1/10 “Naitwa William Adam Lukoo ,mzaliwa wa mkoa wa Morogoro. Mwaka 2003 familia yetu ilihamia jijini Tanga kwa ajili ya harakati za kimaisha. Haikua rahis kwa sababu ya ugeni lakini wazazi walipambana kuhakikisha napata elimu bora. Licha ya kutoka kwenye familia ya kimaskini...
2/10 ..nilihakikisha nafanya vizuri kwenye masomo kiasi cha kuwavutia walimu na kujizolea umaarufu shuleni. Nilifanikiwa kuhitimu mwaka 2010 shule ya msingi Majani Mapana wilayani Tanga mjini. Mwaka 2011 nilianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Usagara..
3/10 ..lakini kutokana na ugumu wa maisha, wazazi wangu wote hawakuwa na kazi. Ikawalazimu kufikia hatua ya kuuza vitu vya ndani ili kuweza kunilipia ada. Maisha yalikuwa magumu mno nyumbani kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa kupata chakula na kodi.
4/10 ..Lakini Mungu hamtupi mja wake mimi niliendelea kupambana kwenye masomo yangu na kuendelea kufanya vizuri sana. Na bahati nzuri wazazi wakapata kazi zingine tena japo majukumu yalikua mengi mno.
5/10 .. Mwaka 2014 nikachelewa kulipa ada ya mtihani wa kidato cha 4 ikapelekea matokeo yangu kufungiwa. Nilihuzunika sana. Ikabidi kupambana kupata ile pesa matokeo yakafunguliwa na nilifanya vizuri nikajiunga na kidato cha 5 shule ya sekondari Nachingwea mkoani Lindi.
6/10 ..Nilipambana sana kuhakikisha ndoto zangu zinakuwa kweli ,tulishirikiana na wanafunzi wenzangu kusoma kwa bidii na juhudi zilizaa matunda kwa kufanikiwa kufaulu vizuri..
7/10 ...na Mimi nilipata nafasi ya kujiunga chuo kikuu Cha Dar es Salaam (2017-2020) kwa ajili ya masomo ya shahada ya elimu na Mungu mwema mwaka huu nimehitimu masomo yangu.
Ushauri wangu kwa vijana wasikate tamaa na wala wasikatishwe tamaa na hali za maisha za familia zao bali wachukulie kama fursa ya wao kuongeza nguvu katika mapambano ya kufanikisha ndoto zao ili ziwe kweli na waokoe familia zao kutoka kwenye umasikini.” #WatuNiStory
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
"Harakati za shule na kusoma nikajikuta nimepangiwa shule moja huko Mtwara inaitwa Ndanda.
Kiukweli nilikuwa sijawahi kufika na sijui kabisa tamaduni za watu wa kule. Nikasema Tanzania ni moja hakuna sehemu nitashindwa kuishi,
hivyo mwanaume nikajipanga tayari kwenda kuanza safari ya masomo huko.
Kumbuka ile likizo ya kusubiri matokeo ya kwenda kidato cha tano, nilikuwa mtu shamba. Yaani nilipiga sana jembe na kazi nzito kusaidia mishe za home. Hivyo nilikuwa nakula saaana.
Sasa kufika shule, nakuta dishi la msosi yaani ugali ambao ningeweza kumaliza mimi na dada yangu, tunakula wanaume kama saba.
Hili lilinitesa sana aisee kipindi cha kwanza. Nakumbuka ilipita miezi kama mitatu mwanaume sijawahi kushiba.
"Ipo hivi, mimi ni kijana wa miaka 25, nilikuwa na mpenzi wangu ana mtoto sio wangu. Kipindi nipo nae nilikuwa sina kazi na tulikuwa tumepanga tunaishi pamoja lakini yeye alikuwa na kazi. Sasa hakutaka kubeba mimba yangu akihofia hali ngumu ya maisha ambayo ninapitia.
Kile kitendo kikaniumiza sana, nikaja Dar kutafuta maisha, ikawa kila baada ya miezi mitatu narudi nyumbani kumtembelea.
Sasa mwezi wa tisa nikashindwa kwenda kwa wakati, lakini tulikubaliana kwakuwa mkataba ulikuwa karibu kuisha, nimalizie mkataba ndio niende nyumbani.
Kweli, nikaenda mwezi wa 12 ila cha ajabu namkuta na mimba ya mwezi na ananieleza kuwa aliempa mimba hakuwa na mahusiano nae na hamtaki tena.
Kwa hasira nikaondoka, nikamwacha. Ety katoa mimba ananiomba msamahe na turudiane.
"Ilikuwa Jumapili weekend moja nimekaa ghetto kwangu nimefulia mbaya. Simu yangu inaita, kucheck alikuwa mwanangu.
Kupokea ananiambia ana msala inabidi nimsaidie kuu-solve. Inakuaje? nikauliza.
Ndio ananiambia amempa mimba binti wa kidato cha nne hivyo anaomba aje kwangu kufanya harakati za kuitoa. Ashaongea na dokta, na dogo yupo tayari bado eneo la tukio tu sababu hawawezi kufanyia hospital.
Daah!nikicheck ni mwanangu sana. Na kwao ana mke na mtoto.
Nilipokua chuo mwaka 2018 nikisomea course ya IT nilibahatika kupata mdada ambaye niliishi nae kama mchumba na kumpa mahitaji yote na tulikubaliana tuzae.
Basi nikampa kweli ujauzito huku nikimhudumia kwa kila kitu bila wazazi wangu kujua na hakuwahi kukosa kitu alichohitaji kwangu japo sikuwahi kuomba msaada kwa mtu, ila niliendeleza life langu kwa mishe zangu za kitaani(kwa wanaoelewa IT huwa hatukosi mishe za hapa na pale).
Ilipofika mwezi mmoja na nusu kabla ya binti kujifungua alisema anaenda jifungulia nyumbani.
Sikumkataza kwa vile na mimi niliona sitaweza ghaili masomo nisaidie malezi. Hivyo nikamruhusu aende na kumpatia vitu vyote muhimu alivyohitaji kwa ajili ya safari na mambo mengine.
"Kuna demu mmoja nina urafiki nae kiasi kwamba binafsi nikiwa na shida yoyote ananisaidia. Mara nyingi huwa anakuja home hata nguo zangu huwa anafua na usafi anafanya. Chochote nitakachomwambia anafanya.
Alishaniweka wazi kuwa ana ngoma na mambo yake yote huwa hanifichi hata awe na mahusiano basi ataniweka wazi kwa kila kitu hata akalale na huyo mwanaume.
Tatizo linakuja sehemu moja, hatujawahi kuongelea swala la kuwa na mahusiano. Mimi na yeye huwa ni stori za kawaida tu.
Mimi nina mahusiano na demu mwingine na anamfahamu hata nikikosana na demu wangu anakuwa wa kwanza kutusuluhisha. Alishawahi kuolewa wakaachana na mume wake kisa huyo mwanaume alimwambia aache mazoea na mimi akakataa.
"Miaka kadhaa iliyopita Vijana mtaani kwetu waligundua kuwa Kuna mama huwa anaacha wazi madirisha ya nyumba yake pindi akiwa anabadilisha nguo. Ni mama mgeni ambae alikua kahamia miezi michache tu iliyopita.
Alikua akifanya hivyo kila siku mida ya saa moja na nusu usiku akitoka kuoga.
Yule mama MashaAllah alijaliwa shape. Yani alikua na shape moja ya ukorofi sana. Alienda hewani.. huko nyuma ni kama pembe la ng'ombe tuu.. halifichiki.. hatari sana.
Basi Vijana ndo ukawa mchezo wao.. Taarifa ziliponifikia nikawa natamani nikamwambie yule mama kuna raia wanamla chabo maana alikua ni jirani yangu na ananifahamu vizuri tunaheshimiana halafu alikua mwalimu wa shule ya msingi.