usitumie kwa biashra zako.
Kuanzisha biashra ukiwa umeajiriwa sio kazi ndogo lakini INAWEZEKANA. Kuna njia nyingi za kua mjasiriamali hii ni moja wapo. #ElimikaWikiendi
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Kwa vile bado ni January, Tujikumbushe zile shule 10 zenye ada(Fees) ghali Tanzania 2023 Update. Mtoto wako utampeleka shule ipi? #UZI 🧵
Morogoro International School (MIS)
Location: Morogoro
Curriculum: Cambridge.
Nursery: 6.4 Million Tshs Per Year
Secondary: 18 Million Tshs Per Year
Michango Mingine: Not Included
International School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
Location: Kilimanjaro
Curriculum: International Baccalaureate (IB).
Nursery: 17.5 Million Tshs Per Year
Secondary: 43.8 Million Tshs Per Year
Michango Mingine: Not Included
Kila siku tunajishughulisha ili tutimize malengo yetu. Katika maisha kuna watu ambao wanafanikiwa katika mambo yao na kuna watu ambao hawafanikiwi. Tunajishughulisha kila siku kuyatimiza malengo hayo. Malengo yanaweza yakawa ni maswala ya Elimu, Kazi, Biashara, Uongozi nk.
Tafiti zinaonyesha ni watu wachache sana wanaotimiza malengo yao duniani kote, inawezekana ukawa miongoni mwa watu ambao hawajafanikiwa kutimiza malengo yao. Zifuatazo ni njia 9 bora zitakazokufanya ufanikiwe katika maisha yako.
𝑰𝑳𝑰 𝑾𝑨𝒁𝑶 𝑳𝑨𝑲𝑶 𝑳𝑨 𝑩𝑰𝑨𝑺𝑯𝑨𝑹𝑨 𝑳𝑰𝑭𝑨𝑵𝑰𝑲𝑰𝑾𝑬 𝑽𝑰𝑻𝑼 𝑽𝒀𝑨 𝑲𝑼𝒁𝑰𝑵𝑮𝑨𝑻𝑰𝑨: 𝑼𝒁𝑰 𝑷𝑨𝑹𝑻 2
Vitu vingine vya kuzingatia wakati unakuja na wazo lako la biashara.
Yes unaweza fungua biashara kutokana na kitu unachokijua mfano Kinyozi ukafungua saluni yako au mpishi ukafungua restaurant yako. Kumbuka kwakua wewe ni mpishi mzuri sio kwamba utafahamu jinisi ya kuendesha restaurant yako vizuri. Kuna mambo mengi ya kuzingatia
Kama unataka biashara endelevu make sure huduma au bidhaa unayouza wateja wako watarudi kwako tena. Inabidi uwe na bidhaa au huduma ambayo wateja wataendelea kununua kwa muda mrefu. Mfano ni bora uwe na kampuni ya kusafisha swimming pool kuliko kua na kampuni ya ujenzi wa pool.
𝑱𝑰𝑵𝑺𝑰 𝒀𝑨 𝑲𝑼𝑱𝑨 𝑵𝑨 𝑾𝑨𝒁𝑶 𝒁𝑼𝑹𝑰 𝑳𝑨 𝑩𝑰𝑨𝑺𝑯𝑨𝑹𝑨. Ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kuwa na wazo zuri la biashara. Je unajua jinsi ya kupata wazo hilo zuri la biashara? 𝑼𝒁𝑰, 𝑷𝑨𝑹𝑻 1
Watu wengi wamekuwa wakiniomba ushauri ni wazo gani zuri la biashara ambalo linaweza kuwapatia faida na mafanikio. Ukweli ni kwamba wazo ambalo ni bora kwa mtu fulani linaweza lisiwe bora kwako.
Moja ya sababu zinazofanya biashara nyingi kufa au kutokuendelea ni kuiga, yaani mtu akianza biashara leo baada ya muda unakuta watu wengine wameiga biashara ile ile, wanaifanya eneo lile lile na kwa mbinu zile zile. Hii ni njia rahisi sana ya kushindwa kwenye biashara.
NJIA (Business Models) 10 ZA KUPATA PESA ONLINE. UZI Nimeshindwa kupata kiswahili cha Business Model (Mtanisaidia) Kwa uzoefu wangu watu wengi wanapotaka kuanza kufanya biashara Online or Offline. Hua wanafikiria njia moja au Mbili. #GillMadini
Kununua Bidhaa kutoka sehemu fulani au Kutengeneza hio bidhaa na kuiuza dukani or ikizidi sana mtandaoni kupitia Instagram au Facebook wachache kwenye website. Leo nimewaletea Business Models zingine 10. Ambazo unaweza kutumia kupiga hela.
Tukirejea kwenye UZI nilioandika mara ya mwisho. Kama bado haujausoma tafadhali usome Halafu rudi kumalizia Uzi huu. Leo nitatoa mfano wa wazo moja la biashara mbalo unaweza tumia njia zaidi ya 10 (10 Business Models) tofauti kuweza kufanikisha kujipatia pesa.
BIASHARA MTANDAONI: Kuna njia nyingi za kuanza kufanya biashara mtandaoni (Facebook, Twitter, Instagram). Watu wengi hua tunakwama ni wazo gani la biashara au bidhaa gani niuze itakua na wateja. Nimekuletea UZI huu ukusaidie njia fupi ya kupata bidhaa ya uhakika kuuza #GillMadini
Kuna njia 2 ambazo ntazielezea kwa ufupi. 1. Kama tayari ushafahamu ni bidhaa gani utaenda kuuza mtandaoni 2. Hufahamu bidhaa au huduma gani uchague na kuuza mtandaoni.
Last time niliongelea hili swala lakini leo pia ningependa kutoa msisitizo, Idea za bidhaa za kuuza zipo nyingi sana lakini kuna maeneo haya ukipata bidhaa zake unatoboa faster Afya, Urembo, Passion, Hobby, Interest, Activities, Self Improvement, Wealth and Money, fitness.