Kikundi cha watalii kilitembelea mto wa kufugia mamba na walikuwa wakielea kwenye meli ndogo katikati ya mamba wenye njaa. Ikasikika sauti ya mmiliki wa eneo hilo ikisema: "Atakaye ruka kwenye maji na kuogelea kutoka nje atazawadiwa dola milioni 10".
Kila mtu kimya, ghafla mwanaume mmoja akajirusha majini. Alikimbizwa na mamba kwa bahati nzuri alitoka salama. Akatangazwa mshindi. Wakati anarudi hotelini na mkewe akamwambia mkewe "Aisee sijajirusha mwenyewe majini, kuna mtu alinisukuma nikapambana niokoe maisha yangu".
Mke wake akatabasamu na kusema "Ni mie ndio nilikusukuma". Wewe ungemfanyaje kama ni mkeo? Simulizi linatufundisha: "Nyuma ya kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke anayemsukuma kufikia mafanikio". #ElimikaWikiendi
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Wanawake wanene au wenye uzito kupita kiasi au waliozaa huwa na matumbo makubwa au vitambi vinavyoharibu muonekano wao mzuri. Ili kuwa na tumbo zuri (flat belly) bila ya kuwa na mtaalamu wa mazoezi (waist trainer) fuatilia huu uzi (thread). #TibaFasta
Aina ya Mazoezi Yanayofanya Tumbo Zuri Bila ya Kuwa na Mtaalamu wa Mazoezi (Waist Trainer): Side plank with twist~> Lala ubavu, weka mkono wako mmoja nyuma ya kichwa kisha fanya kama unajaribu kuleta kiwiko chako chini. Fanya hivyo walau mara 15 kwa kila upande. #TibaFasta
Aina ya Mazoezi Yanayofanya Tumbo Zuri Bila ya Kuwa na Mtaalamu wa Mazoezi ya Kiuno (Waist Trainer): Heel grabbers ~> Lala chali huku mikono ikiwa chini pia, inua kifua chako huku ukijaribu kushika visigino vyako kwa kila upande mara 15. #TibaFasta