WatuNiStory Profile picture
Sep 24, 2020 5 tweets 2 min read Read on X
1/5 “Nilisoma chuo UDSM hadi mwaka wa tatu lakini sikuhitimu. Sikuhitimu kwa sababu ukweli ni kwamba, sikuzingatia masomo ipasavyo, nilipata ajira nikashindwa ku-balance kati ya shule na kazi. Nikaishia kufeli mitihani kadhaa. Ilikua nihitimu mwaka 2015. Miaka yote nimeendelea.. Image
2/5 ...kufanya kazi mbalimbali kwa kutegemea kipaji changu tu. Japo kuna nyakati nilikosa kazi zilizohitaji mtu mwenye degree na sikua na hizo sifa. Ni jambo ambalo limekua likiniumiza na kunifanya nijiskie vibaya. Familia yangu pia iliumizwa na hilo sababu walilipa ada miaka..
3/5 ..yote mitatu ya chuo. Na niliumia sana kuiumiza familia yangu. Namshukuru Mungu mwaka huu baba yangu amenipa nafasi tena ya kurudi chuo na kunilipia ada. Nime-apply tayari nangoja majibu. Japo naona kama miaka mingi imeshapita, nina miaka 28 sasa..
4/5 ..Ila naamini ni nafasi nyingine ya kusahihisha makosa yangu. Naanza safari ingine ya miaka mitatu kuitafuta degree. Nawashauri watu wanapokua na nafasi ya kusoma, wazingatie masomo. Na hata ambao walianguka kama mimi, kama watapata nafasi ingine, wajitie nguvu na wasiogope..
5/5 ...kuanza upya. Naamini Mungu atanisaidia.” #WatuNiStory

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with WatuNiStory

WatuNiStory Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @watunistory

Mar 26, 2022
"Harakati za shule na kusoma nikajikuta nimepangiwa shule moja huko Mtwara inaitwa Ndanda.

Kiukweli nilikuwa sijawahi kufika na sijui kabisa tamaduni za watu wa kule. Nikasema Tanzania ni moja hakuna sehemu nitashindwa kuishi,
hivyo mwanaume nikajipanga tayari kwenda kuanza safari ya masomo huko.

Kumbuka ile likizo ya kusubiri matokeo ya kwenda kidato cha tano, nilikuwa mtu shamba. Yaani nilipiga sana jembe na kazi nzito kusaidia mishe za home. Hivyo nilikuwa nakula saaana.
Sasa kufika shule, nakuta dishi la msosi yaani ugali ambao ningeweza kumaliza mimi na dada yangu, tunakula wanaume kama saba.

Hili lilinitesa sana aisee kipindi cha kwanza. Nakumbuka ilipita miezi kama mitatu mwanaume sijawahi kushiba.
Read 5 tweets
Mar 8, 2022
"Ipo hivi, mimi ni kijana wa miaka 25, nilikuwa na mpenzi wangu ana mtoto sio wangu. Kipindi nipo nae nilikuwa sina kazi na tulikuwa tumepanga tunaishi pamoja lakini yeye alikuwa na kazi. Sasa hakutaka kubeba mimba yangu akihofia hali ngumu ya maisha ambayo ninapitia.
Kile kitendo kikaniumiza sana, nikaja Dar kutafuta maisha, ikawa kila baada ya miezi mitatu narudi nyumbani kumtembelea.

Sasa mwezi wa tisa nikashindwa kwenda kwa wakati, lakini tulikubaliana kwakuwa mkataba ulikuwa karibu kuisha, nimalizie mkataba ndio niende nyumbani.
Kweli, nikaenda mwezi wa 12 ila cha ajabu namkuta na mimba ya mwezi na ananieleza kuwa aliempa mimba hakuwa na mahusiano nae na hamtaki tena.

Kwa hasira nikaondoka, nikamwacha. Ety katoa mimba ananiomba msamahe na turudiane.
Read 4 tweets
Mar 7, 2022
"Ilikuwa Jumapili weekend moja nimekaa ghetto kwangu nimefulia mbaya. Simu yangu inaita, kucheck alikuwa mwanangu.

Kupokea ananiambia ana msala inabidi nimsaidie kuu-solve. Inakuaje? nikauliza. Image
Ndio ananiambia amempa mimba binti wa kidato cha nne hivyo anaomba aje kwangu kufanya harakati za kuitoa. Ashaongea na dokta, na dogo yupo tayari bado eneo la tukio tu sababu hawawezi kufanyia hospital.

Daah!nikicheck ni mwanangu sana. Na kwao ana mke na mtoto.
Nikaona sio mbaya nilibebe hili nimsaidie mshkaji. Nikamwabia njoo haina noma.

Walipofika ikabidi niwapishe wafanye yao. Nikakaa zangu nje.

Nikiwa na mawazo mengi na dakika nyingi kupita, mshkaji anakuja kunishtua dogo amezima. Haelewi anayeingia wala anayetoka.
Read 10 tweets
Mar 5, 2022
"Ipo hivi mimi ni kijana wa miaka 28 sasa.

Nilipokua chuo mwaka 2018 nikisomea course ya IT nilibahatika kupata mdada ambaye niliishi nae kama mchumba na kumpa mahitaji yote na tulikubaliana tuzae. Image
Basi nikampa kweli ujauzito huku nikimhudumia kwa kila kitu bila wazazi wangu kujua na hakuwahi kukosa kitu alichohitaji kwangu japo sikuwahi kuomba msaada kwa mtu, ila niliendeleza life langu kwa mishe zangu za kitaani(kwa wanaoelewa IT huwa hatukosi mishe za hapa na pale).
Ilipofika mwezi mmoja na nusu kabla ya binti kujifungua alisema anaenda jifungulia nyumbani.

Sikumkataza kwa vile na mimi niliona sitaweza ghaili masomo nisaidie malezi. Hivyo nikamruhusu aende na kumpatia vitu vyote muhimu alivyohitaji kwa ajili ya safari na mambo mengine.
Read 7 tweets
Dec 29, 2021
"Kuna demu mmoja nina urafiki nae kiasi kwamba binafsi nikiwa na shida yoyote ananisaidia. Mara nyingi huwa anakuja home hata nguo zangu huwa anafua na usafi anafanya. Chochote nitakachomwambia anafanya.
Alishaniweka wazi kuwa ana ngoma na mambo yake yote huwa hanifichi hata awe na mahusiano basi ataniweka wazi kwa kila kitu hata akalale na huyo mwanaume.

Tatizo linakuja sehemu moja, hatujawahi kuongelea swala la kuwa na mahusiano. Mimi na yeye huwa ni stori za kawaida tu.
Mimi nina mahusiano na demu mwingine na anamfahamu hata nikikosana na demu wangu anakuwa wa kwanza kutusuluhisha. Alishawahi kuolewa wakaachana na mume wake kisa huyo mwanaume alimwambia aache mazoea na mimi akakataa.
Read 10 tweets
Dec 28, 2021
"Miaka kadhaa iliyopita Vijana mtaani kwetu waligundua kuwa Kuna mama huwa anaacha wazi madirisha ya nyumba yake pindi akiwa anabadilisha nguo. Ni mama mgeni ambae alikua kahamia miezi michache tu iliyopita.
Alikua akifanya hivyo kila siku mida ya saa moja na nusu usiku akitoka kuoga.

Yule mama MashaAllah alijaliwa shape. Yani alikua na shape moja ya ukorofi sana. Alienda hewani.. huko nyuma ni kama pembe la ng'ombe tuu.. halifichiki.. hatari sana.
Basi Vijana ndo ukawa mchezo wao.. Taarifa ziliponifikia nikawa natamani nikamwambie yule mama kuna raia wanamla chabo maana alikua ni jirani yangu na ananifahamu vizuri tunaheshimiana halafu alikua mwalimu wa shule ya msingi.
Read 9 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(