Wakuu, mnisamehe bure, majukumu yalibana mno. Niko na muda wa kutosha sasa.
Nitaweka Parts kadhaa mfululizo kuwafidia uraibu niliowaachia muda wote huu.
Tuendelee
Mara ya mwisho
Nilieleza kuhusu mgogoro ambao ulitokea pale Vodacom Congo.
Ambapo Vodacom Group walikuwa wameingia ubia na kampuni ya Congolese Wireless Network kuunda kampuni ya Vodacom Congo ambapo kwenye ubia huo Vodacom Group walikuwa na 51% ya umiliki huku CWN wakiwa na 49%.
Lakini baada,
ya muda kukaibuka mgogoro. CWN wakiituhumu Vodacom Group kuendesha Vodacom Congo kana kwamba ni mali yao peke yao.
Lakini pia waliwatuhumu Vodacom kwa kutoingiza kiwango chote cha fedha za uwekezaji ambazo walikuwa wanatakiwa kufanya kwenye makubaliano ya mkataba.
Mgogoro huu..
Ukamfikia mpaka Rais Kabila.
Mwishowe yakafikiwa makubaliano kwamba Vodacom wanunue 49% ya umiliki wa CWN na kisha watafute mbia mwingine mzawa.
Lakini mwishoni ulipowadia wasaa wa kufanya malipo, Vodacom wakatangaza kutokubaliana na makubaliano ya awali ya kunununua 49% ya CWN
Serikali ya Congo ikaja juu na kumkamata Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom na Bodi nzima ya Wakurugenzi na kuwasweka Lupango.
Ndipo wakapewa taarifa kwamba yuko mtu mmoja tu mwenye uwezo wa kuwatoa kwenye shimo hilo. Mtu huyu ni Moto Mabanga.
Sasa tuendelee tokea hapo..
Ili kuelewa Vodacom na uhuni ambao waliufanya pale Congo na pia ili kumuelewa Moto Mabanga kuna matukio mawili kwanza nataka niwape.
Yaani kwamba matukio haya mawili yatatusaidia kuelewa sawia zaidi kwa nini Vodacom walifanya kile ambacho walifanya pale Congo na pia tutaelewa
kwa nini ni Moto Mabanga pekee alikuwa ana uwezo wa kuwatoa Vodacom kwenye kile kizungu mkuti pale Congo.
Matukio haya mawili, moja limetokea hapa kwetu Tanzania na la pili limetokea nchini Afrika Kusini.
Matukio haya mawili ni muhimu sana kuyaelewa kadiri tunavyoendelea na hii
Makala.
Nitaanza kwa kueleza tukio ambalo lilitokea nchini South Africa.
Miaka ya nyuma hapa kidogo pale SA kulikuwa na kijana mmoja anaitwa Nkosana Makate (mtu mzima sasa yuko kwenye 40s)
Miaka ya mwanzoni kabisa ya 2000's kijana huyu alipata nafasi ya kufanya internship makao
Makuu ya Vodacom hapo South Africa. Intership hii alikuwa anaifanya kwenye idara ya uhasibu ndani ya Vodacom
Kipindi hicho hicho pia kijana huyu alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa anaishi mjini Polokwane (yeye alikuwa akiishi Midrand).
Polokwane na Midrand umbali wake ni kama
Dar na Tanga hivi. Kwa hivyo mahusiano yao kwa kiwango kikubwa yalikuwa ya simu.
Mara kadhaa walikuwa wakigombana kutokana na binti huyo kutompigia simu Nkosana mpaka pale tu Nkosana akimpigia, na sababu yake siku zote binti huyu alikuwa anasema hana salio la kupiga simu.
Kwenye
Kukereka kwa jambo hili Nkosana akapata wazo.
Kwamba, kwa nini mitandao ya simu isianzishe huduma ambayo itamwezesha mtumiaji akiishiwa salio kubofya namba fulani kisha mtu fulani lengwa apate 'notification' ya kumjuza kwamba fulani anahitaji ampigie simu.??
Kwenye kuwaza kwake
huku ndiko akabuni wazo la huduma ya "Tafadhali Nipigie" (Please Call me)
Aliporejea kazini akamshrikisha bosi wake wazo hili. Bosi wake akalipenda. Akamkutanisha na kigogo ndani ya Vodacom ambaye alikuwa anaitwa Philip Geissler ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Utawala na Product
Development na pia mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom.
Geissler naye akalipenda hili wazo. Akamwambie Nkosana aliandike wazo lake hili vizuri ili amsaidie kulifikisha kwenye vikao vya ngazi za juu.
Nkosana akajipinda akaandika proposal ambayo aliipa jina la Buzz Talk Time
Kisha akawasilisha andiko lake kwa Geissler.
Wakakubaliana kwamba kama wazo lake hili alilobuni litapitishwa na kutumiwa na Vodacom basi atapata 15% ya faida ambazo zitapatikana kutokana na simu ambazo zitapigwa kutokana na mtu ku-respond baada ya kupata "Tafadhali Nipigie"...
Kisha Geissler akachukua proposal na kuiwasilisha kwa Alan Knott-Craig ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom Group kipindi hicho.
Alan naye akalipenda wazo na kuagiza lifanyiwe kazi haraka
Miezi kadhaa baadae Vodacom wakazindua huduma yao mpya ya "Tafadhali Nipigie". Kwamba hata
Kama mteja hana salio anaweza kutuma ujumbe wa kuomba kupigiwa kwenda kwa jamaa na marafiki.
Huduma hii ikapendwa mno pale South Africa na kufanya Vodacom kuianzisha pia kwenye nchi nyingine ambako wana matawi.
Hata hapa Tanzania tukafikiwa na hii huduma ya "Tafadhali Nipigie"
Na tuliipenda haswa kama wakumbuka.
Punde si punde mitandao mingine nayo ikaiga.
Lakini kuna masuala mawili ambayo Vodacom walifanya uhuni.
Mosi, wakati wanazindua hii huduma nchini South Africa, waliwaeleza kwamba wazo hili lilibuniwa na CEO wao bwana Alan baada ya kuwaona..
walinzi wake nyumbani wakitaabika kuwasiliana na ndugu zao pindi wakiishiwa salio.
Pili, ile 15% ya kijana Nkosana hawakumlipa.
Kitendo hiki kilimuuma sana Nkosana. Kwanza wamekataa kumpa credit yeye kama mbunifu wa hiyo huduma na pili wamekataa kumpa hela yake 15% ya faida.
Kwa muda wa karibia mwaka mzima alijaribu kuonana na Geissler au Alan, lakini wote walikuwa wanamkwepa.
Ndipo akaamua kugeukia nguvu ya umma.
Kijana Nkosana akongea na vyombo vya habari na kueleza mkasa mzima namna gani alibuni wazo la tafadhali nipigie na ahadi ambazo alipewa..
akaonyesha na uthibitisho.
Umma wa watu weusi nchini SA ulilipuka kwa hasira. Nchi nzima iliwaandama Vodacom kwa unyonyaji na ukandamizaji wa haki ya kijana huyo mweusi.
Makampuni ya uwakili yakajitokeza kujitolea kumsimamia kesi kijana Nkosana. Hatimaye mwaka 2008 Nkosana..
akafungua kesi ya madai dhidi ya Vodacom kwenye Mahakama Kuu ya South Gauteng akidai fidia ya mamilioni ya Rand.
Hili ni tukio la kwanza ambalo nataka ulikumbuke.
Muhimu sana.
Nimesema yako matukio mawili.
Tukio la pili lilitokea hapa Tanzania. Nieleze,
Katika mwaka wa mwisho
wa utawala wa Mzee Mkapa, yaani mwaka 2005, nchi yetu ilifanya 3rd Round ya mnada wa vitalu vya gesi huko kusini mwa nchi.
Jambo moja ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba vitalu vyetu vilikuwa haviuziki.. yaani vilikuwa havichangamkiwi.
Licha ya kelele zote za wanasiasa..
unazosikia wanapiga kuhusu gesi, ila vitalu vyetu vilikuwa vinadoda havichangamkiwi na makampuni uchimbaji gesi na mafuta. (Ndio maana siku hizi husikii sana kelele za gesi sababu hata mnada wetu wa mwisho wa vitalu (4th Round) uliofanyika mwaka 2014 nao ulidoda pia. Nitaeleza..
Vivyo hivyo pia ilikuwa kwenye mnada wetu wa kwanza 2001. Tuliweka mnadani vitalu 6 tukapata bid kwenye kitalu 1 tu.
Pia mnada wetu wa pili 2002 tuliweka sokoni vitalu 11 lakini tulipata bid kwenye vitalu 4 tu.
Mnada pekee ambao ulikuwa wa mafanikio ni huo wa 2005. Tulikuwa na..
Vitalu 7 tulipata bid vitalu vyote.
Jambo ambalo halijulikani ni kwamba mnada huu ulifanikiwa kutokana na uhusika wa Moto Mabanga.
Siku chache baada ya mnada kutangazwa, Moto Mabanga alifunga safari kwenda Huston, Texas kuonana na mtu anaitwa Dr. Alan Stein
Nisaidie ku-Retweet
Usiku huu naweka Part 4. Nitaweka mfululizo Part nyingi niwezavyo kuwafidia uraibu wa siku kadhaa hizo ambazo nimekuwa kimya.
β’ β’ β’
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Mwaka wa mwisho wa utawala wa Kikwete ulikuwa ni mgumu kuliko umma unavyofahamu.
Alikuwa anapambana na mpasuko ndani ya chama, kushamiri kwa upinzani⦠lakini zito zaidi ilikuwa ni changamoto iliyotokea siku ya 13 May 2015.
Threadβ¦
Hii picha hapa chini ni picha halisi ikimuonyesha Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi Tanzania kipindi kile Bw. Othman Rashid akifanya suala ambalo si la kawaida na hatukuwahi kuliona hapo kabla kwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS kufanya jukumu la βVIP Protectionβ
(Niliyemzungushia duara)
Pichani DGIS Othman alikuwa anamuongoza Rais Nkurunziza na msafara wake kuwaondoa kwa dharura toka Serena Hotel kuwapeleka uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere.
Siku hii 13 May 2015 ilikuwa moja ya siku mbaya sana katika ulingo wa usalama, ujasusi na diplomasia ya Afrika Mashariki
Ukitaka kuelewa chanzo cha vita ya Ukraine basi unapaswa kufahamu mkasa wa huyu unaye muona pichani na Zitto⦠anaitwa Victor Yushchenko
Miaka kadhaa iliyopita huyu somo alikumbwa na kadhia ya kulishwa sumu na kupata madhara kama yale ambayo yalimkuta Dr. Mwakyembe..
Thread..
enzi zile za Richmond na Dowans mpaka akapelekwa India kutibiwa.
Ngozi ya mwili yote iliharibika na kuanza kupukutika kama unga
Huyu Yuschenko yeye kadhia hii ilimtokea mwaka 2004 kipindi hicho akiwa anagombea Urais wa Ukraine
Yushchenko alikuwa anachuana mwanasiasa Yanukovych..
ambaye alikuwa ni Waziri Mkuu wa serikali ambayo ilikuwa inamaliza muda wake
Uchaguzi huu wa Ukraine kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni mchuano wa kiushawishi kati Marekani na Urusi wakitunishiana misuli.
Marekani walikuwa wanamuunga mkono huyu somo pichani Bw. Yushchenko wakati Urusi
Roman Abramovich: Utajiri wa Damu Mpaka Kumuingiza Ikulu Putin
Thread,
Namna ambavyo mtoto yatima aliyelelewa katka umaskini ameweza kuibuka moja ya binadamu wenye ukwasi mkubwa duniani na mpaka kuweza kumuingiza Ikulu Vladmir Putin ni mkasa wa aina yakeβ¦
(Usisahu ku-Retweet)
Wazazi wake wote wawili licha ya kuishi maisha yao yote nchini Russian lakini asili yao ni Waisrael. Mama yake aliitwa Irina na alifariki kipindi Roman bado angali mchanga kabisa wakati baba yake ambaye aliitwa Arkady alifariki kwa ajali ya gari miaka michache baadae Roman akiwa
bado mtoto mdogo kabisa.
Hii ndio ilikuwa sababu ya Roman kwenda kulelewa kwa ndugu zake Komi kaskazini mwa Urusi ambako kuna baridi kali na umasikini uliokithiri
Ujanani mwake, Roman aliwahi kujiunga na jeshi kabla ya kuacha na kuamua kwenda Moscow kutafuta maisha
Akiwa Moscow
TUMEWAHI KUWA NA CHANJO KWA MALENGO YA KISHUSHUSHU
Thread..
Kadiri ulimwengu unavyobadilika, stadi ya Ujasusi inazidi kuwa complex kwa kuhusisha mbinu ambazo nyingine ukizisikia unaweza kudhani labda watazama sinema au waota, lakini ndio uhalisia wa ulimwengu ulipo sasa katika
katika juhudi za mataifa na makampuni makubwa kupanua ushawishi wao juu ya dunia yote na kulinda maslahi.
Kuna kisa cha tofauti sana ningependa nikijadili leo hii. Kisa cha tofauti kabisa..
Wengi tutakuwa tumewahi kusikia shirika linaloitwa βSave the Childrenβ. Ni moja yaβ¦
Shirila kubwa zaidi la misaada ya kibinadamu ulimwenguni ambalo limejikita hasa kwenye kutoa misaada inayolenga kuboresha hali za maisha ya watoto wadogo.
Mwaka 2011 shirika hili lilikuwa kwenye shughuli zake mahala paitwa Khyber nchini Pakistan.
Save the Children walikuwa naβ¦
Siku ya 30 May 2019, maafisa Usalama Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA, Nairobi walimuweka kizuizini abiria mmoja mwenye hati ya kusafiria ya kidiplomasia, mwanaume..
wa asili ya kisomali. Japokuwa watu wenye diplomatic passport wapata exemptions kadhaa kwenye kaguzi za uwanja wa ndege, lakini ilikuwa ni lazima kwa maafisa hawa kumuhoji abiria huyu kutokana na utata wa mzigo ambao alikuwa nao.
Huyu somo alikuwa na briefcase ambalo ndani yake
alikuwa amebeba fedha cash dola za Kimarekani milioni moja na nusu.
Mtu huyu nyaraka zake zilikuwa zinaonyesha kwamba alikuwa safarini kuelekea nchini Ethiopia.
Maafisa hawa wa Usalama. Wakaanza kumuhoji abiria huyu sababu za kusafiri na kiwango kikubwa hivyo cha fedha na pia..
Ukiwa unatoka Lusaka kwenda Jimbo la Magharibi, kabla hujaingia mji wa Mongu kuna kipande cha barabara kinajulikana kama Limulunga Road.
Kipande hiki cha barabara mwaka juzi kimetupa tukio la kipekee
ambalo kwa kiwango kikubwa tukio hili limebadili mwelekeo wa siasa la bara zima la Afrika na hasa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
Pengine pasipo tukio hili huyu Hichilema tunayemuona leo asingelikuwa Rais. Lilikuwa tukio la kipekee kabisa..
Kila mwaka pale Zambia huwa wana
sherehe maarufu zinaitwa "Kuomboka Ceremony".
Wenzetu mpaka leo hii bado wanatambua cheo cha asili cha "Litunga" ambaye ni Mfalme wa kabila la Walozi.
Kila mwaka mwishoni mwa msimu wa mvua mfalme huwa anahama kutoka makazi yake ya bondeni ya Lealui na kuhamia makazi yake yaliyo..