Tangu kuapishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, hotuba zake zimekuwa zikiwakuna wengi—zinakuna panapowasha!
1/
Kwanza alianza kwa kuwaagiza Takukuru na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufuta kesi zisizo na msingi na uhalali wa kupelekwa mahakamani. Halafu majuzi akawaagiza Waziri wa Fedha kukomesha ukamuaji, ubabe na maguvu unaotumika kuwakamua walipa kodi maana watahama nchi
2/
Hotuba za Mama Samia zina maneno rahisi rahisi lakini ukijaribu kuzitafakari vyema zinaweza kukukosesha usingizi. Kwa mfano, unaweza kujiuliza, je, mahakama zetu zimekuwa zikishikilia watu bila misingi ya ushahidi?
3/
Au, idara zetu za kodi zimekuwa zikitumia mabavu badala ya akili na weledi wa kitaaluma?
Imekuwajekuwaje mpaka imefika mahala Mama Samia analazimika kuwakumbusha wataalamu kutumia weledi na miongozo ya kitaaluma ambayo wao wenyewe wamezisomea?
4/
Watendaji waliosemwa na Rais Samia hawako peke yao: Kwa ujumla, utendaji wa idara nyingi nchini mwetu umeacha barabara rasmi na kuhamishiwa vichochoroni.
5/
Mfano mzuri ni wimbi la wakurugenzi ambao miongozo ya kazi inaelekeza kupokea fomu za wagombea na kuratibu chaguzi kwa mujibu wa sheria lakini badala yake wao wamekuwa wakitokea mlango wa uani na kukimbia kila wanapoona au kusikia fununu kuwa mpinzani anajiandaa kurejesha fomu
6
Hizi ni njia za uchochoro maana hakuna chuo chochote cha utumishi kinachomfundisha mtu kukimbia ofisi—ni matumizi ya nguvu bila akili ambayo Rais Samia ameamuru yakomeshwe!
MWISHO
7/
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh