Habibu B. Anga Profile picture
Mar 28, 2021 25 tweets 5 min read Read on X
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

Thread..

Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.

Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani... Image
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi

Namna hii,

Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...
Afgooye wakiwa kwenye barabara ambayo inaelekea mji mkuu wa Mogadishu.

Vijana hawa watatu ndani ya ile gari wote walikuwa wote wanazungumza lugha ya kiswahili.
Lakini ukikisikiliza kiswahili chao utagundua kwamba mmoja anazungumza kiswahili chenye lafudhi ya Kenya, yule mwingine Image
anazungumza kiswahili aina ya Shikomori ambacho chazungumzwa sana kwenye visiwa vya Comoro. Na yule kijana wa tatu ambaye yeye alikaa siti ya nyuma alikuwa anazungumza Kiswahili chenye lafudhi ya Kisomali.

Vijana hao watatu majina yao ni Abu Aish(ndio mwenye kuzungumza Kiswahili
chenye asili ya Comoro), Abdullahi Dere (mwenye kuzungumza Kiswahili cha lafudhi ya Kenya) na yule ambaye alikaa siti ya nyuma mpaka sasa ametambulika kwa jina moja tu la Fouad.

Mji huu wa Afgooye ambao walikuwa wanatoka uko eneo la pwani kabisa ya Somalia.

Ndani ya ile gari..
waliyokuwa wanasafiria, pamoja nao kulikuwa na vitu ambavyo havikuwa vya kawaida.

Kwanza walikuwa wana begi limejaa fedha taslimu kiasi cha dola za Kimarekani 40,000.
Pia walikuwa na boksi limejaa madawa mbalimbali ya binadamu. Pia walikuwa na takribani simu 15 za mkononi na..
kompyuta mpakato zipatazo tatu

Muda mchache uliopita Abu Aish na Abdullahi Dere walikuwa wamewasili pwani ya Afgooye kwa boti ndogo wakitokea Mombasa na kupokelewa na yule ambaye muda huu alikuwa amekaa kwenye siti ya nyuma

Walikuwa wanapiga soga na kucheka huku wakiendesha gar
yao aina ya Toyota Mark II iliyochoka kiasi chake kuifuata barabara iendayo Mogadishu.
Hii ilikuwa yapata majira ya saa tano za usiku.

Wakiwa kilometa chache tu mahala fulani nyikani kabla ya kuingia Mogadishu wakashangaa kuona mbele yao kulikuwa na kizuizi cha ukaguzi cha jeshi Image
ilikuwa ni ajabu sababu siku moja tu iliyopita, Fouad alikuwa amepita njia hii hii na hakukuwa na Millitary Check Point.
Na kimsingi walikuwa wamechagua njia hii ya vumbi ya ndani ndani na kutopita barabara kuu ili kuepuka jambo hilo la vizuizi vya ukaguzi.

Lakini kwa ajabu..
kabisa mbele yao kulikuwa na gari mbili za kijeshi aina ya Humvee na nje ya gari hizo za kijeshi kulikuwa na maafisa wa jeshi wapatao nane.

Wanajeshi hao wote walikuwa wamevalia sare za jeshi la Somalia isipokuwa mtu mmoja tu kati yao ambaye alikuwa amevalia kiraia.

Na sio tu..
kwamba alikuwa anatofautiana na wale wengine kwa kuvaa kiraia, bali pia mtu huyu alikuwa ni mzungu si Msomali.

Alikuwa amevalia buti nzito, suluari ya jinzi, shati ya drafti ambayo juu yake alikuwa ameivalia bullet proof vest na mkononi akiwa amebeba silaha nzito ya kivita....
Abu Aish na wenzake hawakuwa manjuka kwenye masuala ya kiusalama, walielewa huyu mtu aliyevalia kiraia alikuwa ni nani?
Walifahamu fika kwamba mtu huyu eidha alikuwa ni afisa wa jeshi la Marekani au alikuwa ni afisa wa CIA.

Ukweli huu uliwashitua moyo.
Kwamba hiki kizuizi ni cha
kawaida tu au ni wao hasa walikuwa wanasubiriwa hapo.

Moja ya maafisa jeshi la Somalia akafuata mpaka pale walipo na kuwasalimu, kisha akawauliza majina yao.
Baada ya kutaja majina yao kila mmoja, yule afisa wa jeshi akawaomba wawashe taa ndani ya gari maana walikuwa wameizima..
Abu Aish ambaye alikuwa ndiye dereva akawasha taa za ndani ya gari. Lakini akawasha kihuni sana. Yaani aliwasha kwa muda wa kama sekunde tano hivi alafu akazizima.

Yule mwanajeshi wa Somalia akawaambia awashe tena hajawaona vyema
Abu Aish akawasha tena kihuni vile vile, akawasha Image
kwa sekunde kama tano hivi kisha akazima tena.

Yule mwanajeshi Somalia akakasirika haswa.
Kwa hasira akawaamuru wote washuke kwenye gari.

Abu Aish na wenzake wakiwa wanashuka kwenye gari, ghafla tu Abdullahi Dere sijui ni kwa namna gani ya haraka akatoa bastola kiunoni mwake..
kwa kasi ya ajabu na kummiminia risasi yule mwanajeshi aliyekuwa anawakagua.

Wanajeshi wengine wale ambao walikuwa pembeni ya Humvee wakajibu mapigo kwa kuwamiminia risasi akina Abu Aish na wenzake.
Isipokuwa yule Fouad aliyekaa siti ya nyuma ripoti ya jeshi la Somalia inadai..
kwamba alifanikiwa kutoroka (hapo mbele tutaona kwa nini hawakumuua na walisema "alikimbia").

Baada ya wanajeshi wa Somalia kuwamiminia risasi na kuwaua Abu Aish na mwenzake, wakaanza kupekua gari yao.

Ndani ya gari ndio wakakuta vile vitu... begi limejaa fedha taslimu dola...
za Kimarekani elfu 40, simu za mkononi 15, laptop 3 na pamoja na hivyo wakawakuta wote walikuwa na hati za kusafiria za kugushi ambazo zilikuwa zinawaonyesha kama raia wa Afrika Kusini.

Kwa hiyo wakataka kujua identity zao za ukweli.
Wakachukua alama zao za vidole na DNA alafu..
zikapelekwa maabara kupimwa.

La haula.! Achana na yule somo aliyekimbia, achana na yule Dere.. mtazame yule Abu Aish.
Vipimo vya DNA vilikuwa vyaonyesha kwamba Abu Aish jina lake halisi lilikuwa ni Fazul Abdullah Mohammed, top commander wa Al-Qaida kwa ukanda wote wa Afrika...
Mashariki.

Huyu Fazul Abdullah ndiye alikuwa moja ya mastermind wa ulipuaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998.
Fazul Abdullah kijana mdogo msomi muhitimu wa chuo kikuu akiwa na shahada ya mifumo ya kompyuta. Akihitimu kama top student kwenye...
darasa lake.
Fazul Abdullah ambaye CIA wamekuwa wakimsaka kwa muda wa miaka 14 bila mafanikio.

Kesho yake Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani kipindi kile Bi. Hillary Clinton akafanya mkutano na wana habari kutangazia ulimwengu kuhusu ushindi huu mnono Marekani kufanya oparesheni
iliyofanikisha kuuwawa kwa Fazul Abdullah Mohammed.
Oparesheni ambayo ilifanywa na special force ya Somalia ikiongozwa na Kapteni Hassan Mohamed Abukar na mwakilishi wa CIA - Special Contractor Michael Goodboe (yule mzungu ambaye alikuwa amevalia kiraia pale kwenye kizuizi).
Sasa, kuelewa mwanzo wa tukio hili, kunatupa fursa ya kufahamu kuhusu oparesheni za CIA hapa Afrika Mshariki ambazo zafanywa kila siku mitaani kwetu.

Namna gani?
Hebu twende mwanzo kabisa,

Tarehe 14 Oct 2003 usiku wa saa sita maeneo ya Upanga mtaa wa Mfaume, Polisi wawili walio
valia kiraia walifika nyumbani kwa mwarabu anayeitwa Mohammed al-Asad na kumweleza wanahitaji kwenda naye kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano mafupi.

Naomba unisaidie ku-retwee uzi huu tuwafikie watu wengi zaidi.
Nakuja kuweka PART 2.

Habibu B. Anga
To Infinity and Beyond

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

Mar 25, 2023
Ukitaka kuelewa chanzo cha vita ya Ukraine basi unapaswa kufahamu mkasa wa huyu unaye muona pichani na Zitto… anaitwa Victor Yushchenko

Miaka kadhaa iliyopita huyu somo alikumbwa na kadhia ya kulishwa sumu na kupata madhara kama yale ambayo yalimkuta Dr. Mwakyembe..

Thread..
enzi zile za Richmond na Dowans mpaka akapelekwa India kutibiwa.
Ngozi ya mwili yote iliharibika na kuanza kupukutika kama unga

Huyu Yuschenko yeye kadhia hii ilimtokea mwaka 2004 kipindi hicho akiwa anagombea Urais wa Ukraine
Yushchenko alikuwa anachuana mwanasiasa Yanukovych..
ambaye alikuwa ni Waziri Mkuu wa serikali ambayo ilikuwa inamaliza muda wake

Uchaguzi huu wa Ukraine kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni mchuano wa kiushawishi kati Marekani na Urusi wakitunishiana misuli.
Marekani walikuwa wanamuunga mkono huyu somo pichani Bw. Yushchenko wakati Urusi
Read 24 tweets
Aug 18, 2022
Roman Abramovich: Utajiri wa Damu Mpaka Kumuingiza Ikulu Putin

Thread,

Namna ambavyo mtoto yatima aliyelelewa katka umaskini ameweza kuibuka moja ya binadamu wenye ukwasi mkubwa duniani na mpaka kuweza kumuingiza Ikulu Vladmir Putin ni mkasa wa aina yake…

(Usisahu ku-Retweet) Image
Wazazi wake wote wawili licha ya kuishi maisha yao yote nchini Russian lakini asili yao ni Waisrael. Mama yake aliitwa Irina na alifariki kipindi Roman bado angali mchanga kabisa wakati baba yake ambaye aliitwa Arkady alifariki kwa ajali ya gari miaka michache baadae Roman akiwa
bado mtoto mdogo kabisa.

Hii ndio ilikuwa sababu ya Roman kwenda kulelewa kwa ndugu zake Komi kaskazini mwa Urusi ambako kuna baridi kali na umasikini uliokithiri

Ujanani mwake, Roman aliwahi kujiunga na jeshi kabla ya kuacha na kuamua kwenda Moscow kutafuta maisha
Akiwa Moscow
Read 23 tweets
Dec 21, 2021
TUMEWAHI KUWA NA CHANJO KWA MALENGO YA KISHUSHUSHU

Thread..

Kadiri ulimwengu unavyobadilika, stadi ya Ujasusi inazidi kuwa complex kwa kuhusisha mbinu ambazo nyingine ukizisikia unaweza kudhani labda watazama sinema au waota, lakini ndio uhalisia wa ulimwengu ulipo sasa katika
katika juhudi za mataifa na makampuni makubwa kupanua ushawishi wao juu ya dunia yote na kulinda maslahi.

Kuna kisa cha tofauti sana ningependa nikijadili leo hii. Kisa cha tofauti kabisa..

Wengi tutakuwa tumewahi kusikia shirika linaloitwa “Save the Children”. Ni moja ya…
Shirila kubwa zaidi la misaada ya kibinadamu ulimwenguni ambalo limejikita hasa kwenye kutoa misaada inayolenga kuboresha hali za maisha ya watoto wadogo.

Mwaka 2011 shirika hili lilikuwa kwenye shughuli zake mahala paitwa Khyber nchini Pakistan.
Save the Children walikuwa na…
Read 43 tweets
Oct 14, 2021
𝗕𝗜𝗡𝗧𝗜 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗜𝗔𝗞𝗔 25 𝗔𝗡𝗔𝗬𝗘𝗜𝗧𝗜𝗞𝗜𝗦𝗔 𝗔𝗙𝗥𝗜𝗞𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗜𝗞𝗜

Thread..

Siku ya 30 May 2019, maafisa Usalama Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA, Nairobi walimuweka kizuizini abiria mmoja mwenye hati ya kusafiria ya kidiplomasia, mwanaume.. Image
wa asili ya kisomali. Japokuwa watu wenye diplomatic passport wapata exemptions kadhaa kwenye kaguzi za uwanja wa ndege, lakini ilikuwa ni lazima kwa maafisa hawa kumuhoji abiria huyu kutokana na utata wa mzigo ambao alikuwa nao.

Huyu somo alikuwa na briefcase ambalo ndani yake
alikuwa amebeba fedha cash dola za Kimarekani milioni moja na nusu.

Mtu huyu nyaraka zake zilikuwa zinaonyesha kwamba alikuwa safarini kuelekea nchini Ethiopia.

Maafisa hawa wa Usalama. Wakaanza kumuhoji abiria huyu sababu za kusafiri na kiwango kikubwa hivyo cha fedha na pia.. Image
Read 98 tweets
Sep 4, 2021
𝗞𝗔𝗕𝗟𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗞𝗨𝗟𝗨.. 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗔𝗗𝗛𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗙𝗢

Thread..

Ukiwa unatoka Lusaka kwenda Jimbo la Magharibi, kabla hujaingia mji wa Mongu kuna kipande cha barabara kinajulikana kama Limulunga Road.
Kipande hiki cha barabara mwaka juzi kimetupa tukio la kipekee Image
ambalo kwa kiwango kikubwa tukio hili limebadili mwelekeo wa siasa la bara zima la Afrika na hasa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Pengine pasipo tukio hili huyu Hichilema tunayemuona leo asingelikuwa Rais. Lilikuwa tukio la kipekee kabisa..

Kila mwaka pale Zambia huwa wana
sherehe maarufu zinaitwa "Kuomboka Ceremony".
Wenzetu mpaka leo hii bado wanatambua cheo cha asili cha "Litunga" ambaye ni Mfalme wa kabila la Walozi.
Kila mwaka mwishoni mwa msimu wa mvua mfalme huwa anahama kutoka makazi yake ya bondeni ya Lealui na kuhamia makazi yake yaliyo..
Read 41 tweets
Aug 10, 2021
𝗨𝗧𝗔𝗝𝗜𝗥𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔𝗞𝗔 𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗟𝗜𝗡𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗩𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜

Thread..

Mwaka juzi kwenye hafla ya mapokezi ya ndege kwenye nchi fulani hivi hapa Afrika Mashariki kuna incident ndogo tu ilitokea lakini wengi ikatufikirisha sana.

Dakika chache baada ya Rais wa...
nchi hiyo kumaliza kuongoza hafla hiyo ya mapokezi ya ndege akashuka jukwaani na akianza kuandoka.
Lakini kabla hajakwenda kupanda gari, kama ambavyo ilikuwa ada kwa Rais yule akaelekea upande waliokaa wananchi wake na ili awasalimie.
Na kusalimia huku akaanza jukwaa ambalo...
walikuwa wamekaa wageni VIP.

Wageni wale mashuhuri wakasimama na Rais akawa anapita akiwapa mkono.

Mojawapo ya wageni wale mashuhuri alikuwa ni mfanyabiashara maarufu sana mwenye asili ya kihindi.
Rais alipopita mbele yake, mfabiashara huyu akanyoosha mkono ili asalimiane na...
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(