THREAD: Makosa ya kuepuka unapoandika proposal, concept note au expression of interest. Wengi wetu wenye taasisi, asasi au kampuni inatulazimu kuandika proposal au concept note kuweza kupata fedha kama mtaji au kuendesha miradi au strategic partnerships;
1. Zingatia vigezo na masharti. Yes I know this is obvious, lakini huwa kuna dhana ya kupuuzia baadhi ya vigezo ukiamini vigezo vingine vitaziba hilo pengo. Kila kigezo kina sababu, they all count
2. Nyuma ya kila ‘Call for Proposals’ kuna taasisi au Shirika linalodhamini. Kinachotafutwa kwenye hiyo Call lazima kiendane na Values, Objectives na Goals za hiyo taasisi. Yawezekana kabisa Call isieleze kila kitu, usiishie kusoma maelezo yake tu. Research and do your homework
3. Ukiwa kwenye hiyo research, fanya tathmini ya uwezekano wa kushinda au kupata hilo shindano kwa kuangalia washindi wa zamani au wadau wanaofanya nao kazi. Ni mara chache sana hizo taasisi zitachagua kitu kipya au cha tofauti sana. Kuna vitu vya msingi lazima vifanane
4. Kwa minajili hiyo basi, sio kila shindano la sekta yako litakuhusu. Mfano yawezekana taasisi inasupport ideas za elimu, lakini hawasupport ideas za elimu zinazotumia teknolojia pengine wanasupport ujenzi wa madarasa (miundo mbinu). Usipoteze muda ku-apply
5. Tuje kwenye application, hata wazo liwe zuri kiasi gani kama umeshindwa kuliunganisha na matakwa ya Call, ni ngumu kwa anayechuja kuona lina thamani KWAO. Sio kwamba halina thamani, lakini wanaona halitofanikisha malengo yao. Rejea point ya pili. Onesha uhusiano
6. Jieleze kana kwamba anayesoma maelezo yako hajui kabisa mazingira unayofanyia kazi wazo lako na hajui kabisa jinsi wazo litakavyoweza kufanya kazi katika hayo mazingira. Paint a picture. Ni muhimu kujua kujieleza, kama una wazo zuri na hujui kujieleza, it’s okay kuomba msaada
7. Always paint a before and after picture. Onesha changamoto/mazingira, onesha wazo lako likiwa sehemu ya hayo mazingira likitatua changamoto na mwisho onesha matokeo ya wazo lako iwapo litafanikiwa kutatua changamoto. Usi-assume mtu atafikiria kwa niaba yako au atakuwa anajua
8. Onesha timu yenye diversity. Msiwe wanaume tupu. Msiwe programmers tupu. Msiwe madaktari tupu. Diversity inaonesha uwepo wa utofauti wa skills, thoughts, opinions and experiences. Jamii ina watu mbalimbali, solution yenu ni kwaajili yao. Timu yenu iakisi hilo kadri muwezavyo
9. Kama Call ina special preference kwa kijana au mwanamke na kwenye founders kuna kijana au mwanamke, you are better off kumuweka huyo kijana au mwanamke. Increase your chances, kwasababu mwisho wa siku ushindani ukiwa mkubwa huyo kijana au mwanamke watapata nafasi ya upendeleo
10. Tafuta kinachokutofautisha. Kama kipo kielezee, kama hakipo, rudi ubaoni. It is very competitive out there. Unavyokielezea, it is okay kujisifia so long as hausemi uongo. You should be comfortable with bragging, professionally
Mwisho kabisa, DO NOT LIE. Usiseme uongo. Njia ya muongo ni fupi, unaweza ukaandika maelezo ya uongo kwenye kipengele kimoja lakini kuna swali kama hilo kipengele kingine ukajibu tofauti. Pia usidanganye kuhusu faida na hasara, numbers don’t lie. Mwisho wa siku itafahamika tu

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Faraja Kotta Nyalandu

Faraja Kotta Nyalandu Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!