ANDROID 11

Android 11 imetoka, ni jambo zuri kwa watumiaji wa Android, simu za mwanzo Kabisa zilizoanza kupokea Android 11 updates ni Google pixels, OnePlus, Oppo, Xiaomi na Nokia. Simu zingine zitapata Android updates week chache zijazo

Tuangalie features zilizomo [ uzi ]👇
◾️ MEDIA CONTROL

Media players zitakuwa zinaonyesha media controls zote ( prev, stop, next etc) moja kwa moja kutoka kwenye "toggle bar" ( Sehemu ya juu ya simu kwenye notification pannel ambapo itaonyesha wimbo, media husika na control zake)
◾️MEDIA OUTPUT ( Quickly select media output)

Sehemu ya notification pannel ambayo itakusaidia ku-sitch/badili ambapo unaweza kuchagua utumie speaker ya simu au Bluetooth device au device yoyote ambayo iko connected na simu yako kwa haraka zaidi.
◾️NOTIFICATION PANNEL

Moja kati ya maboresho makubwa ni kwenye notification pannel. hapa wamegawa sehemu mbili, hapa kuna internal App notifications na messaging notifications, utapata sms notifications zote kwenye mpangilio mzuri unaweza kugroup aina ya messages au ku-pin user
◾️ CHAT BUBBLES

Chat bubble ni kama ile ya Facebook messenger, ukitumiwa message kinatokea kiduara kwenye screen na dot nyekundu, unaweza kuchat na mtu pasipo kufungua messaging app husika na pia itarahisisha kuonyesha jumbe ambazo hazijasomwa pasipo kufungua chat apps
◾️HOME SCREEN

Kwenye home screen wameongeza kipengele cha " Home screen Apps suggestion" kwenye android 11 unaweza kuchagua ni app gani ikae chini kwenye home screen ili kurahishisha matumizi kulingana na Apps uzitumiazo mara nyingi ikumbukwe home screen ilikuwa na default Apps
◾️DEVICE CONTROLS AND PAYMENT

kama unapata shida ya ku-connect smart devices nyumbani kwako ( Smart TV, Cars etc) basi android 11 ni suluhisho, power button itatumika siyo tu kwa ajili ya kuzima na kurestart bali kutakuwa na option ya ku-connect na ku-control smart home devices
Pia unaweza kupata Google Pay Card bila ya kufungua app husika, Hii itarahisisha malipo ( Google pay) pasipo kuwa na App, ni rasmi sasa power button imepata matumizi mengi zaidi kuliko awali
◾️ PRIVACY

Android 11 Privacy

Ulinzi ni kitu cha msingi kwenye kila program endeshi ( operation system) na moja ya feature iliyoongezwa ni ONE TIME PERMISSION

Je "One time Permission" inafanyaje kazi, unapofungua App kwa mara ya kwanza na kukuomba permission ya kuacess
vitu vyako ( Permission to access photos, contacts, phone book etc) unaweza kuruhusu kwa mda huo na ukifungua hiyo app kwa mara Nyingine unaruhusu "one time permission" kwa mara nyingine tena hii itazuia apps kuacess vitu vyako kwa mda wote
◾️ SCREEN RECORDING

Rasmi sasa screen recording imekuwa built-in feature ya Android 11, kuliko Kudownload Screen recording apps kutoka Play Store unaweza kupata kwenye home screen yako na ukarekodi chochote kwa mfumo wa sauti/audio au maandishi
◾️VOICE ACCESS

Ile feature ya ku-control simu yako kwa kuongea sasa imeboreshwa zaidi na inauwezo wa kutambuana screen contents na kuziweka kwenye sauti kisha ikakuletea majibu ya maulizo yako
◾️PREDICTION TOOLS

Android 11 inakurahisishia kazi. inauwezo wa ku-sort automatically apps ambazo unazitumia mara kwa mara na kuziweka kwenye smart folder, zitakaa kwenye home screen na utazipata haraka zaidi

Pia inauwezo wa kutambua apps zipi unazitumia kwa mda gani
Mfano: kama asubuhi unatumia apps za mazoezi Basi automatically hiyo app itakuwa inapop-up na kutoa notifications kama mda wa mazoezi umefika

Hizo ni Baadhi za features

Uzi umethibitishwa na @chawanyu

Cc: @Mkuruzenzi @razaqdm01 @njiwaflow @chawanyu @ITexpertTz @WizaraUUM

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with #TOTTechs 🇹🇿

#TOTTechs 🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @TOTTechs

23 Aug
ELON MUSK

Alizaliwa South Africa akiwa na miaka 17 alihamia Canada na baadae America, ni mfanyabiashara na mwanzilishi wa makampumi makubwa kama SpaceX, PayPal, Tesla Motors

Leo nimekuletea kila kitu kuhusu Elon Musk

✴️ Historia yake na familia yake

✴️ Biashara zake

Uzi Image
ELON MUSK NI NANI

Ni mzaliwa wa South Africa lakini sasa ana uraia wa Marekani na Canada, ni mfanyabiashara na mwanzilishi wa makampumi ya PayPal, SpaceX na Tesla Motors, alipata pesa akiwa na umri mdogo (20's) baada ya kuuza kampuni yake ya kwanza (Zip2) kwa Compaq computers Image
MAISHA YAKE YA UTOTONI

Elon Musk alizaliwa June 28, 1971 huko Pretoria-South Africa, Musk alizaliwa na tatizo la kusikia ila madaktari waliweza kumtibu akiwa mdogo.

Akiwa na miaka 10 wazazi wake walitengana na aliendelea kuishi na mama yake na ndugu zake wawili Image
Read 25 tweets
28 Jun
JINSI YA KUIFANYA SIMU YAKO IWE NA NAFASI ( SPACE) YA KUTOSHA

Kwa watumiaji wa Android devices nimepata maswali mengi, simu zinajaa pasipo kuwa na vitu vingi kwenye simu

Leo tuangalie namna gani unaweza kuifanya simu yako iwe na nafasi ya kutosha

Twende na uzi
Wewe ni mtumiaji wa Android phone na umekuwa ukipata shida kwenye suala la storage, unaona kama una vitu vichache lakini storage imejaa

Basi jifunze vitu hivi ambavyo vimesaidia wengi katika kuifanya simu kuwa safi katika suala la storage
1: CLEAR CACHE

unapo-install application yoyote huwa zinatumia cache file ili kuweza kukupa urahisi wa kutumia app husika, lakini hili cache file haina umuhimu sana ukifuta vitu vilivyomo haiwezi kuleta madhara

Namna ya ku-clear cache

Kuna njia mbili za ku-clear cache
Read 15 tweets
10 Jun
Je umewahi kujiuliza haya maswali ?

✴️ Taarifa na vitu vyote kwenye mtandao huwa vinatunzwa wapi?

✴️ Serikali na makampuni binafsi yanatunza wapi taarifa zao?

Jibu: Taarifa na vitu vyote vya kimtandao duniani vinatunzwa sehemu inaitwa DATA CENTER

DATA CENTER NI NINI?

Uzi
DATA CENTER ni nini na inafanyaje kazi?

Data center ni sehemu maalumu ambapo vifaa vya computer na mawasiliano vimewekwa kwa ajili ya kukusanya, kutunza, kuchakata (processing) na kusambaza (distribute) taarifa zote za kimtandao Duniani
Data centers zinafanya kazi Mda wote (24/7/365) kuhakikisha haukosi taarifa au kitu chochote unachokihitaji mtandaoni.

Data Center inakuwa na SERVERS nyingi ambazo zimepangwa kwenye msitari pia computer zenye uwezo mkubwa (supercomputer)

Kazi ya SERVER ni
1. kutunza taarifa
Read 11 tweets
27 Apr
Zijue sheria za uhalifu wa mitandao (cyber crimes) na adhabu zake nchini Tanzania

Leo tuangazie sheria mbalimbali za uhalifu wa mitandao na adhabu zake kwa mtu anayekwenda kinyume

Hizi ni Sheria zilizopitishwa mwaka 2015 na Raisi mstaafu Mh J.M Kikwete

Uzi 👇
Act No. 14 ya 2015
Hizi sheria zinatumika Tanzania bara na visiwani

1. Illegal access (upatikanaji wa taarifa kinyume na sheria)

Mtu hapaswi kwa makusudi kuingilia taarifa au kufanya mifumo ya computer kupatikana (accessed) ili kupata taarifa bila kufuata sheria
Kwa yeyote atakayefanya hivyo atakuwa ametenda kosa na atapaswa kulipa faini isiyopungua kiasi cha shilling Million 3 au mara tatu zaidi au kifungo kisichopungua mwaka mmoja (1) au vyote kwa pamoja.

2. Ubaguzi wa Rangi na ubaguzi wa sisi kwa sisi (Racist and xenophobic)
Read 11 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!