Miaka kadhaa iliyopita nilipata mzuka wa kwenda kutimiza moja ya ndoto zangu kubwa - kupanda Mlima Kilimanjaro.
Siku zote nilitamani kufika juu kabisa ya "Paa la Afrika". Nikasema ipo siku tu!
Hatimaye siku zikawadia za kuitimiza ndoto yangu hii kongwe.
Ilikuwaje?
THREAD👇🏾
Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails. Sikusafiri peke yangu, kundi letu tulikua 21. Njia tuliyotumia ni Marangu.
Gharama ilikuwa ni USD 560 kwa kila mmoja na hii ilihusisha kila kitu kuanzia usafiri Dar-Moshi, chakula, hoteli, vifaa, ada za getini, personal guides n.k.
MAANDALIZI YA SAFARI
Baada ya kuthibitisha ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro, jambo la kwanza nilifanya medical checkup. Nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni.
Basi, nikaanza mazoezi. Nakimbia uwanja huki nazunguka mara 7-10 kila siku kuuandaa mwili..
..mazoezi ya kupandisha ngazi wanaojua jengo la Uhuru Heights.. Nimepanda na kushuka zile ngazi saana..
Pia tulikuwa tunafanya Sea Cliff Walk. Haya yalikuwa matembezi kutoka Upanga hadi Sea cliff kwenda na kurudi kila jumamosi kwezi mara mbili. Kim Beach Kigamboni kutembea etc..
Nilijisajili na kitengo cha Flying Doctors Africa. Hawa wako chini ya @Amref_Worldwide. Wanatoa huduma ya helikopta kwa ajili ya kufanya uokozi (rescue) mlimani pakitokea dharura.
Nilikuwa nikiambiwa kina huduma yeyote lazima nijisajili ili kujihami 😃😃
Kusema ukweli nilikuwa muoga sana kwa sababu ya stories niIizokuwa nikizisikia. So nilichukua tahadhari zote ukizingatia ndio mara yangu ya kwanza kwenda kupanda mlima na huwezi jua nini kitatokea huko juu milimani.